Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

UCHAWI NA SAIKOLOJIA YA HOFU

UCHAWI NA SAIKOLOJIA YA HOFU

Mipaka Na Udhaifu Wa Saikolojia Ya Uwezo Wa Ubongo

Mbinu za wasanii wa mazingaombwe za saikolojia, nyingi zina misingi ya kifiziolojia. Lakini kwanini zimewekwa katika kundi la kisaikolojia. Ni kwasababu zinalenga mtazamo wa mtu zaidi uliojengwa katika uamuzi au mazingira yake mwenyewe ya kifikra, Zaidi ya kuchochewa na triki za kudanganywa kupitia milango ya fahamu. Mbinu za mafanikio kabisa za awali ni kama zifuatazo;

Imani (Belief)

Mtu anayenyakua mguu wake Kwenda kuburudika kwa kuangalia sanaa za mazingaombwe. Tayari ndani yake anakuwa ameamini kuwa huko atashuhudia maajabu yasiyo ya kawaida. Mtu anayekwenda kwa Mganga wa kienyeji kuagua, Au kutaka kujua hatma yake, au kusaidiwa, Tayari anaamini kuwa huko anaweza saidiwa. Hatua ya kwanza ya Imani ni kuchukua hatua mara zote. Waganga wengi wa kienyeji husema kuwa, amini kwanza. kitaalamu kuna Nguvu kubwa sana ya Imani. Unapoamini, unakubaliana na matokeo kabla ya hatua. Unapoamini utapona kwa dawa, unaanza kupona kabla hata ya dawa. hii huitwa ‘’Placebo Effect’’. Ukweli ni kuwa, Ubongo unachukua uhalisia wa asilimia 1% kati ya 99%, na kuifanya asilimia 100%. Imani ni nini? Imani ni kuwa na uhakika wa mambo uyasikiayo yasiyoonekana. Unaweza kuwa na Imani kuwa mtu Fulani anakupenda, ijapokuwa huwezi uona upendo wake kwa macho. Mimi naamini Upendo mkubwa wa Mungu kwangu, ijapokuwa siwezi kuuona kwa macho. Sirahisi mtu kukuuliza, je unaamini kuwa una masikio? kama yanaonekana. Kwa kuwa, haihitaji Imani kuwa na hakika kwa vitu vinavyoonekana. Neno Imani ni msingi namba moja kwa vitabu vyote vinavyoelezea sanaa za ‘’magic’’ unavyoweza kuvisoma. Hebu tazama kiundani kwanini?

Ubongo mara zote huwa ukifunga milango yote na kujitengenezea mazingira kana kama umekamilika. Neno ‘’Closed mind’’ hutumika kumaanisha watu wasioruhusu ubongo wao kufunuliwa zaidi kimaarifa, lakini kiuhalisia kila mtu kwa asili hujiaminisha kuwa amekamilika, na ndiyo maana Ubongo huwa unashangaa, Pale unapokutana na vitu usivyovitegemea. Hii ni kumaanisha kuwa, ulishafunga mlango kuamini kuwa haviwezekani. Sasa basi, mtu anapokuwa na Imani Fulani, anakuwa hana uhakika asilimia 100% juu ya hicho kitu, ila sasa, kwa akili yake, na sababu Fulani za msingi sana, anazitengeneza hizo asilimia 100%. Na hii ndiyo sababu, hata kwa kitu kilekile, watu hutofautiana Imani. Hii ni kumaanisha, Imani hutengenezwa na mtu binafsi.Mtu anapotengeneza Imani Fulani, anaruhusu ubongo wake kukubaliana na uwepo fulani, japokuwa anakuwa hauoni kwa macho. Ila anakubaliana nao kwa sababu kadhaa katika kichwa chake. Sasa basi, mtu anapoenda kwa wasanii hawa, anakubaliana na kuwa, watu hawa wana nguvu juu ya uaguzi wao. Kwa kuwa tayari wanajiita wataalamu. pili, anatengeneza njia ya watu hawa kutumia namna yoyote katika uaguzi wao, Hii ni sawa na kusema, anafungua Ubongo kwa ajili ya kudanganywa zaidi, Ubongo anaufungua kama anavyofungua zipu.

Nguvu Ya Imani Katika Ubongo

Imani ndicho kitu pekee ambacho kinaweza kukinzana moja kwa moja na mfumo mzima wa ubongo, unaotawala mwili na maana zake. Hakuna sehemu ya Ubongo inayoweza kukubali kuwa Mtu aliyekufa, anaweza kufufuka. Hakuna msingi wa utendaji wa ubongo unaoweza kukubali kuwa, Maji yanaweza badilika kuunda Divai. Na kama mtu atakubali, basi atakuwa na mashaka. Lakini kwa Imani, sisi tunaamini na hatuna mashaka. Imani huusiana na kuruhusu uwezo mkubwa utendao zaidi ya viwango vya fizikia ya asili, na hiyo ndiyo sababu Imani imekuwa ni ajenda kubwa sana katika sehemu hii.

