Je, Kula sana Mbogamboga kunaongeza sana uhai?
Je, Kula sana Mbogamboga kunaongeza sana uhai?
Hapana, hata bila sayansi, Biblia imeandika watu wanakufa sana kwa kukosa Maarifa, sio mbogamboga na matunda ‘’Hosea 4:6’’. Inashangaza Biblia inasema hata Kuheshimu wazazi ni chanzo cha Baraka za uhai mrefu ‘kutoka 20:12’’.
Kisayansi uhai mrefu unaongezwa kwa kushushwa kwa metabolikia ya mwili, ndiyo maana Kobe anaishi miaka mingi zaidi ardhini, 150. jamii za watu wanaomwamini Mungu huishi maisha marefu sio kwasababu ya vyakula, na ndiyo maana Mungu aliwalisha ‘’Manna na Njiwa’’ wote ila walipishana urefu wa maisha. Wenye Roho wa Mungu huishi zaidi kwa kuwa huwa na Imani, upendo, amani, furaha, ijapokuwa hupitia changamoto ambazo kwa wasioamini huwapa stress, mfano, Paulo alikuwa akiwapa watu moyo akiwa gerezani ‘’Wafilipi 4:12’’. Na hii imethibitishwa sio tu kwa tafiti za wanasailojia, bali hata kwa Centanarians ambao huishi mika 100+, huwa hawazingatii vyakula kama wengi wa watu, lakini wengi huishi maisha rahisi sana yasiyo na tamaa.
Vitu vinavyoshusha metabolikia ya mwili ili kurefusha uhai hasa huwa ni vitu vinavyoutoa mwili katika mazingira ya stress. Na kama daktari vitu vinavyoshusha uhai zaidi kimetabolikia, vyakula huwa ni hatua wenda ya Nne. kwanza ikiwa ni kutokulala kwenye giza kwa wakati unaotosha, hivyo kushindwa kurekebisha mwili, kuzalisha mahitaji ya mwili, na hii huambatana na Kushinda kwenye mianga ya kisasa inayochochea zaidi sumu na stress.
Pili kutokufanya shughuli zinazohusisha asilimia kubwa zaidi ya mwili ‘’50-60%’’, yaani misuli na mifupa, watu hukaa zaidi na kujenga udhaifu kibiolojia na kifizikia. tatu, ni kuongeza kiwango kikubwa sana cha sumu mwilini kutoka kwenye madawa ya hospitali, mifugo, kilimo, maji, vitunza vyakula na rangi za kisasa, bidhaa za kisasa, na stress za mazingira na mifumo ya kisasa. Nne ndiyo hoja ya kutokuwa na maarifa ya kutosha juu ya ulaji kwa afya, na hapa shida sio zaidi aina za vyakula, shida zaidi ni kiasi, maandalizi ya chakula, mida ya ulaji, na changamoto ya kupata vyakula vya asili visivyokobolewa, visivyo na madawa, au visivyo badilishwa kijenetikia.
Kumbuka, kadri unavyoenda kaskazini ndivyo idadi ya Wanyama wakuwala inavyopungua, idadi ya Samaki, mito, na maziwa inavyopungua, ukifika ukanda wa barafu kama Canada ukiwaambia chakula ni ‘’Mbogamboga tu na matunda’’, watakuambia huku huwa hakuna mimea inaota ya kukupa mbogamboga, wala baridi yake kwa kula wanga za mimea huwezi ishi. Na hivyohivyo ndivyo ilivyo kuhusu idadi ya mazao ya kilimo, kadri unavyoshuka kusini ndivyo yanavyozidi kupungua. Mfano, asilimia 70% ya kila kinacholimwa Nchi chini ya sahara sio cha asili yake.
Tazama;
Unaweza gundua kuwa kiwango kikubwa sana cha vyakula ambavyo leo hii watu huisi ni vya muhimu sana, karne mbili tu nyuma wengi wa Babu zetu wasingevifahamu, lakini ajabu ni kuwa, wengi wao walikuwa na afya kuliko kizazi cha sasa. Tafiti kubwa ya Dr Weston Price aliyezunguka Dunia nzima kutazama kila jamii na mtindo wake wa kula, ilihitimisha kuwa jamii zote ambazo ziliacha mfumo wake wa asili wa ulaji, kwa kujaribu kuendana na mtindo wa wazungu, iliishia kuwa na changamoto nyingi sana za kiafya. Na sababu haiwezi letwa na wataalamu wa lishe, kwa katika Uhai lishe ni sehemu ndogo sana.
Blog inayokuja tutaangalia jiografia tu na biofizikia ya mwanga uliopo Afrika unatosha kubadilisha mtazamo wote wa ulaji watu wanaouhangaikia.



Join the conversation