Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Je muda wa kula unaathiri afya ya mlaji?

Je muda wa kula unaamua matokeo ya afya ya mlaji

Je muda wa kula unaamua matokeo ya afya ya mlaji?

Kuna mgogoro mdogo kati ya ni upi muda sahihi zaidi wa kula, na hasa ni kati ya wanaoamini muda sahihi ni asubuhi, wengine wakiamini ni jioni, na wengine wakiamini Muda wa kula hauna chochote cha kuathiri metabolikia na umeng’enyaji. Ukweli ni kuwa, kwa mtazamo wa biolojia ya asili, kwa viumbe wala nyama na wawindaji muda sahihi zaidi huwa ni kati ya mchana na jioni. Kundi hili kula huwa baada ya stress za njaa, ambazo huwafanya nyakati kadhaa kula hata kama ni usiku. 

Waafrika kwa asilia huwa hawali sana asubuhi, wengi huwa na nguvu na nishati sana asubuhi kutokana na mwanga kama tutakavyoona mbeleni. hali ya hewa ya kawaida Pamoja na shughuli za misuli kabla ya kujipatia chakula, kama kuwinda, au kukusanya, huwafanya asubuhi kutokuwa na chakula, na kutohitaji kula mpaka baada ya kazi.

Wanyama wala nyasi na wakulima wengi sana walio mabara ya baridi kama Ulaya-Asia, huanza kula mapema, na hula sana asubuhi. Wengi hula asubuhi kwa kuwa huitaji nishati ya kutosha ya kukabili baridi kali, na ya kufanya kazi. Kama ambavyo Wanyama wala nyama hula kidogo na kulala sana kama paka, na Wanyama wala mimea hutembea sana, kula sana, na kulala kidogo kama farasi. Hii inaweza kukueleza kwanini Waafrika wengi hulala sana hata asubuhi, ni kwa kuwa uvunjaji wa protini hasa, na mafuta, huchochea sana kulala tofauti na uvunjwaji wa wanga, ambao huitaji sana kutolala kwa kuwa huitaji sana mfumo wa ‘’ACTH’’ uisisimue tezi ya ‘’adrenal’’ izalishe ‘’cortisol’’ kuchochea kuvunja ‘’glucose’’, au ‘’glycolysis’’. Ni maajabu kuwa Mimea ina wanga nyingi sana na ina rangi pia, kumaanisha ili uile unahitaji mwanga tofauti na protini. Wanyama wala nyama huwa hawaoini rangi vizuri, huona tu ‘’weupe-weusi’’. 

Watu wanaohisi kula kunaweza kuwa muda wowote kiufupi hawaelewi sayansi kwa kina. Mfano mzuri mtu atakaye kula asubuhi mapema sana kama atakuwa katika mazingira ya joto, mwili wake utapunguza ufanisi wa kazi, kwa kuwa biolojia huhamasisha utendaji kazi ili mtu aweze kula, na yeye ameshakula. 

Watu wanaofanya mazoezi baada ya kula huishia kutumia tu sukari waliyotoka kula katika mfumo wa ‘’glycogen’’, wala huwa hawavunji mafuta ‘’fats’’, wala pia huwa hawasisimui sana uimara wa mifupa kupitia homoni ya ‘’GH’’, kwa kuwa asili huamini unapokuwa na njaa asubuhi, unapaswa kuwa na mifupa imara ili ukawinde. Pia watu wanaokula usiku wanga au protini ngumu, huufanya ubongo kuchochea kipaumbele cha damu kuelekea kwa tumbo, na kuathiri mfumo wake wa kutoa kemikali sumu katika Ubongo wakati wa usiku ‘’Glymphatic system’.

Unaweza jifunza zaidi kupitia kusoma kitabu changu Cha "Vita za Vyakula'