Je ni kweli vyakula vilivyo chacha ni vizuri kwa afya?
Je ni kweli vyakula vilivyo chacha ni vizuri kwa afya?
Kutokana na vyakula vingi vya nafaka kuwa na kiwango kikubwa sana cha wanga, zenye sukari ‘’Glucose’’ katika muundo wa ‘’amylopectin’’, yaani huvunjika haraka sana na kupelekea ongezeko la ghafla sana la Glucose katika damu, na pia kuwa na kiwango kidogo sana cha kambakamba ‘’fibers’’, kitendo cha kuchacha kwa vyakula hivi husaidia mambo matatu.
Kwanza molekuli za wanga zinapopikwa hutanuka na kulainika, hii huzifanya kuvunjika kirahisi sana na kumwaga ‘’glucose’’ nyingi sana katika utumbo hata damu inayoleta shida. Zinapolala husinyaa, na hata zikija kupashwa tena huwa zimeshabadilika umbile, huwa zimeshakuwa ‘’resistant starch’’, hii huzifanya zinapoliwa kutozalisha sukari nyingi katika damu inayoleta shida. Kwa mbinu ndogo ya Kulaza vyakula vya nafaka vilivyopikwa, watu huweza kushusha mhemko wa homoni ya insulin, hata wagonjwa wa kisukari.
Pili hupunguza kiwango cha sukari kupitia uchachukaji kutengeneza pombe kidogo ‘’ethanol’’. Pombe hii huwa kidogo sana, na mwili hauioni kama sumu, na ndiyo maana una vivunjaji vyake ‘’alcohol dehdrogenase’’, kila Ini linapoiona pombe hii na sukari, huachana na metabolikia yake ya kuibadili sukari kuwa mafuta yanayoleta shida mwilini yakizidi, hukimbilia pombe hii kuivunja iunde ‘’acetaldehdye’ na kisha ‘’acetate’’ ambayo hutolewa mwilini. Hii husaidia ndani ya muda mfupi kupunguza kiwango cha sukari. Na hii ndiyo sababu pombe za asili zenye kiwango kidogo cha ‘’ethanol’’ kama Mbege huwa na faida zipotumika mara mojamoja kwa kiasi kidogo. sababu ni hii na na faida zingine za chembechembe za matunda. Unywaji unapozidi wa pombe kwa kiasi kikubwa ‘’acetate’’ hubadilishwa tena kuwa mafuta katika ini ‘’fatty liver’ kupitia ‘’acetyl coA’’.
Tatu chakula kinacholala, hata mbogamboga kama kabichi, huwa na kiwango kikubwa sana cha vimelea ‘’bakteria’’ ambao huja kusaidia kama ‘’Probiotics’’. Kwa kuwa uvunjwaji wa wanga huitaji sana bakteria, ndiyo maana mdomoni kuna bakteria wengi sana na vivunja wanga ‘’salivary amylases’’. Chakula kinapolala huwa ni mithili ya kuanza kukutana na bakteria wa kusaidia kukimeng’enya. Lakini hakipaswi kuharibika kabisa, maana kwa kuharibika huwa na sumu nyingi sana za fangasi, pombe kali, na asidi.
Je ni kipi cha kuliwa zaidi kati ya mbogamboga, nafaka, mbegu, matunda, au kundekunde?
Kwa upande wa kiwango cha virutubisho, Mbogamboga za majani, na Maganda ya matunda yenye rangi mbalimbali ‘’polyphenols’’, haya huwa na kemikali nyingi sana za ‘’flavonoids, kambakamba ‘’fibers’’, na carotenoids’’, na hizi ndizo msingi wa kuishi miaka mingi na matibabu kupitia mimea. Matunda mengi kwa muktadha wa tishu zake huwa yana faida kidogo sana, na hii ni kwa kuwa, huwa tu yamejaa sukari. mbegu za matunda; mfano mbegu za maboga, matikiti, n.k. huwa na madini mengi sana, mafuta sana, protini nyingi sana, na chembechembe zingine kwa wastani. Mbegu za kundekunde ‘’legumes’’ kama maharagwe, njegele, soya, n.k. hufuatia kwa kuwa huwa zina kiwango kikubwa cha protini, madini, na wanga. Na Mwisho kabisa ni nafaka, hizi huwa na kiwango kidogo sana cha virutubisho vya mafuta, protini, flavonoids, ila huwa na kiwango kikubwa sana cha wanga. Kitendo cha kukoboa huzipunguza kabisa virutubisho, na hii ndiyo sababu viwanda huzijaza madini zama hizi ‘’fortification’’.




Join the conversation