SIKU YA O3 YA UUMBAJI KISAYANSI
SIKU YA 03 YA UUMBAJI
9. Mungu Akasema, Maji Yaliyo Chini Ya Mbingu Na Yakusanyike Mahali Pamoja, Ili Pakavu Paonekane; Ikawa Hivyo. Mwanzo 1:9Kumbuka hapo nyuma Mungu aliita katika sehemu zilizopita
‘’Firmament’’ au Anga au Raqia →mbingu ‘’heaven’’
Lugha nyepesi kabisa hii, Maji yaliyo chini ya Heavens ‘’Firmament’’ yakusanyike sehemu moja. Haya ni maji yaliyo juu ya Dunia. Na hiyo kauli ni sawa na kauli ya kusema hivi, Maji yaliyo chini katika mbingu ‘’firmament’’ yakusanyike mahali pamoja ili ‘’firmament’’ ionekane. ambayo ndiyo mstari unaofuata anaiita nchi, na sehemu ya maji anaiita bahari.
Hii ni kama ungelikuwa juu katika helikopta, na kisha ukatazama chini. ukawa unaona maji tu yakiwa yametanda katika uso wa dunia, hata dunia haionekani au haionekani vyakutosha. Basi ungeweza kusema kuwa, ‘’maji yaliyo chini duniani yakusanyike sehemu moja na sehemu kavu ionekane’’ au ‘’maji yaliyo chini ya dunia yakusanyike sehemu moja, ili sehemu kavu ionekane’’. sasa hii kauli ya pili ina utata kwa baadhi ya watu wanao unganisha pale katika ‘’maji yaliyo chini ya dunia, badala ya kuelewa kama, maji yaliyo chini, ya dunia’’ kumbuka Mungu alishaiita ‘’firmament mbingu’’ kwa hiyo hapa anachosema ni kuwa maji yaliyo chini ya mbingu. Na kama tafsiri ya Raqia ya hapa ingekuwa ikimaanisha ‘’anga la hewa’’, basi ingelikuwa ni vema tu ingeandikwa ‘’maji yaliyo chini yakusanyike sehemu moja, maana tayari chini itakuwa haimaanishwi mbingu. Kwa hiyo kusingekuwa na maana ya kusema chini halafu ‘’ya mbingu’’.
SAYANSI NYUMA YA UKUSANYAJI WA MAJI HAYA
Mungu anatenganisha maji kwa kuiinua ile sehemu ya ardhi kavu, na kufanya maji yakusanyike katika mabonde. Mtu anayeweza hisi jambo hili linahitaji Imani, hebu tazama kidogo mtazamo wa uwepo wa maji wa wanasayansi wasio amini Mungu. Ambao nadharia zao zinakubalika katika taasisi za elimu.
Sayansi Ya Asili Ya Maji Duniani Ya Wasioamini Mungu ‘’Big Bang and Evolution’’
Hawa wao kwanza wanaamini Dunia ni matokeo ya kugongana kwa vimondo ‘’meteors’’, na kukusanyika kwa mabaki ya vipande vya milipuko ya vimondo ‘Meteoritic Bombadrments’’. Kwao vimondo ‘’meteors’’ ni matokeo ya milipuko ya nyota zinazokufa ‘’Supernovae’’ tokea awali kabisa katika mlipuko wa big bang. milipuko hii ya nyota huzalisha elements nzito na nyinginezo kutoka mavumbi ya milipuko. hizi meteors huwa na spidi kubwa zikizunguka, na hapo awali zilikuwa nyingi sana kiasi zilikuwa zikigongana, na kupelekea matokeo yaliyopelekea uwepo wa sayari. hizi sayari awali kabisa zilikuwa za Moto sana kutokana na joto kubwa linalotokana na kiwango kikubwa cha msuguano’’frictions’’, mgandamizo ‘’presha’’, na umeme. hii ni kama ambavyo vyuma vinapogongana, au kusuaguana, huwasha moto sana.
