Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Siri ya Afya za Waafrika sio Chakula

Siri ya Afya za Waafrika sio Chakula

Siri ya Afya za Waafrika sio Chakula

Afya bora ya hizi Mitochondria ndiyo huwafanya Waafrika kuishi miaka mingi sana, maana asilimia 95% ya homoni za melatonin hutengenezwa kutoka katika mitochondria. Na hizi ndizo hutawala kuondoa kemikali sumu zote katika ubongo na mwilini. Kemikali sumu za mwili ‘’free radicals’’ hutokana na uharibifu wa Mitochondria, ambao hupelekea electrons kuponyoka kuungana na Oksijeni, na kuunda sumu zinazoshusha maisha kama ‘’Superoxide, hydrogen peroxide, n.k.’’ kwa mfumo wa maisha ya Afrika ya kulala Mapema, kutembea pekupeku, kutotumia vifaa vya elektronics, na kula sana Samaki, nyama, mbogamboga za msimu, na matunda pori madogomadogo, haya yote huwafanya kuwa na kemikali sumu kidogo sana. 

Waafrika Huweza kujiponya kirahisi wanapopata vidonda mwilini, kwa kuwa mwanga wa jua huzisisimua seli kujibadilisha kuunda tishu zilizoathiriwa, kupitia ‘’Mitosis’’. huu ni ugunduzi uliofanywa na Alexander Gurstwich aliyeshinda tuzo bora ya sayansi kwa kugundua Vitamin C, na ulithibitishwa na Mwanabiolojia mwingine Fritz Pop. Hawa walitengeneza njia ya kugunduliwa kuwa mfumo wa umeme wa ‘’DC’’, unaotembea katika sehemu ya nje ya seli za neva ‘’perineural cells’’, zilizojaa mafuta ya DHA; huu mfumo ndiyo huongoza taarifa za mwili kujiponyesha kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Dedifferentiation’’. huu ni ugunduzi mkubwa alioufanyia sana kazi Mpasuaji wa Mifupa na mtafiti Robert Becker.  

Hii ndiyo sababu Waafrika huwahi kupona vidonda, na utaratibu wao wa kuamka mapema, hufanya mwanga wa jua wa alfajiri ‘’IRA na Redlight’’, kuwasisimua sana kemikali za ‘’Nitric Oxides’’, ambazo hupunguza uzalishaji wa ATP zisilete shida zinapokuwa nyingi kwa kupelekea kujaa kwa mafuta mwilini, pia Nitric Oxides’’ huchochea seli za damu kuundwa, na chembechembe za kinga za mwili. Haya yote huwanufaisha Waafrika hata kabla hawajala chakula, ni Mwanga tu.

Waafrika wanatunza Nguvu za Mwanga sio Vyakula

Waafrika muda mwingi huwa katika hali ya nishati ya uundwaji ‘’Biosynthesis’’, na hii ndiyo sababu kubwa ya asili yao ya maumbile makubwa, na ndiyo maana pia Waafrika wanapokula sana wanga, wanapata shida nyingi zaidi, maana tayari wao wanatunza, kuongeza kutunza zaidi kunawafanya kuwa na shida za moyo, maini, kongosho, n.k. Wazungu wengi kutokana na baridi huwa katika uvunjaji zaidi, na hii ndiyo sababu huitaji sana ‘’ATP’’, na hula sana wanga bila kudhulika sana. Ajabu zaidi ni kuwa; homoni ya MCH ambayo kwa Waafrika ipo juu sana, kulingana na kiwango chao kikubwa cha melanin, huwa na kazi pia ya kutawala hisia za kuridhika, na mfumo wa balansi ya nishati wa mwili ‘’homeostasis’’. 

Chini ya ngozi kuna tabaka la mafuta ‘’subcutaneous adipose fats’’, haya mafuta ndiyo huzalisha homoni ya kuridhika ‘’Leptin’’, na hizi zote huwa kwa kiwango kikubwa sana kwa watu wa Afrika. Ni kama unavyoona Waafrika ni wanene. Waafrika sio walaji sana, mwanga wa jua huwa unawasisimua sana sensa zinazoitwa ‘’melanopsin’’, zilizopo katika macho, nyuma ya jicho katika ukuta unaoitwa ‘’RPE’’, na pia husisimua sensa zilizo katika ngozi, kama ‘’Neuropsin’’, hizi zote husisimua chaneli za macho zinazoenda katika ubongo zinazoitwa ‘’Central retinal pathway’’, ambazo hizi huenda na kusisimua vinasaba vinavyoitwa ‘’POMC’’, hiyo ndiyo huchochea karibia mfumo wote wa homoni kwa kusisimua tezi ya pituitary, kuzalisha alpha MSH ambayo huchochea homoni zote za uzazi, na hali ya kutohisi maumivu. Pia huisisimua Beta MSH, na hata ACTH, ambayo husisimua mfumo wa kuwa makini, na stress za kumfanya mtu atende. 

Waafrika huendana na mfumo wa Mwanga vizuri sana na ndiyo maana afya zao za kihomoni huwa shwari, wao huupata mwanga asubuhi sana, na huuacha jioni sana. huu mwanga huisisimua sensa ya ubongo katika hypothalamus inaiyoitwa ‘’SCN’’, na hii ndiyo huamasisha tezi ya ubongo ya ‘’Pineal’’ kuzalisha ‘’Melatonin’’, na kuwafanya walale mapema, hushusha homoni za stress, Waafrika kwa milenia wamekuwa ni watu wanaotumia usiku kwa ajili ya kusimuliana visa, kufanya mapenzi, kutafakari, n.k. 

Haya yote hayawezekani na usasa wanaoukimbilia wa kuangalia Televisheni, au kukesha na simu za smartphones, zinazoathiri huu mfumo wote. homoni zote ambazo huanza kuundwa saa 06:00PM hushindikana, na mionzi ya hivi Vifaa huwafanya wapungukiwe Oksijeni, maana chembechembe za kuibeba za Hemoglobin zenye madini chuma ‘’Iron’’ hubadilishwa toka Iron-2 kuwa Iron-3, ambayo haiwezi beba Oksijeni. na Oksijeni inapokuwa chini huizima ‘’POMC’’, yaani homoni zote huwa chini. Pia mionzi ya vifaa vya kisasa ‘’nnemf’’ na blue rays, husababisha sukari katika damu kuwa juu ‘’blood glucose’’, hii huchochea zaidi tatizo. Waafrika zama hizi ni watu wenye stress sana, sio kama zamani; Serikali zao zinawachochea kuishi mfumo wa maisha tofauti na asili yao. 

Afrika ina kiwango kikubwa sana cha mwanga kutoka katika jua, pia ina kiwango kikubwa sana cha maji kutokana na uwepo wa bahari, maziwa, mito mikubwa, na chemchemi. Kama tulivyoona awali mazao au mimea mingi ya Afrika haitunzi matunda na mizizi mikubwa sana, hivyo ndivyo ilivyo kwa watu. Watu wa Afrika hawali sana kama ilivyo kwa maeneo mengine. Bara la Afrika watu wametofautiana sana, na kila eneo jiografia yake imepelekea biolojia za watu wake kuwa tofauti na sehemu zingine.