Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

UCHAWI, UBONGO & MEDITATION

Ubongo, Uchawi, na Meditation

Wachawi Wanavyowanga kiroho

Wachawi huwa na mbinu kadhaa ambazo huwa wanazitumia kujipoteza fahamu. Mbinu hizi huwa na matokeo madogo na makubwa katika fiziolojia ya jumla ya kujitoa ufahamu, katika mantiki ya kutenganisha mfumo wao wa uamuzi na utambuzi, katika ubongo wa mbele na ndani kama tulivyoona, na sehemu za ubongo zinazohusiana na uchakataji wa taarifa za mazingira ya nje na ya ndani.

MEDITATION

Hii ni tabia ambayo imeshamiri sana kwa wachawi, tena wachawi wote. Wengi wa wachawi huwa hawaelewi hata kama huwa wanaifanya, na pia, wengi wa watu wanaoishabikia hii sanaa, hata hawaielewi maana yake, wapo wataalamu wa ubongo wengi ambao wanaiandikia ripoti kadha wa kadha, wakiiamini ina mapinduzi makubwa sana katika matibabu ya shida za misongo ya kiakili, lakini wengi wao pia, bado huwa hawaielewi kiundani.

Meditation ambayo nimekosa neno lake zuri la Kiswahili, ni tabia ambayo inatofautiana katika namna ambayo huwa ikitendwa, lakini msingi wake ni huu, mtu hutuliza kabisa Mawazo yake, huwa katika mazingira ya utulivu, huelekeza Mawazo yake katika kitu kimoja, na huanza kukirudiarudia mara nyingi. Na baada ya muda, katika hali kubwa sana ya utulivu na urudiaji mwingi, hujikuta akiwa katika hali nyingine ya uwepo. Hujikuta akiwa katika hali ya raha, hujikuta akiwa katika hali kubwa ya tamaa alizokuwa akilengesha Mawazo yake. Kwa wachawi ambao hulenga uwepo na miungu yao, hujikuta sasa wameshaingia katika ulimwengu mwingine. Meditation wengi wamewahi ifanya. Mara nyingi huwaletea hisia za utulivu na raha. Katika matibabu ya watu wenye misongo sana ya maumivu, mbinu hii pia hushauriwa kwa wagonjwa. Na huwa na matokeo mazuri. Ukienda katika nchi za mashariki, kule ndipo kitovu cha mbinu hii, na huwa na namna mbalimbali za utendaji wake. Lakini wengi hawajui hata katika Imani ya kikatoloki, mbinu hii hutumika. Wao hutumia Rozari, na hurudia rudia sana maombi yaleyale kwa muda mrefu, katika mazingira ya utulivu. na hata ‘’Ignatius Loyola’’ ambaye aliiandika hii mbinu kwa kanisa lake la katoliki, miaka mingi nyuma, alitambua matokeo ya mtindo huuhuu. Hii mbinu ni mbinu ambayo sasa hivi imekuwa na nguvu sana, hasa katika jamii za magharibi, marekani, na ulaya namaanisha. Lakini hebu tuangalie lengo la wachawi kutumia mbinu hii kama hatua yao ya kwanza katika shughuli zao.

Malengo Ya Meditation

Kutenganisha mfumo wa ubongo wa fahamu za utambuzi, na mfumo wa ubongo wa kuchakata taarifa. Kama unakumbuka, hiki ndiko kiini cha fiziolojia ya uchawi. Sasa basi, kupitia ‘’meditation’’, mtu anaweza fikia hii hatua ya muhimu ya kuanza hisia za uchawi.

Kivipi? Mfumo wa ubongo wa utambuzi na uamuzi, huwa una network zake kuu mbili, zile za kipindi mtu ametulia ‘’default mode network’’, na zile za mtu anapokuwa anatafuta mbinu au utatuzi na kazi zingine ‘’frontal-parietal netwerk’’. Mawazo huwa katika Ubongo hayatulii hata siku moja. Mawazo mara zote huwa yanazunguka, katika kielelezo cha mfumo wa kumbukumbu uliokuwa unaitwa ‘’papez circuit’’. Yaani ukitulia, yatakuja Mawazo ya nyumbani, mara ghafla yatakuja ya kazini, mara ghafla ya michezoni, mara marafiki, mara maadui, mara njaa, mara ulivyovaa, mara unachosoma, n.k. hii ndiyo tabia ya ubongo. na katika Mawazo haya, ubongo huwa unayapa kipaumbele sana Mawazo yanayohusiana na changamoto na shida. Ubongo haupendi shida, na hivyo huyapa Mawazo ya shida kipaumbele. Lengo ni ili sehemu za mbele ziyatatue, ubongo ukiamini kuwa, ukimaliza kuyatatua, basi utajisikia raha. Lakini Looh, Matatizo hayaishi. Kwahiyo taarifa za maumivu huwa nyingi sana. Msomaji ukumbuke taarifa hizi zinahusiana na za ndani za mwili, kama vile stress, maumivu ya mwili, magonjwa, n.k.Taarifa hizi huufanya ubongo kuwa mtumwa wa maumivu mara nyingi zaidi.

Sasa basi, mtu anapoamua kufanya meditation, mfano mzuri ni ‘’focused attention meditation’’. Huelekeza Mawazo yako yote katika jambo moja tu. Taarifa za mifumo yote zinakuwa hazina nguvu. lakini shida haiwi hapo, Shida huwa hapa, kwa kuwa unalazimisha ubongo ufikirie jambo moja, na wenyewe hautaki, Kwa kuwa sio tabia yake, kwa kujilazimisha kufikiria jambo moja, basi unakuwa unakinzana na fiziolojia ya utendaji wa ubongo wako mwenyewe. Kumbuka, ubongo kwa asili haupendi kurudiarudia jambo moja, Jambo moja linaporudiwa rudiwa mara nyingi, sehemu za ubongo wa mbele huzima umakini wake na utendaji wake kwa ujumla juu ya hilo jambo. hata kazi zake hupungua kiufanisi. Katika Vol 02 tulipoangalia sayansi ya muziki katika ubongo tuliliona hili kiundani, hata muziki ukiurudiarudia sana, hautaupenda, na baadae utakuwa hauusikii. Hata kitabia, mtu akirudiarudia kukuita kama ulishaitikia, hukusisimua mfumo wa ghadhabu. Kurudiarudia kuwaza jambo lilelile huathiri utendaji wa sehemu zote zinazohusiana na utambuzi binafsi, hukata mawasiliano na sehemu za taarifa kwa kuwa, umejilazimisha kutozisikiliza.

