SHERIA YA MIFUPA & KAZI
NONDO YA TANO
Sheria ya "Wollf's law' inasema kuwa, "kadri unavyoongeza kani katika mifupa, basi mifupa huongezeka uimara". Hii ni sawa na Sheria ya zamani ya Lamarck iliyosema, "kiungo unavyokitumia ndivyo kinakuwa Bora, na usipokitumia kinakuwa dhaifu". Kadri usivyotumia mifupa yako kupitia shughuli za kuinama, kukimbia, kusimama-kaa, kuruka, n.k. Mifupa hupunguza sana uimara wake Kwa kujisimenti zaidi na Madini ya "calcium'. Kadri watu wanavyopunguza shughuli za kazi za kuchosha mwili, mifupa huzidi kuisha kupitia kitendo kinachoitwa "osteoporosis', na hii Ndiyo sababu ya watu kuzidi kupinda migongo Kwa kadri miaka yao inavyozidi kwenda.
Hii ni Sheria kubwa sana inayofanya Binadamu kutoweza ishi hata katika Sayari ya Mars, mwezini, na hata angani "space'. Katika anga Kani ya gravity huwa ndogo sana, hivyo mifupa huona hakuna kazi na hivyo kutokuwa na uhitaji kabisa wa "calcium', madini ya "calcium' hujaa sana katika damu na kupelekea shida za Moyo, na mifupa huisha haraka sana hata mtu akapungua sana kiasi cha kutoweza kuishi. Watu Pekee wanaohisi unaweza ishi katika Sayari ya Mars ni Elon musk ambaye anaamini Roboti zake Zinaweza kuwa zaidi ya Daktari ndani ya miaka 3, ilihali mpaka Sasa haziwezi hata kusolve baadhi ya logiki za kawaida sana.
Kwa mfumo wa Maisha ya usasa ya kukaa chini zaidi mifupa huisha sana, na jambo ambalo nililigundua awali kidogo ni kuwa, Kuna uhusiano wa Moja Kwa Moja kati ya Afya ya mifupa kupitia "calcium', na afya ya uzazi. Asili huamini kiumbe aliye imara kimifupa ana uwezo wa kuzaa Kwa kuwa ataweza mbeba Mtoto wake, ataweza mpatia calcium za kutosha Kwa kuwa mifupa ya Mtoto yote hutoka katika Akiba ya mzazi ya calcium, ataweza mpatia calcium ya kutosha kupitia maziwa, Kwa kuwa maziwa huwa na calcium nyingi sana. Kizazi Cha Leo kina watu wadogo sana Kwa kuwa mifupa yao huwa midogo, kwa kuwa pia huwahi kubalehe kutokana na kuzoeshwa taarifa za Mapenzi na sex tangia Umri mdogo kupitia mitandao ya kijamii, na miziki ya kisasa. Kuwahi kupevuka huwa-Fanya kingo za mifupa yao kuwahi Kufunga "Epiphyseal plates closure", na hivyo kutoendelea kukua kama wanaochelewa kubalehe ambao huendelea kuwa na homoni za ukuaji 'GH" Kwa muda mrefu.
Misuli mikubwa hubeba mafuta "adipose', ambayo Huchochea uzalishwaji wa Cholesterol ambayo hutengeneza homoni zote za uzazi "Estrogens, testosterone, PGs, DHEA, na ajabu zaidi, ni vitamin D". Hii vitamin D hufyonza zaidi Calcium kuifanya mifupa na misuli kuwa imara zaidi. Wanawake wengi Kwa kutofanya kazi za kunyakua, kusimama-kaa, au tembeatembea, asili huamini hawana watoto wakuwalea, hivyo kama mtu usiozaa wakatwa. Tezi za Ubongo "Pituitary' na hata adrenali huanza kupunguza uzalishwaji wa homoni za uzazi na kupelekea shida inayoitwa"pregnenolone steal syndrome". Ambapo Mwili hustop kutumia zaidi homoni za thyroid "T3,T4", vitamin A, na Cholesterol kuunda homoni za uzazi na Vitamin D, bali huanza kuunda homoni ya "Cortisol', jambo ambalo Huumaliza zaidi mwili, Huchochea shida za insulin na uzazi, na matokeo yake watu hushindwa kuzaa na hufa Kwa changamoto sugu.
Siri nyingine ambayo wengi hawajui ni kuwa, Mfumo wa usasa unawaua wanaume haraka zaidi ya wanawake kwa kuwa, wanawake wameumbwa Walahu kuwa wastahimilivu wa kukaa muda mrefu kama namna yao ya kukaa na watoto. Wanawake hata wanapokula Vyakula vya Wanga mwili wao huweza kupokea sukari nyingi na kuitunza katika seli za mafuta "Adipocytes', katika makalio yao, Matiti yao, na hata matumbo. Ni kama asili hutumia mafuta kama "Cushion', au Kochi la kukalia unapobeba Mtoto. Lakini wanaume wanapokula sana Wanga huwa hawana sehemu za kuipeleka wasipofanya mazoezi, yote huishia katika damu, katika matumbo, na kuleta shida za insulin na Ubongo. Na hii Ndiyo sababu idadi kubwa ya watu wenye shida za Kisukari, Alzheimer's, na Vitambi 'obesity' ni wanaume. Inapotokea shida ya kihomoni Kwa wanaume hasa kuwa juu sana kwa enzyme "aromatase', ambaye ndiyo hubadili Kwa wanawake homoni za kiume "androgens' kuwa za kike 'Estrogens", matokeo yake wanaume huanza kuwa na mafuta mengi mwilini kama ya wanawake, mfano ni "gynecomastia', ambapo wanaume huwa na mithili ya Matiti ya kike.
Asili ni ya ajabu sana Kwa kuwa huanza kwa kutoa Kisha ndiyo hupokea. Waandishi, wasanii, na Wahandisi wanaweza lielewa zaidi hili. Pia unapoanza kufanya shughuli za kimisuli au mazoezi Kwa kuwa unatoa ndivyo utakavyopokea zaidi. Tafiti zinaonyesha watoto ambao hushiriki zaidi katika shughuli za misuli, michezo, na Mazoezi, huwa na akili nyingi zaidi, na ajabu ni kuwa, wameonekana kuwa na huruma zaidi. Uhusiano huu unatokana na kuwa sehemu kubwa zaidi ya Ubongo "Gray matter', na sehemu ya nyuma ya Ubongo "Cerebellum", zote zinahusiana zaidi na misuli na miondoko. Watoto ambao huwa na shida za usonji "Autism' huwa na shida za miondoko na uwezo wa kujifunza, na wengi wao huwa wanaume zaidi. Hii ni Kwa kuwa, wanaume wameumbwa kutembea zaidi. Ubongo wa wanaume ni mkubwa Kwa asilimia 9-10% zaidi ya Ubongo wa wanawake, kutokana na ukubwa zaidi wa misuli na uwezo wa kimiondoko Kwa wanaume.
Pata Nakala kamili
.....


Join the conversation