Waafrika wagonjwa wanakula sana
Waafrika wagonjwa wanakula sana
Waafrika wengi wamekuwa waraibu sana wa vyakula vya wanga kwa zama hizi, na hii ni kutokana na ulimaji ulioshamiri sana wa mazao kama mahindi, mpunga, mihogo, n.k. vyakula hivi kwa asili vilikuwa ni vya wakoloni kutokana na kanda za baridi walizotoka. matumizi ya vyakula hivi na matunda ya sukari sana kwa Waafrika hupelekea uraibu sana na changamoto nyingi sana za kiafya, kuanzia katika kinywa, mpaka katika ukuaji wa kimwili. Waafrika kwa asili ni walaji sana wa nyama, mbogamboga za msimu, na matunda madogo madogo.
Waafrika wanapokula sana wanga ilihali wapo katika joto, wanapelekea kiwango kikubwa cha sukari katika damu kuwa juu kwa muda mwingi bila kutumika, hii huchochea homoni za insulini kushamiri kwa muda mwingi zaidi, hizi huchochea kushamiri sana kwa uundwaji wa mafuta tumboni hasa kuzunguka ini, na mafuta haya hupelekea homoni za kuridhika zinazoitwa ‘’Leptin’’ kuzalishwa. Homoni hizi zinapozalishwa endelevu hupelekea mfumo wa kuridhika kuathiriwa, na matokeo yake; Ubongo wa Waafrika huathiriwa na uraibu wa ulaji wa wanga zaidi hata ya wazungu wenyewe, ambao kutokana na mazingira yao ya baridi, wanga yote huvunjwa kuzalisha nishati katika chembechembe za seli za nishati ‘’Mitochondria’’, na hii ni kutokana na chembechembe zinazotoka katika wanga zinapovunjwa ‘’Electrons’’, huchakatwa kuzalisha Joto kipindi cha baridi kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Uncoupling’’, yaani ‘’elektroni’’ hutumika kuzalisha joto moja kwa moja bila kuzalisha ‘’ATP’’.
Afrika haipendi Sukari, ukiona Mwembe ujue umepandwa
Katika maeneo mengi sana ya Afrika ambayo hali yake imekuwa ni ya Joto kiasi, au joto sana. Maeneo hayo watu wake wamekuwa kwa asili sio walaji sana wa vyakula vya mazao ya sukari, hasa yaliyoshuka kipindi cha wakoloni. Maeneo ya Afrika kwa asili hayana sukari nyingi sana. Vyakula vya sukari ambavyo huupatia nishati sana mwili huwa na umuhimu sana katika maeneo yenye ukame, au vipindi virefu vya baridi, na hii ni kutokana na kuwa; watu wa maeneo ya baridi huitaji sana wanga ili kuiwezesha miili yao kuzalisha nishati, kukabili hali ya upotevu sana wa nishati unaotokana na baridi. Lakini kwa maeneo ya joto vyakula hivi vya wanga huwa havina umuhimu mkubwa, kwa kuwa watu hawa tayari huwa katika maeneo wasiyo na upotevu mkubwa wa nishati.Ni rahisi sana kuona Ulaya-asia ikiwa na matunda mengi sana ya sukari kama tulivyokwisha kuona, ukanda huu una ukame na baridi sana na hivyo kiwango cha maji ni kidogo sana, mimea yake huwa na sukari nyingi sana kwa kuwa sukari hufyonza sana maji, na pia sukari hutunza sana nishati ya mwanga kipindi cha utengenezaji wa chakula cha mimea ‘’photosynthesis’’. Kumbuka kanda kadhaa za Ulaya-Asia miezi kadhaa hukosa kabisa mwanga wa kutosha wa jua. Unapokuja Afrika maji ni mengi, mwanga ni kila siku masaa 12, hivyo mimea huwa haitunzi sana sukari nyingi, na hivyo hutaona matunda mengi makubwa wala yenye sukari sana kwa asili.



Join the conversation