Wachawi Na Meditation

Wachawi wanapohitaji kuzungumza na mapepo yao, huitaji kupitia hatua hii, ili kuvunja geti la ubongo la taarifa za mazingira ya nje na ndani ya mwili, na kisha kujiweka katika hali ambayo wanaweza kujiunganisha na matrela ya mapepo yao. Kumbuka zipo tafiti ambazo zinaonesha kuwa, tabia za meditation, husaidia kuongeza uwezo wa kutafakari jambo. Hii ni kwa kuwa, sehemu za kutafakari huwa zinaboresheka sana, kwa mazoea ya kutafakari jambo moja tu. Na huonesha kuwa, sehemu mbalimbali za ubongo wa wanaotafakari, huwa kubwa na pana kwa wastani kidogo ukilinganisha na wasiofanya meditation. Lakini kamwe hawatakwambia madhara chungu mzima, ikiwemo na kukosa nguvu za usingizi ‘’insomnia’’, ambayo hutokana na ubongo kuwa na kiwango kikubwa cha msisimko hata wanapolala. Hii ni kwa kuwa nguvu kubwa sana hutumika kwa meditation, hawatakwambia madhara ya kuzuia taarifa zote za muhimu za ubongo, hawatakwambia hali za kisaikolojia, kama kuongezeka kutojikubali, wivu, n.k, hawatakwambia uraibu, kuna tafiti zinaonesha watu wanakuwa vichaa ‘’psychotic’’ kupitia meditation, tena kwa sababu za kukosea tu misingi ya kuifanya, watu wengine hulemewa na mawazo wanayoshindwa yatawala, na kibaya zaidi, Kitendo cha sehemu moja kuongezeka zaidi ya sehemu nyingine, huharibu kabisa balansi ya ubora wa utendaji wa kifiziolojia, hata kwa kawaida, haipaswi figo kuongezeka kama mishipa yake ya damu haijaongezeka, na moyo pia, na hypothalamus pia, na mwili wote kwa ujumla, hivyo inavyosemwa kuwa sehemu moja ya ubongo, kama vile ‘’insula’’ au ‘’sehemu moja wapo ya cingulate gyrus’’ imeongezeka zaidi, Hiyo ni sawa na kusema, shepu ya ubongo hubadilishwa kwa watu wanaofanya ‘’meditation’’.

Nimewahi kutana na wakristo baadhi ambao walikuwa wakihamasisha ‘’meditation’’, haya ni matokeo ya kutoelewa Biblia inaposema, ‘’Mshuruni Mungu kwa kila jambo’’, Yesu anasema ‘’sikuja duniani kuleta amani, bali Upanga’’ kukazia pia aliposema ‘’Duniani kuna dhiki, lakini jipeni moyo, Mimi nimeushinda ulimwengu’’, haya yote ni maneno ya Biblia ambayo yanahamasisha watu, kutoyakimbia matatizo. wala hakuna sehemu katika Biblia alipokuwepo mtu akifanya shughuli hiyo. Yesu anapowaasa wanafunzi wake, anawaambia, ‘’Muombapo, msipayukepayuke kama wamataifa, wao huamini kwa maneno yao mengi, nitawasikia’’ hapa anasema kinamna nyingine kuwa, haimaanishi kwa kurudiarudia mara nyingi, na kwa muda mrefu, ndiyo mtu huongeza ukaribu na Mungu, labda miungu.

Fahamu Zaidi Meditation ni mbaya kuliko unavyoweza fikiria. Inatengeneza njia ya kuua Ubongo moja kwa moja hata milele. Mtu anayeanza hupata wakati mgumu kuzoea, lakini mzoefu, kama monk au mchawi mzoefu, ndani ya sekunde tu huwa ameshaanza safari ya kusipojulikana. Ubongo haupendi vitu vya kuvirudia kwa kuwa, ubongo hupenda vitu vipya, na visivyotabirika. Aina kadhaa za Wachawi wanapoanza kujifunza, huzoeshwa kutazama picha au taswira moja, na kisha Huambiwa kuanza kuivutia picha mpaka mwisho. Hufundishwa meditation kiufupi. Huu msingi huanza kama kuvutia taswira kitu, yaani ‘’visualization’’

Msingi wa tamaa zote duniani, ni kuzivutia taswira. Wachawi hawapendi maendeleo ya wengine, wengi wao huwa na tamaa sana. wengi wao hawajui kwanini, macho ya wachawi ambayo tuliyaona yakiwa na uwezo mkubwa wa kuvutia taswira, kwa namna zao za kutazama ‘’blink strangely’’, yamejawa na tamaa. Biblia inaandika, ‘’ukimtazama mwanamke ukamtamani, umeshazini naye’’ hapa kutamani, kumelenga kuonesha kuvutia taswira, na kuirudiarudia, na kuiboresha kabisa anapokuwa uchi, na kuanza kuishi naye. Hii ni namna ya ‘’meditation’’, wanaume wengi ambao huwa wakifanya ‘’masterbation’’, hufanya ‘’meditation’’, huvuta taswira baada ya kuangalia picha ya mwanamke, humvua nguo kimawazo, na huzini naye kimawazo. Namna zote za kishetani au kichafu, zimejaa mitindo ya kuvuta taswira, ‘’wengi hawajui kwanini soko la filamu za ngono, miziki ya nusu uchi, n,k. ndiyo huongoza kuuza, hizi ni mbinu za awali za meditation. Ila meditation ya kiwango kikubwa zaidi, huendelea na kuendelea kama tulivyokwisha kuona.

