Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Wanawake wa Kiafrika na Sifa kubwa ya Uzazi

Wanawake wa Kiafrika na Sifa kubwa ya Uzazi

Wanawake wa Kiafrika na Sifa kubwa ya Uzazi

Wanawake wa kiafrika wanafahamika kwa sifa yao kubwa sana ya uzazi, na hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha melanin ambayo huwachochea kuweza kufyonza mionzi ya mwanga, na kusisimua uzalishaji wa chembechembe zinazoitwa ‘’alpha-MSH’’, ambazo hizi ndizo husisimua sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’Hypothalamus’’ kuzalisha homoni inayosisimua homoni zote za uzazi inayoitwa ‘’GnRH’’. Hii ndiyo homoni inayosisimua homoni za kike za ‘’Estrogens, na Progesterone’’, ambazo hizo ndizo huchochea tabia za kike, na maumbile ya kike ya Waafrika hasa maungio yao makubwa ya mwili, kama makalio, hips, matiti, n.k. 

Maumbile makubwa ya nyonga huwawezesha kuzaa watoto wengi bila shida zozote zile za uzazi. Wanawake wa Kiafrika huwa na uwezo mkubwa wa uzazi na huwa na hisia za mapenzi kwa muda mwingi zaidi ukilinganisha na kanda za Ulaya-Asia, kutokana na ukweli kuwa; kiwango kikubwa cha mwanga kipindi cha siku, hata na usiku wa mwezi, hupunguza kiwango kikubwa cha homoni za melatonin kutoka katika tezi ya ubongo inayoitwa ‘’Pineal gland’’. Melatonin inapokuwa chini, alpha-MSH huchochea GnRH kuzalisha homoni za uzazi, na hasa homoni ya LH, ambayo huwafanya wanawake kutoa yai ‘’ovulation’’, au kuwa na joto, au hamu ya mapenzi, ambapo kwa sehemu nyingi huwa zaidi kuanzia msimu wa Kiangazi kuelekea kipupwe, hasa mwezi wa Kumi ambapo huwa na mwezi kamili ‘’full moon’’. 

Kwa Afrika hali hizi huwa kwa nyakati nyingi zaidi. Kiwango kikubwa cha LH pamoja na homoni za Progesterone huwapandisha Joto la mwili wanawake hawa katika siku zao, na hili Joto huwa kubwa zaidi kwa Waafrika kutokana na asili yao ya melanin nyingi ambayo hufyonza mwanga, na kusisimua Kuzalishwa kwa chembechembe za ‘’Nitric Oxides’’, ambazo hufungua zaidi mishipa ya via vya uzazi na kuongeza msisimko, na pia huongeza maji kusaidia homoni ‘’PGs’’ kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya utungwaji wa mimba.

Mfumo wao imara wa ulaji huwafanya kuwa na balansi nzuri ya homoni za testosterone, ambazo huwafanya kuwa na hamu ya mapenzi. Asili yao ya Estrogens nyingi huwafanya kutokuwa na hasira sana kutokana na kuwa na homoni nyingi za serotonin, ambazo huwafanya hali zao ‘’mood’’ kuwa sawa kwa hatua karibia zote za mizunguko yao ya mwezi.

Je Wajua

Kuna uhusiano wa neno "Menstrual" na "Moon". Kuna uhusiano wa mzunguko wa mwezi wa siku 28, na wastani wa mizunguko ya wanawake ya siku 28. Ijapokuwa wengi huwa na wastani wa siku kati ya 25 mpaka 35. Mwanga unaratibu mzunguko mzima wa homoni na uzazi, kitendo Cha Afrika kuwa na urefu sawa wa Usiku na siku, huwa-Fanya wanawake kuwa imara sana zaidi ya wanawake waliopo sehemu ambazo mzunguko wa siku na Usiku nyakati kadhaa huwa si sawa kabisa. Hata hivyo wanawake wengi saivi wanashida bila kujali mazingira waliyopo kutokana na matumizi ya mianga ya kisasa Wakati wa Usiku.

Mwanamke Wa Kiafrika haitaji Maji ya Manispaa, anahitaji Vyungu na visima

Waafrika na serikali zao wanahangaika kumtua ndoo mwanamke, kwa kumpelekea mfumo wa maji mpaka bafuni, lakini matokeo yake wanamfanya akifika miaka 28 tu anaanza kuisha; kwa kuwa tezi ya pituitary husisimka kuzalisha homoni kila mwanamke anapobeba uzito kichwani mwake. Waafrika walipokuwa wakibeba vyungu vya maji vichwani, waliuambia ubongo wao kuwa bado wanahitaji madini ya Calcium, ili kuimarisha mifupa yao kwa kuwa bado wanabeba watoto. Waafrika wameishi miaka milenia 2 na maji safi toka ardhini, mitoni, na katika chemchemi zao, lakini ndani ya karne washaharibu maji yao kwa makemikali sumu. 

Ukiachana na makemikali yanayotoka shambani, yapo wanayoyaita Dawa za maji kama Fluorides ambazo ni hatari kwa kudaka electrons mwilini ‘’strong electronegative’’. Na ukweli ni kuwa; mwili wenye afya ni wenye chaji hasi ‘’Negative’’, kitu ambacho kimelenga biolojia ya mwili kupitia mizunguko yake ‘’all metabolic cycles are enzymes oriented which are negatively charged’’. Maji ya manispaa yenye ‘’Fluorides’’ yanawaua bakteria wazuri wa tumboni, na wa kwenye ngozi. 

Waafrika wa leo na serikali zao wamejikita kuwashusha wamama watoto migongoni, kwamba sasa wapo vizuri kiuchumi. lakini madhara yake wote wanaishia kupata shida ya ‘’Pregnenolone steal syndrome’’, hawawezi kuzaa watoto sio 10 tena, bali hata watano tu bila upasuaji. Tena wanauchochea pia kwa mfumo wao wa kukesha usiku wakijiona wameendelea kwa kufanya kazi usiku, kukesha kwenye masinema, na kusikiliza sana miziki ya kisasa inayoathiri kemia ya maji iliyo nyuma ya biolojia ya ukuaji wa mtoto tumboni, aliye zaidi ya asilimia 85% maji, Afrika ina safari ndefu sana.