Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

MIMEA NI KAMA JAMII ZA WATU

Namna mimea inaishi kama jamii

Kwanini Mimea mingi huota jamii mbalimbali katika sehemu moja?

Ukiona sehemu kuna aina moja tu ya mimea basi ujue imepandwa, kama ukiona Mimea aina mbalimbali imeota eneo moja basi ujue hiyo ndiyo asili. Mimea kwa asili huwa jamii mbalimbali katika eneo moja kwa kuwa huwa inategemeana. Kila mmea una udhaifu na ubora wake. Na huu huwa katika namna ya madini unayoyahitaji, na unayoyasambaza zaidi, lakini pia kupitia uwezo wao wa kuchangamana na wadudu, na vimelea mbalimbali. Kuna mimea inaweza kuua zaidi vimelea kadhaa tu, na mingine huwa hivyohivyo kwa aina nyingine. Mimea hushirikiana sana kuliko wengi wanavyofahamu, kwa mfano;

Je Mimea huweza kuwasiliana?

Inafahamika kwa kitambo sasa, Mimea inaweza kuwasiliana kupitia network za mizizi yake, ambayo hushirikiana pia na jamii za fangasi ‘’Mycorhizzal connection’’. Mimea huambiana uwepo wa hatarishi kama aina moja ya mmea unapoliwa na mnyama kuwa mingine iongeze kuzalisha kemikali chungu katika majani yake, ili mnyama ashindwe kuendelea kula. Na hii ndiyo sababu Wanyama hula wakitembea, kwa kuwa kila baada ya muda eneo lililoliwa la mimea huwa limeshakuwa chungu.

Pia imeonekana mimea hutambua hata Watoto wake, Mmea huonekana kuusapoti mmea mdogo wake kwa kupunguza kufyonza maji ili usikose maji. Pia mimea hushea hata chembechembe za kinga kati yake. Mimea imeonekana kuwasiliana pia kupitia mawimbi madogo sana ya sauti ‘’Infrasonic frequencies. 

Kwanini Mimea hukua Misimu tofauti-tofauti?


Mimea hulenga mabadiliko madogo madogo sana ya hali za hewa, vipindi vya jua, na mzunguko wa dunia. Mbegu za mimea huwa mithili mfu, lakini husubiria tu wakati sahihi kufika. Kila Mmea huwa na mithili ya ‘’Codes’’ maalumu ya wakati wake maalumu wa kukua, kutoa maua, kuzaa matunda, na kupukutisha.

Kwanini ni vigumu kuona mazao porini ila magugu ndiyo hushamiri?

Hili lilikuwa swali langu nikiwa mdogo shule ya msingi. Mazao mengi hayashamiri misituni kwa kuwa mazao karibia yote tunayolima sio asili yake katika mazingira yetu. Vyakula vyote 12 nilivyoviorozesha awali havikutoka Afrika ukanda wa Tropiki hata kimoja. Magugu hushamiri sana Tropiki kwa kuwa Mimea ukanda huu huwa haitunzi matunda na mizizi mikubwa, kwa kuhofia vipindi virefu vya baridi na jua bila mvua. Huku mvua hunyesha kila wakati, na maji ni mengi, Mimea hutunza tu vitunda vidogo, na vimizizi vidogo. Kilimo cha kisasa kinachoathiri ardhi huchochea zaidi ishamiri mimea sugu tu, au Magugu ambayo wadudu hawawezi kuyala, au yanayoweza kustahimili zaidi kwenye ukame na stress kwa kuwa na biolojia complex zaidi. 

Kabla ya ujio wa wakoloni, na wapelelezi wa awali kabisa mfano toka Ureno, Uarabuni, na China, ukanda wa tropiki japokuwa kuna historia ya kilimo kwa jamii za kwanza kabisa za baadhi za wabantu, lakini bado jamii kubwa zaidi ziliegemea zaidi katika uwindaji. Kumbuka asilima 25% ya Wanyama wote wa duniani wapo Afrika peke yake, asilimia 20% ya ndege wote, na ndivyo ilivyo hata kwa wadudu, na 67% ya Samaki wote ‘’cichlids’’. Waafrika walikuwa wala nyama sana, na mizizi, mbegu, mbogamboga, matunda madogo, lakini hasa Mwanga kama nilivyoeleza katika blogs kadhaa.

To be continued....