GHARIKA, KUPAA KWA MAJI & BARAFU
Gharika Ya Nuhu: Kupaa Kwa Maji Angani
Maji yalitoka kutoka vilindi yakiwa na spidi kubwa kutokana na presha kubwa iliyokuwa ikiyakandamiza, kuendelea kuvunjika kwa miamba iliyokuwa ikishikilia sehemu ya juu ya nchi, na kubwa Zaidi ni Nguvu iliyotokana na milipuko ya Nyuklia iliyotokana na umionzi wa dunia. Maji haya yalisukumwa na nguvu inayokadiriwa kuwa sawa na mabomu ya hydrogen trilioni 1800, yalikuwa yana kiwango kikubwa sana cha joto, na pia yalibeba kiwango kikubwa sana cha udongo wa miamba ya chini ya dunia. Maji haya yalipaa juu yakiwa na nguvu ya kuvuka kabisa kani ya mvuto wa Gravitation ya dunia. Kutokana na maji haya kupaa na maudongo yote ya miamba, kulipelekea matukio yafuatayo katika sayari ya Dunia, na katika ulimwengu, yaani katika sayari nyingine, na hata mwezi na space kwa ujumla.
kunyesha kwa mvua ya barafu kwa maeneo kadhaa. ‘’rapid hail formation’’
Kutokana na maji ‘’supercritical water’’ kuwa na joto kubwa sana na presha kubwa, kitendo cha maji haya kufika angani kwa msukumo mkubwa toka kwenye mpasuko, maji haya yalitanuka ghafla ‘’expansion’’, yakashuka presha, na kuganda. hii ilitokana na kuwa, anga lina presha ndogo. na hivyo basi, maji yale ya moto haraka sana yaliganda ‘’rapid freezing’’.
je wajua ‘’mpemba effect’’
Maji ya moto huganda haraka zaidi ya maji ya baridi, hali hii inaitwa Mpemba Effect, iligunduliwa na Mtanzania, Mwanafunzi mwenyeji wa Tanga. Kutokana kuleta changamoto kubwa katika nadharia ya upoaji wa vitu ya Bwana Isaac ‘’Newton law of Cooling’’, uchunguzi wa kina ulifanyika na kugundulika ukweli wa ugunduzi huu wa bwana Mpemba hata kupatiwa Tuzo, na heshima ya hali hii kuitwa ‘’Mpemba Effect’’. Lakini kutokana na asili ya Ubongo mweusi, hakuna Mtanzania anayemfahamu bwana huyu, wala walimu hawamfundishi hata na yeye aliishia kusomea Misitu katika Chuo kikuu cha Sua, Morogoro. Hii ni ishara ya kuwa ni kweli Waafrika wana asili ya Kupuuzia Maarifa, na ndiyo maana watu wengi Afrika ndiyo wanaongoza kwa Umasikini, Ujinga, na Maradhi kwa mujibu wa Nyerere, lakini Binafsi Waafrika wanaongoza kwa Ubinafsi, na imani Potofu.Maji haya yaliyoganda mengi yake yalishuka kwa maeneo yenye viumbe wengi, na kupelekea kufukiwa kwa Wanyama wengi wazima kwa barafu, ambayo imewafanya mpaka hivi leo kuwa wamekufa lakini miili yao bado haijaharibika, kutokana na baridi huwa ikitunza miili isiharibike. pia kuna Ushahidi mkubwa katika miili ya Wanyama wengi wakiwa wanamivunjiko midogo ya mifupa ya aina ya mgandamizo tokea juu.
Watu wengi hujiuliza kiasi kikubwa sana cha barafu katika maeneo ya nyanda za juu sana, na chini za dunia ina maana gani? Kuwa Mungu aliumba dunia ambayo haitakuwa ikisapoti Maisha katika baadhi ya maeneo. ili nini sasa aumbe hivyo? au aliumba mfumo wa jua ambao utaathiri hali za hewa katika baadhi ya maeneo? Kama jibu ni hapana. Sababu ni ipi iliyosababisha? Dhambi ilipelekeaje barafu? Au ni muujiza? Maswali haya yote yanajibika kiurahisi sana kwa kutumia nadharia hii, kiwango hiki cha barafu kilichozalishwa ndicho kilishuka na kusababisha dhahama kubwa katika maeneo ambayo Wanyama wengi kama Tembo waliishi.
Kwanini Mungu Hakuumba Dunia Yenye Mabarafu Yasiyosapoti Maisha?
Uwepo wa kiwango kikubwa cha tembo ‘’mammoths’’ katika maeneo yale pamoja na wanyama wengine. ambao si hata wa jamii za maeneo ya barafu, au baridi kali, kunadhihirisha kabisa kuwa kulikuwa na maisha kabla ya barafu. Na hapo mbele tutaangalia kwanini maeneo yale ambayo tembo waliishi, yapo katika nyanda za juu badala ya ikweta, sababu ni kuwa, dunia ilishift uzito ‘’mass’’, yaani ilizunguka ‘’roll’’ na kupelekea maeneo yale kupanda juu. tutaangalia Ushahidi ambao pia ulichangia kubadilika kwa spidi ya dunia na idadi ya siku.
Kuna kila Ushahidi unaonyesha Wanyama hawa waligandishwa wakiwa wanakimbia, wengine wakiwa wanavuka mto.
Maelfu ya tembo mammoths wamepatikana, tena huku nyama zao zikiwa bado mbichi kabisa, huu ni Ushahidi kuwa gharika ya Nuhu haikuwa miaka mingi huko nyuma.
Picha chini inaonesha ziwa likiwa katika bara la Antarctica, hii inadhihirisha kabisa kuwa, awali maeneo haya yalikuwa maeneo mazuri kabisa yaliyosapoti Maisha ya viumbe wengi.
To be continued...






Join the conversation