Watu wengi hawajui kuwa, Imani ni matokeo ya kiwango kikubwa zaidi cha tafakari. Sio rahisi mtu kuamini kuwa ulimwengu ulio complex katika kila mfumo, unaweza kuwa ni kama Gari lisilo na dereva. Na hoja hii, ndiyo huwafanya watu kuanza kutafuta madereva kwa watu wanaohisi wanaweza kujua siri hizi. Kumbuka, Katika Viwango vya chembechembe ndogo zaidi ‘’Atomic level’’, vitu vyote hufanana, Atomu zinazoniumba mimi ndizo hizohizo zilizopo katika mchicha, mchanga, na hata moshi wa gari. Kama ukipiga picha inayoonesha atomu tu. Basi utaona kila kitu kikifanana, na vikipishana tu ujazo na nishati za kuchezacheza. Hivyo maji na divai, kwa Muumbaji ni sawa tu na barafu na mvuke. Hata swala la kifo, kwa aliyeumba uhai halina mdahalo. Hoja ya msingi ni kuonesha kuwa, Imani hujengwa katika msingi wa sababu nzito sana. Wengi wa watu wanaoamini, huweza kukubaliana na vitu ambavyo, kwa ubongo wa kawaida, mtu asingekubali, lakini kutokana na fikra pana zaidi, watu hawa hukubali. Leo hii, mtu akikwambia alivuka Bahari, kwa kuwa ilitenganishwa kwa fimbo, kama ilivyokuwa kwa musa, Watu wengi watacheka sana. Hii ni kwa kuwa, Ubongo utaona anayeongea sio timamu, au anachekesha. Maana miongoni mwasababu za watu kucheka ni kudharau, kuona dhaifu, kutotegemea ,furaha, na hatari. Mtu anayeenda kwa Mganga huwa pia anaamini kuwa, kwa kupitia Mganga, anaweza tatua matatizo ambayo, sayansi ya kawaida, ina ukomo.

Hitimisho ni kuwa, kwa hoja za juu zote ni rahisi sasa mtu kutambua kuwa, kama Mtu anaamini kitu Fulani, maana yake anakuwa ameshauthibitishia Ubongo wake yeye mwenyewe kuwa haujui. Unauambia Ubongo kuwa bado hautambui vizuri hapa. Imani ni hatari sana pale mtu anapoitengeneza kwa sanaa hizi ambazo hazina msingi mzuri kama tutakavyoona. Mkristo wa kweli anapokuwa anahasira ya kutaka kumuua nduguye akiwa na sababu njema sana, mfano, atauwawa yeye asipofanya hivyo, Anaendelea kuamini kuwa, Biblia iko sahihi zaidi yake. na hatachukua uamuzi wa kuua. Atachukua uamuzi mwingine bora zaidi. Lakini kuna Imani mtu anaweza ambiwa aue ndugu yake, na achukue damu yake, Mtu huyu hutenda kama ilivyozoeleka kwa visa vingi vya namna hii. Maswali kama amewezaje? Hivi hana akili? Anafikiria kweli huyu? Huwezi yajibu kama hujui kuwa, Imani hukinzana moja kwa moja na sehemu za ubongo wa kutafakari.

Imani Inavyosaidia Sanaa Za Mazingaombe Na Uganga

Unapoenda kwa mganga au msanii wa mazingaombwe, unapomwamini kama tulivyoona katika sehemu iliyopita. Unapelekea mabadiliko yafuatayo katika ubongo. kwanza, sehemu ya Ubongo inayoitwa ‘’Anterior cingulate cortex’’ au ‘’ACC’’ huzima, sehemu hii huusiana na tabia za ubongo za ukosoaji wa ajenda yoyote ile, na kwa namna hii, husababisha mtu huyu kila anachoambiwa kukikubali, na Kupungukiwa uwezo wa kupima uzito wa hoja anazoambiwa. Pia Imani hii humsababisha sehemu ya ubongo wake wa mbele ‘’prefrontal cortex’’, kutotumia nguvu kutafakari na kutengeneza uhalisia wa mazingira yake. Na kwa Pamoja, haya hupelekea sehemu za hisia za Ubongo kama Amygdala, kuzidi kuwaka na kumfanya mtu awehuke zaidi kihisia.Magician sasa huwa na uwezo wa kuingizia triki zake tutakazo ziangalia mbeleni kiurahisi zaidi kwa mteja wake.