Meditation na Saikolojia ya Kujichukia. Kuna msingi mkubwa kabisa wa kujichukia baada ya kufanya ‘’meditation’’, kama wengi wanavyolalamikia mtindo huu. Hii ni kwa kuwa, unapokuwa unafanya meditation, unazuia sehemu za ubongo zisichakate taarifa za kukuumiza ‘’ni vizuri kutambua ubongo wa kati -parietal lobe-huusiana na utambuzi wa taarifa zinazokuzunguka , pia huwa unaitwa -attention brain’’. Ukiwa na shida hupelekea kushindwa kutambua taarifa na matatizo ya maumivu ya hisia za mwili, hali ambayo huitwa ‘’neglect-syndrome’’, sasa basi, ripoti kadhaa zinaonesha, meditation hukata network inayoitwa ‘’fronto-parietal network’’, kwa hiyo mtu huwa hana taarifa nyingi za kumhusu, shida huwa pale anapoacha sasa kufanya ‘’meditation’’, anapoungana na trela lake la uhalisia, huwa anajisikia vibaya kwa kuwa, huwa anaona mambo mengi ya kumhusu ni kama mzigo, yapo mengi zaidi hapa, lakini hiki ni kama kielelezo kidogo.


Rejea tafiti juu, na unaweza ipitia yote, nukuu maelezo yenye paragraph zenye rangi za njano. Paragraph yenye njano ya kwanza inasema ‘’unapoanza meditation, kwa kuwa unatumia ubongo wako kulazimisha fikra zako kwenye wazo moja, basi sehemu zako za ubongo wa kufikiri, ambazo hasa ni ‘’prefrontal-parietal’’ zinakuwa zikisisimka sana, kwa kuwa unakuwa unazilazimisha. Na ndiyo maana tuliona, watu huwa na shida ya kukosa usingizi ijapokuwa huwa wanalala. hii ni kwa kuwa, Ubongo wao huwa na msisimko mkubwa sana. Paragraph yenye njano ya pili, inaeleza kuwa, mtu akishakuwa mtaalamu, sehemu za ubongo zilezile, hazifanyi kazi kabisa au zinafanya kidogo sana. Hili halimtishi mtu kweli, hata kama itakuwa katika kuanza meditation. Tena ajabu ni kuwa, maeneo mengine ya mfumo mzima wa utambuzi, yaani Anterior cingulate cortex au ACC, prefontal cortex, au PFC na Insula, yapo yakifanya kazi. Hii ni sawa na taa ya gari izime usiku, na gari liendelee kutembea. Paragraph ya mwisho kulia inakazia msingi niliosema awali kuwa, lengo la hapa ni kuua mfumo wa utambuzi wa taarifa za mwili, na ndio maana, kuna statement inasema ‘’changes in PFC-amygdala connectivity’’, kumbuka nilishaonesha kuwa,amygdala ndiyo sehemu kubwa zaidi ya uchakataji wa hisia hasa za hofu. sasa basi, hapa kinachoelezwa ni kuwa, wanaamini hisia za ahueni toka kwenye Hofu kubwa ‘’anxiety’’, kipindi cha meditation, hutokana na mabadiliko makubwa ya sehemu za mfumo wa ubongo wa mbele wa kuchakata taarifa za hisia, ambao ndio huo PFC-amygdala connection. Wasomi hawa wajanja sana, Lakini kadri siku zinavyoenda, watu watazidi kugundua uchawi huu.

Miziki Na Ngoma Za Kichawi

Kama tulivyoona katika vol 02, miziki kwa asili huwa na mitindo kadhaa ya kulevya watu. Katika mitindo hiyo, kwanza kupitia miziki yenye ngoma zenye mapigo ya kujirudiarudia, miziki hii huamasisha zaidi hisia za ‘’meditation’’, kwa kuwa, kwa Pamoja huchochea zaidi hali za kutoka kwenye ufahamu wa kawaida. Huyapa nguvu Mawazo ya kujirudiarudia. Miziki hii huchochea mawimbi ya ubongo yanayoitwa ‘’Alpha waves’’ ambayo huamasisha hali za meditation, pia miziki ya ngoma, Huamasisha hali za ubongo zinazoitwa ‘’Syncopation’’. Hii ni ile hali ya kuhisi raha ya muziki. Hali hii hutokana na kuwa, mabiti huufanya ubongo kutafuta biti kuu la muziki. Na katika miziki hii ya kichawi, huwa kuna mabiti mengi sana yanayopigwa kwa wakati mmoja. Kitendo hiki cha kupiga mabiti mengi kwa wakati mmoja, au ‘’polyrhythms’’, huuchanganya Ubongo, ubongo hutafuta biti kuu kwanza, na hilo tuliona huambatana na hisia za kucheza, na pia tukaona, kadri ubongo unavyokosea, unaongeza hamasa ya kulitafuta, ambapo ndipo mtu anajisikia raha zaidi ya muziki ‘’groove’’.