Milipuko katika kuunda sayari ilikuwa na nguvu mamilioni Zaidi ya kawaida. sasa hili joto kubwa sana la Dunia ya awali wanasema ndilo ambalo limeendelea kupoa hata leo. Kiukweli sio kwamba kuna namna nina upendeleo ‘’bias’’, hata wao wenyewe wanajua kuwa ni kwasababu tu huko ndiko unapaswa kushikilia, lakini nadharia hizi zimejaa fikra zisizoleta mantiki. Mfano, Kama ukitafuta kujua maji yangewezaje kukaa katika dunia ya moto kiasi hiki, maana tunategemea yote yangeyeyuka! hata wao wanakiri kuwa hiyo ni changamoto. suluhisho wanalokuja nalo ni kuwa, ‘’ kulikuwa na meteors’’ au vimondo vingine, ambavyo hivyo vilileta maji duniani!
Wanatumia Ushahidi wa kuwepo kwa mabaki na barafu kwenye vimondo ‘’comets na meteors’’. vitu ambavyo hata wao hawaelewi imekuwaje? na ni katika nadharia za sayansi ya Biblia tu, mtu angeweza pata majibu kama tutakavyo ona hapo mbele kidogo. Kusema vimondo vilileta maji, si kweli kwa kuwa hakuna kimondo ambacho kimewahi onekana kikibeba maji hata sasa! na Dunia ndiyo sayari pekee yenye maji, na ndiyo maana, huitwa ‘’Water Planet’. hakuna sayari yeyote nyingine katika ulimwengu ambayo ina maji. na pia wengi hudanganywa hapa, wakihisi mantle au sehemu ya kati ya dunia ni uji uji, kumbe si kweli, mantle ni ngumu au solid. na hata core nayo ni solid, hizo zote tutakuja kuziangalia vizuri baadae.
Hakuna Nadharia yoyote inayoweza elezea namna imewezekana kuwepo kwa maji ndani ya dunia. Uwingi wa maji katika miamba ya dunia ndio unathibitisha Zaidi uumbaji wa Mungu. kwa maana, hakuna namna maji yangeweza kupenya miamba migumu ya dunia, kuingia maili nyingi ndani ya dunia. na pia maji hayawezi kudidimia kwa njia yoyote ile, kuingia ndani ya dunia.
Kitaalamu Zaidi ‘’Technically’’ uwepo wa milipuko ya migongano ya vimondo, ungepelekea kiwango cha Joto ambacho kwa namna yoyote ile, kisingeweza kupoa hata hii leo.
Kumbuka: hakuna Ushahidi wa nadharia hii, ni makisio tu ambayo yanatokana na mitazamo ya kuunganisha uwezekano wa matendo ya kifizikia, na kwa msaada wa hisabati. hii ndiyo sababu inakosa Ushahidi wa uhalisia, na Ushahidi wa kuhusiana na kweli zingine. Mfano,
Kiwango cha Argon katika vimondo ni kikubwa sana, kiasi kwamba kama ingelikuwa ni migongano na vimondo ndiyo iliyoleta maji duniani. basi kiwango cha ile argon kingekuwa kikubwa sana katika anga la dunia. na kwa kiwango cha idadi ya vimondo vya kutosha kujaza maji ya Bahari, basi Maisha yasingekwepo duniani kwa uchafuzi wa kiwango kikubwa sana cha hewa za uhai.
Mvuke pia ungelikuwa mkubwa sana katika dunia, kiasi cha kwamba, isingewezekana kwa namna yoyote ile kuwepo kwa Maisha katika sayari ya dunia.
Sayari za karibu na dunia zote, yaani Venus, na Mars. zina kiini au ‘’Core’’ iliyo ya baridi! hii inapingana na asili ya sayari kwa kutumia milipuko. na hata kukosekana kwa maji katika sayari ya Mars, kunaleta swali la kwanini yasingekuwepo au hakukuwa na milipuko ya vimondo huko? Huko mbele tutaona namna ambavyo sayari ya Mars, ina baadhi ya mabaki ya vitu vyenye Ushahidi wa Maisha toka duniani, na mwezi pia tutauangalia.
