HISTORIA NA KIINI CHA MAGONJWA YOTE
SURA YA SABA
MAGONJWA YA MADAWA
Historia ya matibabu
Heshima na shukurani kubwa sana huwa
zikienda kwa mtaalamu, Edward Jenner. Kwa kuokoa mamilioni ya Maisha ya watu.
Kwa kugundua Chanjo ya kwanza kabisa ‘’vaccine’’. Neno vaccine likitokana na
neno ‘’Vacca’’, linalomaanisha Ng’ombe. Hata kabla taaluma ya chanjo,
ilishakuwepo katika falme za china, india, na Ottoman. Hawa waligundua unaweza
jikinga na virusi vya smallpox kwa kugusana, au kukutana na mabaki ya vitu
vilivyoambukizwa na virusi hivyo vya smallpox. Taaluma hii ililetwa maeneo ya
Uingereza, Ulaya. Miaka ya 1800’s na Mwanamama Maria Wortley Montagu.
Mwaka 1796 Edwerd Jenner Daktari
mwingereza, aligundua wakamuaji wa maziwa ambao walikuwa wakipata homa ya mafua
ya Ng’ombe ‘’cowpox’’, walikuwa hawawezi kupata ugonjwa wa virusi vya smallpox.
Na mwaka huohuo akamwekea mtoto mdogo wa miaka 8 aliyeitwa ‘’James Phipps’’
vitu vyenye vimelea vya mafua ya ng’ombe ‘’cowpox’’,mtoto alionesha dalili za
kuumwa, lakini baadaye kidogo alipona. Baadaye Daktari Edwerd akamwekea virusi
vya smallpox, na Mtoto kweli hakuumwa kabisa. Na hapo ndipo akaipa jina hii
mbinu Chanjo, au ‘’Vaccination’’.
Kilichofanyika mwaka 1828 na bwana Johann
Buchner kuitoa kemikali ya ‘’salicin’’, toka mti unaoitwa ‘’Willow’’, au Mkemia
‘’Felix Hoffmann’’ mwaka 1897, yeye aliitoa kabisa chembechembe
‘’Acetylsalicyclic acid’’ (ASA), toka kwenye mti huuhuu. Ndicho kilichokuwa
kikifanywa kwa milenia nyingi sana na waganga wengi sana, kuanzia misri,
sumeritan, mpaka na Hippocrates. Hawa wote walitambua kuwa magamba ya huu mti
yana uwezo wa kuondoa maumivu, homa, na uvimbe. Hivyo mwaka 1897 kilichofanyika
tu, ni kuchukua kiini chake cha ASA, na kukiuza kama Aspirin.
Mti wa aspirin
Miaka ya 1800’s, walifanya ugunduzi
mwingi sana wa kuchukua viini vya dawa ambazo zilikuwa zikitumika kwa miaka
mingi sana. Mojawapo pia, ni Maua ya Poppies. Ambayo yalitumika sana kutulizia
maumivu kwa miaka mingi sana. Tena miaka milenia nyingi tangia zamani. Waganga
wazamani walichanganya tangawizi, na maua kadha wa kadha kama ya chamomile,
kupunguza shida za uvimbe, na nyingine mbalimbali.
Friedrich serturner alichukua maua ya
poppies, na kuchukua kiini chake ambacho ndicho huitwa ‘’opium’’, miaka 28
mbele, mwaka 1832, mwenzake Pierre Robiquet wa ufaransa, akagundua na Codeine.
Hizi zote ni dawa zinazotumika mpaka leo mahospitalini kupunguza maumivu. Karne
hii hii wakagundua mpaka na Paracetamol. Dawa za kutuliza maumivu zilizochelewa
kugunduliwa ni za steroids tu, ‘’Cortisone’’. Ambazo ziligunduliwa miaka ya
1949. Kumbuka miaka ya 1800 ndiyo iliyokuwa na mapinduzi makubwa sana ya
sayansi, na teknolojia, hivyo wazungu wengi wa maeneo ya ulaya walitumia faida
ya masomo, na taaluma nyingi sana ambazo zilikwisha sambaa ulaya yote.
Ikihusiana na za afya, hasa toka kwa waislamu wengi wa zamani, ambao nao
walizikusanya sana toka miji ya neo-medopersians, ambayo ilijumuisha taaluma
zote toka kwa maeneo yote ambayo yalikwisha ambukizwa elimu za kigiriki,
zilizohusisha elimu za afya. waislamu wanakumbukwa kwa kuandika awali kabisa
machapisho makubwa, na kuyakusanya kwenye maktaba zao za awali kabisa kama za
Baghdad, na kuzisambaza baadae ulaya yote enzi za kukua kwa dola yao.
Kushoto ni Poppies wenye ‘’opium’’, na
kulia ni chamomile.
.........,...............(nunua kitabu kupata picha kamili)...................
Mwaka 1895 mpaka mwaka 1930 ndiyo miaka
ambayo ilihusika na ugunduzi wa mionzi katika tasnia ya udaktari. Wilhelm
conrad Rontgen, mwanafizikia wa kijerumani, ndiye hupewa heshima kwa ugunduzi
wa mionzi ya X-Rays, miaka ya 1895. Na ugunduzi wake ulichochea tasnia ya
matibabu, mwaka 1900, ikaibuka namna yake nyingine inayoitwa ‘’Fluoroscopy’’, ambapo
bado mionzi ya x-rays ilichochea maendeleo zaidi, na mwaka 1970’s ikagundulika
CT-Scan, ambayo ni namna ya kisasa zaidi ya kupata taswira ya 3D ya viungo.
Miaka 1950’s iligundulika Ultrasound, ambayo hutumika kutazama taswira za
viungo hasa vya tumboni.
Miaka kumi nyuma yake iligundulika namna
ya kutazama miili kwa kutumia chembechembe za Nyuklia, au ‘’Nuclear medicine’’.
Miaka ya 1980’s ikagundulika MRI mtambo
ulioniwezesha hata mimi kuweza kuuelewa sana Ubongo, katika masomo ya
fiziolojia ya ubongo kwa kutazama maumbile yake ‘’neuroanatomy’’. Japokuwa tuzo
hakupatiwa mgunduzi wa kweli, Daktari, na engineer, Damadian Raymond, na sababu
iliyojificha ni kwasababu ni ‘’Mkristo wa dhati sana’’.jambo ambalo linaonekana
kwa wengine kama, linaitia doa sayansi.
Mwaka 1928 umeandikwa katika historia ya
ulimwengu kwa kazi kubwa sana ya mwanabiolojia ‘’Alexander fleming’’, kwa
ugunduzi wake wa dawa ya kwanza kabisa ya kuua bakteria ‘’Penicillin’’, au
‘’first antibiotic’’. Lakini hata hivyo miaka 1500 kabla hata ya Yesu, tayari
ilisharekodiwa kuwa Wamisri walishakuwa wakitumia mikate iliyochacha na asali
kutibu vidonda. Bado walitumia mimea mingi na mabaki, kama yenye vitunguu
saumu, n.k. fleming aligundua fangasi ‘’penicillium notatum’’ aliua bakteria
‘’Staphylococcus notatum’’, na akarekodi ripoti yake mwaka 1929. Lakini kina
Florey na wenzake ndiyo waliochochea uzalishaji wa chembechembe za
‘’penicillin’’ hasa kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia, miaka ya 1940’s. baada
ya hapo miaka ya kuanzia 1940-50, ilishamiri kwa utafiti wa dawa zaidi,
waligundua streptomycin, tetracycline, erythromycin, na chloramphenicol.
Miaka mingi sana kabla ya Yesu, Misri
walikuwa wakitibu saratani, au Cancer, kwa kuichoma ‘’cauterization’’. Hata
Hippocrates, miaka 400 kabla ya Yesu, naye aliripoti namna hii. namna bora
zaidi na ya kwanza ya matibabu ya saratani, ilikuwa kupitia upasuaji
‘’surgery’’ kuiondoa. Jambo ambalo liliwezekana kwa kuwa, miaka ya 1846,
walishagundua dawa za kwanza kabisa za nusu kaputi, ambazo tulishaziona, kama
‘’opiates’’, miaka ya 1860’s, pia waligundua namna bora kabisa za kusafisha
vifaa, na vidonda, ‘’antiseptic techniques’’, visishambuliwe na vimelea. Hivyo
ikawezekana kwa urahisi sana hata kwa wataalamu wa upasuaji wa kwanza kabisa
kama ‘’Willium Halsted’’, kuondoa saratani ya Titi kwa mafanikio. Miaka ya 1895
ilipozaliwa mionzi kama tulivyokwisha ona, ikawezekana zaidi kuua saratani.
Miaka ya 1940’s walianza matibabu ya
saratani kwa njia ya homoni kutokana na taaluma ya matibabu ilishakuwa kubwa
sana. Miaka ya 2000 wakaanza kutumia matibabu yaliyolenga zaidi seli za
saratani moja kwa moja. Na mpaka 2010’s wakawa wakitumia mbinu za kuusaidia
mfumo wa kinga moja kwa moja kuua seli
za saratani ‘’immunotherapy’’. Pia zipo mbinu za kijenetikia ‘’gene therapy’’,
zinazolenga kuua moja kwa moja jenetikia za saratani ‘’genes of neoplasms’’.
Kuanzia miaka ya 1980’s mpaka leo unaweza
kusema matibabu yamebadilika na kuwa ya kisasa zaidi. Yakihusisha taaluma pana
sana za kijenetikia, zinazowezeshwa sana na teknolojia za akili za kisasa
‘’artificial intelligence’’. Katika Q4 nimeelezea teknolojia kama za CRISPR Cas
9 Technology, namna zinavyoweza kumuathiri mtu. Watu wengi hawajui matibabu
toka historia mpaka sasa, yanaonesha kabisa kufika kikomo. Lakini cha ajabu
magonjwa ndiyo kama yanaanza.
MSINGI WA SAYANSI ZA MADAWA YOTE
Madawa yote yanayotumika duniani, huwa na
sheria, na sababu zake kuu. Matumizi ya madawa yalianza kutumika awali kabisa
katika historia ya mwanadamu. Kilichokuwa kikibadilika, ni urahisishaji wa
namna ya kuitumia dawa, kwa kuiboresha zaidi kadri teknolojia inavyozidi
kuongezeka.
