Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Siri ya Mimea Michungu kama Mwarobaini, Aloe vera, na Majani ya Mpera, katika Tiba?

Siri ya Mimea Michungu kama Mwarobaini, Aloe vera, na Majani ya Mpera, katika Tiba?

Ipi ni Siri ya Mimea Michungu kama Mwarobaini, Aloe vera, na Majani ya Mpera, katika Tiba?

Mimea hii imekuwa ikitumika kutibu shida mbalimbali bila wengi kujua. Kwanza kabisa Uchungu wa Mimea hii ambao hutokana na kemikali zake, mfano kwa Mwarobaini ‘’Limonoids’’, huufanya mwili unapohisi tu kuwa zipo tumboni, kubadilisha kabisa vipaumbele vingine vyote vya mwili, kama vile kubalansi joto, au kusambaza damu kwa kasi kama mtu angekuwa na homa kali. Inapofika tu mdomoni mpaka tumboni Ubongo na mwili hushtuka na kuisukuma damu sana kuelekea tumboni, na kuanza kuongeza zaidi metabolikia ya Ini kuhangaika na hizi kemikali ambazo huonekana sumu. Kipindi haya yanaendelea, Mwelekeo wa kwanza wa Homa wa mwili hushuka kwa kuwa ili homa iendelee, Damu inapaswa kujaa zaidi mwilini kwenye Ngozi na misuli, lakini sasa Presha ya damu hushuka kwa kuwa mwili huwa katika Emergency.

Kemikali hizi sumu kweli huua sana seli hasa za bakteria na fangasi ambao utakutana nao, na Mwarobaini kama ambavyo huonekana kwa rangi ya kijani kikali sana, ni kutokana na kuwa na ‘’chrolophyll’’ nyingi sana, hivyo huwa na madini mengi sana hasa ya Magnesium, haya husaidia kuufanya mwili kutulia ‘’relax’. Uchungu wake huufanya Ubongo kung’ang’ania mfumo wa ‘’PSNS’’, ili kuuondoa wote mwilini, jambo ambalo huondoa kabisa stress za mwili, na Mwarobaini huwa na ‘’Carotenoids, na Flavonoids kama Quercetin ambazo utengenza urangi wake wa njano’’, hizi huusaidia zaidi mwili kuondokana na madhara ya stress za magonjwa.

Aloe Vera kwa asili imetokea Peninsula ya Uarabuni, hivyo ni Mmea ambao umeshazoea hali ya ukame, na joto kali sana. Aloe vera huwa na chembechembe za rangi ya njano zinazoitwa ‘’Anthraqionones’’ ambazo huwa chini tu ya Ngozi kama tulivyoona awali sababu ya hizi rangi. Aloe vera hushusha joto la mwili kama namna yake ya kudumu kwenye jua kali, husaidia sana seli za kinga ‘’macrophages’’ kuponyesha tishu kupitia kuwa na kemikali yake inayoitwa ‘’Acemannan’’, na pia husaidia sana kujenga tishu za mwili kwa kuwa huchochea sana uundwaji wa ‘’Collagen’’. Na hii ndiyo sababu Mafuta mengi sana huitwa kwa ‘’Label’’ ya ‘’Aloe vera’’.

Majani ya mpera ambayo wengi huyatumia kwa shida za matumbo, kwa asili Mipera ni mimea ya Marekani ya kati na kusini. Mimea hii huwa na kiwango kikubwa cha ‘’Flavonoids’’ zinazoitwa ‘’Quercetin, na Guaijaverin’’, ambazo huonekana zaidi kwa rangi ya njano. Pia huwa na kemikali ‘’Tannins’’ ambazo huwa na rangi za Weusi, hivyo huyapa majani rangi za wekundu-kahawa ambazo tukiwa wadogo tulizichezea sana kwa kuyasugua majani ya mpera katika maji. Majani ya mipera huzuia kuharisha kwa kuwa hupunguza kazi ya kemikali ‘’Acetylcholine’’ katika tumbo, Mipera huzuia pia chaneli za madini ya ‘’Calcium’’, na hivyo kuzuia misuli kuchochea tumbo la kuhara, hii kazi hufanywa na kemikali za ‘’tannins, na Quercetin’’. Majani ya mipera huzuia uvunjwaji wa wanga kupitia vivunjaji wake ‘’alpha-amylase, na alpha-glucosidase’’, hii huwasaidia sana wagonjwa wa kisukari ‘’DM-2’’, lakini lengo la mpera lilikuwa ni kuua vimelea waliokula jani lake. 

Mimea hii yote Mitatu, na jamii za mimea michungu yote, kutokana na uchungu wake ambao ndiyo kiwango kikubwa cha ‘’Flavonoids’’, huua Vimelea sana, na hii ni kwa kuwa, huaribu kabisa mfumo wa mawasiliano wa bakteria kwa kuungana na kuta zao na kutengeneza ‘’complexes’’. Chembechembe kama za ‘’Quercetin’’ hufanya mfano majani ya mpera kuwa kama dawa za moyo, kwa kuwa huzuia sensa za ‘’ACE2’’ na kuchochea ‘’Nitric oxide’’, hivyo hushusha presha na kutanua zaidi mishipa ya damu.