Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

KWANINI GHARIKA SI YA KUSADIKIKA

Sayansi ya Gharika kuu

Sayansi Ya GharikaKuu 

Gharika kubwa ilitokea katika zama za Nuhu. Gharika hii ndiyo chanzo cha Dunia na ulimwengu kuonekana na kuwa katika namna tunaushuhudia kwa jinsi ulivyo hivi leo. Gharika ilikuwa ya ulimwengu wote na sio sehemu tu za dunia.  

Kisa Kizima Cha Gharika Mwanzo 6-8

Mwanzo 6:13 ‘’Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.’’

Mwanzo 6:14 ‘’Ujifanyie Safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya Safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.’’

Mwanzo 6:17 ‘’Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa,’’

Mwanzo 6:18 ‘’Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika Safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe.’’

Mwanzo 6:19 ‘’Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya Safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke.’’

Mwanzo 7:11 ‘’Katika mwaka wa mia sita wa Maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.

Mwanzo 7:12 ‘’Mvua ikanyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.

Mwanzo 7:18 ‘’maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile Safina ikaelea juu ya uso wa maji.’’

Mwanzo 7:19 ‘’Maji yakapata nguvu sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa’’

Mwanzo 7:20 ‘’Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.’’

Mwanzo 7:21 ‘’Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;’’

Mwanzo 7:24 ‘’Maji yakapata nguvu juu ya nchi kwa siku mia na hamsini.’’

Mwanzo 8:1 ‘’Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na Wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika Safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;’’

Mwanzo 8:2 ‘’Chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;’’

Mwanzo 8:4 ‘’Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, Safina ikatua juu ya milima ya Ararati.’’

Mwanzo 8:13 ‘’Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha Safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.’’

Mwanzo 8:18-19 ‘’Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika Safina.’’

Mwanzo 8:20-21 ‘’Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliyesafi, na katika kila ndege aliyesafi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, sitailaani nchi tena baada ya hayo kwasababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kila kilicho hai kama nilivyofanya.’’

Unaweza pia soma kisa chote tokea mwanzo sura ya sita mpaka sura ya nane. Haya ni baadhi ya mafungu muhimu ambayo yatatusaidia tunapoenda rasmi kuanza mjadala wa sayansi ya Gharika hii kubwa Zaidi kuwahi kutokea, na haita tokea tena kwa mujibu wa Biblia.

Kabla hatujaianza hii mada nitajibu maswali kadhaa ili kujenga mantiki ya uhalisia.

Maswali Yanayoulizwa Sana

1. Maji yangewezaje kujaa hata kufunika milima kama ya safu za milima ya Himalaya au Ararat?

Jibu: Milima kabla ya gharika haikuwa mikubwa kwa kiwango hiki.

2. Viumbe wote duniani wangewezaje kujaa katika Safina, tena viumbe wakubwa kama Dinoso?

Jibu: Samaki wasingeingia. na Wanyama wadogo wangekuwa mbadala wa wakubwa.

3. Samaki wa maji ya kawaida wangechanganyikaje na wachumvi?

Jibu: kwanza awali bahari hazikuwa na maji chumvi, yalikuwa ni matokeo ya gharika. na pili samaki huwa na uwezo wa kubadilika na mazingira, na mabadiliko ya muda mrefu ndiyo yaliyowatofautisha Zaidi.

4. Wanyama wangetokaje mabara ya mbali na visiwani kuja kwenye Safina?

Jibu: Nchi haikuwa imegawanyika mabara.

5. Mvua haiwezi nyesha kujaza maji dunia nzima kwa siku arobaini, maji yalitoka wapi mawinguni?

Jibu: maji hayakutoka hasa kwenye mvua, yalitoka chini ya dunia.

6. Maji yote ya gharika yalienda wapi?

Jibu: litajibiwa katika maelezo ya nadharia.

7. Sababu ya kisayansi ya Gharika ilikuwa ni nini?

Jibu: Litajibiwa katika maelezo ya nadharia.

8. Kama Imethibitishwa kisayansi kwanini isifundishwe mashuleni?

Jibu: kama Muumbaji wa ulimwengu hafundishwi?

9. Kama ni nadharia, je inaweza kuwa sio sahihi?

Jibu: Unaweza boresha nadharia kwa kuirekebisha mapungufu, ila sio kwa kuipoteza kabisa. kwa kuwa ili iwe nadharia ‘’Theory’’, lazima iwe na ushahidi wa kisayansi, ila inahitaji kufanyiwa kazi Zaidi. Mfano, Gravitation ni nadharia mpaka leo, ijapokuwa Newton aliianzisha, na Einstein akaiboresha. Na ndivyo ilivyo pia kwa gharika kuu.

