Kwanini Maziwa Hayana Chumvi Kama Gharika Ilifika Kote?
Kwanini Maziwa Na Mito Haina Chumvi Nyingi Kama Gharika Ilifika Kote?
Sifa moja ya supercritical water ni kuwa, huwa na nguvu kubwa sana ya kuyeyusha madini hata kufikia viwango vya kutengeneza chembechembe za madini kama Na⁺, CL⁻, Ca²⁺ n.k, madini haya inapofikia wakati ambapo maji haya yanakuwa yanapoa, baada ya kupungua presha, huungana na kuunda chumvi haraka sana. hiki kitendo huitwa ‘’out salting’’. Hivyo basi, kiwango kikubwa cha chumvi ambayo ilitoka ndani ya vilindi vya dunia, ilijikusanya maeneo kwa maeneo na haikusambaa sana. na hii ndiyo sababu ya uwepo wa vitu vifuatavyoMiamba Chumvi ‘’Salt Domes’’
Haya ni matokeo ya kiwango kikubwa sana cha chumvi kukusanywa katika sehemu moja. kiasi kwamba chumvi hii baada ya gharika kama tutakavyoona huko mbele, ilifunikwa na baadhi ya miamba, au ardhi iliyokuwa matope awali. baada ya muda ilipotokea mikunjo ‘’compression’’, tutaiangalia huko mbele, baadhi ya sehemu hizi ziliinuliwa na kupelekea matokeo haya.
Rejea picha chini.
Miamba Ya Chokaa Na Madini Mengi Ya Chokaa
Chokaa ambayo ni madini ya CaCO₃. Nayo huundwa kwa msingi ule ule wa tabia ya supercritical water. Uwepo wa miamba mingi katika chini ya ardhi yenye madini ya calcium na carbonate, ukijumlisha na sifa ya maji ya scw kuyeyusha madini haya. ilipelekea madini mengi ya calicium na carbonate kuyeyuka, na kisha baadae kuja kujiunda au kuprecipitate ‘’out salted’’ katika sehemu kadhaa ikiwemo katika Bahari, ambapo maji hayo yalitoka. Kiwango cha madini ya chokaa ‘’limestone’’ ambacho kiko katika Bahari, kisingeweza undwa na matokeo ya kuvunjika kwa mifupa ya Samaki, na wanyama wa Bahari, ni kikubwa sana. Lakini pia baadhi hutumia mifupa kama chanzo cha madini ya limestone, haileti maana kwa kuwa, hata aina ya limestone inayotokana na mifupa, haiwi ya aina moja yaani ‘’uniform’’ kama iliyopo baharini. na pia piga picha kuhusu miamba ambayo huwa na limestone safi kabisa, ungewezaje elezea vitu kama hivyo bila kutumia dhana ya gharika.
Muhimu sana kutambua kuwa, madini ya chokaa ‘’limestone’’ huathiriwa na kiwango cha hewa ya kaboni dioksaidi kwa mlinganyo huu.
H₂O(l) + CO₂(aq) + CaCO₃(s) ↔ Ca²⁺(aq) + 2HCOË¡⁻(aq)
Kutokana na mlinganyo huu, ni Dhahiri kuwa, kama kiwango cha hewa ya kaboni dioksaidi kitapungua, basi kiwango kikubwa Zaidi cha madini ya chokaa ‘’limestone’’ yataundwa. na hiyo ndiyo iliyotokea baada ya gharika, kiwango cha hewa ya kaboni dioksaidi kingi kilielekea kwa mimea, ambako huko kilisaidia kukua tena kwa kasi kwa mimea. Lakini pia kabla ya hapo, kaboni dioksaidi hii ingeungana na maji na kuunda ‘’weak acid’’ ambayo hiyo ilihamasisha mmemenyeko Zaidi wa miamba na madini mengine. hii ni kama inayotokea leo pale ambapo hewa nyingi ya kaboni dioksaidi inapozalishwa, hupelekea kuongezeka kwa mvua za asidi ‘’acid’’.
Hii ni picha ya miamba ya chokaa ‘’limestone’’
hebu jaribu kutafakari unawezaje elezea maajabu makubwa kama haya bila ya kutumia nguvu ya supercritical water, iliyopelekea huu mkusanyiko kipindi yanatoka ‘’massive out salting’’.Hii inaitwa limestone chimneys. zipo sehemu mbali mbali, na huwa ni kama mithili ya mji ambao watu waliishi wakahama. Sababu kubwa ni supercritical water ambayo kipindi cha kupasuka kwa vilindi vya maji, ilipelekea kuundwa kwa madini haya ya limestone kwa haraka sana. na sasa miaka mingi baadae, hizi zinabakia kama ukumbusho wa njia za maji ya scw. Huwezi elezea mabadiliko haya kwa matendo ya muda mrefu.
To be continued...





Join the conversation