Asilimia kubwa kabisa ya madawa, tangia
awali kabisa. Ni kemikali zinazotoka kwa mimea, na viumbe wengine. Jamii
mbalimbali zimekuwa kwa milenia nyingi, zikitumia sana mimea yake kadhaa,
kwasababu za kimatibabu. Kabla ya wakoloni kufika maeneo mengi ya Afrika,
tayari watu walikuwa na namna zao za kitabibu. Ambazo ndizo zilizowafanya
wakaweza kuishi kwa maelfu ya miaka katika bara lao. Na ndivyo ilivyo hivyo
hivyo kwa kila eneo.
Magonjwa
Msingi wa dawa yoyote ile, ni kuweza
kuchangamana na chembechembe zingine, au sehemu zingine za mwili, kama Funguo
inavyoweza kufungua Kufuri. Hii kitaalamu inaitwa ‘’Key and Lock mechanism’’.
Dawa ni chembechembe ambazo zinaweza Kwenda aidha kwa tishu za mwili wa
mgonjwa, au tishu za kimelea, au sumu yenye madhara, na kisha kuibadilisha
utendaji wake ili isilete madhara, au kuuongezea mwili uwezo wa kujikinga.
Magonjwa marazote huusisha athari katika
mfumo wa fiziolojia ya mwili. Mfano, magonjwa yanaweza kupelekea mwili
kusisimka zaidi ya kawaida, wenda kutokana na sumu kadhaa za vimelea, au kitu
chochote kile. Na mwili unaweza kusisimka kwa kuongeza sana Joto lake kupita
joto la wastani linalohitajika, na hivyo kujikuta ukiathirika kabisa hata ukiua
protini zake wenyewe. Magonjwa yanaweza kupelekea kuharibika kwa mtiririko wa
utendaji sahihi wa fiziolojia ya mwili, na kupelekea baadhi ya homoni
zisizalishwe. Homoni ambazo zingesaidia kuongoza hisia za hamu ya kula, msukumo
wa presha ya damu, n.k.
Magonjwa huusisha vimelea ambavyo huwa
vikizaliana sana katika mishipa ya damu, vimelea kama ‘’plasmodium’’ huwa
wakila damu moja kwa moja, huivunja ‘’hemoglobin’’, kuna vimelea ambao huwa
wakishambulia kuta za Mishipa ya damu, maini, tishu za ubongo, kuta za utumbo,
mpaka katika misuli. Hawa wote husababisha madhara kwa kuzaliana katika tishu
hizi, na kuathiri utendaji wa hizi tishu. Kwa kuzalisha uchafu wao, kuzalisha
sumu zao, kuzuia damu katika hizi tishu, vimelea wengine kama virusi huathiri
mpaka DNA za seli za wagonjwa, kwa Kwenda kuzaliana moja kwa moja katika
nyuklia za seli.
Kuna magonjwa ya sumu ambayo huusisha
madhara katika matendo ya metaboliki ya mwili moja kwa moja. Mfano, sumu baadhi
hung’ang’ania chembechembe za mwili, au huzuia au kufungua chaneli baadhi za
matendo ya kibiolojia, hata kuathiri mwili. Zipo sumu baadhi ambazo huchochea
sana utendaji wa mifumo ya seli kuliko kawaida. Lakini zipo ambazo hupooza
kupita kawaida. Matendo haya katika mishipa ya fahamu huweza kupelekea kiumbe
kuparalaizi ‘’paralyze’’, kukakamaa ‘’tetany’’. kuna zingine huzuia damu
kuganda. kuna ambazo hupoteza balansi ya madini na chembechembe kama
‘’enzymes’’, na kupelekea madhara ya mifumo mbalimbali yasiyotabirika. Na kuna
sumu na vimelea ambao huathiri sana mifumo ya kinga, na kupeleka madhara kutoka
kwa vimelea ambao hawakuwa hatari mwanzoni.
Mwili huwa na uhusiano wa hisabati ya
jumla ya matendo yote unayoyatenda. Hii huitwa ‘’coordination’’. Kitendo cha
matendo, au seli baadhi kuathiriwa na vimelea, au sumu. huwa hakiwezi kuleta
madhara moja kwa moja. Hii ni kwa kuwa mwili huwa una namna ya kubalansi
changamoto za maeneo baadhi, kwa kuyafidia. Lakini inapofikia hatua ambayo
changamoto zimekuwa nyingi kiasi kwamba madhara ya seli, au matendo kadhaa,
hayawezi kubalansiwa ‘’compensated’’, basi matendo yale huanza kuonesha udhaifu
moja kwa moja kwa nje. Mfano, kama mfumo wa damu umeathiriwa sana, basi mnyama
ataanza kuonyesha upungufu wa damu ‘’anemia’’, kama ni mfumo wa nishati, basi
utaona ‘’mnyama hana nguvu, au kakonda’’, kama ni kuongezeka kwa asidi au
‘’respiratory or metabolic acidosis’’, basi utaona mnyama akiwa na mapigo ya
juu sana ya moyo, akitapika, n.k. kama ni upungufu wa madini ya ‘’Calcium’’,
basi mnyama atachanganyikiwa, misuli itaisha nguvu, n.k.
Mara zote ugonjwa unaoonekana kwa nje, ni
matokeo ya upungufu wa mifumo ya mwili ambayo ilipasa kufanya matendo Fulani.
na yanapofeli, basi yanapelekea udhaifu.
Yapo magonjwa pia ambayo hayatokani na
vimelea, wala sumu. Bali hutokana na mwili wenyewe. Haya huwa ni matatizo ya
kuzaliwa, kama ulemavu. Na mengi huwa na changamoto zinazohusiana na mifumo ya
kijenetikia. Magonjwa ya muundo huu wakati kadhaa pia huchochewa sana na
matokeo ya sumu, ambazo awali ziliathiri utendaji wa biolojia ya uumbaji wa
mtoto alipokuwa tumboni ‘’embryology’. Wakati mwingine huwa ni mionzi, lishe
mbaya, n.k. mfano mzuri ni matokeo ya mionzi ya madini mazito ‘’heavy metals
radiation’’, huwa na madhara sana katika seli kadhaa, kuliko zingine.
Na hii huwa hivi, ndani ya seli kuna
chembechembe zinazoitwa ‘’DNA’’, hizi chembechembe ni ndogondogo sana, na
zinahusisha madini madogo madogo sana. Haya madini ni rahisi sana kusisimuliwa
na kiwango cha nishati kama za mionzi. Hivyo mama mwenyeujauzito anapokuwa
katika maeneo haya. kwa kuwa mtoto wake anaundwa tumboni. na seli zinafanya
kazi ‘’Mitosis’’, (seli zinaji ‘’double’’, mara 36 ili kumuunda mtoto kutoka
kwenye sperm na ovary tumboni, wakati huji double mara tano tu akishazaliwa).
Tumboni huwa ni kwa spidi kubwa sana. hivyo DNA zinakuwa zikiwa kazini sana
‘’more active’’. kwa kuwa karibu na mionzi, basi mionzi huenda kwenye zile DNA
za mtoto, na kuzisisimua chembechembe zake, na kupoteza mtiririko wa utendaji
wake. Na madhara yake ni kuzaliwa kwa mtoto mwenye makosa katika uundwaji wa
baadhi ya viungo vyake, hizi huitwa ‘’malformations’’, au ‘’teratogenic
effects’’. Kuna nyakati husababishwa pia na sumu, ambazo nazo huenda kuathiri
hatua zilezile za kijenetikia.
Magonjwa baadhi huleta madhara kutokana
na msisimko mkubwa zaidi wa mwili, kuliko hata uhalisia wa vimelea, au sumu.
Mfano mzuri ni asthma. Mwili husisimka na kuminya mishipa yake, aidha ya hewa,
kama asthma, au ya damu. Na matokeo yake mwili huongeza spidi kubwa sana ya
damu, hata kupelekea presha, ‘’Hypertension’’, wakati mwingine mirija ya mapafu
‘’bronchioles’’, huweza kujiminya ‘’constrict’’, hata kushindwa kuvuta hewa, na
mtu kuathirika kwa kupungukiwa oksijeni. Wakati mwingine mwili husisimka na
kupelekea Ngozi kusisimka kwa kiwango kikubwa sana kwa uvimbe. Mwili hupelekea
uvimbe ‘’inflammation’’, kama namna ya kujilinda na vimelea, au hatari. Na
kumbe unajiathiri wenyewe.
Kuna uhusiano wa moja kwa moja, wa
magonjwa na utambuzi, au akili ya mtu. Saikolojia ni hali ya juu ya
kifiziolojia, ijapokuwa watu bado hawaielewi saikolojia kiundani, maana wengi
wanaosoma saikolojia, huwa hawaijui fiziolojia. Akili ni sehemu ya kwanza ya
kinga ya mwili, kwa kukuonesha kile ni hatari kinaweza kukuathiri. Na ndiyo
sehemu ya mwisho ya kinga ya mwili, kwa kukuambia utapona tu wala usijali.
Wataalamu hutambua, hisia za kuamini kupona, huwafanya watu hata wasiotumia
dawa sahihi, kupona. Hii huitwa ‘’Placebo effect’’. Husomwa katika matawi ya
sayansi yanayoitwa ‘’Psychoneuroimmunology’’. Hoja ni kuwa, watu huonesha hisia
wanapoumwa, kuelezea kiwango cha ugonjwa wao ulipofikia, bila wao kujitambua.
ASILI YA MADAWA
wengi sana hushangaa maajabu ya madawa.
Lakini kibaya zaidi ni kuwa, wameshindwa kunufaika nazo. Dawa nyingi sana
tunazozitumia, zimetokana na mimea. Ipo mimea ya madawa ambayo ina dawa katika
magamba yake, hasa miti. Kuna maua. Kuna mizizi. kuna poda na majivu.
Kwanini mimea baadhi ina madawa?
Kwanini mti wa pillow unatuwezesha kwa
dawa ya ‘’aspirin’’, au maua ‘’poppies’’ ya ‘’opium’’, yanatuwezesha kupata
dawa za nusu kaputi ‘’anaesthesia’’ au kutuliza maumivu, mimea kama ya vitunguu
saumu ‘’garlic acids’’ inaua bakteria, mbegu za maboga zinaua minyoo
‘’anti-helmintics’’, matunda ya Kigalia Africana yanazuia tishu kuharibika
‘’antioxidative’’ na kuua vimelea kama bakteria’’, aloe vera inasaidia
kupambana na virusi, vimelea, inazuia tishu kukakamaa ‘’antioxidative effects’’.
muarobaini, mti wa Quinine, vitunguu saumu, mdalasini, majani ya mpera, n.k.