Mpangilio Wa Matukio Ya Gharika Na Siku.


Taswira Ya Dunia Kabla Ya Gharika Kuu



Picha ya pili ni dunia ya awali kama ungeikata katikati ilionekana kama hivyo, na picha ya kwanza ni mwonekano wake wa nje ulikuwa wa namna hiyo. Dunia ilikuwa na sehemu kuu mbili, sehemu ya ndani na sehemu ya nje. zilizokuwa zimetenganishwa na uwepo wa maji kati kati. Sehemu ya nje pia ilikuwa na Maji, Ijapokuwa maji yake hayakuwa mengi kama ilivyo hivi leo. Dunia sehemu ya nje ilikuwa imeshikiliwa na miamba, na sio kuwa ilikuwa ikielea juu ya maji. na maji yaliyokuwa ndani ya dunia yalikuwa yamefungiwa humo, na sio maji yaliyokuwa na nafasi za kutoka nje. Sehemu ya ndani ya dunia ilikuwa na mgandamizo mkubwa, lakini ilikuwa ni sehemu yabisi, au ngumu, na ya baridi, sio moto kama wengi wanavyohisi.

Sehemu inayofuata tutaangalia namna ambavyo kila hatua katika gharika ilivyofanya mabadiliko katika mwonekano wa dunia, na ulimwengu kwa sehemu. pia muhimu sana kumbuka, hii ndiyo nadharia pekee inayoweza jibu maswali karibia yote ya sayansi za dunia, hakuna nadharia nyingine inayoweza. mchango mkubwa sana wa hii nadharia unatoka kwa Dr. Walter Brown. wapo wengi wenye michango baadhi, kama Dr. Robert na David Gentry, na baadhi ikiwemo Michael Oard. Lakini sayansi kubwa hujieleza yenyewe, sisi ni kama walaji tu, ila mwili humeng’enya chakula wenyewe na hulilima shamba lake wenyewe.

Zama Ya Gharika ‘’Flood Phase’’ Siku 0-150.

maji ya ajabu ‘’supercritical water’’

Dunia ambayo ilikuwa na sehemu kubwa ya nchi iliyokuwa juu ya maji, ilikuwa ikipitia kama ilivyo kawaida vipindi viwili vya mvuto wa mwezi, wakati wa siku na usiku. vipindi hivi hupelekea kupanda na kushuka kwa sehemu ya dunia. Ambavyo huambatana na mawimbi ya maji kupwa na kushuka. Huku kupwa na kushuka kwa maji kukikandamizwa na maili kama 60 za nchi, kulipelekea mgandamizo mkubwa sana wa maji, na pia Joto lilizidi kuongezeka katika ujazo wa maji. Kadri hali hii ya kupampiwa kwa mawimbi, kutokana na matokeo ya mwezi ‘’Tidal pumping’’ kulipozidi kuendelea, kadri muda ulivyozidi kwenda mbele, kulipelekea Maji kuzidi kuwa ya moto kabisa, na hata presha ya maji ikazidi kuwa kubwa sana. 

Maji kwa kawaida huwa na nyuzi za kuchemka ‘’boiling point’’ ambazo ni 100 celcius degrees, na kadri unavyozidi zaidi kuongeza nyuzi za joto, joto kali na presha yake huongezeka maradufu, maji hufikia point inayoitwa ‘’critical point’’. Hatua hii maji huwa katika hali ya matone ya mvuke, na mengine katika kimiminika. na hautaweza tenganisha sifa za haya maji kama ni gesi au kimiminika. maji haya huwa na sifa tofauti na sifa zake za awali, na maji haya hata unapoongeza Zaidi joto, hayaongezeki tena joto, bali huongeza zaidi nishati ya spidi ya molekuli zake, yaani ‘’kinetic energy’’. maji haya huwa na sifa ya kuyeyusha vitu kwa kiwango kikubwa sana, huyeyusha madini mengi sana ambayo yasingeweza yeyushwa kwa kutumia maji ya kawaida. Haya maji yanaitwa ‘’Supercritical water’’. Haya maji pia huwa yakitumika viwandani kwa baadhi ya kazi. 

