Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

NADHARIA HASI ZA UBONGO KIJINSIA

NADHARIA HASI ZA UBONGO KIJINSIA

Nadharia Za Utofauti Wa Ubongo Zilizopitwa Na Wakati

1.


watu walioendelea zaidi katika ubongo wa kushoto au ubongo wa kulia

Ilikuwa na imekuwa, na inaendelea kuwa kwa baadhi ya wasomi, nadharia yenye mapenzi makubwa sana kwa watu. Nadharia hii ijapokuwa imepitwa na wakati, lakini ilikuwa na nguvu sana hata kumfanya mgunduzi wake, mtaalamu wa Ubongo, Sir.Rogers kupatiwa tuzo ya mwanasayansi bora wa mwaka ‘’Nobel Prize’’. Hii ni baada ya kusema kuwa, amegundua kuwa ubongo wa kushoto sio sawa na ubongo wa kulia. Sir.Rogers na mwenzake mwanasaikolojia waligundua hili kipindi wanafanya matibabu, kwa kuja na mbinu ya kukata Katikati ya pande mbili za ubongo ‘’Interhemispherectomy’’, kwa lengo la kuzuia magonjwa kama ya Kifafa kinachosambaa kati ya pande mbili zote za ubongo, yasiuathiri sana ubongo. Lakini pia kuzuia shida zingine nyingi ambazo zinaweza athiri pande zote mbili za ubongo. Katika ugunduzi wao, waligundua kuwa, Upande wa kushoto wa ubongo ni kana kama una kazi zake maalumu kabisa, na upande wa kulia nao una kazi zake maalumu kabisa. Sasa, katika kuziunganisha kazi hizi, ndipo ikaonekana kama vile, kazi Fulani za ubongo hufanyika zaidi upande Fulani, na zingine hufanyika sana upande mwingine. 

Ubongo wa kulia siku zote huongoza upande wa kushoto, na ubongo wa kushoto huongoza upande wa kulia, hivyo basi, kama ilivyo kwa upande wa mkono wa kushoto usivyokuwa na uwezo mzuri wa kupangilia au kulenga, basi na hata upande wa kulia wa ubongo, hauna sifa ya mipangilio. na hapo ndipo ikazaliwa nadharia ya kuwa, watu wote wenye sifa nyingi sana za upande Fulani wa ubongo, basi wao wameendelea zaidi katika upande huo. Na hapa unaweza ona kama ifuatavyo,

Watu Waliobora Upande Wa Kushoto _Left Brained

huwa wana uchambuzi wa kina sana wa mambo ‘’Analytical’’. Huwa wana ufatiliaji na uchambui wa kina wa mambo ‘’Logical’’. Huwa wanapitia hatua baada ya hatua katika njia zao ‘’methodological’. Huwa wanajua sana Hisabati na taaluma za lugha

Watu Waliobora Upande Wa Kulia _Right Brained

Huwa wana uwezo mkubwa wa kutengeneza taswira. Huwa wana uwezo mkubwa wa Ubunifu ‘’creative’’. Huwa wana uwezo mkubwa katika sanaa na muziki. Wana uwezo mkubwa wa kusoma hisia za wengine na huguswa sana na jamii zao. Si wazuri sana katika taaluma za upangiliaji wa kina.

Changamoto Kubwa Za Nadharia Hii

  • Hoja ya ubaguzi na ukandamizaji wa kijinsia na kijamii

Rejea tafiti zifuatazo kwenye vyanzo vikubwa vya taarifa kama WIKIPEDIA

Chanzo hiki kinatoa taarifa katika Nukuu zake ambazo Msomaji wake lazima ataishia kwenye hitimisho la kuwa , ni kweli kuna tofauti za Ubongo kati ya ubongo wa kushoto na kulia hata kwa Jinsia, ikinukuliwa kutoka kwa hiki chanzo inaonekana kama vile wanaume wana uwezo mkubwa katika upande wa kushoto wa ubongo, na wanawake upande wa kulia. Mbinu ambayo Wikipedia wameitumia inatia mashaka sana, kwa kuwa, wanasema tafiti iliyofanywa mwaka 2008, ilionesha hakukuwa na tofauti kijinsia kwa pande mbili za ubongo yenye maana, ‘’lakini ipo, wanachomaanisha’’ halafu wanatumia hoja hiyo kukinzana na tafiti inayofanywa mbeleni zaidi, yaani mwaka 2014, ambayo hii inakazia zaidi uwepo wa tofauti za ubongo kati ya pande mbili za ubongo. ‘’ukikumbuka pia na namna watu huamini mara zote tafiti zinazofanywa mwishoni zaidi’’ unapata jawabu kuwa, hii nadharia ambayo haina nguvu kisayansi, bado ina nguvu sana kwenye baadhi ya vyanzo vikubwa vya taarifa.

Ubaguzi Uko Wapi?