Hitimisho
Ninaposema kuwa Mungu alitenganisha maji ili mahala pakavu paonekane. namaanisha kuwa kuna chanzo cha Nguvu kisichotokea ndani ya dunia yenyewe ‘’External Force’’, na ndiyo maana, fizikia yake inakuwa inaleta maana kirahisi ‘’cause and effect’’. lakini kama ukitumia chanzo cha ndani ‘’inside force’’, basi utapata wakati mgumu kama wanasayansi hao ambao wanateseka kupata mantiki ya nadharia zilizowekwa.
10. Mungu Akapaita Pale Pakavu Nchi; Na Makusanyiko Ya Maji Akayaita Bahari; Mungu Akaona Ya Kuwa Ni Vyema. Mwanzo 1:10
Sasa hebu angalia sehemu ya ardhi kavu tu inaitwa ‘’Nchi’’. ila utakaposikia ikisemwa mbingu mpya na nchi mpya, basi ujue haimaanishi ‘’sehemu ya ardhi tu’’ bali na sehemu ya bahari. Hivyo ndivyo inavyoandikwa Biblia. ni kitabu cha watu wenye akili timamu, sio ya maroboti. na ndiyo maana ukiharibu sehemu moja tu, umeharibu sehemu zote. Biblia inasema aliyesema usizini, ndiyo aliyesema usiue. Vyote vimeungana.
Sasa hapa kuna kitu cha msingi sana ambacho msomaji anapaswa kujua. Dunia ya awali haikuwa kama hii ya leo. Dunia ya awali ilikuwa na kiwango kidogo cha maji katika nchi. Hayo maji yalikuwa katika makusanyiko ‘’sea’’ sio ‘’ocean’’.
1. Dunia hii ilikuwa imeungana katika nchi yote. Hakukuwa na utengano wa mabara kama ilivyo leo, na sehemu kubwa sana ilikuwa ni Nchi na sio maji kama ilivyo leo hii.
2. Kulikuwa na mito kadhaa ambayo, ilikuwa ikikatisha katika sura ya dunia kutokana na utofauti wa kimo cha ardhi ‘’altitude’’, kati ya sehemu na sehemu.
3. Hakukuwa na milima mirefu kama iliyopo hivi leo, milima ilikuwa ni miinuko ya kawaida. Ambayo ilikuwa na wastani sawa kwa sehemu kubwa.
4. Hakukuwa na haja ya mvua kama ilivyo leo.
5. Hakukuwa na miisho ya dunia yenye barafu kama leo, Arctic na Antarctic poles.
Sababu Ya Kukosekana Kwa Mvua Kwa Dunia Ya Awali
Kwanza kabisa kwa Ushahidi wa uwepo wa mabaki mengi sana katika ardhi ya makaa ya mawe, na miti iliyofukiwa. ‘’tutaangalia Zaidi baadae’’, kulikuwa na kiwango kikubwa sana cha miti, ambacho kilipelekea kiwango kikubwa sana cha umande kwa dunia, na oksijeni, na kaboni dioksaidi kwa ujumla.
Dunia ilikuwa na kiwango kikubwa sana cha maji yaliyokuwa chini ya dunia. kama ambavyo inaelezwa kuwa vilindi hivyo vilipasuka kipindi cha gharika. sasa basi, kiwango hiki cha maji kilikuwa kimefungiwa chini ya Nchi ‘’Locked in’’ na kuna Ushahidi wa uwepo wa ngome zilizokuwa zikisaidia kushikilia sehemu ya juu ya nchi, na sehemu ya chini ya dunia ‘’mantle’’. ambapo hapo katikati kulikuwa na maji. Sasa basi, kwa kila siku kunapokuwa na mzunguko wa Mwezi, ambao huwa ukivuta maji na kupelekea mawimbi wakati wa usiku, na kutokuwa kwa mawimbi kwa wakati mchana. hii inasababisha kama kupanda na kushuka kwa nchi ‘’Tidal Pumping’’.
