Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Mwafrika Haitaji Serikali Kibiolojia

Mwafrika Haitaji Serikali Kibiolojia

 Mwafrika Haitaji Serikali Kibiolojia

Mwafrika alikuwa bora sana kiafya, na hata kimazingira baada ya kugunduliwa Bara la Afrika na wakoloni. Lakini baada ya kuendeleza Serikali ambazo zilikuwa ni mnyororo wa ukoloni ulioshikiliwa na Waafrika wenyewe, kila kitu kikaharibika kwa kuwa badala ya kurejea katika hali yao ya awali na kuiboresha zaidi, Viongozi wote wakaanza kupambania falsafa wasizozielewa, huku wengi wao wakionekana aidha ni waraibu wa mamlaka, au mfumo wa maisha mapya na tamaduni za ukoloni, au bado hawajawa werevu wa kugundua Afrika haiwezi kuwa kama Ulaya maana Afrika sio Ulaya. 

Afrika haiitaji serikali maana kero zote za Afrika za kiuchumi na umasikini, zinatokana na dhiki kubwa za kuwekeza katika mambo ambayo kibiolojia hayana faida kwa Waafrika, yanawamaliza tu. Kilimo kikubwa wanacholima sio kwa faida yao, wanaua tu Ardhi zao kwa mbolea za kisasa, sumu za magugu zinazoathiri mpaka vyanzo vyao vya maji na samaki, mfano; RoundUp zenye kemikali sumu ya ‘’Glyphosate’’ zinaathiri sio tu mimea yote, bali mpaka bakteria walio katika udongo, na tena hata walio tumboni zaidi ya trilioni 30. Bado dawa hizi na zinginezo kama 2,4 D, au Atrazine, hufanania homoni za mwili, na matokeo yake huwaathiri zaidi Waafrika. ‘’Glyphosate’’ iliyo kwenye Dawa ya kuua magugu ‘’RoundUp’’ huvuta na kutawanya madini yote yaliyo katika matendo ya kuzalisha nishati, hii huitwa ‘’Metal chelation’’, na hiki kitendo humaliza kabisa mfumo wa nishati mwili na kuchochea kemikali sumu mwilini.

Waafrika ukiwa makini kuwaangalia kila wanachopambania Kuwekeza hakina maana yeyote ile kwao, ndiyo maana unaweza kuta Binti wa Kiafrika anapaka na yeye ‘’Sunscreens’’, au ananunua mafuta ya gharama kujichubua ‘’Creams za Ngozi’’, yaani anachezea ‘’melanin’’ iliyo msingi wa biolojia yake. Waafrika wanawekeza kwenye Taasisi na Majumba makubwa sana ya thamani, yanayowagharimu Mabilioni na mamilioni ya fedha za wakulima wadogo wanaowalalia kupitia kodi zao; kwa kuwa wanatumia pesa zao kuwekeza kwenye Vitu vyenye maslahi ya wachache, na visivyo na tija, na vitu Mfu, yaani ‘’ni kama kutumia asilimia 90% ya hela ya kula kununua redio, halafu kupambana kwa kujibana sana kumudu gharama za chakula’’. Matokeo yake kwa kulima sana kila mwaka kuziba magepu na madeni, wanaua ardhi zao, wanakufa kwa mitindo hatarishi wasiyoielewa, wengi wao ni wagonjwa wa kiakili kwa stress za maisha.

Kama ningewashauri Waafrika, basi Warejee kuishi katika nyumba zao za kawaida, zilizo za wazi kwa sehemu kubwa, wasitumie kabisa mfumo wa umeme kwa lolote lile mbali na usafiri, au viwanda vya kutengeneza mavazi au bidhaa zisizo na madhara kabisa; hawana haja ya kutengeneza vyombo vya plastic, au mashuka na nguo za Polyesters, watengeneze karatasi za kutunzia kumbukumbu badala ya Softdrives, wasipendelee mavazi ya pamba warejee katika mavazi ya ngozi yanayowaacha wazi kwa sehemu lakini pia yakiwasitiri, waachane na matumizi ya bidhaa zozote zile za vyakula za viwandani, wavae viatu vya ngozi au Leather. kuliko kuvaa Raba au Plastic, ni bora wakatembea pekupeku.

Wasikubali kuingia katika malengo ya kujenga mitambo yeyote ile kama hawajui inawasaidiaje wao katika kiwango chao cha chini kabisa cha maisha yao. Ni muhimu kuwa na miundombinu mizuri ya usafiri, lakini ni muhimu kutoishi maisha ya matabaka, wala kuwa na mifumo Complex ya uongozi isiyo na tija yeyote kwa raia. Hakuna haja ya kulima mazao mengi ya biashara na wanga, au mafuta ya mbegu, warejee katika asili yao ya kilimo cha mazao yao ya asili tu, tena walime kwa kiasi cha matumizi yao tu au na ziada kidogo; sio kilimo ambacho kinaishia kuharibu uoto wa asili, na balansi ya madini katika udongo, na tena ikiujaza makemikali sumu. 

Badala ya serikali moja kubwa, kila kanda za makabila Fulani, au hata kila kabila liwe na serikali yake ndogo kama enzi za Uchifu. Nchi za Afrika ni kubwa, Tanzania moja ni sawa na Israel zaidi ya 100. Nchi za Ulaya zote mfano, Uingereza au Ujerumani, zina uzalendo sana kwa kuwa Nchi nzima huwa ni kabila moja tu, au makabila Manne tu yaliyo Ndugu. Ni rahisi kuwa na Nguvu, umoja, na Upendo, kuliko serikali kubwa zenye Vita kubwa ya ukabila kuliko ya Uchumi. 

Mfumo wa serikali zinazowafaa Waafrika ni ndogo, sio kubwa zilizopo. Tena wanahitaji serikali zisizo na maslahi makubwa kwa viongozi, na Elimu itolewe kwa Dhumuni la eneo husika tu. Vipaji vihamasishwe lakini mtazamo wa jamii ujikite katika kutambua maisha yanahitaji chakula bora, usingizi bora, familia bora, mazingira bora, uhusiano bora na majirani, burudani zenye kiasi, na mwisho ibada kwa imani husika. Na sio mengineyo kama kuwekeza katika majeshi na mabunge, yanini hayo yote kama idadi ya watu ni ndogo, na mnaweza zungumza lugha moja, na kutatua changamoto zote za wenye matatizo. Askari wote wawe wanafahamika, sio askari mzawa wa Manyara awe mlinzi wa watu wa njombe, hatakuwa na Uchungu wa kulinda maana damu ni nzito kuliko maji, na wawe ni wachache. Kuwekeza katika majeshi na mabomu, ni kama kuandika Katiba kwa Kiingereza na wananchi ni wabantu, hizi zote ni Ishara ya makovu ya ukoloni.