Mabiti haya ya miziki, huingia hata ndani kabisa ya ubongo na kusababisha ‘’entrainmenet’’ au ‘’embodiement’’, yaani hisia za kuunganishwa na mabiti ya muziki, mwili mzima huendana na frequency za muziki. Hii huongeza nguvu za misisimko ya hisia ya raha na kuwehuka ‘’hysterical activity’’. Kibaya Zaidi, Miziki hii ya kichawi mara zote, huwa ikiambatana na midundo yenye kujirudiarudia mara nyingi. Kama mziki wa kujirudia rudia sana umekuwa maarufu leo duniani, basi asili yake ni katika jamii za kichawi, kama tulivyoona muziki wa voodoo, ndiyo asili ya muziki wote wa magharibi. Muziki huu ambao huwa unajirudia rudia, mara zote huwa unakinzana kabisa na utendaji wa sehemu za mbele za ubongo, kwa kuwa, unakuta muziki una maneno machache, na yanajirudiarudia hayohayo kila wakati. Na unaambatana na mabiti ambayo, nayo yanajirudia hayohayo kila wakati. Hii tayari ni hatari. Kwa kuwa, ubongo wa utambuzi sasa unaenda kuzima, ubongo hauoni maana ya kuongeza umakini kwa kitu ambacho tayari kinafahamika. Hiki kitendo cha kuzimisha sehemu za mbele za ubongo, kinachochea zaidi kiini cha fiziolojia ya uchawi, yaani kutenganisha sehemu za mbele za mfumo wa fahamu, na mfumo mzima wa ubongo wa uchakataji wa taarifa za nje na ndani ya mwili.

Watu wengi hawatambui kwanini katika kila historia ya mwanadamu, kabla ya ibada, muziki hupigwa. katika zama za Danieli, kabla ya kumuabudu Mfalme Nebukadreza, muziki ulipigwa, wana wa Israeli walipomuabudu dagoni, muziki ulipigwa. Leo hii miziki ya dunia imeshamiri aina zote za miziki ya ibada za wapagani, maana namna wanavyopiga miziki yao, ndivyo namna ileile ilikuwa ikifanywa kwa waliokuwa wakiabudu miungu wapagani. Na hii ni kwa namna ya kutumia mabiti mengi sana ndani ya muda mfupi, huku mabiti yakiwa yakujirudiarudia, yanayoongezewa tu vichocheo ‘’harmonies’’, utakuta wachezaji wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, hata na kuvua nguo kwa baadhi ya wakati. Wengi hawaelewi nguvu ya muziki, kuelewa zaidi, rejea Vol 02, ambayo hiyo inaelezea msingi wa muziki huu, Pamoja na kucheza.

Lakini kwa upande wa maneno, maneno ambayo wachawi huwa wakiyaimba, huwa ni maneno ambayo huwa hayana maana sana, hayana ‘’logic’’, huwa yakujirudiarudia, na kadri mtu unavyoongea sana maneno yaleyale, ndivyo uwezo wa ubongo kuyazingatia unazidi kupungua, wengi wao huwa na mashairi yaleyale, na haya huwachochea zaidi kuwalevya kiakili. Hisia za mihemko ni jambo la msingi sana kwa mchawi, kwa kuwa hisia za kucheza zinapoongezeka, zinakinzana na utendaji wa ubongo wa utambuzi, ambao huwa unahitaji utulivu, mazingira ya kutulia, na sio ya kuchezacheza kwa msisimko wa ubongo usio na uelekeo.

Shughuli Nyingi Usiku

Wachawi hutumiwa sana usiku kwa ajili ya kazi zao. Usiku huwasaidia sana kuweza kufanikisha kazi zao. Hii ni kwasababu zifuatazo, kwanza kabisa, usiku kifiziolojia huusiana sana na uzalishaji wa kiwango kikubwa sana cha kemikali za utulivu wa ubongo ‘’melatonin’’ ambazo huamasisha hisia za kulala, uzalishwaji wa kemikali zingine za histamine, ambazo huupooza ubongo, na ndio maana usingizi pia husaidia kupunguza uvimbe wa ubongo. Pia usiku huusiana na kushuka kwa kemikali za mihemko ya mwili ‘’kemikali za noreadrenaline’. Kitendo cha kufanya shughuli za kichawi usiku, hupelekea ubongo wa wachawi kuwa na mhemko hafifu sana wa mfumo wao wa umakini.

Giza la usiku hupunguza kiwango cha taarifa zinazoufikia ubongo, kwa kuwa macho hayaoni, kwa hiyo hayapeleki taarifa. Kelele ni chache, watu na wanyama wamelala, kwa hiyo masikio hayapeleki taarifa, na hata hisia za harufu pia huwa chini kwa usiku. Ubongo wenyewe kwa kufuata mzunguko wake wa asili wa kulala na kuamka ‘’circardian rhythm’’, huwa hauna kipaumbele cha kufikiria. Wala pia hauna kipaumbele cha kutafakari. Sasa basi, mfumo wa ubongo wa ‘’fronto-parietal network’’ huwa umelala, na sehemu nyingi za hisia zinaposisimka, huwa hazina control kubwa toka kwenye ubongo.hii ni kama inavyotambulika kuwa, ni rahisi sana mtu kufanya maamuzi mabaya kadri usiku unavyozidi kusonga.

Mfano wa Nguvu ya Usiku. Wakati wa usiku ukivuta taswira kichwani mwako kuwa kuna pepo anakukaribia, Na kisha ukaangalia hewani au kwenye mti Jirani, au hata ndani, kutokana na giza, ni rahisi sana kutengeneza taswira yenye uhalisia sana, ukilinganisha na wakati kukiwa na mwanga. Hii huwafanya Watoto wengi sana kuogopa wanapotumwa usiku na wazazi wao. Ni rahisi sana kuvuta picha katika mazingira yenye giza, kuliko kuvuta picha katika mazingira yenye mwanga. Wakati wa mwanga ubongo huwa na nguvu sana, na network za kutafakari tu ndizo huwa zina nguvu sana, sio za kuvuta taswira.