Hii hupandisha Joto katika sehemu ya chini ya nchi, kutokana na mgandamizo mkubwa ‘’pressure’’, na msuguano ‘’friction’’. Ambazo hupelekea maji kuchemka sana na kiwango hiki cha joto hupanda na kufikia katika bahari ‘’seas’’. na kusababisha mvuke, na joto pia hupotea kwa njia ya kawaida ‘’conduction’’. Pia maji haya upande wa pili huwa kinyume chake, na ule mvuke wakati wa usiku hupoa. na kutengeneza maji ya kiwango cha kutosha kumwagilia mimea na mito ya awali. Huu mzunguko kwa kila siku husababisha uwepo wa hali bora wa hewa, bila uhitaji wa mvua.
Sababu Ya Kutengwa kwa Mabara Ya Arctic Na Antarctica
Wengi hawajui kuwa yale mabara yana Ushahidi asilimia 100% ya kuwa na viumbe hapo zamani. Tena ambao walikuwa wanaishi kule. Visiwa vingi sana, na maeneo katika maeneo ya kaskazini sana ya dunia, mfano Alaska, Siberia n.k kuna mabaki mengi sana ya Tembo wanaoitwa ‘’Mammoths’’. hawa ni kama tembo wengine, sio tembo tu, kuna mabaki ya Wanyama wengi sana nitakuja waelezea baadae. Pia kuna sehemu za Antarctic ambazo kuna maziwa ambayo yamefunikwa na barafu. Kiufupi maeneo yale yana kila kitu kama katika mazingira na mabara mengine. watu hawawezi amini uwepo wa miti mingi sana iliyofunikwa na barafu katika maeneo yale. Haya mabara zamani yalikuwa ni maeneo ambayo watu na Wanyama walikuwa wanaishi. Tutakuja kuangalia kipi kilikuwa chanzo mpaka imekuwa hivi ilivyo leo.
Je Nchi Ya Kwanza Ilikuwa Kama Pangaea
Ni kweli, lakini katika mfumo wa wazo la kuungana. Hata hivyo Kuna makosa mengi sana yaliyofanywa ya kulifanya bara la Afrika kuonekana ni dogo ukilinganisha na uhalisia wake. michoro mingi sana ililifanya lisikidhi katika uhalisia wake kabisa. wanakubali kuwa Nchi ilikuwa ni moja, lakini sasa hawawezi kuelezea ni vitu gani viliifanya itengane. na pia zipo nadharia tofauti tofauti za namna dunia ilivyotengana. huko mbele tutaziangalia zote. Ila kwa sasa cha msingi ni kupata picha ya dunia ya kwanza.11. Mungu Akasema, Nchi Na Itoe Majani, Mche Utoao Mbegu, Na Mti Wa Matunda Uzaao Matunda Kwa Jinsi Yake, Ambao Mbegu Zake Zimo Ndani Yake, Juu Ya Nchi; Ikawa Hivyo. Mwanzo 1:11
Mungu alipoiumba Nchi katika siku ya pili, alishaiumba katika namna ambayo alijua itakuja kuwa ndiyo msingi wa Maisha ya mimea. Mimea ili ikue, inahitaji sana madini. hasa madini ambayo yapo katika kundi la periodic table elements 26 za kwanza. Elements kama vile potassium, phosphorus, nitrogen, carbon, oxygen, calcium na baadhi ya Iron na Copper. Mimea inahitaji maji, na ndiyo maana akaumba mito ya kulowesha ardhi. Mimea inahitaji mwanga wa nyota, na ndiyo maana, awali kabisa nilionesha uwepo wa madude makubwa ‘’massive bodies’’ yanayotoa mwanga dunia inapojizungusha.
