MAKOSA MAKUBWA GYM & MAZOEZINI?
NONDO YA 4
Ijapokuwa wengi hushinda gym na katika vituo vya mazoezi wakifanya aina mbalimbali za mazoezi, wengine kwao mazoezi ni ajira kabisa. Lakini kama nilivyosema awali, mwili Wala asili haitambui mazoezi, mwili unatambua shughuli za misuli ambazo zinahusiana na Biolojia yake ya kuweza kuishi "survival'. Kama ambavyo Mamba ana misuli mikubwa sana ya mdomo Kwa kuwa huishi Kwa kuwinda Kwa mdomo wake, wanyama Wala Mimea huwa na Nguvu sana ya miguu ya nyuma kama namna yao ya kujilinda Kwa kupiga mateke, au namna yao ya kubeba uzito wao mkubwa zaidi wa matumbo. Wanyama Wala Nyama huwa na misuli yenye Nguvu sana ya miguu ya mbele, shingo, na Taya zao kama namna ya kuangusha, Kuvuta, au kutafuna. Vipi kuhusu Binadamu?
Asili kibiolojia inamtambua Binadamu kama Mkimbiaji "Marathoner' Kwa asilimia karibia 70%, huku zilizobakia 30% ikimtambua kama mnyakuaji au mbebaji "splinter". Binadamu hukimbiza wanyama anaowawinda Kwa umbali mrefu sana bila kuchoka, au kuzidiwa Kwa Joto Kali, na Kisha akishawakamata huwabeba Kwa kuwanyakua ili kuwarudisha nyumbani. Tofauti ya Binadamu na Sokwe ni kuwa, Binadamu ana asilimia ya tishu za ustahimilivu wa kazi "type-1 fibres, au slow twitch muscles" Kwa asilimia karibia 70%, Wakati Sokwe huwa asilimia 67% akiwa na tishu za mlipuko wa Nguvu "type -2 fibres au fast twitch muscles ". Hii unaweza iona Kwa namna sokwe wamekatia misuli zaidi ya Binadamu, na huku wakiwa na mikono mikubwa zaidi ya miguu, kama namna asili imewafanya wapanda miti haraka sana shida inapotokea. Binadamu Wana miguu mirefu zaidi ya mikono, na hawana misuli sana yakukatia Kwa kuwa "type-1 fibres" hufanya misuli kutoonekana mikubwa sana.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema, asili inamtambua Mwanadamu anayefanya shughuli za misuli za kukimbia, na shughuli za kunyakua. Watu wote watakaofanya shughuli hizi kupitia kazi zao, au kupitia mazoezi, hunufaika sana. mazoezi ya kunyakua -uzito "Weight lifting' yameonyesha matokeo makubwa Sana katika afya ya Wana mazoezi, hasa katika kushusha hatari ya kuzidi Kwa uzito, kujaa Kwa mafuta mwilini, kudhoofika Kwa misuli, na kuboresha afya hata Wakati wa Uzee Kwa kufanya uimara wa mwili. Mazoezi ya Kukimbia "Cardio' yanafahamika Kwa Karne Kwa faida yake kubwa zaidi ya kuvunja mafuta, kuboresha afya ya Moyo na mapafu, na kuufanya mwili kuwa na ustahimilivu sana wa kazi "endurance'.
Tafiti zimeonyesha watu ambao hufanya mazoezi haya Kwa pamoja hunufaika zaidi ya wanaofanya aina Moja tu ya Mazoezi. Na Sababu ni kuwa Binadamu tayari ameumbwa kufanya aina hizi zote za shughuli za misuli. Kama mtu atakimbia au atatembea tu, atapungukiwa "type-2 fibres' ambazo hujenga uwezo wa misuli kuwa na Nguvu na ukubwa ambao huifanya isiishe haraka unapozeeka "Sarcopenia". Lakini kama mtu atanyakua tu uzito, hatakuwa Bora katika ustahimilivu na mfumo imara zaidi wa mapafu Kwa kazi endelevu.
