JE NGURUWE, BATA, KAMBARE NI NAJISI KISAYANSI?
Je kuna sababu za kisayansi za Kutokula Nguruwe, Bata, Kambare, kama Walawi 11?
Wapo Wanyama wengi sana ambao ukila tu unaweza kufa papohapo, mfano; Samaki puffer, Chura ‘’golden poison’’, Ndege ‘’Hooded pitohui’’, n.k. Hawa nimeanza kwa kuwaorodhesha awali kabisa ili kuonyesha Sio kila kitu cha kula kama wengi wanavyojidanganya. Tulipokuwa tuliangalia Mimea pia tuliona kuna mimea ukila unaweza kufa moja kwa moja, na hata Wanyama tuliona huchagua sana, hasa ‘’nightshades plants’’.
Wanyama wote waliozuiwa kuliwa katika Walawi 11 ukifuatilia utagundua hoja zifuatazo; kwanza wengi wao huishi katika mazingira yenye uchafu ‘’vimelea wengi sana’’, au kiwango kikubwa sana cha sumu. Nimekuwa katika mazingira ya ufugaji wa nguruwe nafahamu namna nguruwe hula katika mazingira machafu sana, na pia nilikuwa muopoaji sana wa Samaki, na nafahamu namna Samaki kambare ‘’cat-fish’’ huweza kudumu katika tope kabisa, na hasa katika madimbwi ya maji machafu, ambayo Samaki wengine wote hufa.
Nyumbani pia tulifuga sana Bata, niligundua kuwa bata nao walikuwa na uwezo wa kudumu katika mazingira machafu ambayo kuku hushindwa.
Nilipozidi kusoma sayansi, na hasa za Wanyama, na kuelewa siri nyuma ya fiziolojia na metabolikia, ndipo nilipoanza kugundua kuwa kuna uhusiano mkubwa sana wa kiwango cha mafuta yaliyomo kwa kiumbe, na sumu, au stress zinazomsibu. Binadamu akiwa na stress sana, sumu sana kama za unywaji wa pombe, soda, au sukari za bidhaa za kisasa, ataanza kunenepa sana, kuanzia Ini ‘’fatty liver’’, jambo ambalo wasomi wadogo hupeleka lawama kwa ‘’LDL-cholesterol’’, lakini kumbe mwili huongeza mafuta kama namna ya kujilinda na sumu.
Ubongo una mafuta mengi sana maana unajilinda zaidi na sumu kutokana na metabolika kubwa sana yenye hatari ya kuzalisha kemikali sumu nyingi ‘free radicas’’, au za kutoka ‘’UV’’. Mwili wa binadamu huwa na mafuta mengi sana katika jointi kumaanisha unajilinda na hatari za msuguano, na ndivyo hata seli za mwili hulindwa na ukuta wa mafuta ‘’phospholipids’’.
Wanyama wengi najisi kwa mtazamo wa walawi 11, ukianza na nguruwe, bata, na hata Samaki kambare, huwa na kiwango kikubwa sana cha sumu hizi kutokana na mfumo wao wa ulaji, na maisha yao. Nguruwe wengi wanaofugwa ni matokeo ya teknolojia za ‘’breeding’’ zilizofanywa zamani sana, ambazo ziliwafanya kuwa wadhaifu na kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta kama namna yao ya kujilinda. Wengi wao hulishwa pumba ambazo huwafanya kuwa wanene zaidi kwa kuwa huwa zina wanga nyingi, na mafuta mengi ya omega-6 ambayo yote huwa hatari. Na hii ndiyo huwa pia kwa Kuku wa broiler ambao hula pumba, hukesha usiku kwenye taa ili washindwe kutoa sumu zao mwilini kwa kukosa kulala, na matokeo yake hunenepa zaidi.
Pichani Niko nikitazama Hali za kiafya za kuku-broiler, wengi wao huwa na mafuta mengi sana na shida za kimetabolikia.
