Gharika & Sayari Ndogo ‘’Asteroids’’
Asili Ya Sayari Ndogo ‘’Asteroids’’
Asteroids au sayari ndogo, nazo ni kama tu ilivyokuwa kwa Comets, asili yake ni gharika ya Nuhu. Ambapo kiwango kikubwa cha uchafu na miamba iliyotupwa na supercritical water, ilipelekea uwepo mkubwa sana wa miamba katika space. Ambayo hii ilijikusanya na kuunda asteroid.Uundwaji wa Asteroid nao ulianza kwa matokeo ya miamba kuanzisha maeneo yenye mvuto wa gravitation au ‘’sphere of influence’’. miamba hii ikapelekea miamba mingine, na maudongo kujikusanya kwa Pamoja. Kumbuka si kana kwamba ni uundwaji wa muda mfupi. ni matokeo ya kiwango kikubwa cha mvuke wa maji ambao ulichangia kwa kiwango kikubwa kuungana kwa miamba hii. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa, kuna uwepo mkubwa wa kiini cha barafu katika miamba ya asteroid.
Asteroid nyingi hupatikana katika eneo linaloitwa ‘’asteroid belt’’, lililopo katikati ya sayari ya Jupiter na Mars. Uwepo wa asteroid katika eneo hilo huwapa changamoto kubwa sana wanasayansi wasio amini katika nadharia hii. zipo nadharia mbili ambazo hujaribu kuelezea uumbaji wa asteroid.
Asteroid ni sayari iliyopasuka
Hawa hukosa Ushahidi maana tafiti za karibuni zimeonesha hata ukiunganisha asteroid zote, hazifikii ukubwa hata wa sayari ndogo. hivyo haiwezekani kuwa zilitoka kwenye sayari, na pia hakuna maelezo ambayo yangetosha kueleza ni kwa namna gani sayari ingeweza kupasuka.
asteroid ni sayari isiyokamilika
Hawa nao hukosa Ushahidi wa kujibu maswali kama kwanini zinapatikana tu Zaidi katika eneo la katikati ya Mars na Jupiter?
Asteroid ina sifa nyingi sana Ambazo zinadhihirisha kuwa inatokea duniani. Mfano, Asteroid zina miamba ambayo ina mikunjo ya maji, hapa ili unielewe vizuri chukulia mfano huu, ukiona chungu au mtungi wa udongo Utajua tu kuwa awali ulipindishwa kwa maji. Hii ni kwa kuwa, maji huwa yanatabia za kupindisha sura za vitu ‘’curve surfaces’’. na ndivyo ilivyo pia miamba ya kwenye asteroid, huonekana kama matokeo ya matope yaliyoganda. Hiyo inatudhihirishia kuwa ilikuwa ni matokeo ya gharika ya nuhu.
kwanini iwe asteroid na sio comet?
Tofauti kubwa ya comets na asteroid ni kuwa, comets ni matokeo ya miamba midogo midogo, na mavumbi ya udongo uliokuwa umebebwa na maji na mvuke, lakini Asteroid ni matokeo hasa Zaidi ya miamba. Kumbuka miamba mikubwa na midogo hurushwa na kuwa na spidi tofauti. Ambazo hupelekea kwenda kujikusanya katika maeneo tofauti tofauti katika space. Na pia, kuna kiwango kikubwa sana cha barafu iliyoganda ‘’frost’’ katika comets ukilinganisha na kwenye ‘’asteroid’’. na utofauti huu unatokana pia na uhusiano wao toka kwenye jua. Ambapo kwenye asteroid lilipelekea mabadiliko ya jua kali sana, na baridi kali sana, kutokana na uchache wa anga ‘’atmosphere’’, ukilinganisha na comet, Ambayo ilikuwa na kiwango kikubwa cha molekuli za anga dogo ‘’atmosphere’’, na kupelekea madhara kidogo ya jua. hii unaweza elewa kirahisi katika namna hii, comets zilikuwa na mavumbi mengi, na mvuke mwingi mithili ya anga ambalo lilizuia jua kali. ila asteroid zilikuwa hasa ni miamba.
kwanini asteroid nyingi zipo katikati ya Mars na jupiter?
Miongoni mwa sababu zinazoweza pelekea kitu kikasogezwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ni tofauti ya nyuzi joto, hasa katika upande wa mwanga na giza. Hii huitwa ‘’radiometer effect’’. yaani huwa hivi, unapokuwa na kifaa kama radiometer, ambacho kina sehemu ya weusi na weupe. Ukikimulikia, utaona kikizunguka. Hiyo ndiyo namna pia ilivyokuwa kwa asteroid ambazo zilikuwa karibu na Jua. tofauti kubwa ya upande wenye mwanga, na wenye giza, ilipelekea kiwango kikubwa cha hewa yenye joto iliyokuwa ikitoka maeneo ya ndani ya karibia na jua, ‘’inner solar system’’ kusukuma Zaidi maeneo yaliyokuwa meusi ya asteroid, kuliko yaliyokuwa meupe.
kumbuka kuwa kitu cheusi hupata joto Zaidi ya cheupe. na pia hupoteza fasta Zaidi joto dhidi ya cheupe. tofauti hizi za joto zilipelekea asteroid kuanza kuzunguka huku zikielekezwa nje Zaidi ya mfumo wa jua, hata zilipofikia karibia na maeneo ya Jupiter na Mars, ambapo zilitulia. na hiyo ni kutokana na kupungua kabisa kwa hewa zilizotoka kwenye gharika. ambazo zilikuwa zikisukumwa kwa matokeo ya kuchomwa ‘’heated’’ na jua.
Juu ni picha za radiometer. radiometer effect iliweza kutoa nguvu ya kutosha ya kuweza kusukuma asteroid, kwa kuwa tayari asteroid hazikuwa katika kani ya mvuto wa gravitation ya dunia. na hivyo hazikuwa na kiwango kikubwa cha ukinzani wa msukumo kama ambavyo zingeweza kuwa zikiwa duniani.
Picha chini ni sayari ndogo ‘’asteroid’’ kubwa Zaidi inayoitwa ‘’Ceres’’. hii ni kubwa kwa saizi ya 1/3 ya saizi ya ukiunganisha asteroid zote zilizopo. pia katika picha, unaweza ona ‘’asteroid belt’’ ambayo inaonesha matokeo ya gharika ya nuhu. Lakini pia unapaswa kukumbuka kuwa, asteroids zote na vimondo na TNOs na comets zote, ni kama asilimia 3% tu ya dunia. na wala hupaswi kuaminishwa kwa picha zake, ukahisi ni kweli walikuwa ni Watoto wa sayari kama wengine wasiojua ukweli huu, wanavyoaminishwa na wanaanga wasio jua kisa cha gharika na sayansi ya gharika.
Pia katika picha hii unaweza pata taswira ya asteroid belt na hata Kuiper belt tutakayo iona baadae, lakini kumbuka huu ni mchoro na sio picha. hivyo mtu asihisi kuna uwingi wa kiasi kama kinachooneshwa hapo wa asteroids na kwa saizi hizo.
Hizi ni picha za satalaiti za asteroid ceres unaweza ona namna miamba yake inavyoonekana kuwa ni matokeo ya maji.






Join the conversation