KWANINI KUNA MIMEA NI DAWA NA MINGINGE SUMU?
Kwanini Mimea mingi ni Dawa?
Mimea yote ni sumu kama Sumu itatumika kumaanisha kitu ambacho kinaweza kuleta hatari mwilini bila kujali kiwango chake cha hatari. na ndiyo maana idadi ya mimea inayoweza kuliwa ni asilimia 5-23% tu ya Mimea yote duniani, jamii kati ya 350,000 mpaka 400,000. Binadamu anaweza kula mimea aina 20,000 mpaka 80,000 tu. Katika mimea hiyo yote mpaka sasa binadamu hulima aina 150 mpaka 200 tu. Asilimua 95% ya mimea yote ambayo binadamu huila hutoka katika aina 30 tu za mimea. Asilimia 50% ya mimea anayokula huweza kuila akiipika tu. Kwa sasa binadamu anakula asilimia 1% tu ya aina zote za mimea anayoweza kula. Asilimia 75% ya vyakula vyake vyote vinatoka katika Mimea 12 tu, yaani; ‘’Ngano, Mchele, Mahindi, Miwa, Soya, Viazi mvirino, Mihogo, viazi vitamu, Mtama, uwele, Karanga, na Mawese’’. Pia asilimia 60% ya nishati yake yote ‘’Calories’’ ikitoka kwa vyakula vitatu; Mchele, Ngano, na Mahindi.
Sumu zote ni Dawa. Unapotumia Penicillin kama dawa ni kwa kuwa huwa ni sumu kwa Bakteria. Dawa nyingi sana hutokea kwa mimea, mimea kama ‘’Opium’’ ndiyo msingi wa dawa za Nusu kaputi, Mti kama wa ‘’Quinine’’ ndiyo msingi wa dawa za Malaria, Majani ya Miti kama Muharobaini, ni msingi wa dawa nyingi za kuondoa kemikali sumu mwilini kwa kuwa zenyewe pia ni sumu. Mbeleni tutaona hii siri ndiyo msingi wa kwanini wala mbogamboga wengi huishi miaka mingi sana.
Kwanini jamii za Mimea ‘’Nightshades’’ kama Mabilinganya, nyanya Chungu, n.k. huwa sumu?
Huu ni mmea sumu wa nightshade
Miongoni mwa vitu ninavyovikumbuka sana nikiwa mdogo ni kuzidiwa kwa mdogo wangu aliyekula ‘’Nyanya chungu pori’’ akizani ni nyanya. Na hii huwa hata kwa Wanyama wanapokula matunda haya kwa Bahati mbaya. Watu hufahamu pia ni hatari sana kula viazi vinapokuwa na rangi ya kijani, sababu pia huwa ni sumu hizi. Viazi vinapogundua kuwa havijafukwa ardhini vipo juani, huzalisha hizi sumu zinazozifanya zionekane za kijani, lakini lengo lake huwa ni kujilinda.
Katika blogs zijazo tutachimbua Kwa kina zaidi Siri ya matibabu kupitia hii mimea.




Join the conversation