Mazingira Ya Kutisha Kama Makaburini

Iwe kwa makaburini, au msituni, au pembezoni mwa mji. Mara nyingi na zote, mazingira haya huwa na hisia za asili za hofu kwa binadamu. Binadamu huogopa kifo mara zote, kwa kuwa kuna maswali mengi sana kuhusiana na kifo kuliko majibu. Hofu ya kifo pia, ni msingi wa fiziolojia ya mwanadamu na saikolojia, ambazo zote zimejikita katika kupambana kadri iwezekanavyo, kuzuia kifo kisitokee. Sasa basi, sehemu ambayo watu waliokufa huwekwa, lazima itakuwa na hisia za kutisha, hii ni kwa kuwa, ubongo huwa na network ya kuvuta taswira wa kuiga unachokitazama ‘’mirror neuron system’’ au MNS. Sasa basi, kwa kuangalia mwili wa mwenzako umelazwa pale, lazima ubongo utavuta picha nawewe wa kwako umelazwa. Lakini hofu zaidi hutokana na stori za kuwa, makaburini huwepo watu hatari, Wenda mapepo au wafu waliokufa. Ijapokuwa ubongo unaweweza usiamini, ila unapokuwepo usiku maeneo haya, ubongo huvuta taswira, vipi kama ni kweli, kwa mifano hii na zaidi, maeneo ya makaburini, huwa ni ya kutisha sana.

Wachawi mara nyingi wanapopendelea mazingira haya ya makaburini, hutengeneza hisia za hofu, na hizi hisia huambatana na athari katika mfumo mzima wa utambuzi. Kama tulivyotazama katika hatua ya nne ya hofu, na madhara yake katika mfumo wa ubongo wa fahamu. Hivyo hivyo kwa maeneo ya misituni, ambayo huwa sio rafiki sana kwa watu, binadamu kwa asili huwa na amani zaidi anapokuwa katika jamii zenye watu wengi zaidi, kitendo cha wachawi kupendelea usiku na maeneo yenye misitu na vitisho, hulenga zaidi kutengeneza hisia za kutojiamini, na hisia hizi huambatana na kudhoofika kwa uwezo wa kuchakata taarifa vizuri.

Michanganyiko Ya Kemikali Za Kuvukiza

Wachawi hutumia formula mbalimbali za michanganyiko ya mimea mbalimbali, na hata vitu mbalimbali, Ambavyo vitu hivi huvichanganya, na hata kuvipasha moto, matokeo yake, huwa wananenea maneno mbalimbali michanganyiko hii. Hoja ya msingi ni kuwa, michanganyiko ya mtindo huu, na harufu kama za ubani, mara zote huwa na matokeo ya moja kwa moja katika eneo la striatum, kiini cha motisha za ubongo. na kwa hivyo sasa, kadri ambavyo watumiaji hawa wanajivukiza, ndivyo wanavyojilevya zaidi.

Sehemu iliyopita tuliona kuwa kemikali hizi, huwa na chembechembe ambazo huwa na sifa za kulevya akili, kama ilivyo kwa marijuana, au heroine na cocaine. Chembechembe hizi ambazo huwa na sifa za kuusababisha ubongo kutengeneza taswira feki ‘’hallucinations’’, huwa ni kwa kuwa huwa zinasisimua sana sehemu za hisia, kiasi cha kuathiri uchakataji wa maeneo ya mbele ya ubongo, yanayohusiana na utambuzi wa taswira. Wachawi huwa na matumizi ya kemikali nyingi sana za kulevya akili, sio tu kwa za namna ya ubani, pia na za kujipaka katika sura, na hata mwili mzima, wachawi hupendelea hata na aina Fulani za perfumes au spray, ziwe za asili au za kutengeneza, kwao huwa na lengo la kuita mapepo yao, lakini uhalisia huwa ni kuathiri kabisa utendaji wa ubongo.

Adhabu Kali Za Kutisha Na Kafara

Mtindo huu wa kutoa adhabu kali sana kwa wachawi, ambao huwa wanapovunja viapo vyao. Huwa na matokeo makubwa sana katika saikolojia za wachawi. Kwanza, huwafanya kuwa ni watu wasio na uhuru wa kifikra. Pili huwafanya kuwa ni watu wahofu sana ya kuvunja uhusiano wao na mitindo yao ya kiimani. Jambo hili huwaathiri uwezo wao wa ubongo wa utambuzi, hii ni kama ilivyo kwa mwanafunzi ambaye unamuahidi adhabu kali sana akifeli mtihani, kuna hatihati kubwa sana ya kuwa na ufaulu mbaya kabisa, kutokana na kushindwa kuwa na uwezo mzuri na utulivu wa akili.

Hivi ndivyo ilivyo kwa kila eneo ambalo hofu itachochewa sana. Kumbuka, hofu ni jambo ambalo laweza athiri uwezo wa kifikra moja kwa moja, mtu mwenye hofu, na akawa akitambua kuwa hakuna namna ya kujikinga na tatizo lake, basi huzima kabisa uwezo wa ubongo wake wa mbele kama ambavyo tuliona katika sehemu zilizopita.

Falsafa Ya Kiini Cha Uwezo Wa Utendaji Wa Kichawi Shoo Hypothesis

Mtazamo pekee ulio bora kabisa wa kuutazama uchawi katika jicho la kisio bora zaidi la utendaji wake, Ni kuwa uchawi hutenda katika namna ya kinyume ukilinganisha na utendaji wa kawaida, yaani ni kuwa, kwa kawaida, mtu angeona taswira baada ya kitu kuwepo, na kisha taswira ya kitu hiko kumfikia katika ubongo wake, toka kwenye mazingira. Lakini katika uchawi, taswira inaanza kumfikia mtu katika ubongo, bila hata kitu chenyewe kuwepo, na hivyo mtu anaona, na kisha anategemea kukipata hicho kitu katika mazingira.

Mchawi anaona watu na mazingira yao, Na kisha anawatengenezea matokeo katika akili yake, Kupitia zile sheria zake kuu za utendaji. Na baada ya hapo, anategemea ayapate matokeo ya uhalisia kabisa wa mitazamo iliyotoka kichwani mwake. Mfano mzuri ni huu, mchawi kupitia akili yake huwa akimwona mtu Fulani na mazingira yake Fulani, na hujiona yupo pale, na humsumbua mtu au kumlaani mtu apatwe na jambo Fulani baya, Na kisha hutegemea mtu huyo apatwe na tatizo lile katika ulimwengu wa kimwili au katika fizikia ya kawaida kabisa. Hii namna katika fizikia tungeweza iita kama ‘’Retro-causality’’, namna hii ili iwezekane, lazima kuwepo makisio makubwa zaidi mawili.