Sababu pekee ambayo inafahamika ni kuwa,
vita ambayo marazote amekuwa akiipigana binadamu, amekuwa akipambana Pamoja na
mimea. Mimea inapitia changamoto marazote mwanadamu anapopitia changamoto.
mfumo wa kwanza wa kinga ambao ndiyo akili ya viumbe. Huwa na namna pana zaidi
ya kujikinga, na hapo ndipo inapohusiana na kila kiumbe ambacho kipo nae
sambamba katika kujiokoa.
Mimea kama Pillow ambayo inaota sana
maeneo ya baridi, ‘’temperate areas’’, kama ukanda wa ‘’mediterranean’’, huwa
inaota sana kando na vyanzo vya maji. Ambapo huwa kuna maji, na madini mengi
toka katika ardhi. Lakini kando ya vyanzo vya maji huwa na wadudu, na vimelea
wengi sana. Kama bakteria, minyoo wadogo, protista, virusi, na fangasi. Hawa
vimelea japo si wote, lakini huwa wanaathiri sana mimea iliyopo karibu. Na
mimea mingi sana hufa. Lakini mimea ambayo huwa kando ya vyanzo vya maji huwa
na sifa nyingi sana za kitabibu. Hii ni kwa kuwa, hutengenza chembechembe za
kinga ‘’bioactive molecules’’. ambazo hujua kuwa kama vimelea wataishambulia
hii mimea, basi itawaua. Na kwa namna hiyo mimea itabaki salama.
Na mimea mingi iliyopo katika maeneo
mbali na kingo za maji, hushindwa kutengeneza hizi kemikali. Hii ni kwa kuwa,
huwa na virutubisho na maji machache, ya kuweza kuwa na nishati ya kuweza
kutengeneza mpaka na chembechembe za kujilinda. Na mimea hii inapotengeneza
chembechembe hizi, basi kiumbe yeyote atakayetumia, naye anaweza kufaidishwa na
utabibu wake. Hivi ndivyo ilivyo pia kwa maua kama ya ‘’poppies’’, nayo
huzalisha chembechembe za ‘’opium’’, kwa lengo la kuwazubaza Wanyama
watakaotaka kuimaliza yote, kwa kuila. Na kwa kufanya hivyo, mimea itabaki
salama.
Misitu ya Congo
Hii misitu ina asilimia 50-70% ya aina
zote za mimea iliyopo katika dunia nzima. Na ndiyo misitu ambayo ina aina
mbalimbali zaidi za mimea yenye nguvu za kiutabibu ‘’therapeutic properties’’.
Mimea mingi katika misitu hii huwa na misimu mirefu sana ya mvua, na huwa pia
na viwango vikubwa sana vya viumbe mbalimbali, na hata vimelea mbalimbali vinavyoizunguka.
Mimea hutengeneza kemikali zake za kujilinda dhidi ya kila namna ya uuaji
unaouelekea. Dawa kama za Quinine zimetokana na miti ya misitu hii ‘’miti ya Cinchona’’,
dawa za Curare ‘’zinazolegeza misuli’’, hutoka katika misitu hii, dawa za
‘’Reserpine’’ hizi hutibu shida ya presha kubwa ‘’hypertension’’, nazo hutoka
katika mimea ya hii misitu. Zipo dawa nyingi sana.
Jangwani, Ukame, na milimani
Mimea ya maeneo ya jangwani, na hata
milimani pia huwa na sifa kadhaa za utabibu. Hii ni kwa kuwa, mimea hii huwa
katika maeneo ambayo huwa na hali zisizo tabirika za hali za hewa, huwa
zinapambana na vipindi virefu sana vya ukame. Na mimea huzalisha aina
mbalimbali za kemikali, za kuisaidia kupambana na hizi hali. Maeneo ya milimani
pia huwa na oksijeni chache, na stress huwa ni kubwa sana. Hivyo mimea huunda
kemikali za kupingana na hizi hali.
Mfano, Aloe vera ambayo husaidia sana
kupona kwa vidonda, na afya ya Ngozi Imejaa ‘’antioxidant’. kama ambavyo
mazingira yake huuhitaji kuwa na sifa ya ‘’anti-oxidation’’. kuna mti wa Yew,
huu huwa na sifa ya kupambana na seli za saratani ‘’cancer cells’’, ambapo ili
uziathiri hizi seli, unabidi kuzizuia zisiwe na hali za asidi, na ziwe na hali
za oksijen, jambo ambalo mimea hii hufanikiwa. Kuna mimea ya ‘’Ephedra’’, hii hutanua
njia za mapafu ‘’bronchodilators’’, nayo hutoka katika hali hizi.
SIRI YA TEKNOLOJIA ZOTE ZA MADAWA NA
MADAWA YA KISASA
Kila dawa inayotumika popote pale, kama
sio vitamini, au madini, au chembechembe zozote zile za vyakula kama sukari, au
protini, au mafuta, au homoni, Basi ni Sumu. Dawa zote ni sumu ambazo zinaua
seli za viumbe. Na teknolojia kubwa kabisa ya utabibu wa sasa, imejikita katika
kutafuta namna za ndani kabisa za kuua vimelea, kwa kuwasoma namna ambavyo wao
kwa wao wanauana. Mpaka sasa hivi teknolojia ya CRISPR-Cas 9 ambayo ndiyo ya
kisasa zaidi katika utabibu, inahusisha kuiga namna Virusi wanavyowaua bakteria,
na kuiga namna hiyo kama itawezekana kuua seli za Cancer, kwa binadamu.
Mara zote dawa ni sumu lakini hutumika
kwa sababu kadhaa. Kwanza, ni
Binadamu ni mabilioni ya seli, lakini
vimelea wengi wana seli chache sana. Hivyo kwa kutumia kiwango cha kawaida sana
cha uuaji wa seli, vimelea wengi hufa. huku binadamu akibakia salama.
kwasababu, yeye bado anaseli nyingi sana, ukitoa chache zilizokufa. Na hata
zikiathirika, bado zinaweza kujitengeneza tena upya atakapopona.
Hii ndiyo sababu watu wanaweza kutumia
dawa za mbu katika majumba yao. Dawa za mbu huwa mara nyingi na viwango vidogo
vya ‘’cypermethrins’’, sumu ambazo ni hatari hata kwa watu. Lakini ukubwa wa
binadamu, sumu zile huwa hazina madhara, huku udogo wa mbu, ukimfanya kuangamia
haraka. Na ukipima madhara ya binadamu kuzuliwa na dawa ya mbu, na madhara ya
binadamu kupata Malaria. Basi chaguo sahihi ni kwa kutumia tu dawa za mbu. Wataalamu
wanatambua madhara ya matumizi ya viwango vidogo vya sumu kwa muda mrefu sana.
Na ndiyo maana hushauri watu wasafishe mazingira yao, ili mbu wasizaliane. Kwa
kuwa kwa kutumia kila siku madawa, kiwango kidogo kidogo huzidi kukaribia hatua
hatari zaidi ya sumu.
Unapofanya matibabu ya seli za saratani
kwa kutumia mionzi ‘’radiotherapy’’, au kwa kutumia kemikali sumu
‘’chemotherapy’’. Matibabu haya yote huua seli nyingi sana za saratani, lakini
huua pia na za mwili. Na ndiyo maana watumiaji wa madawa ya saratani, nywele
zao huisha kwa haraka sana. Hii ni kumaanisha, dawa zao huathiri seli zote za
mwili zinazojizalisha haraka haraka ‘’fast multiplying cells’’, na miongoni ni
seli zinazoongoza uotaji wa nywele, na hata seli za uzazi. Lakini kwanini bado
tunatumia matibabu haya? Ni kwa kuwa kiwango cha seli nzuri tunazozipoteza, ni
ndogo sana ukilinganisha na seli zinazobakia hai. Na seli mbaya tunazoziua, ni
nyingi sana ukilinganisha na seli mbaya zinazobakia hai.
Kwa kuupunguzia mwili seli hatarishi,
wenyewe humalizia kazi ya kujiponyesha, Kwa kuua seli hatari chache
zilizobakia, na kuzizalisha sana seli nzuri zilizopotea, kulipia deni ya seli
hai zilizokufa.
Utofauti
Dawa nyingi huegemea katika utofauti
kadhaa uliopo baina ya viumbe. Kuna baadhi ya chembechembe, chaneli, sifa, na
hata viwango vya fiziolojia, huwa tofauti kwa kila kiumbe. Kwa mantiki hii,
unaweza kuzuia chaneli Fulani iliyopo kwa bakteria, ukijua kabisa kuwa chaneli
hiyo haipo kwa binadamu. Na kwa mantiki hiyo, unaweza kumuua bakteria, bila
kumuua binadamu. Kwa kuwa, sumu imekuwa kwa bakteria, ila sio kwa binadamu, au
mnyama.
Sumu nyingi ambazo hutumika kuua mimea,
kama ‘’Glyphosate’’, ambazo huwepo kwenye ‘’Roundup’’, hulenga kuathiri chaneli
ya mimea inayoitwa ‘’shikimate pathway’’, ambayo huusika na uzalishaji wa
protini za muhimu sana, zinazotengenezwa na mimea tu ‘’essential amino acids’’.
Na cheneli hii haipo kwa Wanyama, na hivyo kwa kupulizia katika mimea,
tunategemea madhara yasiwepo kwa Wanyama. Bakteria wanayo hii chaneli, na hivyo
tunategemea watayapata haya madhara.
Huchelewesha Kifo
Pamoja na yote, dawa huusaidia sana
mwili. Mtu mwenye presha iliyopanda sana. Matibabu kwa ‘’statins’’ kwa wakati
mchache sana, humpatia ahueni, na mwili wake huweza kujiweka vizuri ili
kutoruhusu tena tatizo lifikie hatua ya hatari sana. Madawa mengi huupa mwili
muda zaidi wa kujipanga.
Hebu tazama hili. Mtu mzima ukimpatia
sumu ambayo huchochea moyo wake kudunda kupita kiasi, basi utamuua. Lakini mtu
huyu atakapokuwa anaelekea kufa kwa moyo wake kudunda kidogo kidogo sana,
ukimpatia sumu hii ya kuongeza mapigo ya moyo. Basi atakuwa salama. Hii ni kwa
kuwa, umerudisha mapigo yake ya moyo kwa wastani, ijapokuwa umetumia sumu.
