Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Mwanga Ni Chakula Kikuu Afrika

Mwanga Ni Chakula Kikuu Afrika

Mwanga Ni Chakula Kikuu Afrika

Kabla hatujaanza kwa kina ni muhimu kutambua maisha yanatumia nishati ya mwanga wa jua, sote tunakula mwanga. Mimea hutumia maji, mwanga wa jua, na hewa ya kaboni dioksaidi kutengeneza chakula chake cha wanga. Na pia hutunza hii nishati yake kwa kuibadilisha kuumba kemikali zingine kama za protini, au mafuta, na kutawala matendo yake kwa kutumia mabadilishano ya kikemikali yanayohitaji madini, na chembechembe saidizi kama Vitamini. Wanyama hula hii wanga, na kemikali zingine kama protini, yaani wao hupata nishati kutoka katika mwanga, kupitia kemikali vyakula au wanga, protini, na mafuta. Asilimia 97% ya mmea unaouona ni mwanga wa jua ambao umebadilishwa kuwa kemikali kupitia hiki kitendo cha usanisinuru ‘’Photosynthesis’’.

Mwanga hubadilishwa kuunda wanga katika mimea kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Calvin benson cycle’’ kuashiria kuwa, nishati ya mwanga hubadilishwa kuunda kitu ambacho ni wanga, sawa na mlinganyo wa fizikia unaosema ‘’E=mc²’’. Mtu anapokula hiki chakula, ili apate nishati; anahitaji hii nishati ya wanga ibadilishwe tena kuunda nishati ya mwanga, na hii ndiyo sababu wanga huvunjwa katika seli hata kuzalisha chembechembe za umeme zinazoitwa ‘’electrons’’, katika matendo ya ‘’TCA-cycle’’, hizi electrons hubebwa na wabebaji kama ‘’NADH na FADH’’ ambao ni matokeo ya Vitamini B2, na B3, hata kufikishwa katika mtambo wa seli kuzalisha nishati, au mitochondria, ambapo huko hupita katika mithili ya waya za umeme, yaani ‘’madini ya ‘’chuma, na sulfur’’, na protini ‘’Cytochromes’’, na kusukuma chembechembe za chaji chanya ‘’Protons (H⁺)’’ kupita katikati ya ukuta wa mtambo ‘’Mitochondria ‘’IMM’’, ambapo husukuma mithili ya kichwa cha Rotor, inayoitwa ‘’ATPase’’, na kadri inavyokisukuma, basi huunda chembechembe za nishati zinazoitwa ‘’ATP’’. Hii nishati huwa ni mithili ya mwanga unaotunzwa Katikati ya muunganiko wa kemikali ADP, na inorganic Phosphate.  

Mwili hubalansi nishati yake kupitia matendo ya uvunjwaji ‘’Catalysis’’, na hapo ndipo unapata nishati kama hii ya ATP, au kupitia matendo ya uundwaji ‘’Biosynthesis’’, na hapo ndipo unapata nishati kama ya NADPH na Glutathione. Nishati katika mwili ni balansi ya uundwaji na uvunjaji, yaani ‘’Redox balance’’. Mwili unapataje nguvu na kujiongoza kiuhai? Kemikali hizi zinapovunjwa au kuundwa huzalisha mawimbi madogo sana ya mionzi yanayoitwa ‘’UPEs’’, haya ndiyo hufungua mifumo ya homoni, hufanya metabolikia zifanye kazi. Haya mawimbi huwa na vipimo tofautitofauti, na yanapokuwa ya kiwango maalumu tu kwa kazi fulani, ndipo husisimua hiyo kazi. 

Mwili huratibu matendo yake kupitia uhusiano wa haya mawimbi. Namna kemikali za mwili huitikia kwa kusisimuliwa na mawimbi haya kuwa ON au OFF, huu mfumo kwa urahisi sana huitwa ‘’Quantum Coherence’’. Chembechembe mwilini marazote hufyonza mwanga ‘’absorption’’ au kuutoa ‘’emission’’ kwa mawimbi maalumu tu, na hii huwa kwa kemikali kama homoni ‘’leptin, dopamine, tryptophan, tyrosine, porphyrins, hemoglobin, melanin, n.k.’’ 

Uhai kimetabolikia ni kama mitambo inayoongozwa na mawasiliano kupitia mawimbi haya madogo ‘’UPEs’’, kama ambavyo ijapokuwa sote tunatumia mawimbi kuwasiliana na simu, lakini hayaingiliani kwa kuwa ni madogo sana, na yana utofauti, hivyo mawimbi ya simu yangu kuelekea kwa Mama yangu, hayatakamwe sisimua ‘’receiver’’ ya simu ya askari magereza. hivi ndivyo mawimbi maalumu tu husisimua metabolikia au fiziolojia Fulani tu, na kwa wakati Fulani tu. 

Waafrika Wanaishi Miaka Mingi Kwa Kula Mwanga

Mwili hufyonza mwanga wa jua kupitia ‘melanin’’ zilizopo kuanzia kwenye Ngozi, mpaka ukuta wa ‘’Mitochondria’’ kusisimua uzalishaji wa nishati. Mwanga wa jua ndiyo hufanya maji yaliyo ndani ya chembechembe za nishati ‘’mitochondria’’ kujichaji, kutengeneza mithili ya battery ‘’EZ’’, kama ilivyogunduliwa na Mwanabiolojia Gerald Pollack, hii chaji huruhusu mwili kuzalisha nishati bila hata kula. Kumbuka tulishaona ni electrons zinazoupa mwili nguvu, ambazo Dunia inazaidi ya chaji 6 Sextillion (6 ifuatiwe na sifuri 21). kwa kutembea pekupeku mtu huzipata hizi chaji, na kumsaidia kupata nishati ukiachana kabisa na chakula. Mwili huzalisha mwanga wenyewe wakati wa usiku, kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Photobiolectric’’, kama ilivyoelezwa na Mpasuaji wa Ubongo na Mwanabiofizikia Jack Kruse. 

Mwili huwasiliana na mfumo mdogo wa umeme wa dunia ‘’electric field’’, kutawala matendo mengi sana ya ndani ya mwili wakati wa siku au mchana, na hutumia sana mfumo wa usumaku ‘’geomagentic field’’, wakati wa usiku jua linapokuwa limetulia.