Upi ni mlo unaotibu magonjwa mengi zaidi ukilinganisha yote?
Upi ni mlo unaotibu magonjwa mengi zaidi ukilinganisha yote?
Mlo aina ya ‘’Ketogenic diet’’, ambao unahusisha kutumia kiwango kikubwa sana cha mbogamboga za majani, mbegumbegu, matunda mengi hasa yasiyo na sukari, na kiwango kikubwa cha nyama; umeonekana kitabibu, kitakwimu, na kisayansi kusaidia sana mwili kujikimu dhidi ya shida nyingi sana za mwili. Na hii ni kwa kuwa, Msingi wa magonjwa yote umejikita katika shida kuu mbili, uvimbe ‘’inflammation’’, na usugu wa sensa kwa homoni ya insulin ‘’insulin resistance’’. Mlo huu unasaidia sana kuondoa shida za insulin ambazo ndizo msingi wa uzito mkubwa, mafuta mengi katika mishipa ya damu na mwilini, na Pamoja na uvimbe ‘’inflammation’’.
Mlo huu umeonekana bora katika kusaidia sana kushusha hatari kubwa sana ya shida za saratani. Seli za saratani hutumia sana sukari, mara 16 zaidi ya seli za kawaida. Kwa kiwango kidogo cha sukari kwa mlo huu hupungukiwa kabisa nishati na kupungukiwa nguvu. Mlo huu pia husaidia sana kwa wagonjwa wa kisukari ambao huteswa na usugu wa insulin, husaidia sana wenye shida za Ngozi kama ‘’psoriasis’’, na uvimbe wa tumboni ‘’IBS’’, kwa kuwa msingi wa shida hizi ni insulin, na uvimbe unaotokana na allergies ‘’autoimmune’’. Mlo huu husaidia sana kwa shida za uzazi, kwa kuwa hurejesha uzalishaji wa homoni zote, na pia hutoa madini yote kuwezesha metabolikia za mwili. Kwa kushusha kiwango cha sukari, na insulin, hushusha presha ya damu, na husaidia sana ubongo kuwa sawa na kuondokana na msongo wa Mawazo na uraibu wa kulakula sana.
Unapovuka miaka 42 hasa kwa mwanamke, na kwa wote kwa ujumla umri unapozidi Kwenda, uwezo wa mwili wa kujitengenezea mfumo wake kuondosha kemikali sumu ‘’Glutathione’’ hushuka sana. Na hii ni sawa na kusema, kwa kula sana mbogamboga na matunda, mwili huongeza sana ‘’antioxidants’’ kama ‘caretonoids, flavonoids’’, Na hizi ndizo msingi wa kupunguza kemikali sumu zinazowaisha mtu kufa.
Pichani nikiwa na Baba yangu "Godwin Shoo"


Join the conversation