SIRI NYUMA YA MISULI & UHAI
NONDO YA 3
Shughuli za misuli husapotiana na Biolojia nzima ya Mwanga Kwa Wakati wa asubuhi, Mchana, mpaka jioni. Asubuhi siku hukucha ikichochea zaidi mfumo wa stress kikazi "ACTH' ktk Ubongo, kitu ambacho huonyesha Biolojia huchochea stress ili uamke ukatafute Chakula. Na hii Ndiyo sababu wanyama wengi karibia wote huamka jua linapokucha tu. Kiwango Cha homoni ya "Cortisol' huvunjavunja sukari na hata protini katika misuli asubuhi ili kukupa nishati ya kwenda kuwinda au kutafuta Chakula. Ndani kabisa kibiolojia nimeeleza sana katika Vitabu vyangu kuwa, "Mwanga wa asubuhi wenye mionzi ya 'IRA na Red light" Kwa kupenya 10-30cm chini ya Ngozi hata kufikia ukuta wa ndani wa Mitochondria wenye "melanin, na VDR', huchochea kuzalishwa kwa kemikali "Nitric oxides" ambazo hufungua zaidi mishipa ya damu, lakini pia mionzi hii husisimua "Complex ya IV-CCO' ktk chembechembe za nishati "mitochondria', jambo ambalo humpatia mtu nishati hata kabla ya kula. Wengi wetu tuliosoma na kuishi vijijini tulikuwa tukienda shule au shamba asubuhi bila kula na Wala hatukuwa tukihisi njaa, sababu kuu ni hii.
Asili iliwafanya viumbe wote kuwa wafanya kazi za misuli hasa kuanzia Wakati wa asubuhi. Asili huchochea stress mwilini kama msukumo wa kumfanya kiumbe akafanye kazi ya kutafuta Chakula. Viumbe wote huamka si Kwa kutaka, ila kutokana na mfumo wa stress ambao huwa ishara ya kuwa unapaswa kwenda kufanya kazi ya kutafuta Chakula. Kiwango Cha lactate asubuhi ndicho huifanya misuli iwe kama ikiwaka moto, ajabu zaidi lactate imeonekana kuwa na manufaa sana katika afya ya Ubongo Kwa kuchochea kuzalishwa kwa kemikali "BDNF', zinazochochea Ubongo kuzalisha homoni nzuri zote kuanzia "dopamine, serotonin, n.k.', ukiachana tu na taswira mbaya ya kuonekana inachochea kukaza Kwa misuli pale mtu anapolala. kumbuka unapolala unavuta Oksijeni kidogo ndiyo maana unaizalisha hii kupitia "anaerobic glycolysis" kama namna ya kupata nishati bila kula Kwa kuvunjavunja wanga ya mwilini. Kiufupi lactate hulenga kumfanya mtu aamke atembee.
Asili inatambua kazi ya kutafuta Chakula huwa Sio kazi ya kukaa, huwa ni kazi ya kushurutisha misuli, na hii ni Kwa kuwa, Misuli pamoja na mifupa ndiyo huchukua asilimia kubwa zaidi ya mwili. Swali jepesi tu la kujiuliza la Kwanini una misuli mikubwa sana kuliko hata Ubongo", linaweza kukueleza kuwa asili inajua unapaswa kuitumia sana misuli kuliko hata Ubongo katika kazi. Asili huchagua saizi ya viungo kulingana na matumizi yake, na hii Ndiyo sababu via vya uzazi huwa ni vidogo sana Kwa kuwa viumbe hawakuumbwa kuwaza sana uzazi au sex. Watu wanavunja hii Sheria Kwa kutotumia sana misuli yao mikubwa Kwa kufanya kazi zinazotumia zaidi viungo vidogo, mfano; kazi za kuzungumza, kazi za kuandika, kazi za kufuatilia taarifa za kidijitali, kazi za kuendesha mitambo, n.k.