Ufanywaji wa mazoezi haya huambatana na aina nyingine ya Mazoezi inayoitwa "High intensity interval training, au HIIT". Hii ni pale mtu anapoweza Fanya kazi Walahu dakika 4 akitumia Nguvu zake zote, bila kuzungumza au kuhemea mdomo, na Kisha kutumia Tena dakika 4 akifanya Kwa kutulia. Hii ni kama mtu angekimbia Kwa dakika kadhaa Kwa spidi kubwa sana hata kuhema Kwa shida, na Kisha kukimbia zingine kadhaa akitulia. Tafiti zimeonyesha namna hii ya utendaji imeonyesha hata ikifanywa mara Moja Kwa wiki hufanya watu kuwa na mfumo imara sana wa Moyo, mapafu, misuli, mifupa, na hata Ubongo Kwa miaka mingi sana. Ukiwa makini utagundua hii Ndiyo namna wawindaji hufanya wanapomkaribia mnyama. Wanawake huweza kuishi miaka 3 zaidi ya wenzao wasiofanya. Wanaume huweza kuishi miaka 4 zaidi ya wenzao wasiofanya. Dakika 90 za mazoezi haya ndani ya wiki hupunguza hatari ya Kifo toka sababu yoyote ile Kwa asilimia 15%.
Changamoto kubwa ambayo huwapekea wanamazoezi wengi pia kutonufaika na Mazoezi yao, ni kutoelewa kuwa mazoezi ni namna ya kukuwezesha kufikia malengo yako, na Sio Malengo kuwa nyuma ya mazoezi. Watu walikimbia ili wapate Chakula, hivyo hawakujitesa kushindana na jambo lisilo uhalisia wao. Kazi zao zilikuwa ni mazoezi hivyo hawakuwa wakishindana dhidi ya wao wenyewe. Watu wengi hawaelewi kwanini wanafanya mazoezi wanayofanya, ni kama wanajilazimisha kukimbiza upepo. Na hii Ndiyo sababu wapo wengi wanaojilazimisha kukuza sana misuli yao ilihali maisha yao hayahitaji ukubwa sana wa misuli yao.
Kibiolojia kazi za misuli hupaswa kufanywa zaidi asubuhi, lakini wengi hufanya zaidi Wakati wa jioni na usiku. Hawa huanza kutengeneza matatizo makubwa zaidi, maana baada ya Mazoezi huitaji kula sana Usiku jambo ambalo Sio sahihi. Hufanya mazoezi katika taa za usiku ambazo huua zaidi mfumo wa "Mitochondria', Kwa kuwa "Blue light' hubadili "oxidation state' ya madini Chuma kuwa "Fe3+' katika Hemoglobin' , jambo ambalo huifanya ishindwe kubeba Oksijeni, husisimua "HIF-1 alpha', na haya yote hupelekea "Mitochondria' kufa zaidi, na mwili kujawa zaidi Kwa kemikali sumu 'free radicals', maana msafishaji mkuu "melatonin' huzalishwa na "Mitochondria' Kwa asilimia 80%. Hili linaweza kukueleza kwanini watu wengi wa "Gym' kama "Bodybuilders' hufa mapema sana, Tena miaka 35 tu nyakati kadhaa.
Haimaanishi watu wasifanye mazoezi haya, Kwa kuwa tafiti zinaonyesha pia kama Mzee wa miaka kuanzia 60+ atashindwa kufanya vizuri katika mazoezi ya " Simama -kaa', ana wastani wa kufa mara tatu zaidi haraka ya mwenzake anayeweza. Kama watu watakuwa Wana uwezo wa kufanya mazoezi ya "Squats' ya kusimama na kuinama, inamaanisha mpaka watakapozeeka hawatashindwa kusimama baada ya kukaa, hawatashindwa kusimama baada ya kwenda Chooni, na faida zingine zote. Tafiti zimeonyesha Kuna uhusiano wa Moja Kwa Moja kati ya uwezo wa Miguu na Urefu wa maisha "Lifespan'. Watu wenye miguu imara huishi zaidi maana huweza kubeba miili yao Kwa maisha yao yote. Pia tafiti zinaonyesha Kuna uhusiano kati ya uwezo wa viganja vya mikono na urefu wa maisha "Grip strength'. Hizi zote zinathibitisha kuwa kwa kutojishughulisha kimisuli watu hufa haraka sana.