Samaki kambare ambaye naye hula wenzake huwa na mafuta mengi sana kama namna ya kupambana katika mazingira hatarishi zaidi kwa Samaki wengine. Ulaji wa samaki wengine huwa-Fanya viumbe kuwa na sumu nyingi zaidi na protini nyingi zaidi jambo ambalo hufanya hata wengi wa wanyama Wala Nyama kutoliwa kutokana na uchungu wa Nyama zao, au hata hatari ya kiwango kikubwa Cha Sumu na vitamin A katika maini yao.
Ushawahi jiuliza kwanini ni hatari Kula nyama au ini la Simba au Paka? Pichani Niko na Paka wangu anayeitwa "Chino'
Hivyo kwa mtazamo wa kwanza kabisa, ulaji wa viumbe hawa najisi huwahatarisha sana watu kwa kuwaongezea kiwango kikubwa sana cha vimelea wanaoweza shindwa wamudu, au kiwango kikubwa cha sumu, na hata kiwango cha mafuta ya omega-6 ‘’linoleic acids’’ ambayo huwa kwa wingi zaidi kwa Wanyama hawa, na hii ndiyo sababu mafuta ya nguruwe huwa hayagandi sana kama mafuta ya Wanyama wengine. Kumbuka, awali nilisema viumbe wala nyama wote kwa asili ni wasafi, na wana asidi nyingi sana tumboni kumaanisha hawana uwezo mkubwa wa kupambana na vimelea wengi kama walio kwa Wanyama hawa.
Kipindi watu kadhaa wanaweza hisi mpaka waone tatizo maalumu kama minyoo ya ‘’Taenia solium’’ toka kwa nguruwe, inayoweza penya kwenye tumbo mpaka kwenye Ubongo, sayansi ya kisasa haiyatazami matatizo katika mfumo wa uhusiano wa chanzo na tatizo moja kwa moja, inatazama kwa mtazamo wa uhusiano wa vitu vingi, na ndiyo maana sumu ni tishio sana kuliko vimelea.
Sababu ya pili ni changamoto ya nishati.
viumbe wengi ambao Walawi 11 inaonyesha kutokuliwa pia ni Wanyama ambao huwa sio walaji wa kwanza. Unapokula majani unaanza na kula chakula chenye nishati asilimia kubwa zaidi. Unapokula nyama ya ng’ombe unakula mlaji wa pili, ambaye angalau ana nishati ya kukutosha. Wanyama najisi wengi wapo hatua ya tatu, mfano; Mbwa, paka, nyoka, simba, n.k. Wanyama hawa hata nyama zao huwa chungu kwa kuwa kwa ulaji wao wa Wanyama, huwa na kemikali nyingi za ‘’Nitrogen kama Urea, ammonia, na alkaloids’’. huwa na kiwango kikubwa cha vitamin A katika maini yao ambayo inaweza kuwa sumu, na huwa na enzyme za ‘’lactic acid’’ ambazo ni hatari kwa mlaji, na nyama yao huwa na nishati kidogo sana, na watu huwa tu hawapendelei kuzila.
Wanyama ambao hawacheui ila hula nyasi ‘’hindgut fermentors’’, mfano Tembo, farasi, na sungura, wengi wao tumbo lao la kwanza huwa kama la Wanyama wala nyama, hivyo hufyonza sukari nyingi sana ‘’Glucose’’ baada tu ya kula nyasi, na hii huwafanya kuwa na nishati sana za misuli kwa kuwa na ‘’Glycogen’’ nyingi sana.
Pichani Niko nyuma ya Tembo tuliyemlaza Kwa dawa za Usingizi Kwa utafiti zaidi.
Shida yao huanza huwa na ufanisi mdogo sana wa kuvunja kambakamba ‘’cellulose’’, huwa na ufanisi wa asilimia 45-60% tu, tofauti na wanyama kama ng’ombe ambao hufikia asilimia mpaka 75%. Ili kuepuka tatizo hili huwabidi kula sana, muda wote, huku sungura kwa kushindwa kabisa, na hatari ya kupungukiwa vitamin B-12, hubidi kula kinyesi chake ili akivunjevunje tena. Wanyama hawa ukiwaangalia kikemia ya misuli yao, kwa namna hutunza sana Glucose kama glycogen hata kufanya misuli yao kuwa na nyama isiyo na mafuta sana ‘’lean’’, mafuta mengi yasiyoganda ‘’PUFAs-Omega 3 ‘’alpha-linolenic acid’’, moja kwa moja wanaonyesha wanafanana sana na wanyama wala nyama. Misuli yao ipo kwa ajli ya shughuli kama safari ya ghafla, haipo kama chanzo kizuri cha chakula. Na hili linathibitishwa kwa ‘’IQ’’ yao ambayo huwaonesha kuwa na akili za kijamii kwa uwezo chini kidogo tu na Mbwa, simba, na juu ya Paka, na Sungura.