Hoja hii inaonesha kana kama uwezo mkubwa wa kitaaluma wa vitu kama sayansi pana, hisabati n.k. ni uwezo ambao huwepo kwa baadhi tu ya watu walio na sifa pana zaidi za ubongo wa kushoto, na kuwa, watu wenye ubongo wa kulia zaidi, wao huwa ni watu wenye uwezo mpana tu katika ugunduzi, au sanaa za kijamii, na uwezo wa kujali jamii zao kwa kuweza kuelewa hali za wenzao. Na kwa tafiti kama ya Wikipedia tuliyoiona, inaweza jenga msingi wa kuonesha kana kama uwezo mkubwa wa kushoto upo zaidi kwa wanaume, ukilinganisha na wanawake. Lakini haishii hapo tu, huwaweka wasanii wengi kama watu wenye uwezo wa kulia zaidi wa ubongo, na wanasayansi au watu wenye kufikiria sana kama watu wenye uwezo sana wa kushoto wa ubongo.

Kufeli Kutokana Na Tafiti Za Ubongo Za Kisasa Zaidi

Kadri sayansi ya ubongo ilivyozidi kupiga hatua ndipo ilipogundulika kuwa, Ubongo ni mpana sana na huwezi kuupunguza kwa kuuelezea kwa kutumia upande mmoja zaidi wa ubongo. imeonekana kuwa, Pande zote za ubongo huwa zikishirikiana kwa Pamoja, katika kufanya jambo lolote lile. Hata mtu anapokuwa akifanya mahesabu, kipindi ubongo wake wa kushoto ukiwa unatengeneza mpangilio wa hisabati, ubongo wake wa kulia huwa ukizichunguza namba vizuri. Kwa hivyo, hakuna kitu kinaitwa ubongo wa kushoto zaidi au ubongo wa kulia zaidi. Mara zote huwa kuna ushirikiano katika sehemu zote mbili za ubongo hata kwa kazi ambazo huwa zinaonekana kutegemea zaidi upande mmoja.

Pichani ni Mwasayansi wa Ubongo Dr. Lain McGilchrist. Ni mwanafalsafa ambaye anaamini Tofauti za Ubongo wa kushoto na kulia ni dhahiri na chanzo Cha shida nyingi za kiakili na kitabia ni kushindwa kutawala udhaifu wa upande mmoja wa Ubongo, hasa wa kulia.



2.

Nadharia Za Kuwa Ubongo Wa Kiume Na Wa Kike Ni Sawa Kabisa

Nadharia hizi zilizaliwa kipindi cha sera kali za usawa wa kijinsia. Na hizi nadharia zilikuwa na ajenda nzuri tu ya kuonesha kuwa, hakuna kitu kama jinsia moja kuwa, haina uwezo mkubwa wa kufanya kitu Fulani ukilinganisha na jinsia nyingine. Kwa kweli kulikuwa na ugandamizaji sana wa kijinsia, na hasa maeneo ya Afrika ambayo hata Watoto wa kike walikuwa hawasomeshwi kwa kuaminiwa kuwa hawawezi kabisa. Na siyo hivyo tu, hata nafasi za uongozi na zozote zile za juu, ilionekana kana kama haziwezi shikiliwa na wanawake. 

Na kipindi wanahistoria wengi wananukuu kuhusu Afrika, wanasahau kuwa hata Ulaya pia mifumo hii ya kiugandamizaji ilishamiri sana, unaweza rejea tafiti kadhaa ambazo ziliwahi fanywa huko nyuma ulaya na kuonesha kuwa, kwa Ujumla IQ test za wanawake na wanaume zilionekana kwa matokeo ya wanawake kuwa chini kidogo ukilinganisha na wanaume. Na kipindi mtu anawaza sana kuhusu hilo, walionesha pia hata IQ test za watu Weusi, na weupe au wazungu, zilionesha watu Weusi kuwa na matokeo kidogo chini ya watu weupe. Binafsi naona hizi zilikuwa ni zama za ujinga hasa, na watu hawakupaswa kuzichukulia kwa hisia kama ilivyochukuliwa kwa miaka kadhaa mbele, ambapo watu wakaanza rasmi kupambana na chochote kile, kinachohusiana na kuonesha kuwa kuna uwezekano wa kuwa na utofauti.

Ni kama Spring ukiiminya sana, utakapoiachia, itajinyoosha hata kuzidi urefu wake. Kutokana na ugandamizaji sana uliokwisha tokea, nadharia zilianza kurekebishwa kurekebisha hata visivyorekebishika, na hapa hasa ndipo tunapozungumzia nadharia hii, ambayo ilizaliwa na kuja na msingi wa kuwa, ubongo wa mwanamke ni sawa kabisa na ubongo wa mwanaume. Nadharia hii inakinzana hata na Vitabu vya Imani, vinavyomtambua mwanamke kama mwanamke na ubongo wake, na mwanaume kama mwanaume na ubongo wake. Hakuna aliye bora zaidi ya mwenzake, lakini hakuna aliye sawa kabisa na mwenzake.

