Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Ipi ni Siri ya Tiba ya Maua ya Hibiscus, Michaichai, Ukwaju, Liliki, na hisia zake za Baridi?

Ipi ni Siri ya Tiba ya Maua ya Hibiscus, Michaichai, Ukwaju, Liliki, na hisia zake za Baridi?

Ipi ni Siri ya Tiba ya Maua ya Hibiscus, Michaichai, Ukwaju, Liliki, na hisia zake za Baridi?

Mimea hii yote kuanzia Maua ya Hibiscus ambayo huwa na kiwango kikubwa sana cha ‘’Anthocyanins’’, Michaichai yenye kiwango kikubwa sana cha ‘Luteolin’ ambayo hutengeneza asili ya Ladha yake ya kutuliza, Dania, Mimea jamii yote ya ‘’Mint’’, ambayo ipo mingi sana, na kutokana na kemikali yake ya kupooza inayoitwa ‘’Menthol’’, Mingi huwa kwenye Mafuta mengi sana ya Massage, kupooza Ngozi, mfano; peppermint ambayo huwa kwenye mafuta mengi sana.

Mikwaju ambayo ni Miti ya asili kabisa kwa maeneo ya Afrika mashariki, huwa na rangi ya kahawia ambayo hutokana na kiwango kikubwa sana cha ‘’Anthocyanins na flavonoids’’, Mikwaju huwa na kiwango kikubwa cha asidi ‘’Tartaric acid’’, ambayo hutengeneza asili ya Ladha yake ya ukali, na hisia za kupooza. Mimea hii yenye wekundu wa ‘’anthocyanins’’ kama nilivyoelezea awali huweza kudumu sana kwenye mazingira yenye stress za ardhi, na jua kali, huwa na mkakati wa kushusha kiwango cha Joto na ndiyo msingi wa hisia zake za kupooza.

Watu ambao huumwa kwa shida za kuwa na presha kubwa sana ya damu, presha kubwa ya damu katika viungo husababisha joto kali sana ‘’P∞T’’, Juisi ya Maua ya Hibiscus huwasaidia sana kushusha sana Joto na presha, maana kwa asili ‘’anthocyanins’’ hupooza sensa za mwili ‘’ACE2’’ ambazo huwa mtari wa mbele kuchochea presha ya damu.

Maumivu ya uvimbe wa Tumbo ‘’Gastritis’’, na shida za asidi tumboni ‘’GERD’’, hutulia sana kwa matumizi ya Liliki ‘’Cardamon’’, na hii ni kwa kuwa, huwa ikishusha ‘’neutralize’’ asidi ya tumboni, na kupooza hisia za maumivu ya tumboni. Mimea mingi ya asili ya kupooza, hata ‘’Aloe vera’’ huwa na sifa hii, huwa na tabia ya kutengeneza Uteute mzito, huu hufunika sana tishu zisiletewe shida na asidi, na pia ukiona uteute marazote ujue kiwango kikubwa ni ‘’alkali’’, au kitu kisicho na asidi, maana asidi huwa na tabia ya kuvunjavunja na kutengeneza majimaji kama ilivyo limao.  

Michaichai husaidia sana dhidi ya Kikoozi kikavu, Maumivu ya koo ‘’sore throat’’, hasa yanayoambatana na joto la mwili. Joto kwa asili hukausha sana uteute unaolinda koo, kinywa, na chemba za hewa ‘’sinuses’’. Mimea ya asili ya kupooza, mfano Mchaichai husaidia kwanza kupooza Ubongo, hivyo kuhamasisha mfumo wa mwili wa kupoa unaohusiana na kuzalisha uteute ‘’Parasympathetic nervous system’’, na kitendo chake cha kuwa na chembechembe inayoitwa ‘’Citral’’ husaidia sana kushusha joto katika mfumo wa hewa, linalohusiana na kikohozi kikavu. Shida nyingi za Ngozi, uvimbe mfano ‘’eczema’’, husababishwa sana na kiwango kikubwa cha joto katika damu, na hii inahusiana sana na kiwango kikubwa cha insulin na stress za kimetabolikia. 

Dania ‘’Coriander’’ ambayo huwa na rangi ya ukijani sana unaotokana na kiwango chake kikubwa cha ‘’Chrolophyll’’, husaidia sana kupooza joto la mwili, na metabolikia ya ndani, hata kuwa na ushahidi sana wa kusaidia shida hizi za Ngozi.