Uwepo Wa Mapepo. uwepo wa roho au mapepo ‘’free spirits’’hufanya kazi kama ‘’free channel’’ yaani, Zenyewe zitakuwa kama mawimbi ya usumaku wa umeme ‘’electromagnetic fields’’ zikiweza kuwa sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja. Na hivyo sasa, mchawi hufanya kitu kimoja tu kuweza kujiunganisha na channel hizi, Nacho ni hiki, wakati anapokuwa akifanya hatua zote za fiziolojia ya kutenganisha mfumo wake wa ubongo wa fahamu toka mfumo wake wa ubongo wa uchakataji wa taarifa, Pale huwa anatengeneza namna ambayo mfumo wake wa taarifa huwa una jiunganisha na hizi roho ‘’free spirits’’, na kwa mantiki hiyo, Mchawi badala ya kuona taarifa zinazotokana na mfumo wake wa ubongo unaochakata taarifa, basi huwa anapata taarifa toka kwa haya mapepo.

Namna gani mapepo yanajazia gepu hili lililowazi katika akili ya mchawi, ni kupitia kisio la namna za mapepo ambazo ni mithili ya mifumo ambayo inaongoza utambuzi. Kumbuka hata kinachoongoza utambuzi nacho ni mifumo ambayo sio kemikali katika seli za ubongo, kama tulivyoona katika tafiti za Michael Levin, au Michael Persinger, au Jose Delgado. Mifumo hii ambayo ndiyo inatawala utendaji wa seli na utambuzi, ndiyo ambayo huchangamana na roho hizi. Kumbuka, huu mtazamo una nguvu kisayansi kwa kuwa, umejikita katika ukweli wa kuwa mifumo yote ya ubongo hutenda sawasawa na fiziolojia ya seli zilizopo pale, na sio nadharia za roho iliyo sehemu mbali na seli za ubongo.

Ushahidi wa Mapepo na uchawi. Mchawi yeyote duniani huamini asilimia 100% ulimwengu anaoishi ambao wengine huuona kama wa kiroho, Yeye huuona kabisa ni wa kimwili. Mchawi atakwambia alikuwa akienda Malawi, Au alikuwa chini ya Bahari, Au alikuwa akielea hewani, Alikuwa akizunguka sehemu mbalimbali tena kwa urahisi sana, Mchawi atakwambia kuwa tulikuwa tukienda katika nyumba ya mtu Fulani, tulikuwa tukienda sehemu za juu sana, Nilikuwa nimeoana na pepo Fulani, hizi stori zote zimejaa katika visa vya wachawi, wanaoendelea, au hata walioacha. Kitu ambacho wengi wao huwa hawajui ni kuwa, Katika sehemu za Ubongo wao wa mbele, ambazo zilipaswa ziunganishwe na trela la mifumo ya taarifa za mwili, Wao walijifungamanisha na roho. ambazo zenyewe zina uwezo mkubwa sana wa kuwepo sehemu mbalimbali. na huwa zikizunguka zunguka mahala tofauti tofauti. na pia roho hazifungwi na sheria nyingi za kimwili za fizikia ya kawaida, ikiwemo kwa kuwa hazina miili, huweza pita sehemu zozote zile, na hivyo sasa, kitendo cha kuungana na ubongo wa mchawi, Sasa mchawi naye anapata taarifa kupitia hizi roho. Anajiona ni yeye ndiye mhusika. 

Ni kama vile mlevi wa madawa ya kulevya, au kichaa wa ‘’schizophrenia’’, ambavyo hujiona kabisa ni yeye aliye katika ulimwengu mwingine kupitia taswira ‘’hallucinations’’, kumbe watu wengine kwa wakati huo mnamwona kama mtu aliyekufa kifahamu. Na ndiyo maana wachawi ili kuanza shughuli zao huitaji giza, au sehemu za siri, Au hata kutulia kimya kimawazo na meditation. Kiufupi hizi hali huchochewa na msingi huu. Mchawi huitaji kwanza kutenganisha mfumo wake wa ubongo wa fahamu na wa kuchakata taarifa, Na kisha hujifungamanisha na sehemu yake ya pili. ambayo ndiye pepo lake. Na hili pepo humpatia taarifa ambazo mchawi huzihisi katika namna ya kuwa yeye ndiye mhusika. Kwa kuwa hivyo ndivyo inavyokuwa katika ubongo wake.

Mchawi au Mganga anapokuambia kuwa amezungumza na mtu Fulani aliyekufa, Usihisi kuwa ni kichaa, kweli huwa ni kichaa. Mchawi anapochukua tu hatua zozote zile kama tulivyoona katika sura zilizopita, za kujitoa ufahamu. Huanza kupata taarifa lakini toka kwa roho zilizohuru ‘’pepo lake’’, hizi humfanya kuona dunia katika namna ya tofauti. Hujiona akiweza kuwa popote, kielelezo kizuri ni pale ndoto inapokolea, unaweza ushindwe kabisa kujua kuwa unaota, Mpaka inapokaribia kukata. Ndivyo mchawi naye, hawezi kuamini kuwa siyo yeye na mwili wake huwa wanakuwa pale, Ila kwa kuwa sehemu ya ubongo ya mbele ndiyo mhitimishaji mkuu, ukimpa taarifa feki, huitimisha kwa hilo. Ni sawa na ugonjwa wa ‘’anton syndrome’’ mgonjwa kiuhalisia huwa ni kipofu, lakini ubongo wake huwa bado unaunda taswira. Na mgonjwa mara zote hukataa mnaposema yeye haoni, na huwa anajigonga kwenye vitu na ukuta kwa kutoona kama hamtamsaidia. Lakini shida ipo tu katika ubongo wa mbele unaporishwa taarifa feki. Mapepo wanapoungana na mchawi humpa uhuru wa kutawala tamaa zake kiutendaji kupitia ubongo wake wa mbele moja kwa moja, na hii humpa kiburi mchawi cha kuamini anatenda.