Mbinu Za Kusukuma Ajenda Hii

Kupingana na nadharia nyingi za sayansi ya ubongo ambazo zinaweza tengeneza msingi wa kuonesha kuwa kuna tofauti za ubongo kijinsia. Na hii ni Pamoja na kusukuma zaidi nadharia ambazo zinazonesha kuna kundi hata makundi mengine ya kijinsia ambayo yanaweza wekwa Katikati, kama Mashoga. Ukirejea hoja nyingi za kundi la watu linaoitwa ‘’Bisexual’’, hawa ni watu ambao hujiweka katika namna ambayo wanaweza kuwa na jinsia yoyote ile, na sayansi inasukumwa kutoa sababu zao. ‘’hii ni sawa na kusema, Ubongo wa mwanamke, au ubongo wa mwanaume pia, unaweza jibadilisha na kuwa popote pale. hoja hizi zinajenga msingi wa kuwa, hakuna kabisa tofauti za ubongo kijinsia.

Kuonesha kuwa sayansi zote zinazolenga kuonesha kuwa kuna tofauti za kijinsia, basi ndani yake kuna hoja za kiugandamizaji wa kijinsia na hazipaswi kukubalika.

Kutumia Filamu nyingi sana kuonesha namna ambavyo wanawake, wanaweza kufanya hata kazi ambazo jamii isingeamini kabisa kama wanawake, wangeziweza kuzifanya, kama wanavyofanya wanaume, na hivyo hivyo kwa upande wa wanaume. Watu wengi huwa hawajui kwanini filamu nyingi huwa zina ajenda za ushoga, ajenda za wanawake wenye sifa za kiume n.k. Biblia imeandika kuwa, haimpasi mwanaume kuvaa nguo za mwanamke, na mwanamke kuvaa nguo za mwanaume. Hapa haimaanishi tu mavazi, mavazi ni kielelezo cha tabia. Haiwapasi wanawake kufanya majukumu ya kiume, na wanaume ya wanawake. Haimaanishi majukumu ya Maisha kwa ujumla, bali yale majukumu yanayotambulisha jinsia Fulani.

Kufeli Kwa Nadharia Hii

Kila siku tafiti mpya huonesha zaidi tofauti za ubongo wa kike na wa kiume. Na hizi tafiti zimejikita zaidi katika kuchambua namna bora zaidi za matibabu, kwa kuwa inaaminika sasa kuwa, hata baadhi ya matibabu ambayo huwa wanapatiwa jinsia Fulani, yanaweza yasiwe bora sana kwa jinsia nyingine. Hii ni kwa kuwa, zipo tofauti nyingi sana za kijinsia hasa katika ngazi ya chini kabisa ya kibiolojia, kumbuka hata kila seli ya mwanamke sio sawa na ya mwaname, (XX sio sawa na XY chromosomes). ijapokuwa tofauti hizo zipo kwa ngazi ya chini zaidi, ila kumbuka, binadamu tunafanana na tunatofautiana pia.

Kufeli kwa pili huwa pale ambapo, kila mwanaume anapokuwa katika nafasi ambayo alipaswa awepo mwanamke, huaribu kweli kweli. na hata pia kila mwanamke anapokuwa katika nafasi ambayo alipaswa awepo mwanaume, anaharibu pia. Hii ni kwasababu ambazo hata ukizijua, huwezi zibadilisha. Mfano mzuri ni huu, mwanamke hata akijua kuwa kazi hii wanaume huifanya vizuri zaidi kwa kuwa wana misuli mikubwa zaidi, hawezi badili uhalisia huo, hawezi jibadilisha, hata akijibadilisha awe na misuli zaidi, hatakuwa tena mwanamke, ila hatakuwa pia mwanaume, atakuwa tu amejiharibu. na mwanaume pia hata akijua kuwa, mwanamke hapa anaweza vizuri zaidi kwa kuwa anakumbuka na kuzingatia vizuri zaidi, hawezi jibadili akawa hivyo, na hata akijaribu kuchukua hatua kujiboresha zaidi, atajiharibu tu au jichosha zaidi. Asili ina machaguo yake.

Msingi Wa Hisia Za Ugandamizaji Wa Kijinsia Uliofichika

Shoo Hypothesis

Inahitaji akili nyingi sana na hisia chache kuelewa hapa. Kama ilivyokuwa katika Biblia Mwanzo3:5, Shetani alimwambia Eva, ‘’Mungu anajua siku mtakayo kula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu’’. Shetani alikuwa ana ajenda ya usawa wa kila kitu tokea awali sana katika historia. Hapa alikuwa na ajenda ya usawa wa Binadamu na Mungu. Lakini pia shetani akiwa kabla hajaasi mbinguni anaelezewa ukisoma Isaya 14:13 inasema ‘’nawe ulisema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbinguni,nitakiinua kiti changu kuliko nyota za Mungu, nami nitaketi juu ya mlima wa makutano, katika pande za mwisho za kaskazini. 14, nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na Aliye juu.’’ Hapa inaonesha ajenda yake ya usawa ilianzia mbinguni, ya yeye kutaka kuwa sawa na Mungu.

