Waafrika ni Wakubwa kimwili kiasilia, Hawali sana
Waafrika ni Wakubwa kimwili kiasilia, sio kwamba wanakula sana
Waafrika wengi wa kanda za Tropiki wana asili ya miili mikubwa, hii ni kutokana na namna ya mwili kuongeza eneo la kupoteza nishati ya Joto kutokana na mazingira yao. Miili mikubwa ya watu hawa huwafanya hali zao za kimetabolikia kuwa chini kwa muda mwingi zaidi, yaani ‘’low metabolic rate’’. Kitendo cha metabolikia kuwa chini huwasaidia wasizalishe nishati nyingi sana ya joto mwilini ilihali tayari wapo katika mazingira ya joto.
Miili yao mikubwa inamaanisha kuwa huwa na nishati nyingi sana ambayo, imetunzwa katika namna ya kikemikali katika misuli na mifupa yao. Na hii nishati katika misuli yao ndiyo ambayo huwawezesha kuzalisha nguvu nyingi ndani ya muda mfupi, hata bila ya kutumia Oksijeni, kupitia kitendo cha ‘’Anaerobic glycolysis’’. hii inakueleza ni kwa namna gani asili imewatengeneza watu hawa kwa ajili ya shughuli za muda mfupi, zenye kutumia nguvu nyingi kama mawindo, na siyo kama ilivyo kwa watu wa nyanda za baridi, ambao huwa kinyume chake, wao huwa wadogo kutunza joto lisipotee sana, huwa na metabolikia za juu zinazowafanya joto lao kuwa juu, na hii huwafanya kula sana. hii ni kama ambavyo panya hula sana ukilinganisha na Tembo ndani ya siku, ukilinganisha na maumbile yao. Pia panya hufa haraka sababu metabolikia inapokuwa juu maranyingi kemikali sumu ‘’free radicals’’ huzalishwa sana. ijapokuwa sio marazote mfano kwa ndege.
Waafrika kimwonekano wametofautiana rangi kutokana na kupishana kwao kwa kiasi cha chembechembe za melanin katika ngozi zao, na hata katika nywele zao. Tofauti hizi za melanin si katika ngozi tu, zipo katika kila sehemu ya mwili. Chembechembe za melanin hazina kazi moja tu ya kuukinga mwili dhidi ya mionzi hatari ya mwanga ya UV, chembechembe hizi zinahusiana na mfumo mzima wa homoni na taarifa kuhusu uhusiano wa mwili, mazingira, na majira.
Jamii za Waafrika wafupi sana zina maana gani?
Jamii za Waafrika wafupi zinamaanisha Waafrika wanaweza kujitegemea wao wenyewe bila kuungana katika jumuiya kubwa. Uwepo wa jamii za watu wadogo sana kimaumbile ni matokeo ya jamii nyingi Afrika kuishi bila kuchangamana kwa kuzaliana na wengine, hivyo watu hawa hurithishana wao wenyewe tu vinasaba vyao vya jenetikia. Wengi wao wako vizuri sana kiafya na kiakili, na pia huchangamana vizuri sana na jamii zingine hasa katika biashara za pembe za ndovu, n.k.Je Wajua
Shughuli za misuli kabla ya kula Huchochea zaidi ukuaji wa misuli mikubwa. Hii inafanana kabisa na mfumo wa Waafrika ambao huwa-Fanya kuwinda asubuhi kabla ya kula, na hii huwa-Fanya misuli yao kuwa imara sana.
.jpg)


Join the conversation