Hofu (Fear)

Hofu ndiyo kiini cha sanaa zote za mazingaombwe ‘’magic’’. hofu hutokana na sababu ya kwanza ya Imani. Mtu anayeamini kuwa, kuna uwezo zaidi ya uwezo wake wa utambuzi, au ‘’control’’ , maana huwezi control usichokitambua, Mtu mwenye Imani hii huwa na mashaka na Hofu. Hofu ni kuwa na wasiwasi juu ya kupatwa na tatizo. Hofu ni matokeo ya kutambua kuwa upo hatiani katika kuelekea kuumia. Kabla ya kupatwa na maumivu ya mwili, huanza maumivu ya kiakili, ambayo ndiyo msingi wa kuwehuka na kutotulia. Ubongo huchukulia uhalisia wa tatizo kabla halijatokea, huisi itakavyokuwa kabla haijawa. Na hatimaye husisimua mwili mzima kwa kila hali kuikimbia hali ya hatari ambayo umekwisha itabiri, kabla haijatokea.

Kifiziolojia huwa kuna swali linauliza, Unakimbia kwasababu unaogopa? Au unaogopa kwasababu unakimbia? Majibu kwa maswali yote ni kweli, Hofu haiwezi tengenishwa na hisia zozote zile za kujiepusha na tatizo. Hofu ni matokeo ya uchambuzi wa tatizo na uamuzi bora zaidi wa kujiepusha nalo. Mwili husisimka kuongeza ufanisi na nguvu za kujiepusha. Mtu anayekimbia mafuriko, ni kwakuwa ameshatafakari na kugundua upande mmoja hauna maji, Kama pande zote kuna maji, maamuzi ya kukimbia hayana maana tena. Hofu huelekeza hisia za mhemko, ijapokuwa wengi hawaligundui hilo

Hatua Za Hofu

Hatua ya kwanza

Hofu huwa na hatua zilizojipangilia kulingana na viwango au uwezo wa ubongo wa kuweza kujiokoa toka kwenye tatizo. Hofu huanza kwa kiwango kidogo kabisa pale tatizo linapokuwa ni dogo, na Ubongo una Nguvu kubwa za kujiepusha. Mfano, Mtu anayekutishia kuwa hatakupa chakula mchana, na kwa siri kumbe una mbinu yako nyingine ya kupata chakula, Hofu huwa ndogo sana kutokana na nguvu ya utatuzi wa tatizo kwa hatua hii ya kwanza. Hatua hii huwa na Nguvu kubwa sana ya Uwezo wa Ubongo, na Ubongo husisimka kidogo sana kihisia, ‘’Mtu haoneshi kuogopa’’ , kwa kuwa tayari ana suluhisho.

Hatua ya Pili 

Hofu huwa ya wastani, hii ni pale ambapo Nguvu ya tatizo na suluhisho lake hulingana. Mfano, mtu anayehofia Kuumwa ugonjwa fulani, ilihali anajua tiba yake ipo. Katika hatua hii matokeo ya tatizo yanaendelea kuwa juu, hata kama utatuzi upo. Mazingira yote ya namna hii, huwa katika kundi la hofu katika viwango vya wastani. Hatua hii huwa na Nguvu kubwa ya Ubongo, na Ubongo husisimka wastani kihisia, kuepukana na tatizo kwa ufasaha zaidi, au kwa gharama ndogo zaidi.

Hatua ya Tatu

Hofu hapa ni Kubwa. Haya ni mazingira ambayo Nguvu ya tatizo huwa mara kubwa sana ukilinganisha na nguvu ya utatuzi wake. Mfano, ikiwa namna pekee ya kumuepuka simba anayekuja uelekeo wako, na amekuona, Ni kumkimbia, Ukipiga mahesabu ya kumshinda spidi simba, Ubongo huchanganyikiwa sana, hii ni namna ya tatu ya Hofu. Hatua hii ya hofu, Ubongo huwa dhaifu sana kimipango, na husisimka hata mwisho kwa hisia. Ubongo hutumia kila njia unayoweza itumia kuepukana na tatizo, hutumia nguvu zote za mwili, hisia ambazo husisimua mfumo wa kupambana au kukimbia ‘’fight or flight’’, hulenga kuongeza mapigo ya moyo ili damu ipite kwa wingi kwenye misuli kusambaza oksijeni na sukari ‘’Glucose’’ kuzalisha Nguvu za kutosha, Uhemaji huongezeka kuruhusu hewa nyingi ya Oksijeni kuingia ndani, Macho huwa wazi sana yakiangalia kila mahali kujiokoa, sehemu zote za Ubongo wa mbele, kwa ndani na nje, huwa zinafanya kazi kwa kiwango kikubwa sana kutafuta kila mbinu ya kujiokoa.