Lakini umemuongezea wakati zaidi wa kuishi, na sasa, anaweza kutafuta namna
bora za kujizuia kufika katika hatua hiyo.
SIRI ILIYOJIFICHA
Madawa na teknolojia zote za matibabu. Ni
neema za Mungu. Mungu wetu alitupatia neema za kuongeza wakati wa kuishi pale
tunapoelekea kikomo kabisa cha Maisha yetu, ili tuzitafakari njia zetu. Hata
Mungu alipomwambia Adamu, hakika utakufa. Bado hakufa ghafla, alimpatia neema.
Unapokuwa unaumwa unaelekea kufa, madawa hukusaidia kupingana na kifo kwa
wakati Fulani, huwa ni alarm ya kuwa kuna jambo kubwa zaidi linaweza kutokea.
Unapotumia dawa, maana yake mwili wako
ulishashindwa kuishi, ulikuwa unaenda kufa. Mtu anayetumia zaidi dawa, maana
yake alitakiwa awe alishakufa, na kifo kinamfatilia sana. Mwili ni hisabati ya
maelfu ya matendo ya kibiolojia. Lakini dawa huenda kurekebisha sehemu za
muhimu sana ambazo zingeweza kupelekea kifo kwa ghafla sana. Na kwa hivyo,
huwezi kuishi kwa kutegemea madawa. Kwa kuwa madawa ni moja ya elfu katika
kuwezesha Maisha. dawa ni kama usukani wa gari, husaidia kuzuia hata gari bovu
lisitumbukie mtoni. Lakini haziwezi kulifanya likawa zima.
Jambo pekee ambalo watu walipaswa
kulitambua ni kuwa, mpaka mtu anapoumwa. Mwili wake wote umepoteza mahesabu. Na
mahesabu ya mwili yote yanategemea madini, na virutubisho. Ambavyo watu
huvipata kupitia vyakula vyenye afya, na mazingira yasiyo hatarishi. Hivyo kama
dawa itatumika kumaanisha kemikali ya Maisha, basi kemikali ya Maisha yenye
matokeo Chanya zaidi, ni vyakula bora. Magonjwa yamezidi kuwa na nguvu kwa kuwa
hata vyakula ambavyo watu wanavitumia, navyo ni sumu, kama madawa wanayotumia.
CHANZO CHA KUFELI KWA
MADAWA YOTE
Madawa yamekuwa yakifeli sana katika
utabibu wake, kwa sababu kubwa mbili. Kwanza, Vimelea
vina maarifa kuliko dawa. Na pili, sumu ni hatari
kuliko vimelea.
VIMELEA VINA MAARIFA KULIKO DAWA
Huwezi kuua aina fulani ya vimelea kwa
mafanikio makubwa sana, na kisha hiyo mbinu ikaendelea kuwa na mafanikio kila
siku. Vimelea huwa na tabia ya kubadilika, kulingana na mazingira. Kwanini
vimelea huwa na maarifa kuliko dawa, ni kwa kuwa vimelea hubadilika, kipindi
madawa huwa hayawezi badilika.
Kadri unavyotumia zaidi madawa, ndivyo
kadri vimelea vinavyobadilika zaidi. Vimelea havina kikomo cha kubadilika.
Lakini dawa zina ukomo wa kubadilika. Inahitaji wataalamu walio na upendo wa
dhati kwa jamii, na akili nyingi sana, kutengeneza aina tofauti ya kitabibu ya
dawa. Itakayo kuwa na sumu kidogo kwa mwili, na mpya kiuuaji kwa vimelea. Jambo
ambalo mpaka sasa hivi tulivyofikia, limezidi kuwa gumu kama ilivyo ngumu
kuwatokomeza vimelea.
Namna Kuu Nane za utendaji wa Madawa
Dawa zote huwa na namna kama nane kuu
zaidi za kuwaua vimelea, ambazo huwa zikilenga
1.Ukuta wa seli wa nje wa Bakteria ‘’Cell
wall synthesis’’
Hizi dawa hulenga kuzuia ‘’cell wall’’ za
bakteria zisiundwe. Hii ni kwa kuwa, bakteria hutegemea sana ukuta wao wa nje
wa seli ‘’cell wall’’, kwa ajili ya shughuli zao. Bakteria huwa na chembechembe
zinazoitwa ‘’Peptidoglycan’’, wakati fangasi huwa na ‘’chitin’’. dawa kama
Penicillins, Ceftriazone ‘’power safe’’, Vancomycin, n.k. hulenga kuua hizi
chembechembe za ukuta, mfano penicilins na cephalosporins, huua Beta-Lactams
zilizo kwenye ukuta wa bakteria, na kuwaua. Dawa za fangasi kama Echinocandins
huua ukuta wa fangasi, na kuwaua.
2.Ukuta wa seli wa ndani ‘’Cell
membrane’’
Ukuta wa ndani huwawezesha sana bakteria
na fangasi, kuweza kuchangamana na mazingira yao, katika ukuaji na shughuli
zao. Kwa fangasi mfano huwa wana chembechembe zinazoitwa ‘’ergosterol’’, ambayo
huwasaidia sana. Na dawa huua hizi sehemu. Mfano, dawa kama ‘’Polymyxins’’ huua
‘’cell membrane’’ kwenye bakteria, hasa ‘’gram negative’’, ambao kwenye ukuta
wao wana chembechembe zinazoitwa ‘’lipopolysaccharides’’, hizi ndizo huwafanya
hawa bakteria kuwa hatari sana. Lakini kwa fangasi pia kuna dawa zinaitwa ‘’Amphotericin
B’’, nazo huwaua sana fangasi, kwa sheria hii.
3.Uundwaji wa Protini ‘’Ribosomes’’
Vimelea huitaji protini kwa ajili ya
kukua. Na ili kuunda protini huitaji kuwa na ribosome (70s) ambayo ni tofauti
na ribosome ya binadamu (80s). na dawa nyingi sana za bakteria hulenga kuua hii
ribosome. Dawa kama Gentamicin, Tetracyclines, Erythromycin, linezolid, n.k.
zote zimelenga kuathiri uundwaji wa protini kwa bakteria.
4.Chembechembe za Nyuklia ‘’nucleic
acids’’
Kila kiumbe kinahitaji DNA ili kiweze
kuishi. Maana hizi ndizo zinazowezesha uwepo wa kila chembechembe ya uhai, kwa
kuziunda. Na DNA huitaji marazote kuendelea kujizalisha yenyewe ‘’DNA
replication’’, kwa msaada wa mashine za seli ‘’enzymes’’, na hivyo basi, kama
utaathiri matendo haya ya DNA, kwa kuiathiri yenyewe moja kwa moja, au kwa
kuathiri mashine zake ‘’enzymes’’, basi unaweza kumuua kimelea. Na hapa kuna
dawa nyingi sana.
Mfano, Ciprofloxacin, enrofloxacin, rifampin,
n.k. hizi huwaua sana bakteria. Kwa virusi kuna dawa kama Acyclovir,
zidovudine, efavirenz, n.k. na kwa protista kuna dawa kama ‘’chloroquine’’
inayotumika sana kwa malaria.
5.Matendo ya Kimetaboliki ‘’metabolic
pathways’’
Vimelea huwa na matendo mbalimbali ya
kibiolojia ya kuendesha Maisha yao, ndani, na nje ya seli zao. Matendo haya
huwa hayafanani marazote na ya kwa binadamu. Na hivyo, ni rahisi kutengeneza
dawa ambayo, inaweza kulenga kuwaathiri vimelea hawa tu. Mfano wa matendo ya
kipekee kwa bakteria, ni uundwaji wa vitamini B9 kwa bakteria ‘’folic acid
synthesis’’, ambayo huwasaidia sana katika uundaji wao wa protini, na
chembechembe za nyuklia. Dawa kama Sulfonamide, Trimethoprim, n.k. huathiri
matendo haya, na kuwaua bakteria.
Minyoo wengi sana huuwawa kupitia namna
hizi, hasa zinapolenga kuathiri mfumo wao wa fahamu. Kwa kuruhusu madini ya
calcium mengi sana, hata kimelea kuanguka na kufa. Mfano ni Praziquantel. Nyingine
husisimua sana sensa, au ‘’receptors’’ za msisimko, hata kiumbe huanguka na
kufariki. Mfano ni ivermectin, pyrantel, n.k. Zingine hublock mfumo wa nishati
‘’ATP’’ za kimelea, na kimelea hulegea mpaka kufa.
6.Mpangilio wa Virusi, na namna za
Kuvamia ‘’viral entry, assembly and relaese’’
Virusi huingia ndani ya seli ya mtu na
kutumia mtambo wake huyo mtu, kujizalisha. virusi hujipangilia kuwa sawa
kupitia aina zao kadhaa za protini. Kwa kutumia dawa ambazo zinaweza kuzuia
mipangilio hii ya virusi, ni rahisi sana kuwaua. Hapa zipo dawa nyingi sana,
kama vile enfuvirtide, maraviroc, ritonavir, oseltamivir, n.k.
7.Mhimili wa Kimelea ‘’Cytoskeleton’’
Vimelea wengi, hasa aina za minyoo.
Huitaji sana protini ambazo ndizo huunda mhimili wao, au ‘’skeleton’’ yao, kwa
ajili ya kujizalisha, na kutembea. Ukiathiri protini hizi, huwa ni rahisi sana
kuwaua. Dawa kama Albendazole, huua minyoo wengi sana kwa kuwatibulia mhimili
wao ‘’microtubules’’. Hata Griseofulvin ni dawa ya kuulia fangasi, ambayo
hutumia sheria hii hii.
8.Kulenga Sumu za Vimelea ‘’virulence
factors’’
Vimelea wengi huwa na chembechembe zao za
sumu, ambazo huzitumia ili kushambulia viungo vya wanaowashambulia. Hizi huwa
ni kama majiko yao ya chakula, yasipowaka hawali. Dawa kadhaa huzimisha
‘’neutralize’’, hizi kemikali. Na matokeo yake, kimelea hufa. Mfano mzuri ni
‘’anti-toxins’’ zote, au pia chembechembe za kinga ‘’antibodies’’
Namna Vimelea vinazishida Dawa Akili
1.Huimeng’enya dawa.