Kwa msomi wa Biolojia lazima atambue kuwa, hakuna kitu Usawa katika sayansi. Ila kuna Utofauti ambao ndiyo unatengeneza msingi wa uhitaji. Hisia za kuamini mwanaume na mwanamke ni sawa kabisa na hata majukumu yao yanaweza pishanishwa tu, huondoa utaratibu wa asili wa fiziolojia za utendaji. Hata mwonekano wa simba dume au Jogoo, sio sawa na mwonekano wa simba jike au temba. Hawa wote ni kundi la Mammalia ambalo na Binadamu tupo Pamoja nao, kama leo hii mwanamke anayeamini kuwa anaweza fanya kila kitu kama mwanaume anavyofanya, au mwanaume anaemini anaweza fanya kila kitu mwanamke anachoweza fanya, mtu huyu angezaliwa katika namna ya simba dume au jike, au kuku, yaani jogoo au temba, sidhani kama angeamini kama hiyo ingeweza kuwa hoja yenye mashiko. Biolojia yote inakataa usawa wa kijinsia mpaka katika sayansi za Ubongo.

Tatizo Lililoibuka Karne Ya 17 & 18

Miaka ya 1700’s-1900’s kuliibuka kundi kubwa sana la wanasayansi ambao zaidi walikuwa ni wanafizikia, na kisha wanakemia na wanasayansi wa asili, na Maisha, wa awali kabisa (biolojia na sayansi za dunia). Hawa jamaa wafizikia na falsafa walikuwa na matokeo makubwa sana katika jamii zao, hasa kwa kuja na maendeleo makubwa sana ya fizikia na hisabati ambazo, ndizo zilikuwa misingi mikubwa sana ya gunduzi za teknolojia za miundombinu, hasa ya vifaa vya kisasa, ikiwemo na teknolojia za anga. Jamii ilianza kuamini kuwa, Taaluma za mtindo wa hawa jamaa ndizo kipimo pekee cha uwezo wa kiakili. Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Hii ni kwa kuwa, sifa kubwa sana ya hawa jamaa ilikuwa ni uwezo wa kutengeneza miundo mbalimbali katika vichwa vyao, kwa kutumia hisabati. na walikuwa wakishindana sana wao kwa wao, na walikuwa wakishindana sana katika kupambania nchi zao, ambazo zilikuwa katika vipindi mbalimbali vya mpito, na kwa baadhi ya zama zilikuwa ni vita. Jamii ilipoaminishwa kwamba hiki ndicho kipimo pekee cha akili, ikaanza kuwalinganisha watu hawa na kila kundi la watu, na kupima kama hao watu watakuwa na akili sana au kidogo. Kwa msingi huu, ikaanza kuonekana kuwa, jamii nyingi ukiachana na ulaya, wana uwezo mdogo kidogo ukilinganisha na jamii za ulaya, kwa kuwa hawana maarifa kwa kiwango cha yaliyokuwepo ulaya. Lakini pia, ikaonekana, kwa kuwa, wimbi lile kubwa lilihusisha zaidi wanaume, basi wanaume wana wastani wa kuwa juu zaidi ya wanawake kimaarifa. 

Na kama mwanamke atataka aonekane kuwa ana kiwango kikubwa cha maarifa, naye awe na uwezo wa mtindo huo waliokuwa nao wanaume wale wachache. Kwa hiyo sasa, Falsafa ya kuwa ukiwa na uwezo mpana zaidi katika sayansi, basi una uwezo mkubwa zaidi wa kiakili ikazidi kupamba moto. Watu wakawa wakishindana sana katika sayansi ili kuonesha kuwa wanauwezo mkubwa sana kiakili. Wataalamu wa elimu zingine wakawa hawaonekani tena kama watu wenye uwezo wa ziada, na hapo tatizo likawa likizidi kupamba moto bila kujua yafuatayo.

Sababu Za Ubora Wa Wanaume Katika Hisabati Na Fizikia


Mwezi wa kwanza, mnamo mwaka 2005. Aliyekuwa Raisi wa moja ya Chuo kikubwa zaidi duniani, Harvard University, aliyeitwa Lawrence Summers, aliwataharuki sana wasomi na jamii yake kwa ujumla pale alipokuwa akitoa hotuba katika moja ya mikutano ya taarifa za matokeo ya tafiti ‘’National Bureau of Economic Research’’, alisema, ‘’Inaonekana Dhahiri katika Nyanja mbalimbali za shughuli za kibinadamu kuwa, uwezo wa Hisabati na uwezo wa kisayansi. Kuna Ushahidi wa wazi kabisa, unaoonesha tofauti yoyote ile katika wastani wa Nyanja hizo, ambayo inaweza fanyiwa mdahalo, itaonesha moja kwa moja kuwa, kuna upishano wa wastani. Pia kuna tofauti kubwa kati ya jumuiya ya wanawake na wanaume. Na hiyo ni kweli kulingana na sababu ambazo zinasababishwa na mitazamo ya kijamii, au tamaduni, na zisizosababishwa nazo” Jamii yote ilipigwa butwaa kuwa anasema kuwa, wanawake wana uwezo mdogo katika Nyanja hizo na hivyo hawawezi kuwa wanasayansi na wanamahesabu wa juu kabisa.

