Kwanini Parachich lina Mbegu moja, na huku Limao lina mamia ya mbegu?
Tunda lolote linapokuwa na mbegu moja humaanisha kuwa linawekeza zaidi kwa mtoto huyo mmoja. Hii ni kama ambavyo tembo huzaa mtoto mmoja tu, huku panya akizaa Watoto kuanzia 10 mpaka 18 kwa mzao mmoja tu. Mimea ambayo huzaa mbegu moja tu huwekeza virutubisho vingi sana kwa mbegu zake, mimea ambayo huwa na mbegu nyingi huwekeza kidogo sana kwa mbegu zake, na hili lina siri kubwa sana.
Kwanini kuna matunda yasiyo na mbegu siku hizi?
Mmea kama viumbe, huwa na nishati ambayo unaweza wekeza aidha katika ukuaji wake, au katika uzazi wake. Mmea unaowahi kuzaa hukua kidogo, na huwahi kufa pia. Kama mmea utawekeza sana katika uzao wake utakufa haraka zaidi. Na hii ndiyo sababu mimea ya matikiti na maboga hufa haraka sana, kwa kuwa Watoto wake huwa wakubwa sana. Mimea kama ya Mapera huchelewa sana kuzaa na huwa na matawi, mizizi, na mashina makubwa na imara sana.
Wana teknolojia wa kilimo hujitahidi kucheza na jenetikia za mimea kwa kutafuta mimea yenye shida za vinasaba vya kuzalisha mbegu, au kubadilisha jenetikia kwa kuathiri vinasaba vinavyohusiana na ukuaji wa tunda baada tu ya mbegu, vinasaba mfano vya ‘’AGL11, INO, SIMBP3, IAA9, ARF7, n.k. teknolojia hizi nimezielezea kwa kina sana katika blog yangu ‘’Dr Brighton shoo’’, hasa teknolojia za CRISPR/cas9, GMO, n.k. Wanabioteknolojia kwa kuzuia ukuaji wa mbegu hufanya matunda kuwa makubwa sana, hii ni kwa kuwa, hufanya nishati yote ya Mmea ya uzazi, kutoelekezwa zaidi katika Mbegu kama ambavyo huwa katika asili, na hivyo nishati hii yote kutumika kutengeneza sukari, au wanga, ambayo ndiyo hulifanya tunda kuwa kubwa.
Je wajua!!
Asilimia 70% ya antioxidants zote zilizopo katika Parachichi huwemo katika Mbegu yake tu. Matumizi ya unga wa mbegu ya Parachichi Kwa kiasi kidogo huwa na faida kubwa sana katika afya.
Kwanini mbegu nyingi ni nyeusi?
Mbegu nyingi hupelekea, au huwa ni nyeusi sio kumaanisha kuwa, ‘’Hapana, usimle mwanangu’’, huwa nyeusi kwa kuwa Weusi ni rangi ambayo hufyonza miale yote ya mwanga. Mbegu huwa na metabolikia kubwa sana inayohitaji kufanya mtoto akue. Na hii huitaji Weusi, au Giza, ni sawa kabisa na ambavyo Mimba nyingi za Wanyama huwa ndani ya tumbo kwenye giza. Kama tulivyokwisha ona kuwa mwanga, hasa ‘’Violet-blue range’’ huua sana seli kupitia ‘’oxidation’’. Kama mwanga utapita kwenye gamba la nje la mbegu, basi huweza kuua kiini cha mbegu alipo mtoto.
Mimea huwekeza kemikali nyingi sana nyeusi ili kufyonza mwanga, zinazoitwa ‘’Melanin’’, Ambazo hufanana na za Wanyama ila tu huwa hazina ‘’Nitrogen’’. Na kumbuka hata Weusi wa Wanyama huwa ni namna za kujikinga na mionzi ya ‘’UV’’, na ndiyo maana nywele zako ni nyeusi kuzuia UV kichwani kwenye Ubongo. Kemikali hizi huambatana na chembechembe zinazoitwa ‘’Phenolic compounds’’, ambazo huwa na lengo moja kuu, kufyonza mawimbi ya frequencies mbalimbali ili kuratibu metabolikia za ukuaji, sasa basi, kemikali hizi kama Tannins, alkaloids, terpenoids, saponins, n.k. huwa ni Chungu sana. Hii Biolojia kwa namna nyingine ni kama inasema, ‘’Nikishindwa kuishi nitamuua aliyeniua’’
Ni kweli kuwa ulaji wa mbegu huwa na faida sana kwa mwili, hii ni kwa kuwa, huwa zina madini mengi sana kama ya Magnesium, virutubisho kama protini na mafuta mengi sana hasa ‘’Omega-3, MUFAs, n.k. ’’ ambayo hutumika kuunda ubongo, macho, na neva’’, lakini ni kweli zaidi kusema kuwa huwa unamwibia mtoto wa mmea, na ndiyo maana naye hukupiga kwa kemikali sumu ‘’Antinutrients’, ambazo kwa baadhi ya watu husababisha kabisa allergy, mfano za Lectins, Glutens, Phytates, oxalates, n.k. Mwishoni mwa kitabu hiki utagundua kuwa maisha ni vita, maamuzi yako ndiyo huchagua urefu wa mbio zako, ukichagua vibaya ukala Mmea kama jamii za Nightshades kama Nyanya na viazi unaoitwa ‘’Atropa belladoma’’, au mti wa ‘’Cerbera odollam’’, utakufa ukiuacha Mmea unaishi kwa kuwa umekuzidi akili ‘’Hosea 4:6’’.
Join the conversation