Vimelea kama baadhi ya bakteria,
huzalisha vimeng’enyaji mfano, Beta-Lactamase, ambao huivunja dawa ya
Penicillin, isiweze kuharibu ukuta wake wenye Beta-lactam. Na hii hupelekea
dawa kama penicillin, na Cephalosporins, kama Ceftriazone kushindwa katika baadhi
ya mazingira.
2.Hubadili Target ya Dawa.
Mfano dawa zinazolenga Kwenda
kujishikisha katika 70s ribosome, bakteria hubadilisha hii ribosome yao. Na
dawa kama macrolides ‘’erythromycin’’ hufeli, au tetracyclines, zote hufeli
katika baadhi ya mazingira. Hasa kwa watumiaji wa muda mrefu, au walaji sana wa
nyama za Wanyama waliochomwa sana dawa hizi.
3.Husukuma nje dawa
Bakteria wengi huwa na protini maalumu
kabisa, ambazo hutoa nje ‘’pump out’’ dawa zote walizozipata. Tena kabla
hazijaleta madhara. Na hii huwa ni sababu ya kufeli sana kwa dawa za
tetracyclines, na ‘’fluoroquinolones’’ kama ciprofloxacin, ‘’enrofloxacin’’ au ‘’fluban’’ kwa baadhi ya
‘’trade names’’.
4.Kutotumia njia za kimetaboliki
zilizolengwa na dawa
Mfano zile dawa za ‘’sulfonamides’’,
ambazo zililenga sana uundwaji wa vitamin B9 kwenye bakteria ‘’folic acid
synthesis’’, bakteria wengi huiruka hatua ile, na kutumia hatua nyingine. Hii
hupelekea dawa hizi kufeli.
5.Kuunda Koti la kujikinga na dawa
‘’Biofilm formation’’
Bakteria huunda koti, au hujizungushia
protini, na chembechembe zingine. Na kuzifanya dawa zinazotaka kuwashambulia,
kushindwa. Na hii hutokea sana kwa magonjwa ya muda mrefu. Mfano, bakteria
wanaoitwa ‘’Pseudomonas aeruginosa’’, huunda koti hili, kwa wagonjwa wa
‘’cystic fibrosis’’.
6.Bakteria husambaziana mbinu zao za
kujikinga na dawa. Hii huwa kupitia chembechembe zinazoitwa ‘’plasmids,
transposons, au kwa kutumia virusi wanaoitwa ‘’phages’’. Na hizi njia huitwa
‘’horizontal gene transfer’’. Bakteria wengi kama ‘’staphylococcus aureus’’,
huwa fasta sana katika kusambaziana hizi sifa.
7.Vimelea kama Bakteria huzaliana haraka
sana. Na hubadilika haraka sana. Hii huwafanya ndani ya muda mfupi sana, kuweza
kuizoelea dawa, na kuishinda. Na upande wa virusi, mfano ‘’RNA-Viruses’’, kama
virusi wa UKIMWI, na Influnza. Hawa hubadilika kwa spidi kubwa sana. Na hii ni
kwa kuwa, huwa na makosa mengi sana katika uzalishaji wa DNA zake
‘’DNA-replication’’, makosa haya yanatokana na mashine zake za seli ‘’enzymes’’
zinazoitwa ‘’reverse transcriptase’’, kufanya makosa sana katika utendaji wake.
Hivyo kila wakati huwa wanabadilika. Na ni ngumu kutengeneza dawa yoyote ile ya
kuwamaliza.
8.Virusi huwa wakiichangamanisha
‘’integrate’’, DNA yao, kwenye DNA ya mtu wanayemshambulia. Mfano, Virusi wa
UKIMWI, au virusi wa Herpes. pia huwa wanaweza kuingia katika hatua ya kulala
‘’dormant stage’’. Katika hatua hizi zote, hakuna Dawa inayoweza kuwapata. Huwa
hawapatikani kwa dawa yoyote ile. Na baada ya muda, huwa wanarudi na kuendeleza
madhara.
9.Huwa wanatumia mtambo wa seli wa
mgonjwa mwenyewe. ‘’host’s machinery’’.
Na hii ndiyo hufanya kazi kuwa ngumu sana kuwapata virusi wa Hepatitis
B. kwa kuwa hujishikisha katika chembechembe ‘’enzyme’’ ya nyuklia ‘’ DNA Polymerase’’ ya mtu husika. Na kwa
mantiki hii, ni ngumu sana kuweza kumuua kirusi huyu.
10.Virusi huwa na ujanja wa kubadili
sensa zao ambazo mfumo wa kinga ungeweza kuwagundua. Hii huitwa ‘’antigenic
variation’’. Na hasa kwa ‘’influenza’’, au ‘’UKIMWI’’, ambapo kirusi
anabadilisha ‘’MHC’’ au ‘’major histocompatibility class’’, ambazo mfumo wa
kinga unazitegemea ili kuweza kuwaua virusi kwa kuwakamata.
11.Kumuua kimelea, hasa wanaojificha
sana. Hupelekea kiwango kikubwa sana cha sumu kujaa katika seli. Na hii
hupelekea madhara makubwa zaidi ya dawa au sumu zenyewe katika seli, kuliko
hata kimelea mwenyewe.
vimelea wengi tu wangeweza kufa kwa dawa
baadhi, lakini viwango vya dawa za kutosha kuwaua, tayari zinaweza muangusha
mtu kwa kumuua kwa ‘’overdose’’. Hivyo ukaribu wao sana na metaboliki za
wanaowaathiri, huwapa faida sana. Maana kinachoweza kumuua yeye, kinaweza
kumuua pia na mgonjwa wake.
JE MFUMO WA AFYA UNAWEZA KUOKOKA?
Katika hatua hii ya kwanza. Hakuna
kipingamizi cha kuwa, safari ya kushindana na vimelea kwa kutumia madawa ya
kuwaua. Hakuna namna ya kuweza kuwafikia kiutaalamu. Vimelea ndiyo wanazidi
kuwa bora, walioshindikanika. Huku taaluma za afya, tukiwa tumeshamaliza mbinu
zetu.
Tangia historia za misri, mpaka leo hii,
tumeshamaliza mbinu zote za kitabibu, na kwa mantiki hiyo, kuna kila sababu ya
kuhofia kuwa kama watu hawatakuwa makini kujilinda na afya zao, wakitegemea
dawa kuwasaidia, wanaweza kujikuta wakiangamia na matumaini yao.
SUMU NI HATARI KULIKO VIMELEA.
Kadri watu wanavyohangaika na vimelea, wakiamini kuwa
hao ndiyo tatizo kubwa sana. Kumbe vimelea ni kama watu wanaobeba maiti Kwenda
kuizika. Wao hawamuui mtu, ila wanaenda kumzika, na kumfukia ardhini. Vimelea
huja dakika za mwisho kuamua hatma ya Maisha ya mtu, na kushindana nao
tumeshaona kwa sasa hivi sio kazi rahisi. Lakini hebu tumwangalie muuaji
mwenyewe kwanza.
Muuaji mkubwa kabisa wa Maisha ya watu,
ni sumu. Sumu ni chembechembe zote ambazo hazihitajiki katika miili ya watu.
Sumu hazina kituo maalumu, huenda na kuathiri seli, au tishu, au chaneli, au
chembechembe, mpaka nyuklia za seli, sumu huathiri chochote kile mwilini. Sumu
huwa zina ngazi, kuanzia sumu hatari kabisa ambazo zinaweza kumuua mtu ndani ya
sekunde chache, mpaka zinazohitaji kipindi cha miaka kumi kuonyesha madhara
yake.
Hakuna kitu kigumu kukidhibiti kama sumu,
maana huwezi kuiua sumu. Japokuwa tumeshindwa kuwaua vimelea, lakini sumu ndiyo
hatuwezi kabisa. Vimelea huelekea katika sehemu moja, na unaweza kuwagundua,
lakini sumu huwezi kuzigundua. Vimelea huwa na matokeo ya ghafla ambayo unaweza
yagundua na kuyabadilisha, lakini matokeo ya sumu yakishatokea huwa
hayabadilishiki kirahisi. Watu wengi wana maarifa na vimeleaa, lakini watu
wachache sana wanazifahamu sumu, na matokeo yake. Inahitaji akili nyingi sana
kuzitambua sumu. Maana huwezi kuzingundua. Sumu huwa chache sana, na uelekeo
wake huwa haueleweki.
Historia za Sumu
Kwa miaka mingi sana nyuma, kiwango
kikubwa sana cha magonjwa kilikuwa kinatokana na magonjwa ya vimelea. Kama vile
magonjwa ya virusi, na magonjwa ya bakteria. Sehemu zingine magonjwa kama
malaria ‘’protista’’, na hata minyoo kama kichocho ‘’schistosomiasis’’ kwa
baadhi ya sehemu. Magonjwa kama ‘’smallpox’’ yameshika sana rekodi huko nyuma
ya kuua watu wengi zaidi. Lakini sasa mambo yamebadilika.
Baada ya kuvuka miaka ya 1800’s, na
kuingia miaka ya 1900’s, tena hasa baada ya kumaliza vita ya pili ya dunia
1945’s, dunia iliingia katika namna mpya
ya ulimwengu, ambayo ilikuwa ni ‘’zama za viwanda’’. Katika zama hizi,
kuliambatana na kiwango kikubwa sana cha usasa ‘’modernization’’. Watu wengi
sana walikimbilia mitindo ya usasa, kutokana na namna ilivyokuwa na mwonekano
wa mvuto, na anasa.
Kadri miaka ilivyokuwa ikizidi Kwenda,
ndivyo watu walivyogundua hata namna za vifo nazo zimekuwa ni namna za usasa.
Watu wakaanza kufa kwa namna tofauti kabisa na namna za zamani. Watu wakawa
wakifa kwa magonjwa mapya kabisa. Kwa mara ya kwanza kukaibuka Ugonjwa mpya kwa
kushamiri kwa ‘’Saratani’’. Ilikuwepo zamani, lakini sio kwa namna kama ya
kisasa. Lakini pia kukaibuka matatizo ya mfumo wa moyo ‘’cardiovascular
problems’’, ambayo ndiyo yanaongoza kwa idadi kubwa zaidi ya vifo mpaka sasa.
Kukaibuka matatizo ya mfumo wa mapafu, ambayo yameshamiri sana hasa
yakiambatana na saratani. Zikaibuka changamoto za mfumo wa nishati, na insulin,
shida za kisukari ‘’diabetes mellitus’’, watu wengi wakaanza kupata vitambi, na
kuathirika mifumo yao ya kihomoni.