Mmea uliokufa unakila kitu ambacho kinapaswa kwa Maisha ya mmea, lakini hakuna anaeweza ufufua mmea ule ule, ila tunaweza zalisha Maisha toka kwenye mmea ule ule. Hii ni sawa na namna ambavyo tunaweza tumia Ngozi ya maiti kwa kiumbe asiye maiti. baadhi ya viungo vya maiti vinaweza waiwa na kutumiwa na mtu mzima kwa kuvihamisha, inaitwa ‘’organ transplants’’, Lakini sio mtu yuleyule. Hoja ni kuwa, Maisha hayaanzishwi kwa uwepo wa madini ya Maisha tu, yanahitaji Nguvu au Power. Nadharia za mabadiliko ya viumbe hai hufeli sana hapa kwa maana, hakuna ushahidi wala uwezekano wa kuanzisha Maisha, kutoka katika madini peke yake. Katika blog yangu mtandaoni nimeelezea kwa upana sana hisabati ya mimea, unaweza rejea uone namna mimea inavyofanya hisabati kubwa sana. Haina mantiki inaweza kuwa ni viumbe vya milipuko ya bahati. Pia nilielezea namna mwanasayansi Haeckel aliyejaribu kutaka kuunda japo chembechembe za uhai ‘’protini’ katika maabara ‘’laboratory’’, kwa kujaribu kutengeneza mazingira ya ulimwengu wa awali kabisa, na experiment yake ilifeli kwa kiwango kikubwa sana kwa kushindwa hata kutengeneza chembechembe zinazofanania na uhalisia wa Maisha.
hii ndiyo siku ya kwanza ya Mungu kusema ‘’akaona vyema’’, na anaanza na kuikuza mimea, na miti ya matunda. hii inakubaliana na kuwa, lengo la Mungu lilikuwa ni kuunda dunia itakayo kuwa makazi ya uhai, au namna ya kufanana naye. hii pia inaweza kuongezea hoja ya kuwa, mbingu ya siku ya pili, haikuwa anga au space, au atmosphere, bali ni firmament au dunia. na ndiyo maana inapewa kipaumbele kwa kila mstari, hata mstari wote wa nane. Mungu anaipenda sana Dunia, na alipanga yawe makazi yake na viumbe wake, na mfano wake mwanadamu, hata akaiita Mbingu ‘’heaven’ sawa na makazi yake ya Mbinguni.
12. Nchi Ikatoa Majani, Mche Utoao Mbegu Kwa Jinsi Yake, Na Mti Uzaao Matunda, Ambao Mbegu Zake Zimo Ndani Yake, Kwa Jinsi Yake; Mungu Akaona Ya Kuwa Ni Vyema. Mwanzo 1:12
Hebu tazama hisabati ya mimea kiufupi
Hisabati Katika Mimea
Ulimwengu umebalansi Maisha ya mimea kwa kuipatia madini ya kusapoti ukuaji wake. pia maji ya kiwango maalumu. lakini pia mwanga wa jua. ambao unapatikana kwa muda maalumu. hebu angalia hii hisabati. Maji yakizidi mimea isingeweza kukua, pia madini yangezidi sana, au kupungua, yangeathiri mimea. na bado mwanga wa jua ambao huwepo kwa nguvu maalumu, kama miale ingezidi nguvu ‘’frequency’’. au kupungua kidogo tu, mmea ungekufa. halafu bado, usiku mmea ili ukue usingehitaji mwanga wa jua, na dunia ikifahamu hilo, inajizungusha kwa masaa kadhaa tu kwenye jua, ili kusapoti hili. Halafu mmea huitaji hewa ya kaboni dioksaidi, ambayo hutegemea kwa viumbe wengine ambao hao huitoa bure kabisa. Na mmea wakati wa usiku, huwa hauhitaji hewa hii. na wale viumbe nao sasa, huwa wamelala.
Mmea nao husaidia huu mfumo wa akili ya ulimwengu kwa kuwapatia hao viumbe wengine chakula. ili hali wenyewe haunufaiki sana na hiko chakula, ila tu unanufaika na mbegu. Ambazo zingewaishwa kama hiko chakula kingeliwa na hao viumbe.
Ulimwengu hutambua ya kuwa, kama mimea isipokuwa chakula kwa Wanyama wengine, basi ingejazana sana na mbegu zake zisingepata nafasi ya kuota, kwa kukosa eneo. Na viumbe wengine wangekosa kabisa makazi. basi mimea mikubwa hubalansi ukuaji wa mimea mingine kwa kuchukua mwanga mwingi, na kunyonya maji mengi, huku hupunguza kukua sana kwa mingine. lakini bado mimea hii mikubwa, huzuia upepo mkali usiiathiri mimea midogo. Mimea huwasiliana kwa kutumia mizizi kwa chaneli zake zenye uhusiano na viumbe wengine kama fangasi, unaoitwa kisayansi “Mycorrhizal Network’’. hizi husaidiana kubalansi upungufu wa madini pale wengine wanapopata shida. lakini cha ajabu sana ni kuwa, mimea hii ya asili hukua kulingana na mazingira na uhusiano wake na viumbe wengine.