Farasi na hata punda anazitambua sura za mmiliki wake, anaweza zungumza kwa alama, na huwa na kumbukumbu pia za mazingira, watu, na hatari, kumkaribia kabisa mbwa.
Hoja hiyo inapelekea hoja ya tatu, ‘’tunakula ili tuishi, au tunaishi ili tule’’. Maisha ni zaidi ya chakula, uhusiano wetu kijamii kati yetu, kati yetu na Wanyama, na kati yetu na mazingira ni wa muhimu sana. Kama hoja ya kula itajikita asilimia 100% juu ya kile tu unachoweza kivunja na kukila ukaishi, hata nyama ya mtu inaweza kuliwa, na wala si ajabu imesharekodiwa sana katika historia, na hata Biblia, kama nilivyoonyesha awali. Wanyama wote waliozuiwa kuliwa pia ni Wanyama wenye akili sana kufanania Binadamu. Uwezo wao wa kijamii, na utambuzi wao wa stress kijamii, huwa ni mkubwa sana.
Pichani ni wanyama wenye akili zaidi kutoka takwimu za Sayansi za wanyama.
Kwanini Ule Samaki kama Dolphins ambao wanajua hata Kuzika na kuomboleza mwenzao anapokufa. Kwanini ule mnyama kama Tembo ambao wanajua familia, uchumba, huomboleza msiba, na hukumbuka tukio hata kwa miaka zaidi ya 10. Kila kitabu cha shule ya msingi cha Kiswahili kina stori inayoonyesha sungura ni mwerevu, mwana mikakati, na fisi kuwa ni mla mifupa, msafisha dunia, na huweza kula mizoga yenye maelfu ya vimelea, na madini mazito. Kipindi unapomkata Samaki perege hufa maramoja, lakini Samaki kambare hukatwa lakini hudumu kwa maumivu asife hata kama ameshatenganishwa kabisa.
Na hii sayansi ya uhusiano wa maumivu, akili za kijamii, na unajisi ndiyo msingi wa Nguruwe kuwa na akili sana tena akiwa na Ubongo wa kumfanania sana Binadamu, hata timu ya Elon musk ya ‘’Brain-computer interface’’ kuwatumia kutest vipandikizi vyao vya ubongo ‘’Brain implants’’.
Nguruwe hukumbuka jina analopewa akiwa mdogo haraka zaidi ya mtoto wa binadamu. Nguruwe hulia kwa maumivu makali sana wakati wa kuchinjwa kwake. Sio tu nguruwe aliye najisi mwenye akili sana, hata Nyani ambaye husemwa ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni, au Kunguru, ambao hukariri mpaka sura za watu. Au hufanya uchunguzi wa nini kilichomuua mwenzao. Kiufupi Si vema kuua viumbe ambao hisia zao za utambuzi wa maumivu, na uhusiano wao wa kijamii ni mkubwa sana. Kuna namna nyingine nyingi za kushirikiana nao. Na hata kwa Wanyama wengine, namna nzuri zaidi zipo za kuwawinda kwa kutumia njia za kuwapunguzia maumivu, kwa kuwapoteza fahamu, kama ambavyo Wanyama wala nyama hufanya kwa kuwanyonya damu na kuwafanya wapoteze fahamu kwa ‘’hypoglycemia, na cerebral shock’’, kabla ya kuanza kuwala.
Kama Mtaalamu wa wanyama nimekuwa na muda mwingi sana wa kugundua yapo mengi sana watu wasiojua kuhusu wanyama ukiachana na Utamu wa Nyama zao








.jpg)



Join the conversation