Kabla hatujaangalia kwa undani zaidi, Mama Louann Brizendine ambaye ni mtaalamu mkubwa sana wa Ubongo, mtazamo wake juu ya kauli hii, ulikuwa wa pande zote mbili. Anasema Summers hakuwa, na alikuwa sahihi kwa Pamoja. Kwake alisema, kulingana na tafiti za kisasa zaidi inaonekana kuwa, mpaka wanapoingia na kumaliza miaka ya kumi na kitu ‘’teen years’’, hakuna tofauti yoyote ile ya uwezo wa masomo ya sayansi na hisabati kwa wavulana na wasichana. Lakini baada tu ya miaka hiyo, kiwango kikubwa cha Estrogen ambacho huwa kikubwa sana kwa wanawake, huwafanya kuongeza mapenzi yao kwa vitu vya hisia, stori, marafiki zao, mambo ya kijamii n.k. wakati huo huo kiwango cha testosterone kinakuwa hata kikubwa zaidi kwa wanaume, na kuwaongezea zaidi hali ya kupenda upweke, na ufuatiliaji mpaka mwisho. Na hapo ndipo tofauti inazaliwa, na sio kuwa wanawake huwa hawawezi, ila huwa wanasukumwa zaidi kukata Kamba. Kauli yake ilinikumbusha stori zote za wanafizikia wakubwa ambao huwa wanasifa kubwa zaidi ya kufanya mambo yao kipweke, na wengi wao huwa hawana hata muda wa kuoa, au hata kula na usafi kwa baadhi.

Moja, Wanaume hawana uwezo mkubwa katika hisabati na fizikia, ila wana urahisi sana wa kuwa bora sana katika hisabati na fizikia.

Kwanza; masomo haya yanahusisha sana uwezo wa kutengeneza taswira na maumbo mbalimbali katika ubongo, uwezo ambao wanaume huwa wanao kwa asili kama tulivyoona juu tulipokuwa tukizungumzia ‘’spatial skills, mental rotations na parietal networks’’. Wanaume huitwa pia kisayansi ‘’map readers’’ kwa uwezo wao mkubwa wa kuzielewa ramani na michoro vizuri, na haraka zaidi. Fizikia kama ya newton au einstein, imejaa michoro na maumbo ya ulimwengu na vitu, Na pia namna hisabati zinavyosaidia kuunganisha pointi moja na nyingine, na kumbuka, sio kwamba wanawake hawawezi kuelewa hii michoro, ila wanaume huielewa kirahisi zaidi na hivyo huwa na ufanisi zaidi .

Pili; Hisabati na fizikia ni aina ya masomo ambayo hutumia sana mbinu ya test and error au mbinu ya kujaribu sana, na kurekebisha makosa madogo madogo, jambo hili huitaji muda mwingi sana ambao humhitaji mtu kuwa na muda mwingi mwenyewe, akijaribu na kujaribu zaidi ili awe bora. Hii huitaji uwezo mkubwa sana wa kuweza kuishi kipweke, huku ukilazimisha na kukamia sana mpaka utakapotimiza lengo. swala hili huitaji nguvu kubwa sana ya homoni za Testosterone, ambazo humpa mwanaume faida, ukilinganisha na mwanamke ambaye huwa na vipindi mbalimbali ambavyo hujisikia amani zaidi kuhusiana sana na jamii zake, na mwanamke ambaye huwa wakujitenga sana akikamia sana malengo yake, huchukuliwa vibaya na mitazamo baadhi ya kijamii.

Tatu; msingi wa sayansi za fizikia na hisabati pia unahusiana sana na mitazamo ya kiushindani sana. Na ndio maana utakuta timu za wanafizikia zikiwa nyuma ya ujenzi wa makombola ya kivita kama bomu la nyuklia enzi za ‘’manhattan project’’ n.k. hizi sanaa zote za Upambanaji huwa na mvuto sana kwa wanaume kama ilivyo kwa kawaida, wanaume hupenda sana kushindana. Na ndiyo maana maendeleo yote ya fizikia kuanzia enzi za Corpenicus, alikuwa na migogoro na upapa wa kiroma, Keppler na Galileo ambaye pia aliuwawa na waroma, Newton alikuwa na migogoro na Leibniz, Laplace alikuwa zama za Napoleon na alipingana na Newton, fikikia ya zama za 1900’s zama za kina einstein, plank, Bohr, schrondinger, von neuman, feynaman, edward teller, tesla, edison hata kwa wanamehesabu kama euler, Gauss n.k ilijaa migogoro mtupu, ilikuwa ni huyu akishindana na huyu, au huyu akimpinga huyu, hata ukienda kwenye maendeleo ya ufundi wa magari ya kwanza kabisa, utakutana na misukumo ya vita ya pili na hivyo hivyo kwa kila kitu. Hoja ya msingi hapa ni kujua kuwa, kuna nguvu kubwa sana ya ushindani ambayo pia huwasukuma wanaume kufanya vizuri zaidi kwenye masomo haya, na hata katika mazingira ya kawaida, wanaume tangia wakiwa Watoto wadogo, hupenda sana kushindana shindana ukilinganisha na wanawake, hivyo kujaribu kumuweka mwanamke katika vipimo vya muundo huu hupingana sana na uhalisia wa jinsia. kumbuka, sisemi kuwa wanawake hawana uwezo huo, wanao tena mkubwa sana, ila hoja ya msingi ni kuwa, kudanganywa ni kuhisi uwezo mkubwa wa hisabati na fizikia ndio uwezo wa kiakili.