Kwa miaka zaidi ya elfu asili inatambua Binadamu huamka na kwenda kuwinda au kukusanya. Kwa miaka zaidi ya elfu asili imewatengeneza viumbe kula tu wanapohisi njaa, na Kwa viumbe Wala nyasi au Wanga zaidi, "Mimea mingi inayoliwa na wanyama kama Nyumbu, Farasi, sokwe, au Ng'ombe, ni Wanga asilimia kubwa zaidi, hata asilimia 90% mara nyingi". Wanyama hawa hula sana kuanzia asubuhi Kwa kuwa Wanyama huitaji rangi na harufu ili kujua majani yapi ni ya kuliwa na yapi ni Sumu. Jua huwawezesha kuona na kuhisi harufu maana mimea Mingi huitaji Joto na mwanga kutoa harufu. Wanyama Wala Nyama kama Simba, hata Walanyama na Mimea kama "Binadamu', hula sana kuanzia Mchana mpaka jioni pale wanapohisi njaa za kuwatoa nje ya mapango na kuwafanya wakaanze kuwinda.
Tofauti ya Binadamu na Simba ni kuwa; Binadamu Hana manyoya na hivyo anaweza kuwinda zaidi Mchana, huku jioni na asubuhi akiweza kula tu Mizizi na matunda madogo kidogo. Simba ana manyoya hawezi kudumu sana katika jua Kali Mchana, lakini ana macho yenye seli za kuona Gizani zaidi "Rods', hii inamuwezesha kuona na kuwinda vizuri zaidi jioni hata Usiku.
Wanyama wote hata sokwe wanaotumia masaa 6-10 kula tu, hula tu pale wanapokuwa na njaa ijapokuwa wengi hawajui. Wanyama hawa huonekana wakila lakini uhalisia huwa tu wakikusanya Chakula Kwa kukiweka tumbo la kwanza "rumen', au utumbo mkubwa "colon', ambayo huwa hata hayavunji virutubisho vya kuupa mwili nishati pale tu wanapokula. Wanyama hawa nyakati za Mchana mpaka jioni ambapo hutulia na kuanza kucheua ndipo huanza kiuhalisia kula. Na hivyo hii ni sawa na kusema, simba huwa Hali asubuhi mpaka atakapowinda na kupata Chakula. Farasi na Ng'ombe huwa Hawali asubuhi, huwa wanakusanya majani wakitembea "wakifanya kazi", na hatimaye huja kula baadae baada ya kazi.
Katika sehemu hii ni muhimu kutambua kuwa Misuli huitaji kushiriki katika zoezi Zima la utafutwaji wa Chakula hata kama Sio Kila siku. Hata wanyama kama Simba huwa hawawindi Kila siku. Wazee wa zamani hawakuwa wakiwinda nao Kila siku. Lakini stress za kuwinda huja baada tu ya njaa, na hii Ndiyo sababu Vyakula Hushusha stress. Hii ni sawa na kusema, watu hukabiliana na stress za kazi Kwa kuwa hutambua yapo malipo baada ya kazi. Malipo kabla ya kazi huaribu mfumo mzima wa motisha ya kazi, na hivi ndivyo imekuwa katika zama za usasa ambazo watu hula asubuhi kabla ya kazi, au hula Kwa kutofanya kazi za kuwashurutisha misuli yao.
Kibiolojia Usiku huwa ni muda wa uundwaji wa tishu "anabolism", na hii Ndiyo sababu husemwa "Lala ukue". Wakati wa Mchana huwa ni Wakati wa uvunjwaji wa tishu "Catabolism', na hii Ndiyo sababu Shughuli za misuli huvunjavunja mafuta. Kwa kadri watu Wanavyoshiriki katika shughuli za misuli hupelekea misuli kutumika sana, kutengeneza michubuko, na hii hupelekea Wakati wa Usiku watu Hawa wanapolala mwili kurekebisha misuli yao na kuifanya kuwa imara zaidi, na kuwa na nishati zaidi. Watu wanapofanya shughuli za misuli baada ya Kula huwa hawanufaiki sana Kwa kuwa mwili hutumia tu Chakula walichotoka kula, katika mfumo wa "glycogen'. Watu wanapofanya shughuli za misuli kabla ya kula asubuhi miili yao husukumwa kutumia mafuta ya mwilini "fats' jambo ambalo huwa-Fanya kuwa Bora zaidi. Ajabu zaidi ni kuwa, ufanyaji kazi kabla ya kula Huchochea zaidi uzalishaji wa homoni ya ukuaji "GH', ni sawa na kusema, mwili husema unahitaji kuwa imara na mkubwa zaidi.
*******---------**********----------**********---------**


Join the conversation