Kumbuka pia, usipokubaliana na hili, hutaweza kuelewa kwanini katika soshiolojia ya uchawi, waligundua kuwa wachawi huwa wanaweza kuwa katika sehemu mbalimbali, au kwanini hujifungamanisha na Wanyama kadhaa. Hawa hushindwa tu kuelewa biolojia hii ndogo ya ubongo. mchawi hana roho na mwili zinazojitenganisha. Hutenganisha tu mfumo wake, na mchawi huwa muda wote Pamoja na mwili wake. Na ndiyo maana akiumwa asipotibiwa hufa. Akipigwa sana mwili wake hufa. Mchawi hawezi jitenganisha na mwili wake, ni sehemu tu ya mbele ya ubongo wake huwa akijiunganisha na mapepo ambayo humpa taarifa halisi za mazingira yake, Ila humdanganya kana kama ni yeye aliyepo pale kwa kutumia udhaifu wa fiziolojia ya ubongo. kuhusu Wanyama nayo huwa ni kupitia uhusiano wa pepo kwa mnyama pia, kama ilivyokuwa kwa shetani na nyoka. Lakini sasa, pepo hili linapojifungamanisha pia na ubongo wa mtu huyu, Humtengenezea uongo ‘’delusion’’ kuwa na yeye yupo kwa mnyama yule. Lakini kama mchawi akilielewa hili, atagundua anapodanganywa kirahisi.

Kigezo Cha Mtu Kurogeka

Ili matokeo yoyote yale ya kichawi, mfano kurogwa, kulaaniwa ‘’cursed’’, n.k. yatokee. Ubongo wa muathiriwa, unapaswa kuwa katika hali ya Hofu. Ni kweli mchawi anakuona. Na siyo kwa kuwa yupo yeye kama yeye, La hasha. Ni kwa kuwa lipo pepo lake ambalo limeungana na ubongo wa mchawi, na hivyo mchawi hujikuta kama na yeye yupo akikuona tokea ulipokaa au lala. Sasa basi, kama mtu atakuwa ana hofu, kama ile ambayo awali ilimfanya mchawi awe hatarini mpaka kumilikiwa na pepo, huyu mtu naye ana hatihati sana ya kuweza kushambuliwa ubongo wake kwa pepo. ambalo limevaa uhusika wa mchawi Fulani. na pia huwa mara nyingi likishambulia kwa matakwa ya mchawi husika. Hapa inapaswa msomaji aelewe hivi, Mashambulio yote ya uchawi kama yanavyonukuliwa na wanasaikolojia wa tafiti hizi, hutokea katika hatua kadhaa tu za usingizi, na mara nyingi huwa katika hatua za mabadiliko toka ‘’non-REM-sleep’’ Kwenda ‘’REM-sleep’’, na pia katika hatua ya ‘’REM sleep’’ ambayo huusiana na ndoto. Ubongo wa mshambuliwaji unapokuwa na hofu, kwanza huathiri nguvu ya mshikamano au ‘’bond’’ inayoshikilia mfumo wa fahamu na mfumo wa taarifa, mtu muoga sana wa uchawi, Huurahisishia kazi uchawi. uoga huusiana na mashaka na hata uundwaji wa kumbukumbu za mashaka. Kipindi cha hatua za ndoto kinapofika, ambacho huambatana na mawimbi hafifu kabisa ya sehemu za mbele za ubongo kama tulivyoona tulipokuwa tukijifunza kuhusu ndoto, Hakuna mchawi ambaye huwa anakuja, Lakini pepo lenye utambulisho wa mchawi linapofika, Huwa na nguvu sana ya kumshambulia mtu kwa kuwa, mfumo wa ulinzi wa ubongo wake ni dhaifu.

Pepo Hushambuliaje?

Free spirits au mapepo huchukua utawala wa mfumo wa ubongo wa mshambuliwaji, hasa katika ‘’rem-sleep’’, hii ni kwa kuwa hii hatua huwa na shughuli zisizo na mpangilio za ubongo, na pia huwa na nguvu kubwa sana ya kihisia, kama tulivyoona awali katika ndoto. Basi hapa ambacho huwa kinatokea huwa ni hiki, mapepo haya kwanza hutengeneza taswira feki, ikiwemo kumfanya muathiriwa ajione yupo katika maazingira magumu sana, akiteswa kichawi, Au vyovyote vile. Pia mapepo huingiza kumbukumbu feki, Na hizi huusiana na taarifa ambazo ubongo utakapo rejea fahamu zake baada ya hii hatua, utazipokea kama taarifa za magonjwa, hali mbaya, n.k. na mara nyingi wataalamu huwa hawaoni shida yoyote ile kama muathiriwa ataenda hospitali. Mara nyingi magonjwa ya kurogwa hulenga zaidi shida za kiakili, au zilizoanzia akilini, na ndiyo maana hospitali hushindwa kuwasaidia watu hawa. Kumbuka wanawake huwa wadhaifu sana kihisia, na hii ndiyo sababu wengi wao ndiyo huteswa zaidi na shida hizi. Na hasa Afrika ambapo kumetawala imani hizi. Ukienda Ulaya hutakuta stori hizi hakika, ni asilimia ndogo sana sana. Si kwamba Uchawi hauvuki boda, Uchawi huanza na Imani.

Wengi huisi kukabwa na wachawi, na huamini kabisa kulikuwa na uzito mkubwa kifuani. Ni kweli ulikwepo uzito, Ila ni kichwani sio kifuani. Kuna wengine huisi kabisa wamepigwa kofi, Wengine huisi kabisa wamepigwa viboko, Lakini mapigo haya yote huwepo tu kichwani. kumbuka hata vichaa huwa wanabembeleza Watoto, tena kwa kulia kabisa, Lakini Watoto wenyewe huwa sisi tukiona machupa. Waathiriwa wengine wa uchawi huwa wakipokea mapigo mbele ya watu wengi kabisa wanaowazunguka, Na watu huwa hawaoni chochote ila tu huona mtu akilia. Hii hata kwa kutumia mitambo tu midogo ya ubongo ‘’EEG’’, tunaweza thibitisha kwa kuona sehemu za ubongo za hisia za presha za maeneo ya viungo anavyopigwa, zikisisimka.