Uhalisia kuwa uwezo wa hisabati na fizikia sio uwezo mkubwa wa kiakili

Uwezo wa hisabati na fizikia ni sehemu tu ya uwezo wa kiakili, ni kama tawi mojawapo tu katika mti ambao ndio uwezo wa kiakili. Uwezo wa kisayansi kiujumla ni tawi moja tu kati ya sehemu pana zaidi ya maarifa.

Uwezo uliosahaulika Shoo Hypothesis

Huwa napenda kutumia mfano mmoja mwepesi sana, mtu anaeweza kusababisha tatizo kubwa sana halafu akashindwa kulitatua, na mtu ambae anaweza kulitatua tatizo kubwa sana na akashindwa kulitengeneza, nani atakae kuwa akiheshimika sana katika jamii? Jamii huwaheshimu sana watu wanaoweza kutengeneza matatizo makubwa sana, na ndio maana watu huwaogopa sana wanajeshi kuliko madaktari. Asili imewapa faida sana wanaume kuwa na uwezo mkubwa sana wa kupambana, lakini hawana uwezo uwezo mkubwa wa kutengeneza maana ya wanachokipambania. Na ndivyo ilivyo kinyume pia kwa wanawake. Wanawake huwa na uwezo mkubwa sana wa kuelewa na kujali kilicho katika akili za wengine, na uwezo huu huitwa ‘’Emotional Intelligence’’. na kwa kuwa uwezo huu huwa ni mkubwa sana katika msingi wa kutengeneza amani, basi huonekana kama wa kawaida sana. Lakini kwa yeyote anayehisi uwezo huu ni wa kawaida, ni matokeo tayari ya kuathiriwa na saikolojia ya swali nililoliweka hapo juu, kwa kuwa, asili imewapa wanaume faida kubwa ya uwezo wa kupambana, basi imeonekana kana kama ‘’upambanaji ndio sifa pekee ya ubora’’, na kumbe asili pia imewapa wanawake sifa kubwa ya ulezi, lakini ‘’ulezi unachukuliwa sifa ya kawaida sana. hiki kitu sio kweli kabisa.

Na unapo rejea katika Biblia unakutana na nadharia hii tena, Mungu anamwambia Adamu ‘’Utakula kwa jasho na miiba itakuotea’’ na eva anaambiwa ‘’kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa juu ya mumeo naye atakutawala’’. Mwanaume anapewa laana ya kupambana katika hali ngumu zisizoridhisha, na biolojia yake ya homoni inaonesha kiwango kikubwa cha homoni za ghadhabu ‘’testosterone’’, na uwezo mkubwa wa kuvumillia maumivu ‘’kumbuka, PAG’’. hiyo hali ya upambanaji inajitambulisha kwa kila mwanaume, na ndiyo maana tuliona awali, kwa mwanaume na mwanamke wa umri sawa, wanaume huwa na wastani wa ukubwa wa ubongo kwa asilimia 8-13%, Pamoja na misuli na mwili kwa ujumla, huku akizidi kwa homoni ya Ghadhabu kwa mara 25 zaidi ya mwanamke. hii tayari inamtambulisha yeye kama Mpambanaji. Lakini hapohapo tayari mwanamke anaonekana kuhitaji ulinzi na nguvu toka kwa mumewe, na huku akiwa mpole asiye na hasira kama mumewe, hii ni sawa na kutawaliwa katika Biblia. Mwanamke kuzaa kwa uchungu kibiolojia ndio msingi wa uzalishaji wa Oxytocin nyingi zaidi na kuunganishwa kiupendo zaidi na uzao wake ‘’maternal bond’’, huu ndiyo msingi wa wanawake kuumia zaidi kutokana na uharibifu wa uzao wao kihisia. kumbuka wanawake huathiriwa zaidi na stress na huisi zaidi maumivu ya wawapendao kupitia ‘’MNS’’. Hivyo haishangazi kuona uwezo mmoja ukipuuzwa lakini haitabadilisha hoja ya kuwa, Adhabu za Mungu zilikuwa ni sawa, ila zilipishana na ndivyo ilivyo pia katika Ubongo. hitimisho ni kuwa, wanawake hawapaswi kuhisi wanagandamizwa, wanapaswa kutumia zaidi uwezo wao ili hali wakijua, huwa ni uwezo usioonekana kirahisi kama ilivyoandikwa.