Kukaibuka matatizo mengi sana ya Maini,
kufeli kwa figo kukazidi kupamba moto. Idadi kubwa sana ya Watoto wanaozaliwa
na ulemavu ikaongezeka. Wanawake wanatoa mimba ‘’abortions, na stillbirths’’,
idadi yao ikaongezeka. Matatizo ya kiakili yakaongezeka, idadi kubwa sana ya
watu wakaanza kupata changamoto za kisaikolojia, na za kiviungo moja kwa moja.
Kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga, hata miaka ya watu hawa ikazidi
kupungua.
Baada ya matatizo haya kuzidi kusonga, na
kushamiri. Ndipo wanasayansi walipogundua kuwa changamoto kubwa inayochochea
haya yote, ni Sumu. Na sio vimelea. Na sumu nyingi sana zilionekana kutokana na
matumizi ya bidhaa nyingi sana za kisasa.
Kuanzia moshi wa Tobacco
Pombe nyingi sana zinazonyweka kwenye
vilabu
Bidhaa za sukari za kisasa. Juisi za
viwandani, biskuti, pipi, soda, energy drinks, n.k.
Mionzi mingi sana kutoka kwa vifaa vya
kielektroniki.
bidhaa nyingi sana za mafuta mabaya.
hewa chafu sana kutoka katika mazingira
matumizi ya mbogamboga nyingi sana
zilizopigiwa madawa.
Matumizi ya bidhaa za GMO zenye
‘’allergens’’ na ‘’carcinogens’’ nyingi.
matumizi ya madawa mengi sana yanayoua
hisabati za fiziolojia ya miili, mfano kwa kuua bakteria wazuri, na kuongeza
sumu.
kutumia sana bidhaa za nyama.
kutumia maji ambayo yametoka katika mitaro yenye mabaki ya madini chuma, au maji
yenye mabaki ya madawa shamba ‘’viuatilifu’’.
kutokuwa na muda mrefu na mazingira
mazuri ya kupumzika.
kutopata mazingira mazuri ya kufanya
mazoezi na kutoa nje sumu.
Na mitindo mibaya ya kujiathiri
kisaikolojia kama mitandao ya kijamii, miziki mibaya, tabia za uzinifu
zinazoharibu uthabiti wa mifumo ya homoni ya upendo, na haya yote huongeza
zaidi stress, na kupunguza uwezo wa ku refresh mwili dhidi ya sumu.
Baada ya wanasayansi wengi kugundua kuwa
kuna tatizo jipya lililoibuka, linaloua sana watu, ambalo ni sumu, ambazo zimesambaa zaidi katika
matumizi ya watu ya kila siku. Wengi waliandika ripoti nyingi sana, zinazoonyesha
madhara mbalimbali ya sumu, ambapo hata mimi mwandishi pia nimeandika ripoti,
na kitabu kabisa cha ‘’injli ya sayansi Q4’’. Lakini jambo ambalo watu wengi
bado hawajalitambua hapa ni hili.
SUMU NI ZA KITAALAMU ZAIDI YA VIMELEA
|
SUMU |
VIMELEA |
|
Huwa
kwenye vitu vizuri, na vitamu. Kama vile soda, nyama, pizza, pombe, sigara,
dawa za kulevya, filamu za mapenzi, miziki ya mabiti, n.k. |
Huwa
kwenye vitu hatarishi na vibaya kama vile, kinyesi, vyakula vibichi, sehemu
za utoaji taka mwili, vitu vilivooza, n.k. |
|
Huwa
na uraibu, kwa kuwa huwa na matokeo ya kisaikolojia. |
Hazina
uraibu. Huwa na matokeo ya kupooza, au kusisimsha. Matokeo yake ni ya athari
katika fiziolojia ya ubongo |
|
Hutenda
kwa muda mrefu sana. Zinapotenda kwa wakati mfupi sana, huwa hazina mafanikio
ya kuwapata wengi, maana wengi huzikimbia. |
Hutenda
kwa muda mfupi sana. Zinapotenda kwa wakati mrefu, huwa hazina mafanikio.
Wengi hujikinga nazo. |
|
Madhara
yake huwezi yabadilisha, maana huwa yanaharibu hata viungo vya kubadili
madhara yake. Mfano, huaribu sana ini, figo, na ubongo. |
Madhara
yake unaweza yabadilisha. Kama hutakuwa na madhara ya sumu awali yake. |
|
Ni
vigumu kuzigundua. Huwa zinakuwa kidogo kidogo. Ili zikijikusanya kwa aina
zake nyingi, huwa nyingi sana. |
Huwa
ni rahisi sana kuwagundua. Huwa wanakuwa wengi, lakini katika eneo dogo. |
|
Zinaharibu
fizilojia na jenetikia zote za mwili |
Wanaharibu
aina maalumu tu za fiziolojia, na jenetikia za mwili. |
|
Zimeshawateka
wengi, na zinaenda kumaliza uthabiti wa afya za watu kwa kiwango kikubwa
sana. Zina ajenda za kitaalamu sana, na mtu wa kawaida huzigundua akishakuwa
kitandani hajiwezi. |
Wameshashindikana,
na wanasubiria sumu zianze kuonesha mauaji yake, na zenyewe zitamaliza afya
za watu, bila mpinzani. |
Mpaka sasa hivi inatambulika kuna
matatatizo makubwa nane ambayo hayawezi kutibika, yanayosababishwa na mitindo
mbalimbali ya kiafya. Na watu wengi hawajui kuwa kupitia matendo haya, wagonjwa
wengi watarajiwa watajikuta wakiingia katika hatua mbaya sana za Maisha yao.
SHIDA NANE ZA SUMU ZISIZOTIBIKA
1.Kugandana kwa Sukari katika chembechembe
za mwili ‘’Glycation’’
Ulaji sana wa sukari kupitia bidhaa kama
soda, biskuti, keki, n.k. hupelekea sukari Kwenda kujishikamanisha katika
chembechembe zingine za mwili, kama vile Protini, na mafuta ‘’lipids’’, na
kuunda kemikali sumu zinazoitwa ‘’Advanced glycation end products’’, au
‘’AGE’s’’. hii kitaalamu inaitwa ‘’non-enzymatic binding’’. hizi ‘’AGEs, huua
tishu, huchochea uzee, huchochea uvimbe ‘’inflammation’’, husababisha magonjwa
ya kudumu, kama Kisukari ‘’diabetes, alzhemimer’s, and Cardiovascular
diseases’’.
2.Kukakamaa na kuisha kwa tishu
‘’Oxidative stress’’.
Hii hutokana na sumu nyingi ‘’free
radicals’’, Kwenda kuua seli za mwili. Na hii hutokana na matumizi ya bidhaa
kama pombe, vitunza vyakula vingi ‘’preservatives’’, sigara, nyama hasa
nyekundu, n.k. hizi huchochea kuzeeka haraka, kujaa kwa mafuta kwenye mishipa
ya damu ‘’atherosclerosis’’, na matatizo ya kuzeeka au kuisha kwa ubongo
‘’neurodegenerative diseases’’.
3. Kufa kwa Chembechembe za nishati za
seli ‘’Mitochondrial dysfunction’’
Vinywaji vya viwandani vyote vyenye
sukari ‘’fructose’’, mfano, ‘’high corn fructose syrup’’. Huwa na fructose
ambayo huua enzymes tatu za mitochondria
moja kwa moja. Pia uwepo wa vitunza vyakula kama ‘’sodium benzoate’’, huathiri
pia mitochondria. Bidhaa nyingi za kisasa huua hizi mitochondria. Na hupeleka
kupungukiwa nishati ya mwili, kukakamaa kwa misuli, shida za kimetaboliki, na
magonjwa ya kudumu.
4.Kufeli kwa insulin ‘’insulin
resistance’’
Seli inashindwa kuchukua insulin, na
kupelekea sukari kujaa kwenye damu, na mtu anazidi kuwa dhaifu. Wala nyama huwa
ni vigumu kukimbia tatizo hili. Na hasa walevi. Pia wanywa soda huathirika
kutokana na tabia za fructose, kuchochea mafuta mengi kwenye ini. Madhara yake
huwa ni kisukari, kitambi, matatizo ya moyo, kuishiwa nguvu za kiume, kuchelewa
kupona vidonda, n.k.
5. Ukuta wa seli kuathirika ‘’’cell
membrane instability’’
Mtu anayekula nyama anawezaje kukimbia
tatizo hili. Ikiwa mwili wake anaujaza kiwango cha mafuta hatari ‘’saturated
fatty acids’’. Ambazo kadri zinavyolimbikizana katika ukuta wa seli,
zinaharibika haraka kutokana na ‘’oxidation’’, na kupeleka seli kuharibika
kutokana na ukuta wake kuharibika. Mnywa soda naye, na wenzake wengi wa
kumfanania huteseka kwa hili. Hii huua mawasiliano baina ya seli, huathiri
uwezo wa seli kufyonza virutubisho, na seli hufa. Na idadi ya miaka ya mtu
huzidi kupungua.
6.Uvimbe wa kudumu ‘’chronic
inflammation’’
Mtu anayekula nyama huwa na kiwango
kikubwa sana cha asidi katika utumbo wake kutokana na protini nyingi sana za
asidi ‘’acidic amino acids’’. Hizi hupelekea utumbo kuchubuka sana, na kwa
kadri mtu anavyotumia sana. Ndivyo tatizo linavyodumu sana. Mtumiaji wa sembe
naye anajikosesha kambakamba ‘’fibres’’, madhara yake ni bakteria wa kwenye
utumbo wake kupungukiwa chakula, na kuanza kula ukuta wa utumbo, wakila protini
‘’mucin’’, katika uteute wa utumbo ‘’mucus’’, na kisha kuuacha utumbo wazi. Na
sumu za ‘’free radicals’’ huuchubua utumbo na kupelekea uvimbe, na hata kansa
kwa wala nyama. Wanywa soda nao huwa na shida hii hii. na huchochea pia
matatizo ya metaboliki, na magonjwa ya mwili kujidhuru ‘’autoimmune’’.
7.Kufelisha uwezo wa seli kuiongoza
jenetikia yake ‘’epigenetic dysregulation’’.
Hii hutokana na kila mtindo hatarishi.
