MBINU YA BAMIA DHIDI YA PILIPILI
Kwanini Pilipili ni kali?
Pilipili nyingi huwa na kemikali zinazoitwa ‘’Capsaicin’’, ambazo husisimua sensa za Moto ‘’TRPV1’’ kwa Wanyama ambao wanaweza kuzila, lakini ajabu ni kuwa, bado pilipili nyingi zinapokomaa huwa na rangi nyekundu kumaanisha zinahitaji kusambazwa na wanyama, swali bora ni kuwa je hili lina maana gani? Wasomi wengi hukimbilia kuwa pilipili hulenga kuliwa na ndege ambao huwa hawahisi ukali wa pilipili hizi, na huzila na kusambaza mbegu zake hata umbali mrefu zaidi.
Lakini binafsi nikiziangalia pilipili katika familia yake, naona pilipili zimepishana sana ukali kuanzia zisizo na ukali kabisa kama pilipili Hoho, mpaka zilizokali sana kama pilipili kichaa, au ‘’black pepper’’. Pia pilipili zimepishana sana ukali kulingana na mazingira yake, pilipili huwa kali sana maeneo ya Joto kali kama kanda za Tropiki na Equator. Wenda pilipili huvutia ili ziliwe na kisha zitemwe kwa ukali wake ili kusambaza mbegu. Wenda kwa kuwa pilipili huwa na mbegu nyingi hulenga kusisimua sensa za joto ili kufanya viumbe vikimbie baada ya kuzila na kusambaza mbali zaidi mbegu zake kuzuia ‘’inbreeding’’.
Kwanini Mbogamboga na Mimea baadhi hudumu rangi kijani hata katika kukomaa kwao?
Mimea ambayo hudumu na rangi kijani hata baada ya kukomaa kwake huwa maranyingi ni mimea ya muda mfupi sana, au huwa na namna ya kuzisambaza mbegu zake bila kuhitaji viumbe. Hii huwa kwa mbogamboga ambazo huwa na mbegu ndogo sana ambazo husambazwa hata na upepo zinapokauka, na maranyingi mbogamboga hizi huwa ni za muda mfupi sana. Hebu tutazamke kwa mfano;Kwanini Bamia huwa na uteute mzito, na hukomaa zikiwa kijani?
Bamia hutengeneza uteute mzito, na kambakamba ‘’fibers’’ nyingi sana, ambapo uteute huu hulenga kuzuia maji yasipotee, lakini kambakamba hizi huiwezesha inapokomaa na kisha ikakauka kutengeneza kani kubwa ambayo inapopasuka huzirusha mbegu umbali mrefu, bila kuhitaji kuangusha tunda kama ilivyo kwa bilinganya, au nyanya chungu. Uteute wake mzito huifanya kutokuwa na uhitaji mkubwa wa pigmets za njano za kupambana na madhara ya mwanga.
Kwanini Mimea mingine hutambaa, na Mingine hukua kama Miti?
Mimea inayokua sehemu ambazo mwanga huwa ni shida, hushindania sana kuwa na urefu mkubwa. Hii huwa katika misitu mizito, na sehemu ambazo maji huwa mengi, hivyo vita pekee huwa ni mwanga. Sehemu ambazo mwanga huwa ni wa kutosha kama sehemu zenye ukame, milimani, n.k. na maeneo hayo kukawa na shida ya maji, Mimea hupambania zaidi ulalo. Hii ni kwa kuwa, kwa kulala mimea hutunza sana unyevu wake, hutunza chakula chake ardhini, na huitaji virutubisho kidogo sana kutengeneza matawi makubwa, na mashina makubwa.





Join the conversation