Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SIRI YA KABICHI, BROCOLI, & VITUNGUU KUJIFUNIKA

Siri ya kabichi, broccoli, vitunguu, na mchicha

Kwanini Kabichi, na Brocolii huwa na asili ya kujifunika?

Mimea hii ambayo hufanana asili ya familia zake, yote kijiografia imetokea kwenye asili ya maeneo ya baridi kali, mionzi mikali ya UV, na mazingira magumu yenye chumvichumvi. Mimea hii hupambana sana kulinda maji kwa kujifunika kutunza mvuke kwa Kichwa kilicho ndani, na kuacha sehemu ya kijani zaidi yenye chrolophyl kwa nje, ili kutengeneza chakula toka kwenye mwanga ambacho huenda kutunzwa kwa sehemu ya ndani.

Mimea hii huwa na kiwango kikubwa sana cha Vitamini U, au ‘’S-Methylmethionine, hii huiwezesha kuzalisha seli zake haraka sana, na hata kujiponesha haraka tishu zake zinapoharibika. Majani ya ndani maranyingi huwa na caretonoids na chrolophyl kidogo, na huwa na kemikali ‘’polyphenols’’ za ‘’anthocyanins’’ kwa kabichi nyekundu kwa lengo la kujikinga na mazingira ya stress. Kipindi watu huiona kabichi kama mboga iliyopoa sana, kibiolojia ni mmea wenye mkakati mkubwa sana, hata wadudu wengi hushindwa kuiathiri kwa kuishia tu kushambulia Maganda ya nje. 

Kwanini Vitunguu huwa na rangi ya wekundu, na ukali?

Vitunguu huwa na kiwango kikubwa sana cha kemikali zinazoitwa ‘’anthocyanins’’ ambazo huifanya kuwa na rangi ya wekundu. Kemikali hizi huifanya kuwa imara kuweza kustahimili mazingira ya stress, ambayo ndiyo asili ya jiografia yake ilipotokea maeneo ya kaskazini ‘’Egypt’’, na ukanda wa kuizunguka ‘’Iran’’. Kutokana na kushamiri kwake pia ukanda wenye baridi kali sana, anthocyanins huisadia pia kutoganda maji yake. 

Vitunguu huwa na kiwango kikubwa sana cha madini ya ‘’sulfur’’. Haya huifanya kupitia vivunjaji kadhaa ‘’enzymes’’ kuzalisha asidi ‘’sulfuric acids’’, ambayo hutengeneza hisia za ukali na kuwakimbiza Wanyama. Vitunguu navyo huwa vikizunguka shina lake kwa lengo la kutunza maji, na hujifukia ardhini kupambana na mionzi ya UV.

Kwanini Mchicha una wekundu ukiwa imara zaidi ya Chainizi?

Wekundu wa mchicha unatokana na chembechembe ‘’polyphenols’’ za ‘’Anthocyanins, na betalains’’. Hizi huwa maalumu kwa ajili ya kupambana na mazingira yenye stress kama ukame, jua kali, n.k. Mchicha kwa kuwa na kemikali hizi, kiwango kikubwa cha madini ya calcium, na Potassium, huweza kudumu mazingira ambayo chainizi hushindwa kwa kuwa chainizi nyingi ni matokeo ya ‘’selective breeding’’, hivyo nyingi huwa hazina kinga.