Samaki ni zaidi ya Viwanda Afrika
Samaki ni zaidi ya Viwanda Afrika
Waafrika kwa asili huwa na makazi yao kuzunguka sana vyanzo vya maji kama maziwa, bahari, au mito mikubwa. Makazi haya huwawezesha kupata samaki kwa wingi sana; Waafrika kwa asili ni walaji wa samaki, na wanyama pori. Serikali za Afrika zinawekeza sana katika uvuvi kwa kuuza samaki wa maeneo yao kwa nchi za mbali, lakini hawajui maana ya maisha kwao ni hao samaki kutokana na mazingira yao.
Uwingi wa samaki ni kwa dhumuni la kukidhi mahitaji yao kwa kila siku, sio kuwauza ili wapate pesa za kusambaza umeme vijijini. Matumizi ya umeme vijijini hayana faida zozote kwa Waafrika, wameishi milenia zaidi ya 5 bila umeme ila wakiwa na samaki, lakini sasa hivi ndani ya muda usiozidi karne wameshakaribia kumaliza samaki wote kwa ajili ya umeme, ambao hauna unachowaongezea zaidi ya kuwapunguzia muda wa kulala, kuwamaliza uwezo wa kupenda hali zao za kihalisia, na kuwaua ubongo na mifumo yao ya homoni inayohitaji zaidi mizunguko ya asili.
Samaki ndiyo chanzo kikubwa zaidi cha mafuta ya DHA ambayo ndiyo kiini cha mfumo wa Ubongo. DHA inatawala utendaji wa neva za ubongo, mfumo wa umeme wa ubongo, na huu ndiyo hutawala hata uponaji wa vidonda. Waafrika wana maelfu ya wanyama mwituni, lakini wote wanapungua sio kwa sababu wanaliwa sana na wakazi, bali kwa kuwa wanauzwa sana ili kujenga Minara ya simu, au wanawatunza ili wawavutie watalii wapate pesa. Wameishi zaidi ya milenia 5 bila Minara ya simu, lakini kwa muda usiozidi nusu karne wanaelekea kumaliza wanyama wao wote kwa ajili ya minara isiyowaongezea chochote.
Kwa afya yako Kijiografia, hauhitaji mawasiliano na watu wasiokuzunguka katika eneo lako husika katika hali ya kawaida. Ni ulimbukeni tu wa watu kuhisi wanahitajika kuwa na urafiki na ukaribu sana na watu wa mabara ya mbali, au nchi hasa za mbali sana, ambazo kamwe hawataweza kuonana au kufanana. Hii tabia inawafanya kutoweza wajali wenzao wakaribu, na kuishia tu kuishi maisha ya kufikirika. Hii ni kama ya vijana wanaofanya masterbation kwa kutazama picha za wazungu wa mbali, wanaojirekodi wakifanya mapenzi, au mabinti wanaoziremba picha zao katika snapchat, na kutaka sifa kuwa wao ni wazuri. Huwa inanishangaza Waafrika wengi wakishaharibu Nchi zao huwa wanakimbilia Nchi za ugenini kuishi. Mtu anayeishi ugenini, au anasoma ugenini, milele ataishi kama Mfungwa wa kifungo cha nje. Mfano mzuri ni Waafrika wote wanaoishi Ulaya huwa na shida zinazotokana na Upungufu wa mwanga, kwa kuwa mwanga ni dhaifu ulaya na wao wana melanini nyingi. Kiufupi Mwafrika hata aliyesoma kidogo, huwa ana asilimia kubwa sana kuwa hafahamu kabisa anahitaji nini?



Join the conversation