Kuanzia katika kukesha katika screen za video kwa filamu, au mipira. Kusikiliza
sana miziki ya mabiti ya frequency hatari kama 440Hz. Kutumia bidhaa zenye
vitunzaji ‘’preservatives’’ nyingi sana. Kutumia mboga mboga zenye madawa, hasa
za jamii za Chinese, spinach, strawberries n.k. haya yote huifanya miili kuwa
hatarini sana kuweza kupata magonjwa.
8. Kuathirika kwa Mfumo wa bakteria
wazuri wa tumboni ‘’Dysbiosis’’
Hii inatokana sana na vyakula vya
viwandani kama nyama za kusindikwa ‘’processed meats’’, bidhaa za sukari,
nyama, na madawa mengi ‘’antibiotics’’. Na watu hunywa sana madawa kwenye
maziwa, na kwenye kuku wa broiler, bila wao kujijua. Haya yote huchochea
changamoto za mfumo wa ulaji, na umeng’enyaji, changamoto za kinga, na shida za
uvimbe.
MAGONJWA KUMI YA SUMU YASIYOTIBIKA
1.Kisukari ‘’Type-2-Diabetes’’.
Hii ndiyo ile iliyochochewa na kufeli kwa
insulin ‘’insulin resistance’’, uvimbe wa muda mrefu ‘’chronic inflammation’’,
na matumizi makubwa ya bidhaa za sukari na pombe.
2.Presha ‘’Hypertension’’
Hii nayo imesababishwa na kufeli wa
insulin, kunakochochea sukari kujaa katika mishipa ya damu, na kufanya mishipa
kuwa midogo. Pia michubuko ya ‘’oxidative stress’’, hupelekea mishipa ya damu
kuvimba, na pia madini chumvi mengi kutokana na ulaji wa nyama, huchochea
tatizo hili.
3.Mafuta mabaya ‘’Dyslipidemia’’
Changamoto za kuzidi kwa cholesterols
mwilini huwezi kuzizuia, kama unakula nyama za broiler, au zozote zile kwa
wingi, ukiachana na samaki toka maji salama. Mafuta mabaya hujaa zaidi kutokana
na kufeli kwa insulin, kunakochochea kuundwa zaidi kwa mafuta toka sukari, na
pia shida za kufeli kwa mitochondria.
4.Shida za moyo ‘’cardiovascular
disease’’
Kujaa kwa sukari katika mishipa
‘’glycation’’ huchochea tatizo hili, michubuko ya ‘’oxidative stress’’
huchochea tatizo hili, uvimbe ‘’inflammation’’, huchochea tatizo hili, na kujaa
kwa mafuta kwenye mishipa ya damu. Na haya yote ni matokeo ya mitindo ya
kisasa, mtu anakula mkate, na blueband, anategemea sukari, na trans fats zote
zitaishia wapi?
5.Kujaa kwa Mafuta katika ini bila kunywa
pombe ‘’non -alcoholic fatty liver disease’’
Hii hutokana na sukari nyingi hasa za
‘’fructose’’, kubadilishwa, na kuunda mafuta, ambayo hujaa kwenye ini. Kwa kuwa
inatambulika kuwa, sukari ya fructose iliyo kwenye bidhaa za kisasa, yote
huishia tu kwenye ini. Hakuna sehemu nyingine kwenye mwili inapoweza kutumika.
6. Saratani ‘’cancer’’
Uvimbe wa kudumu, mfano kutokana na ulaji
wa nyama, michubuko ya ‘’oxidative stress’’, kupungukiwa kambakamba katika
lishe, mtu hali mihogo, wala magimbi, wala dona. Yeye anakula tu sembe, haya
yote huchochea madhara yanayoweza kupelekea uvimbe wa kudumu katika sehemu
mbalimbali. Kufeli kwa mitochondria huchochea ukuaji rafu wa seli, ambao
huchochea saratani.
Inatambulika kuwa ukuaji wa saratani
huitaji sana uasidi ‘’acidic environment’’, kutokuwa na oksijeni ‘’anaerobic
states’’. Na hizi zote ni hali zinazochochewa kwa utumiaji wa protini za
Wanyama, kama vile nyama, na maziwa. Lakini pia sukari za kisasa na bidhaa za
viwandani huwa na asidi ambazo huongezwa kama vitunza vyakula, na kuwa na
kaboni dioksaidi nyingi. Haya yote huchochea zaidi saratani.
7.Kuisha kwa Ubongo. ‘’Dementia/alzheimer’s’’
Hii nayo ambayo huitwa pia aina ya tatu
ya kisukari ‘’type-3 diabetes’’, huusiana moja kwa moja na kufeli kwa insulin,
kugandana kwa sukari ‘’glycation’’, na hata kuchubuka kwa tishu za ubongo kwa
‘’oxidative stress’’.
8.Shida ya uzazi kwa wanawake. Polycystic
ovarian syndrome ‘’PCOS’’
Hii hutokana na changamoto za kihomoni
zinazochangiwa sana na kufeli kwa insulin, kufeli kwa metaboliki za mwili,
lakini sasa hivi inafahamika hata kutumia sana mbogamboga zenye mabaki ya
viuatilifu ‘’pesticides’’, huchochea tatizo hili kwa wanawake.
9. Kupungukiwa kinga ya mwili ‘’immunity
failure’’
Hakuna namna mtu anaweza kuwa na kinga
kwa matumizi ya bidhaa za viwandani, zenye vitunzaji vingi sana vya vyakula.
Vinavyoua kinga ya mwili. Mfano, emulsifiers, stabilizers, artificial flavors,
artificial sweeteners, preservatives, food colors, n.k. hizi huua chembechembe
nyingi sana za mawasiliano ya kinga, kama interleukins, interferons, cytokines
mbalimbali, n.k.
Kibaya zaidi, kadri unapozidisha sukari
mwilini, ndipo sensa zako zinazoitwa ‘’ACE-2 receptors’’ zinazalisha zaidi
‘’angiotensin converting enzymes’’ ili kuruhusu maji mengi zaidi kufyonzwa kuzuia ‘’hypertension’’, kwa
kubadili ANGI kuwa ANGII, na kuchochea ADH kuzuia upotevu zaidi wa maji. sasa
virusi huitaji hizi sensa za ‘’ACE-2’’ ziwe wazi, maana ndiyo hujishikisha
hapo, kwa hiyo kadri mtu anapotumia zaidi hizi bidhaa, ndipo anapokuwa na
urahisi zaidi wa kupata maambukizi ya virusi.
10. Matatizo ya Ubongo ‘’Neurological and
psychological problems’’
Unaweza kusoma kitabu cha Q4 kuelewa
hili. Kila zinapotumika bidhaa hizi, huathiri ubongo kwa kubadilisha viwango
vyake vya sensa ‘’receptors’’, na kupeleka matokeo ya kudumu ya kiafya ya
ubongo ‘’neuroplasticity disorders’’. Na haya huathiri akili za watu, na afya
yao ya kimaamuzi moja kwa moja. Na kupelekea kizazi cha watu wapumbavu
kwelikweli.
HATMA HATARISHI
KABISA KUHUSIANA NA ONGEZEKO LA SUMU
Marazote mpambanaji mkuu kabisa wa mfumo
wa kinga wa mtu, ni mwili wake. Ukiathiri uwezo wa kinga ya mtu, lazima mtu
ataishia utegemezi mkubwa sana kwa madawa. Kinga za watu wengi sana zimezidi
kuathiriwa sana kwa ongezeko la viwango vya sumu katika mitindo ya Maisha yao.
Kadri ongezeko hili la sumu linavyozidi kusonga mbele, ndivyo hatari zaidi za
afya zinavyozidi kuongezeka zaidi.
Tumefikia hatua ambayo hali za watu za
afya, zipo mashakani sana. Na tunaenda katika hatua ambazo, hali za kimwili za
watu ukichanganya na dhiki za Maisha, hazitakuwa sawa kabisa.
KWANINI MADAWA MENGI YANAZIDI KUFELI ZAIDI
Tunaelekea katika hatua ambayo ni vigumu
sana kuwa na dawa za kuwatibu watu. Hii ni kwa kuwa, kutokana na kiwango
kikubwa sana cha sumu katika vyakula vya viwanda, na masumu ya bidhaa za
viwandani. Magonjwa mengi yanatokana na kufeli kwa mawasiliano ya sehemu
mbalimbali za mwili. Na magonjwa mengi hayana sababu moja. Ni vigumu sana
kuweza kutibu magonjwa haya kwa kutumia dawa moja. Inahitaji dawa nyingi sana.
Na kadri dawa zinavyokuwa nyingi sana, ndivyo zinaleta matokeo hasi ‘’adverse
effects’’ kwa wingi sana. Hii ni kwa kuwa, baadhi ya dawa hupingana katika
namna zake kiutendaji.
Magonjwa mengi tuliyokwisha yaona, na
mengineyo ambayo huwezi kuyatibu. Kadri unavyojaribu kuyatibu, ambapo huwa ni
kupitia kugeuza dalili ‘’reverse symptom’’. Kama presha imepanda, wewe
unashusha. Matibabu ya mtindo huu, huwa
hayaongezi uwezo wa mwili kupandisha presha yake, huwa tu yanalenga utumiaji wa
chembechembe za dawa ambazo huweza kupandisha presha. Matumizi ya chembechembe
humaliza kabisa balansi ya awali ya mwili. Na huwa na matokeo ya utegemezi
zaidi kwa madawa.
Zamani dawa nyingi zilikuwa na mafanikio
makubwa sana. Hii ilikuwa ni kwasababu, miili ilikuwa bado na nguvu kubwa sana
za kiafya. Miili ilikuwa na virutubisho vingi sana. vilivyotokana na mitindo sahihi
sana ya kimaisha. Usasa ulipelekea vyakula dhaifu sana kiafya. Hata kuishia na
sumu nyingi zaidi katika miili. Hizi zimeufanya mwili kushindwa kabisa
kujirekebisha, pale matatizo ya magonjwa yanapotokea. Na hivyo kufeli kwa dawa
kunazidi kuchochewa kwa mitindo hii ya afya.