Ufupisho

Uwezo mkubwa kabisa wa kiakili mtu yeyote yule anaweza uonesha, ni Upendo. jambo lolote lile ambalo mtu atalifanya kwa akili zake zote, kama litalenga katika kupendezesha zaidi jamii yake, kwa kuongezea uzuri au kuondoa matatizo, hilo ndilo linamtambulisha ana akili kwa kiasi gani. Mungu aliumba kila jambo jema na ndiye mwenye akili zote, hakuwaza aumbe mabomu au magonjwa ya milipuko, ila aliumba uwezo wa kuimba miziki mizuri kabisa, na maua ya kupendeza, sayari na nyota n.k. sio kila uwezo utaonekana kwa nje, huwezi ona mwenye Huruma zaidi, ila unaweza mwona mwenye Hasira zaidi kwakuwa hukunjisha sura. hakuna tuzo ya Nobel Prize ya fizikia kwa Afrika, lakini hakuna Bomu la Nyuklia pia lililotua Afrika. Na hata bomu lilikuwa ni matokeo tu ya fizikia rahisi ya ‘’Nuclear chain reactions’’, taswira pekee unaoweza ipata hapa, Kutaka Sifa huwafanya watu wasahau uwezo waliokwisha kuwa nao. Biblia huonesha Yesu na Yakobo na Yusufu wote walikimbilia Afrika enzi za Dhahama kubwa nchini kwao, toka zamani sana, Amani huwa haina mshindi kama ilivyo vita. Hivyo basi falsafa za kigandamizaji zisilete madhara ya kisaikolojia kwa mtu yeyote yule, hakuna Jinsia yenye ubora wa uwezo wowote ule zaidi ya nyingine, ila tu ni utofauti na tafsiri za watu.

Mgogoro Wa Kijinsia Wa Nafasi Za Juu Kabisa Za Uongozi

Kumekuwa na changamoto kubwa sana siku za karibuni juu ya jinsia gani yafaa zaidi kuchukua nafasi za juu kabisa za uongozi. Na kinachoshangaza ni kuwa, mgogoro huu umeingia hata kwa baadhi ya taasisi za dini. Hoja hizi zina nguvu sana kijamii na hata katika dini kwa kuwa, ajenda za usawa wa kijinsia zimeambatana na hoja za kihisia sana, mfano mzuri kabisa ni kama pale ambapo, tuna uwezo wa kusisitiza umuhimu wa malezi ya baba pekee kwa mtoto, kwa kutumia visa vya malezi dhaifu kabisa ya baadhi ya wamama, na visa bora kabisa vya malezi vya baba pekee. Hizi hoja ni kama vile hoja za kisiasa. Na kitabu hiki hakina nafasi ya uchambuzi wa mitindo hiyo, tukirejea katika sayansi huwa tunachambua hoja kwa namna yake ya kihalisia kabisa, bila kuangalia matokeo ya madhara Fulani. ni kama ambavyo tunavyozungumzia sifa za kiume, tunamzungumzia mwanaume alie timamu kimwili na kiakili, kwa asilimia zote na hivyohivyo kwa mwanamke.

Tukianza na maana za Uongozi tunaweza pata jibu haraka sana, zipo maana nyingi lakini zote huwa na misingi hii, Mtu ambaye ni mbeba maono ‘’missions na visions’’ kama ilivyoandikwa Nikimnukuu rafiki yangu Daktari na Mwalimu Mihambo Masasila katika kitabu chake cha Uongozi bora. kiongozi anaongoza uelekeo wa kufikia Dhumuni kuu la jamii yake. Kiongozi hutofautiana na anaowaongoza kwa namna za jinsi yeye ambavyo hutoa Maisha yake, au nguvu zake, au muda wake zaidi katika kukamilisha dhumuni kubwa la jamii yake. huku anaowaongoza wakijitoa kwa kiasi na kwa kuongozwa. Kama tukimtaka kiongozi, lazima tukubaliane Maisha yake lazima yatabadilika baada ya kumpata, na hivyo kama jamii, tutapaswa kuangalia namna za kumuwezesha kwa muda wote wa Maisha atakaoutumia kwa ajili ya jamii yote, ikiwemo na yeye mwenyewe. Akili ya kiongozi inapaswa kuwa ni malengo ya anachokiongoza. na ndiyo maana kiongozi hulindwa maana yeye ndiye kichwa cha jamii yake, ukipiga kichwa, mwili ni mkubwa uliobakia ila hauna tena uelekeo. Sababu bora kabisa za kuziangalia kwa kiongozi anaepaswa kuchaguliwa, zinapaswa kuwa ni Upendo na Maarifa. Kiongozi bila kuangalia jinsia anapaswa kuwa mzalendo wa kwanza, aweze Kujitoa kwa ajili ya jamii yake, lakini awe ana uwezo wa kutosha kiakili wa kuongoza jamii yake na kuilinda.