Hatua ya Nne ‘’Magic-Level’’

Hatua hii nimeiita hatua ya ki ‘’magic’’ kwa kuwa ndiyo hatua ambayo huwa wakiilenga kisaikolojia. Hatua hii huusiana na msisimko mkubwa kabisa wa hisia kama wa sehemu ya tatu, Au kufanania. Lakini hatua hii, haihusishi kabisa matumizi ya Ubongo. Mtu huwa akiogopa mpaka mwisho, lakini hata hivyo, Imani ambayo anakuwa amejengewa, humzuia kabisa kuweza kufikiria au kutumia sehemu zake za ubongo za kujiokoa.

Katika Fiziolojia hatua hii, huusiana na sifa nyingine ambazo sio kukimbia au kupambana, Bali huwa ni ‘’Kuzimia’’ au ‘’Kukata tamaa’’, hizi pia huitwa ‘’Freeze or Faint’’. Hapa Ubongo huzima ufahamu wake ili usiweze kushuhudia hatari ambayo, ulikwisha itabiri kuwa itakuwa mbaya sana. Hoja ya msingi hapa ni kuwa, Hatari imefika, lakini Ubongo umezima. Katika hatua hii, wataalamu wa ‘’Magic’’ ambao katika sura inayofuata tutawaangalia kiundani zaidi, huweza kuwa na mafanikio makubwa sana, kutokana na badiliko kubwa la fiziolojia ya utendaji wa mifumo ya Ubongo. Kitaalamu hapa, Network za Ubongo wa Mbele hujikata kutoka network za Ubongo uletao taarifa. Hii mbinu ya kutenganisha Ubongo wa mbele na ubongo unaoleta taarifa, huaribu moja kwa moja mfumo wa ubongo wa ‘’ Hisia za Mimi’’ tulizoziona katika sehemu iliyopita. Mbeleni tutaangalia kiundani zaidi, mbinu hii inavyochochewa zaidi kwa triki zao hawa watu pana sana za kisaikolojia.

Kukata Tamaa

ni muhimu sana kukumbuka kuwa, Imani ndiyo iliyoufanya Ubongo wa mtu huyu uamini kuwa hakuna Njia, na ukajizimisha. Na pia kumbuka, kujizimisha sio lazima kuhusishe kuzimia mtu apoteze fahamu, Hapana, Huusisha hali ya Ubongo inayoitwa Kiswahili kama ‘’Kukata Tamaa’’. Biblia imesisitiza mara nyingi zaidi kuwa, ‘’Usiogope’’, na kuogopa katika Biblia ni kukosa Imani. Na hapa tena tunaona sayansi inaeleza kuwa, ukiogopa, unakata network za mfumo mzima wa utendaji wa Ubongo, tena zaidi ni mfumo wa ubongo wa ‘’Utambuzi binafsi wa mtu’’. Biblia inathibitisha zaidi kuwa, Mungu yupo na wasiokata tamaa, hata kama mbele kinachoonekana ni kifo kwa ‘’Bahari’’ na nyuma kifo kwa ‘’Jeshi la Farao’’, lakini Usiogope, Mimi Bwana Mungu wako nitakushindia. Mungu anataka mifumo ya Ubongo ya watu ibakie hatua ya tatu ya Hofu kushuka mpaka hatua ya Kwanza, kulingana na imani zao. Mungu hataki network za Ubongo alizoziumba, zizime kama ilivyo kwa sanaa za Magic.

Gunduzi nyingi sana hufanyika katika hatua ya ubongo ya tatu. Na ndiyo maana, kiwango kikubwa zaidi cha teknolojia duniani kilianzia vitani, Hasa vita ya pili. hii ni Kwasababu ya watu ambao hawakuzimia au kata tamaa, wakawa na uwezo mkubwa maradufu wa Ubongo wao wa mbele. kipindi cha Zama za Giza ‘’Dark Ages’’ hasa miaka ya 1500’s kuendelea, cha matengenezo ya Uprostentanti wakati Upapa wa kirumi ukipinga vikali matengenezo. kwa kuua waprostentanti wasoma Biblia, kuanzia zama za John Huss, Wycliffe, Martin Luther, Calvin, Wesley, n.k. changamoto zilivyozidi kuwa nyingi, ndivyo kiwango cha maarifa ya Biblia kilivyozidi kuongezeka. Marazote changamoto sio za kuzikatia tamaa, huwa ndizo Booster za Ubongo kisayansi.