SURA YA NANE
MAGONJWA
YASIYOFAHAMIKA’’
Mshindi wa Nobel prize George Ward
Nukuu Kutoka Kwa Mshindi Wa
Tuzo Ya Mwanasayansi Bora ‘’Nobel Prize’’
George Wald Ambaye Ni Professor Wa Biology Chuo Cha Harvard Kuhusu
Genetic Engineering
‘’Injinia ya mabadiliko ya
kijenetikia, inawasilisha katika jamii zetu matatizo ambayo siyo tu hayajawahi
kutokea katika historia ya sayansi, lakini pia katika Dunia’’.
Ni afadhali ya madhara ya
X-Rays, ambayo, huwa tu ikilemea katika genes Fulani, lakini hili janga kubwa
hupelekea kusukumwa kwa genes mbele na nyuma, sio tu katika jamii ya viumbe
Fulani, bali kuvuka mipaka kwa kushambulia jamii zote za viumbe’’
Kwa mtazamo wa bwana Wald,
ukweli kuwa Samaki hawezi kukutana na kujamiiana na Nyanya! ni kwasababu
tofauti hizi. kati ya nyanya, na Samaki. sio za mlipuko au kujitokea tu.
‘’random’’. bali ni sababu ambazo, ni matokeo ya mabadiliko ya muda mrefu ya
‘’evolution’’, mpaka kupelekea jamii iliyo imara ( msomaji kumbuka sayansi
imejawa na imani ya evolution)
Wald alikuwa akionya kuwa,
viumbe hai ni matokeo ya mifumo iliyojengwa kwa miaka mingi sana. na hivyo, sio
jambo la kubadili tu mifumo hii ndani ya usiku mmoja, kwa kuwa madhara yake,
yatakuwa ni kukinzana na mifumo ambayo, itapelekea madhara makubwa sana kuwahi
kutokea.
Na pia akakazia kuwa, hata
madhara yake yatakuwa makubwa sana. Ambayo, hayajawahi kuonekana au kuelezwa na
mtu yeyote yule.
Wald alisema kuwa, mabadiliko
ya kijenetikia yatapelekea matatizo makubwa katika jamii ya watu. Ambayo, ndiyo
yatakuwa kwa mara ya kwanza kuonekana. na akazungumzia kutokea kwa magonjwa
mapya ya Wanyama, magonjwa mapya ya mimea ,aina mpya za cancer na milipuko mpya
ya magonjwa.
Kadri tunavyoikaribia miisho ya milenia
ya saba. Kumekuwa na milipuko mikubwa sana ya magonjwa yasiyofahamika. Magonjwa
ambayo yamekuwa ni ya kipekee sana. Baadhi ya magonjwa yamekuwa ni matokeo ya
miunganiko ya magonjwa tofauti tofauti, na udhaifu tofauti tofauti. Hata
kupelekea dalili tofauti tofauti zinazotofautiana kati ya mtu, na mtu.
Magonjwa yasiyofahamika asilimia kubwa
sana ni matokeo ya changamoto zinazoathiri mifumo ya kijenetikia. Kadri mtu
anavyoathiri mifumo hii, anapelekea
madhara mbalimbali yanayopelekea matatizo ambayo huwa hayatambuliki
kabisa katika taaluma za afya. Kwa ufupi sana kuna teknolojia baadhi ambazo
huchochea sana matatizo ya kijenetikia. Na hizi ni matumizi ya bidhaa za G.M.O,
na teknolojia za kisasa za kubadili chembechembe za jenetikia ‘’genome’’ za
watu.
Sehemu hii tutaangalia kwa ufupi sana msingi wa uharibifu huu kwa teknolojia hizi zote mbili..
KUPATA FULLCOPY WASILIANA NASI KUPITIA
Email: brightonshoo7@gmail.com
Dr. Brighton Shoo, (+255)7406 109 88
Softcopy price, 7000/=Tsh
Hardcopy Price, 12000/=Tsh
YALIYOMO
JAMII MPYA, NA HALI MPYA ZA KIMAISHA
KUZALIWA KWA HALI KUU MBILI ZA KIMAZINGIRA DUNIANI.
Tofauti za Kijiografia Zilizochochea Biolojia za Kanda hizi
KUINUKA KWA KILIMO KATIKA BONDE LA ASIA-ULAYA, NA AFRIKA KASKAZINI
KWANINI KILIMO KILISHAMIRI ULAYA-ASIA + AFRIKA KASKAZINI, NA HASA BONDE LA RUTUBA?
SABABU ZA KUSHAMIRI KILIMO KATIKA UKANDA HUU
KILIMO NA KUKUA KWA KASI KWA ULAYA-ASIA NA AFRIKA KASKAZINI
WANYAMA WAKUFUGWA NA MAZINGIRA
UGONJWA YA VIMELEA VYOTE NA WADUDU WADOGO’’
UTENDAJI WA KIJENETIKIA ULIOLETA TATIZO KWA VIUMBE WENGINE
Wanapodanganywa watu kuhusu ‘’mutations!!
Mfano wa mabadiliko hatarishi ya vimelea
KUPANDIKIZA WANYAMA ‘’IN BREEDING’’
VIMELEA NA MAGONJWA YA WANYAMA
UBORA WA VIMELEA NI UDHAIFU WA WANYAMA
MAGONJWA YA NYANI, POPO, NA PANYA
VIMELEA HATARI WENGI ZAIDI HUFA
VIMELEA, WANYAMA, MAZINGIRA NA BINADAMU
NJIA ZA AWALI KABISA ZA MAAMBUKIZI
MSINGI WA SAYANSI ZA MADAWA YOTE
Kwanini mimea baadhi ina madawa?
SIRI YA TEKNOLOJIA ZOTE ZA MADAWA NA MADAWA YA KISASA
CHANZO CHA KUFELI KWA MADAWA YOTE
VIMELEA VINA MAARIFA KULIKO DAWA
Namna Kuu Nane za utendaji wa Madawa
Namna Vimelea vinazishida Dawa Akili
JE MFUMO WA AFYA UNAWEZA KUOKOKA?
SUMU NI HATARI KULIKO VIMELEA.
SUMU NI ZA KITAALAMU ZAIDI YA VIMELEA
SHIDA NANE ZA SUMU ZISIZOTIBIKA
MAGONJWA KUMI YA SUMU YASIYOTIBIKA
HATMA HATARISHI KABISA KUHUSIANA NA ONGEZEKO LA SUMU
KWANINI MADAWA MENGI YANAZIDI KUFELI ZAIDI
Mshindi wa Nobel prize George Ward
MATUMIZI YA BIDHAA ZA G.M.O ‘’UKOLONI WA AFYA USIO NA KINGA’
HISTORIA NA STORI KABLA YA SAYANSI YA UUAJI WA G.M.O.
UDANGANYIFU MKUBWA WA MIFUMO YOTE YA FAHAMU
SAYANSI YA UDANGANYIFU NA UUAJI HATARI ZAIDI WA BIDHAA ZA MABADILIKO YA KIJENETIKIA
G.M.O ‘’GENETIC MODIFIED ORGANISMS
MSINGI KATIKA KUELEWA SAYANSI GENES!!!
KUHAMISHA GENES KUTOKA KWA KIUMBE MMOJA KWENDA KWA MWINGINE
MFANO WA MAAJABU YA HII TEKNOLOJIA
kuchelewesha kifo kwa msaada wa genetic engineering!
SAYANSI YA MOTO KATIKA UJENZI WA KIJENETIKIA INAYO UMBUA WATAALAMU WA G.E
kuegemea katika nadharia zilizopitwa na wakati
uwepo wa chembechembe zinazoitwa ‘’spliceosomes’’
molekuli za kusapoti protini!!
uwepo wa viboresha protini ‘’chaperones’’
Namna kadhaa za kuingiza genes katika DNA
kufeli kwa dawa ‘’antimicrobial resistance’’ na kusambaa kwa genes mpya
shida ya switch za kijenetikia ‘’promoter ‘’
G.e na kuamshwa kwa hatari zilizolala
madhara ya kusambaa kwa genes hatari
Kuhusu Kirusi Wa Camv Promoter
kuharibu mfumo mzima wa uhusiano wa mwili
kuharibu mfumo wa code za mwili
kujaa kwa genes mbalimbali‘’gene stacking’’
kubadili viwango vya virutubisho kwa mimea
matatizo ya kibinadamu na giza la maarifa
matatizo ya kwanza kabisa ya kimtazamo yaliyoathiri hata wataalamu wa leo
MISINGI YA KUZINGATIA KABLA YA KUELEWA ‘’GENOME EDITING’’
Mtazamo Uliopitwa Wakati Wa Mendel Wa Mwaka 1856-1863
Upana Wa Kijenetikia Tofauti Na Mtazamo Wa Mendel ‘’Waddington’’ 1957
Hakuna Uhusiano Wa Moja Kwa Moja Kati Ya Gene Na Sifa Fulani ‘’Thomas Woodward Na James P.Gills’’
Msingi Wa Kuelewa Unaoitwa ‘’Weismann Barrier’’
Mtazamo Uliopitwa Na Wakati Wa Dna Kama Msingi Wa Maisha. ‘’Genetic Determinism’’.
lengo la kuwadanganya wengi juu ya dna
TEKNOLOJIA YA KUBADILISHA GENES ZA VIUMBE ‘’GENE EDITING TECHNOLOGY’’
‘’START OF HUMAN GENOME EDITING’’
Namna Dna Inajiponya Au Poneshwa Baada Ya Kuikata Kwa Kutumia CRISPR CAS 9
wanabiolojia wanavyotumia mbinu hizi kuingiza genes zao wanazozitaka kwa kiumbe
Umegundua Namna Dna Yako Inavyoweza Danganywa
faida za hii teknolojia ya kuedit gene ni zipi
Hatari Za Sayansi Ya Mabadiliko Ya Kijenetikia Kwa Jamii Za Binadamu
Daktari wa China aliyebadili genes za mtoto
MATATIZO HALISI YA TEKNOLOJIA YA KUEDIT GENES ZA WATU
Yanaharibu Na Kuhatarisha Kuliko Watu Wanavyojua
Yanahatarisha Kuharibu Vizazi Vya Watu Kama Watu Wabaya Wataamua Kuharibu Jumuiya Kubwa
NAMNA ZA KISASA ZAKUUA HARAKA SANA UBONGO
Kuchochea Uzalishaji Mkubwa Wa Homoni Za Msisimko ya Ubongo
Kwanini Jamii Itapasuka ‘’Collapse’’?
Hatma ya filamu, magemu, na mipira
MAGONJWA YA KUELEKEA KUFELI KWA DUNIA

Join the conversation