Faida Moja ya kujua Hisabati ni kuweza kugundua Njia ipi ni fupi zaidi kati ya Njia nyingi sana. Kati ya hasara zinazoweza tokana na kufanya mazoezi na hasara zinazoweza tokana na kutofanya, na kati ya namna za kupunguza changamoto za ufanyaji mazoezi, na namna za kupunguza changamoto za kutofanya mazoezi, ni dhahiri kuwa ufanyaji wa mazoezi haya wa Gym na Mazoezi ya 'Cardio' kama kukimbia, Kwa Busara ambayo nimeshaonyesha namna ya kuifuata kibiolojia, una faida zaidi.
Mwanamazoezi anapaswa kusikiliza zaidi sauti ya asili na mazingira yake. Ni vema kuwa na kiasi, kulenga muda sahihi, kupunguza urudiaji "Big Volume', Wana mazoezi wa kisasa wanaofatilia tafiti za kisayansi wanatambua unaweza kwenda "Gym' mara mbili tu, au mara 3 tu Kwa wiki, na kufanya "sets" chache sana Kwa kipindi kisichozidi hata dakika 60, na kuwa na matokeo makubwa zaidi ya wajinga wengi wasioelewa asili Haina shughuli ya kukufanya urudierudie mara 100+ msuli mmoja.
Maajabu makubwa zaidi ni kuwa, watu wanaoishi maisha marefu zaidi Sio watu wanaofanya sana mazoezi, au wanaokula vizuri sana baada ya Mazoezi, au waliokatia sana Kwa mazoezi, ni watu wenye maumbile madogo sana "Centenarians', mfano wayahudi katika taasisi ya "Albert Einstein', au Wajapani na Wachina ambao huongoza Duniani Kwa kuishi miaka wastani 84+, huku wengi wakivuka miaka 100 wakiwa imara kabisa bila misuli mikubwa.
Kwa mtu aliyesoma hii blog toka nilipoanza ameshagundua Wachina hufanya kazi zao haraka haraka, hutembea Kwa miguu wanapoenda kazini maranyingi, Japani inaongoza Kwa kuzalisha Magari lakini inaongoza Kwa matumizi ya baiskeli na watembea miguu. Kiufupi Siri Sio Mazoezi, Siri ni kazi za kushughulisha misuli maana hizo ndizo zitakufanya ufanye mazoezi bila kujilazimisha, Kwa kiasi, mwili utajipangia wenyewe ukue Kwa kiwango sawa na uhalisia wa mazingira yako, Sio kujaza misuli ambayo Haina kazi zaidi ya kupost Picha mitandaoni.
Nilipokuwa jeshini niligundua mazoezi mengi yalikuwa katika namna ya maisha ya Kambini, tulivaa viatu vizito miguuni, tulibeba maji kupandisha milima kwenda kumwagilia mazao, tulibeba mafolonya kufyatua tofari, tulinyakua miguu na mikono katika kwata tukijifunza Silaha, tulikimbia ili tukachukue kuponi ya Chakula, tulipiga push ups kama adhabu, au sessions za burudani, kiufupi hatukuwa na session za kunyakua -uzito bila malengo, na tulikuwa imara tukiwa na maumbile sahihi sana Kwa mazingira yetu. Na hii Ndiyo sababu Wana mazoezi kama Messi au Ronaldo, huwa imara sana Kwa kuwa hufanya mazoezi kuanzia asubuhi Kwa malengo maalumu ya kwenda kushindana uwanjani. Unaweza jifunza namna hii kupitia kufanya mazoezi maalumu Kwa malengo maalumu. mfano kutaka kuwa na uimara wa kusimama Kwa kufanya squats, kutaka kuwa uwezo wa kunyakua uzito wa kilo kadhaa Kwa kufanya "bench press', kutembea Kwa miguu kwenda sokoni, n.k. namna hii ya Mazoezi iliyoelekezwa katika kusudi maalumu ni Njia Bora zaidi ya kuwa na kiasi na dira, inafanana asili.
...............
Pata Full document


Join the conversation