Uhusiano wa Nyama, au mimea, na saikolojia ya Mlaji
Je kuna uhusiano wa ulaji wa nyama, au mimea, na saikolojia ya walaji?
Kila ulaji ambao utahusiana na upungufu wa virutubisho kwa afya ya ubongo, na mwili kwa ujumla kwa mtazamo tuliokwisha kuuona, lazima utatengeneza msongo wa Mawazo ‘’depression’’, ambayo ni matokeo ya Ubongo kuona upo hatiani kudhoofika na unahitaji kutoka katika hali hiyo. Huu unaweza kuwa mwanzo wa msukumo wa tabia za uraibu, ulafi, na hata matendo yasiyo mema yanayolenga tu kuufanya ubongo uridhike.
Yohana aliishi kwa kula Wanyama tu ‘’Nzige’, na asali, lakini Biblia imemtaja kama binadamu mwenye Ukuu zaidi katika ‘’Math11:11’’.
Hivyohivyo ilikuwa kwa Danieli 1:12’’ aliyekula mtama, au mbogamboga zaidi.
Tabia sio matokeo ya ulaji, na ndiyo maana tumbo ni sehemu ndogo sana ya mwili kama wasomi kadhaa walishe wanavyofikiria. Tabia njema ni matokeo ya Roho wa Mungu anayemuongoza mtu kuwa mwema bila kujali hali yake ya kimwili. ‘’Gal 5:22’’ inaonyesha ni Mungu tu ndiye awezaye kumfanya mtu kuwa na Upendo, furaha, amani, Fadhili, uaminifu, upole, uvumilivu, kiasi, na utu wema. Paulo akiwa gerezani anahamasisha watu katika ‘’Wafilipi 4: 8’’ kuwaza mambo yaliyo ya kweli, ya heshima, ya haki, yaliyo safi, yenye kupendeza, na yenye sifa njema tu’’.
Je Tanzania inadhihirisha tofauti za ulaji na afya za jamii husika?
Hili lipo wazo kabisa, tafiti kadhaa nilizowahi zinukuu katika kitabu changu cha Ubongo wa Mtu mweusi, vol 1, na hata kwa uzoefu wa kawaida kabisa, na takwimu za afya za miaka kadhaa, Jamii za watu wa nyanda za juu, kaskazini, kusini, na Kisha kanda za kuzunguka maziwa, na kisha Bahari, kama nilivyozipanga ndivyo zilivyopishana Urefu wa miaka na afya ya jamii zao toka mwanzo mpaka mwisho. Jamii za kanda za kati, na kusini chini, zimekuwa na takwimu mbaya sana za afya. Sababu zipo nyingi kama ambavyo marazote nimekuwa nikihamasisha mtazamo mpana zaidi, badala ya kukimbilia vyakula, inaweza kuwa Huduma za afya, elimu, uwezo wa kuchukua takwimu za tafiti kutokana na jiografia, au hali za hewa. Lakini katika mtazamo wa ulaji, jamii za nyanda za juu hasa kaskazini hufanya vizuri zaidi kutokana na kiwango kikubwa cha vyakula vya Wanyama, mbogamboga, baridi, ufanyaji kazi, wenda hata na Imani zao maana hakuna ajuaye.
Badala ya kusema makabila mengi yaliyokuwa na nguvu sana kwa Nchi kama ya Tanzania yametokana na kuzunguka ardhi zenye rutuba, uoto mzuri, mito mikubwa, maziwa, na mbuga za Wanyama, zilizowafanya kuwa na afya sana. Unaweza sema kutokana na makabila kadhaa kuwa na nguvu sana, yaliweza kupambania mazingira yaliyokuwa na rutuba sana, na vyakula zaidi vya mimea na Wanyama.
Je ni sahihi kutengana kwa mitazamo ya ulaji wa vyakula?
Sio kwa tafiti za India tu za Dr na mtaalamu wa Ubongo, Natasha, Toka zamani inafahamika watu wa hali za chini ndiyo hula zaidi mbogamboga, ‘’Warumi 14:3’’ inaandika ‘’ Mtu mmoja anayo Imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga’’. Lakini mstari wa 4 anasema, ‘’ Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali’’. Si vema kubaguana kwa mtazamo wa ulaji, na ni kosa kumuona mwenzako hana haki.
Nyakati za mwisho Biblia katika ‘’1Tim4:3’’ inasema nyakati za mwisho watu wata ‘’..zuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na Imani wenye kuijua hiyo kweli’’. Na hii ni Dhahiri kabisa kwa namna kumekuwa na takwimu za kushuka sana kwa kiwango cha Ndoa zinazofungwa, na sehemu kadhaa kama Japani idadi ya ndoa zimeshuka kwa zaidi ya Nusu, na imekuwa dunia nzima. Watu hawazuiwi moja kwa moja, lakini katika namna ya kitaalamu sana, na hivyo ndivyo ilivyo pia katika vita za vyakula ambavyo Mungu alivitoa vipokelewe kwa imani.






Join the conversation