Sifa nyingine kubwa ya haya maji, kutokana na kuwa huwa katika mgandamizo mkubwa sana, maji haya yana molekuli ndogo sana. na hii ndiyo sababu hata unapoongeza joto, unakuwa tu unaongeza Zaidi nishati ya molekuli hizi. Maji haya yanapotoka nje, hutanuka haraka sana kutokana na presha ndogo ya mazingira ya nje, hii hali ya kutanuka fasta sana, huambatana na kuganda ghafla kwa haya maji. Hii ni sheria pia inayotumika katika ufanyaji kazi wa ‘’ air conditioner ‘’ac’’ ambazo nazo hutumia mabadiliko ya presha kuchemsha na kupooza maji.

Kupasuka Kwa Vilindi Vya Maji 

Chini ya Dunia kuna miamba ambayo hiyo ilikuwa ikishikilia sehemu hii kubwa ya dunia iliyo juu. kadri muda ulivyozidi Kwenda kutokana na maji yale ya supercritical water, ntakuwa nikiyataja kifupi’’ scw’’, kuwa na sifa ya kuyeyusha sana, basi yalisababisha kuyeyuka kwa miamba mingi sana iliyo chini. ambayo hii ilipelekea sehemu ya nchi kuzidi kudidimia kwenye maji hayo ya scw. Na kadri nchi ilivyozidi kudidimia, ikikandamiza maji yale, basi na presha ikazidi kuongezeka, hii ni sawa tu na wewe ungekanyaga puto lenye maji, na ilihali tayari maji yaliyo ndani ya puto yana presha kubwa, basi hiyo itapelekea moja kwa moja sehemu za puto kulegea na hata kupasuka. Presha kubwa ya maji, na nishati kubwa iliyotokana na sababu za joto kali, na mgandamizo mkubwa wa dunia, ulipelekea sehemu kadhaa kulegea, na kutengeneza uelekeo wa udhaifu ‘’line of weakness’’. ambao uelekeo huu, ndiyo uliokuja kujiachia na kupasuka kwa vilindi vya maji. Na maji mengi kutoka nje ya dunia.

Ushahidi Wa Kisayansi Wa Matokeo Ya Supercritical Water

ramani ya dunia 

inaonyesha uelekeo wa mpasuko wa Dunia katika upande wa Bahari ya Atlantiki. ‘’along mid atlantic ridge’’. Tazama picha iliyo chini.

Hii ni picha ambayo nimeitoa mtandaoni, na unaweza ziona zote ni aina hii. huo mstari mwekundu, unadhihirisha kabisa kuwa kulikuwa na mpasuko mkubwa huko nyuma. na kama ilivyo kawaida, hautaona mpasuko huu kwa upande wa nyuma kwa sababu, matokeo ya kitu kupasuka kutokana na mgandamizo wa pande zote, huishia kupasuka kwa upande mmoja. hautawai uone mpira umepasuka pande mbili hata ukikanyagwa na gari.

Kiwango Kikubwa Cha Maji Chumvi

Uwingi wa maji yenye chumvi ni vigumu sana kuelezea kwa nadharia kama vile, maji ya chumvi yanatokana na Wanyama ambao wakifa katika vyanzo vya maji, wanapelekea uwepo wa madini chumvi. Tafiti nyingi sana zimeonesha swala hilo haliwezekani, na halina uhalisia. lakini pia kuna nadharia ya kuwa mkusanyiko wa maji ambao huwa ukieleka baharini, kama vile mito, au maji ya mvua ‘’soil run off’’, vumbi n.k vitu vya namna hii, ndivyo vilipelekea uwingi wa madini chumvi katika Bahari, nalo si kweli, na halina mantiki. wengine husema kuvuka kwa maji ‘’evaporation’’ baada ya muda mrefu, nalo halina uhalisia. maana kwa hizi nadharia zote ukiziunganisha, haziwezi kupelekea kuwepo kwa madini ya kutosha kufanya kiwango cha chumvi iliyopo baharini leo hata kama dunia ingekuwa na umri mrefu kuliko walioukadiria wa miaka bilioni 4.5.

Gharika Inajibu: 

kutokana na sifa kubwa sana ya maji ya scw kuyeyusha miamba, hasa miamba ya chini ya dunia iliyoyafunika na madini kwa ujumla. Maji ya scw yalikuwa na kiwango kikubwa sana cha madini ya sodium, calcium, chokaa, chumvi, sulfate, carbonate, silicate n.k. maji haya yalipotoka na kujikusanya, yalipelekea bahari ambazo zilikuwa zimejaa kiwango kikubwa cha maji chumvi. Kumbuka hata uchukue mabaki ya Wanyama wote na mifupa yao haitoshi kusababisha chumvi za baharini, na ndiyo maana elimu ya miamba kwa wasio amini inaleta changamoto kubwa sana kuleta uhalisia.

To be continued....