JE NI VEMA KWENDA GYM?
Je ni vema kwenda gym?
Wengi wa wafanya mazoezi pia hawajui kwanini wanafanya mazoezi, na hii ni Kwa kuwa kibiolojia Mazoezi Sio jambo linalofahamika. Hakuna katika asili kitu kama gym, hakuna siku utamuona mnyama akikimbia bila sababu eti anapasha. Kabla ya usasa wa vituo vya mazoezi mtu asingeweza pata namna ya kufanya kazi ya kurudiarudia kukunja au kuinua uzito Fulani hata mara 50+ kama wanavyofanya Wana mazoezi Gym. Mazoezi mengi Sio ya asili. Asili Haina namna ya kurudiarudia matendo ya kimisuli ambayo Leo hii huitwa mazoezi.
Kipindi Msomaji wangu mmoja anaweza kubaliana na hoja juu, pia anapaswa kubaliana na hoja kuwa pia asili Haina aina za shughuli za kumfanya mtu akae chini karibia siku nzima. Asili kama ya Afrika haitambui kuwa Kuna uwezekano wa mtu kula Chakula asubuhi kabla ya kazi. Wanyama wote wanatambua inahitaji kazi ya kutembea, Kuvuta, na kukimbiza ili uweze kula. Kiufupi kula ni baada ya kazi. Binadamu ni mnyama ambaye naye anafungwa na Sheria hii.
Kutokana na hoja hizi ni wazi kuwa Binadamu ameshaingia katika mfumo tofauti na asili yake. Na Kwa kuwa Binadamu ameshajitenganisha na asili yake, hakuna namna anaweza kukimbia madhara ambayo ndiyo udhaifu, magonjwa, mateso, na vifo vya taabu. Sikuandaa blog hii ili kutabiri anguko la Binadamu, Lengo langu ni kutumia Busara tuliyopewa na Mungu kuonyesha ni mambo yapi ambayo tunaweza yafanya kupunguza madhara ya Mfumo huu dhaifu wa Maisha.
Kuelewa Kwa kina undani wa hoja hizi unapaswa kurejea ngazi 6 za uelewa#
NGAZI YA 1
Tambua kuwa asilimia 85% ya magonjwa sugu yote yanahusiana na shida katika mfumo wa nishati wa mwili "Mitochondria diseases", hii imeonyeshwa na Mtaalamu Doug Wallace. Pili ni muhimu kutambua kuwa Kiini cha magonjwa sugu yote kinaanzia katika shida za sukari "Insulin Resistance'", na Uvimbe sugu "Chronic inflammation'. Hizi shida zote zinatokana na changamoto za ulaji, na mfumo wa kisasa wa maisha ya kielektroniki, kukesha Usiku, na kukaa chini zaidi.
NGAZI YA 2
Tambua kuwa asilimia 80% ya sukari katika damu "Glucose" huwa inaratibiwa kwenye misuli, na huwa ikitumika Kwa misuli inayofanya kazi. Watu wasiotumia misuli kiwango Cha sukari huwa juu sana katika damu kisiwe na matumizi zaidi ya kubadilishwa kuwa mafuta kama namna ya kutunzwa. Damu inapokuwa nzito kutokana na kuwa sukari huwa inayeyuka ktk damu "water soluble", hupelekea mishipa ya damu kujilinda Kwa kutengeneza tabaka la mafuta jambo ambalo huifanya mishipa kuwa na mafuta mengi hata kuchochea Presha "atherosclerosis".
Kiwango kikubwa Cha sukari katika damu Huchochea kupanda Kwa homoni 'insulin" ambayo kadri inavyokuwa juu Kwa kitambo Huchochea karibia shida zote za magonjwa sugu, kuanzia Kisukari, shida za uzazi mfano 'PCO's, shida za ngozi 'acne', Saratani ambayo hutumia sukari mara 16× zaidi ya seli za kawaida, shida za Ubongo za Uzee "dementia', shida za macho zinazotokana na sukari kuathiri tishu "AGEs", n.k. Misuli mikubwa inapotumika husaidia Sana kushusha sukari hii na insulin, lakini bila kusahau pia kujiepusha dhidi ya mianga ya kisasa Usiku toka katika taa, TVs, Screen za Vifaa vya kielektroniki, n.k., ambayo bila hata kula hupandisha sukari na insulin katika damu.
Shughuli za kuchosha misuli tu ndizo huwezesha misuli kukua. Wengi hawajui ili misuli ikue inahitaji migandamizo ya kazi ili kuzisisimua aina za tishu "type -2 muscle fibres", ambazo huitwa pia "fast-twitch fibres", hizi ndizo hufanya misuli ionekane mikubwa. Bila shughuli ngumu kidogo "tension", misuli huendelea kuwa dhaifu, na kiwango cha chembechembe za seli za nishati "mitochondria' hupungua sana, hii ni Kwa kuwa; ili zizalishwe chembechembe za nishati za kutosha, shughuli tu za misuli ndizo husisimua Chaneli za kijenetikia"PGC-1 alpha' kuanzisha kuunda hizi chembechembe za nishati kupitia kitendo kinachoitwa "mitochondria biogenesis".
Kwa kufanya shughuli za misuli zakuchosha, misuli hukua, seli huongezeka, Hiki kitendo hupunguza kiwango Cha sukari inayoweza kuleta shida ndani ya damu Kwa kuitumia sana. Mitochondria zinapokuwa katika shughuli nzito husisimua Chaneli zake za "AMPK'' ambazo hutumia sukari nyingi ambayo huwa mwilini. Hii huambatana pia na kuvunjwa vunjwa Kwa seli mfu na dhaifu zote, na kuusafisha mwili pia Kwa kuvunjavunja mabaki Kwa kitendo kinachoitwa "Autophagy'. Mazoezi huzalisha kemikali taarifa "myokines kama irisin', ambazo huutaarifu mwili kuvunja zaidi mafuta yaliyozidi mwilini.
*********-------*********------********---------*****
.jpg)

Join the conversation