Teknolojia nyuma ya Mazao yote ya Kisasa ‘’Selective breeding & hybridization’’
Teknolojia nyuma ya Mazao yote ya Kisasa ‘’Selective breeding & hybridization’’
Wataalamu wengi huwa mstari wa mbele kukosoa uundwaji wa kuku wa broiler ambao ndani ya wiki Nne huwa tayari kuliwa, lakini husahau kuwa Michele, ngano, mahindi, nyanya, vitunguu, maembe, machungwa n.k. yote haya nayo ni Kundi lilelie. Wataalamu wa sayansi za kilimo hutafuta mimea ambayo huwa haina sifa za kawaida, ambazo kwa mimea huwa ni udhaifu, lakini kibiashara, na kimazingira duni huwa faida, na huchukua mimea hiyo na kuizalisha yenyewe kwa yenyewe, au na aina kadhaa zingine za sifa hitajika, na kutengeneza aina bora kabisa ya mimea inayoshamiri katika soko la vyakula.
Sifa hizi hulenga zaidi mimea inayokua haraka sana ili kukabiliana na hali zisizoeleweka za hewa. Mimea ambayo huwa na sukari nyingi sana ili kuwa na Ladha tamu sana na umbile kubwa. Mimea hii kwa asili huwa haishamiri kwa kuwa huwa haina kambakamba sana ‘’fibers’’ hivyo huliwa kirahisi sana, na matunda yake huoza mapema sana. Pia mimea hii kwa kuwa na sukari sana, wadudu huishambulia sana na kuiharibu mapema. Wataalamu hufaidika kwa kuuza sana mbegu za mimea hii inayokua haraka kwa wakulima ambao huwahi vipindi vifupi vya mvua, na huweza ipanda kama mbegu fupi zinazoweza kustahimili ardhi isiyo na rutuba sana. Pia wataalamu huuza mbolea, na madawa ya wadudu, kwa kuwa mimea hii dhaifu huwa haina kinga ya kujipambania kutokana na kutokuwa na kambakamba ‘’fibers’’ kwa kuwa na sukari sana, na kuwa na kiwango kidogo cha ‘’polyphenols’’.
Vyakula vyote vikubwa kama Ngano, mahindi, shayiri, mchele, kama ukiangalia mazao ya asili yake hayakuwa makubwa yenye sukari nyingi kama yalivyo sasa. Haya yalitengenezwa kupitia teknolojia hii ili kuyafanya yawe na wanga nyingi, hii ni kama tu ambavyo Nguruwe wengi wanaofugwa si sawa na wenzao wa porini, sababu ikiwa wengi walitengenezwa kwa teknolojia hiihii.
Mfano tazama namna mazao mengi yamezidi kutengenezwa Kila siku zinavyosonga.




Join the conversation