Kumbuka, Madhara haya ni ya uhalisia, kwa kuwa maumivu yote huwa ni katika ubongo, hisia mbaya za magonjwa yote, huwa ni katika ubongo. utambuzi wa shida na changamoto yoyote, huwa ni katika ubongo. hivyo basi, presha kubwa ya hisia za matatizo, hata kama ni feki, lazima yatamuathiri mtu na utendaji wake.

Watu Wanaobebwa na Mapepo au Anguka kwenye Ungo. Kuelewa hili kunahitaji kuelewa kiundani kinachofahamika kuhusiana na fizikia ya mapepo. Lakini hoja ya muhimu ni kutambua kuwa, utendaji wa kichawi na mapepo, una mipaka mikubwa sana inayotegemea zaidi misingi ya kiakili zaidi misingi ya kimwili. Mara nyingi napenda kusema, kama uchawi ungekuwa ni mbinu bora ya kifizikia, ingekuwa mbinu bora zaidi ya kivita na hata teknolojia. Kuna kila sababu ya kuamini pepo lililo umbile la mtu, kuliko kuamini mtu anayeweza kuwa kama pepo.

Usidanganywe Hoja Ya Mafanikio Kwa Uchawi

Hili ni la muhimu sana. Wengi huaminishwa kuwa wanaweza kutajirishwa kupitia uchawi, na huamini kupitia wachawi waliotajirishwa. Yaweza kuwa kweli, lakini sio kwa mantiki ambayo wengi hufahamishwa. Kwanza, taasisi nyingi sana za kichawi, ndizo zinaendesha mifumo mikubwa ya fedha. Hawa hutengeneza fedha nyingi sana kupitia kuwanyonya watu wachini, kwa kuwa, huwa hawana upendo kabisa. Mfano mzuri, mataasisi ya ‘IMF, WB na WEF’’ , taasisi kubwa za burudani, platforms na channels kubwa za sanaa, karibia zote kubwa zimejawa na Imani za kichawi, viongozi wengi wa maserikali na hata taasisi kubwa zaidi za kidini, huwa na ajenda nyingi sana za Imani za kichawi na upagani, hawa huingiza matrilioni ya mapesa sio kwa uchawi, Bali kwa triki za unyanyasaji wa kiakili na kimwili, ikiwemo na kuteka akili za watu kuwa waraibu zaidi wa mitindo ya kishetani. Sasa basi, hawa huwavuta zaidi watu kuingia katika taasisi zao, wao wakionesha kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwasaidia, na kuwa, kwao kuna raha na uhuru. Upande wa pili, ambapo unakuta mganga mwenyewe ni masikini wa kutupwa, au mchawi mwenyewe anaishi kwa shida, Hawa hata mali zao huwa za muundo wa ‘’udanganyifu wa kiakili’’, mtu anaweza pewa pepo, la utambuzi wa Maisha ya kifahari, na anapovunja tu masharti! Anarudishiwa uhalisia wake.

Namuunga Mkono Mpinzani Humes

Mwanasoshiolojia David Humes, aliye maarufu sana kwa upinzani wake hasi, Pia ana hoja baadhi ambazo kama mwanasayansi, ni rahisi sana kuzikubali. Ikiwemo, kwa asili watu hupenda sana stori, na huzikuza. Hivyo stori nyingi za matukio yaliyopita, huwa sio za kuziamini, mfano, mimi nikitunga stori, hata kama inauhalisia kidogo, ila kama itasisimua sana, basi itasambazwa sana huku ikikuzwa. Mfano mtu akisema leo, mtu Fulani maarufu Aliuwawa na mtu Fulani, hata kama sina uhakika, kama nitaongea kwa kujiamini, watu wataikuza na kuisambaza kana kama mimi imetoka kwangu ikiwa na ukweli asilimia mia. Hoja yake David ya pili, anasema, stori za matendo yasiyo na uhalisia, hushamiri sana katika jamii zilizo nyuma kimaendeleo na kielimu, na ni kweli, maeneo mengi yaliyoendelea, hautasikia mtu anatajirishwa kwa Kwenda kwa mganga, au kupewa mafuta na nabii Fulani. hutaona mitindo hiyo kwa walioelimika na walioendelea, hii inanikumbusha vita ya majimaji. Kipindi dunia yote imepiga hatua kwa magobole ya bunduki, jamii Fulani zikaamini risasi inaweza badilika kuwa maji, kwa kusema maji, kwa kuagizwa na mganga. hoja yake ya tatu anasema, kitu chenye uhalisia, huwa kina uwingi wa namna kinavyotokea. Kama kweli kitu hufanikisha, uwe na idadi ya watu wa kutosha, ambao una uhakika, sio umesimuliwa, au unakisia tu kuwa wamefanikiwa kwa uganga, lakini ukweli ni kuwa, mara nyingi huwa hakuna uhalisia wowote. Nakumbuka nikiwa mdogo nilishuhudia Picha za magazetini zikimuonesha Samaki mtu, na niliamini kabisa uwepo wa samaki watu. Miaka mingi mbeleni nilikuja kugundua ulikuwa ni uongo, na kama ulivyokuwa na nguvu kubwa hata kwa ushahidi wa picha zile feki, ndivyo ilivyo imani nyingi za mafanikio kwa njia za kichawi na uganga.

Je! Mchawi Anaweza Kulaani Ardhi Au Mali Yako?

..Unaweza jifunza zaidi kupitia kusoma Kitabu changu Cha Sayansi ya Uchawi"