Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SUMU ZA MBOGAMBOGA NI NINI?

Ni Nini Sumu, Uchungu, au uchachu katika mimea?

Kwanini si kila Mbogamboga Wanyama huweza kuila?

Kama ambavyo watu wengi huwinda na kuwala swala na sio simba na chui, au kama ambavyo simba huwinda nyumbu na sio tembo, ndivyo ilivyo pia kwa Wanyama, wengi hula mimea midhaifu isiyoweza kujilinda kirahisi.

Mimea imara hulinda sana tishu zake kama majani na mashina yake, na hata mizizi kwa kemikali imara zisizovunjika kirahisi, kama ‘’Cellulose, glycoalkaloids, polysaccharides, tannins, n.k.’’ Wanyama aidha hushindwa kutafuna kambakamba hizi ‘’fibers’’ mdomoni, au tumboni. Mimea pia huwa na tabia ya kuzalisha kemikali sumu katika majani yake ili kuizuia isiliwe na wadudu, kama binadamu na Wanyama wanavyojifunika na nguo au manyoya ili kujilinda. Mimea imara yote huwezi kuila kwa aidha hutaweza ivunja, au itakuvunja. 

Wanyama kwa kuwa wameendelea sana mfumo wao wa kuhisi harufu ‘’olfaction’’, huweza kuhisi hizi kemikali na kuacha kula majani hayo. Binadamu hujitahidi sana kuchagua mimea midhaifu sana na kuila mibichi kama Kabichi, au Matango. Lakini kutokana na Ubongo mkubwa wa binadamu ‘’neocortex’’ uliomwezesha kugundua Moto, binadamu hutafuta mimea midhaifu wastani na kuichemsha, kwa kufanya hivi, huweza kuvunja kambakamba za mimea ‘’Glyco-peptides bond’’ na kuiacha mimea ikibakia huru kuibiwa virutubisho vyake. 

Kama ambavyo usipokuwa na akili mwituni utaliwa na simba kwa kuzidiwa mbinu, ndivyo hivyohivyo mbogamboga nyingi huwa dhaifu kuvunjwa kirahisi kwa moto, au hata kwa meno tu. Kumbuka, ujanja ni kuua, na kuweza kufungua seli ya mwenzako na kuchukua kemikali zake za uhai, kwa kuwa; chembechembe zote za uhai mfano magnesium iliyopo kwenye mchicha ndiyo iliyopo kwenye seli zako za ubongo.

Kwanini Machungwa, Malimao, ni Machachu?

Machungwa na malimao huwa na kiwango kikubwa sana cha asidi ‘’Ascorbate’’, ambayo pia huitwa ‘’Vitamin C’’. asidi hii haipo kwa ajli ya kuzuia isiliwe na Wanyama, Mimea hii hushamiri sana sehemu zenye joto, ukame, uwanda wa Mediterranean, na maeneo haya huifanya kuwa katika presha kubwa sana ya stress za jua na joto kali ‘’oxidation’’. Machungwa hutengeneza kiwango kikubwa sana cha Vitamin C kama ‘’Antioxidant’’ kubwa kwa ajili ya kupambana dhidi ya kemikali sumu ‘’Free radicals’’.

Vitamin C marazote huwa ikiyeyuka katika maji, na ndivyo ilivyo matunda haya maranyingi huwa na asili ya maji mengi kama namna ya kuitunza vitamin C idumu. Machungwa hupunguza uchachu kadri yanapoelekea kuiva, kwa kuwa sukari kwa ajli ya mbegu huwa imeshaanza kukamilika kuundwa, na kuonekana kwa rangi ya chungwa kuvutia wadudu ili mbegu ziweze kusambazwa. Mbegu za machungwa huwa si nyeusi na ndiyo maana mchungwa huegemea sana katika ulinzi kwa njia ya kemikali ‘’chemical defense’’.