Kibiolojia wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri sana. ila wanaume wana urahisi zaidi wa kuwa viongozi. Hii ni kwa kuwa, wanawake huwa wanaunganishwa zaidi na familia zao ukilinganisha na wanaume. ni rahisi kwa Jogoo kuacha vifaranga ukilinganisha na temba. ni rahisi sana kwa Baba kuwa na wake wengi, akitumia muda mchache na Watoto wake ukilinganisha na mama, ambaye huwa na ‘’post-partum aggressiveness na strong maternal bond’’. Wanaume wengi ni rahisi Kwenda vitani kupigana, kama mbwa wanavyopigania makoloni yao. kiongozi huleta nguvu zaidi anapokuwa mstari wa mbele vitani, kama alivyokuwa Alexander the Great, au Julius Caesar. Mwanamke hukutana na changamoto za kuguswa sana kihisia kwa baadhi ya mazingira, ambayo hayohayo mwanaume angeyapitia, na kuchukua hatua kirahisi sana, ya kufanyia utatuzi akipuuzia maumivu. Wanaume huwa na faida sana ya kutumia saikolojia za uanaume kusukuma malengo kwa hali na mali, na huku wakitumia wepesi wa miili yao kufanikisha malengo yao ukilinganisha na wanawake. ambao hutumia zaidi akili ukilinganisha na misuli.

Asili ya wanaume ya kupambana, uwezo wao wa ubongo mkubwa wa kuumba mipango ya haraka ya kiupambanaji, na uwezo wao mkubwa wa kutumia vizuri misuli, na hata takwimu zinginezo, huwanonesha kuwa, huwa na urahisi zaidi wa kukubaliana na kifo, hii huwafanya wawe na uwezo mkubwa wa kuchukua maamuzi magumu ya kiuongozi bila kuathiriwa na Hofu. Wanawake wengi sana huamini kuwa, hoja zinazosemwa kuhusu kutowapa kipaumbele cha kuwa wanaweza kuwa viongozi wakubwa, zina ugandamizaji wa kijinsia. Lakini sio kweli, Uongozi kiundani sio kuagiza majukumu Fulani yafanyike, ni Kwenda kuongoza ufanyaji. Uongozi kwa undani kabisa, ni ujengaji wa taswira ambayo inaenda kutimia baada ya hatua Fulani kuchukuliwa. na ndiyo maana ukisoma katika Biblia, viongozi wa awali kabisa kuchaguliwa kuongoza jamii za watu wa Mungu, wengi walikuwa ni wanajeshi, wengi waliishia kuuwawa, kama ambavyo mitume wote waliuawawa kwa kuchinjwa. Kipindi wanasayansi ‘’atheists’’ wengi wakisema, Biblia ina hoja za ubaguzi wa kijinsia kwa kutotumia wanawake katika namna ya uongozi kama inavyowatumia wanaume, wanasahau kiongozi kama Paulo aliyesambaza zaidi ukristo katika Biblia, alipigwa sana viboko, alifungwa sana gerezani, alitoroka sana, alizunguka sana huku na huku, na hata hatimaye aliuwawa, na mitume wengi waliachana kabisa na familia zao. Uongozi sio kitu ambacho wanawake hawawezi, hiyo sio kweli. lakini Maisha ya uongozi kiundani kabisa yanaweza kuwa changamoto kwa wanawake ukizungumzia namna uongozi unapaswa. Mamia ya viongozi watakaokumbukwa duniani, ikiwemo na Hayati Raisi wetu John Pombe Magufuli walikufa katika mapambano, au waliuawawa, haimaanishi kuwa wanawake hawawezi kuuwawa, ila inamaanisha Mungu hakuwaumba wanawake katika namna inayowapasa kuwa wapambanaji vitani. Vuta picha ya mwanamke mzuri na mikono yake laini, aamke usiku akiacha Watoto wake, na Kwenda kusimamia kesi za ujambazi wa mali za umma, au Bahati mbaya akiwa na ujauzito. Hata wanawake wanapovuka umri wa kuzaa, bado homoni na mifumo yao ya ubongo huthibitisha kuwa, Wanawake waliumbwa kwa uzuri, na kujali, na kuelewa maana za uongozi. kiongozi hana maana kama watu hawatamuelewa.

Ufupisho 

Nilieleza awali kabisa kuwa, wote, wanaume na wanawake wanaweza kuwa viongozi. Na hivyo ndivyo ninavyohitimisha, maelezo ya juu yanaonesha tu namna ambavyo wanaume wana urahisi zaidi wa kuwa viongozi ukilinganisha na wanawake, na cha ajabu ni kuwa, kuna viongozi wakubwa kabisa katika historia waliokuwa wanawake. Lakini pia hata viongozi wakubwa kabisa wakiume, walifanikiwa kwa kuwa na wanawake wenye malengo na akili kubwa kabisa za kuwawezesha.