Je wajua?
Mimea huwasiliana kwa sauti ambazo ni ndogo lakini zinasikika, mimea hupashana habari juu tahadhari au uwepo wa chakula. Mbegu za mimea huwa si tamu kwa wanyama, huwa ni sumu, kumaanisha uhai haupaswi kuliwa, au Usiue. Na huwa nyeusi ukilinganisha na tunda linalopswa kuliwa, ambalo huwa na rangi ya kuvutia.
Mtihani Wa Akili Kwa Mimea
Kitu chochote kisicho na akili hufuata uelekeo tu wa kani za mvutano, kama mwanasayansi sir Isaac Newton alivyosema kwenye sheria yake ya mwendo ya pili. mimea huenda kinyume na hizi sheria, au kani za asili kama namna ambayo Mmea Hupanda Juu Kinyume Na Kani Ya Gravity. mmea hupandisha Maji Na Huchuja Madini kama tunavyochambua karanga kwenye mchanga, mmea Hupinda Kona kuutafuta mwanga, kama sisi tunavyozurura kutafuta chakula
Kwanini Baadhi Ya Binadamu Hufikiri Mimea Haina Akili
Binadamu hulinganisha mimea na Wanyama, kumzidi mtu kimo haimaanishi hana kimo. Hisabati ya mimea ni kubwa sana kwa binadamu yeyote kuielewa. hebu tafakari mpaka leo hii, hakuna hata binadamu ambaye angeweza kutatua tatizo la upotevu wa mimea kwa kutengeneza mfanano wa mmea. Ambao ungeweza kuingia kwenye darasa la hisabati la mimea la ulimwengu. si mchezo kuzungumza na ardhi, na jua, na hewa, ili kutengeneza chakula. Ambacho pia kitamsaidia na kiumbe usiemjua, ila tu unajua atakupatia hewa ya kaboni daioksaidi.
Hisabati Ya Ndani Kabisa Ya Mimea
Leo hii inafahamika namna mimea ilivyo na taarifa nyingi za kibiolojia ya ndani kabisa ‘’genes’’ ukilinganisha hata na binadamu. hizi zinauwezo wa kuchambua, au ‘’process’’, taarifa nyingi Zaidi ya kompyuta yeyote. mimea ina uwezo wa kufanya matendo ya kibiolojia ‘’chemical reactions’’ mengi,na kwa umakini mkubwa sana. kama matendo haya yangefanywa na binadamu, basi dunia nzima ingeitambua hiyo maabara kama ni maabara ya Mungu mtu . Picha chini inaonesha moja ya hatua zinazopitiwa na mmea, ili tu kupambana na mazingira hatarishi kama yenye chumvi nyingi kwenye ardhi. Ingelikua ni mfumo taka ambao binadamu angeugundua, angehisi ana akili kuliko chochote kile ulimwenguni. lakini kwa mimea ni teknolojia ya kawaida sana.
Mmea unafanya maelfu ya matendo ya kikemikali ambayo yanafanyika kwa akili nyingi sana, na umakini mkubwa sana. Mtu yeyote yule anayesoma fiziolojia ya mmea, hawezi kukubali kuwa mmea unaweza tokea kwa bahati bahati. Mmea una uwezo wa kujiongeza katika kuchukua hatua mazingira yanapokuwa sio Rafiki kama ulivyo huu mfumo hapa chini. kama mimea isingelikuwa ni matokeo ya uumbaji wa Mungu, yaani ni matokeo tu ya kawaida. hata sisi tungeweza jaribu, au shuhudia, hata ajali tu ambayo ingeweza tokeza kitu cha mfanano huu.
Je Wajua?
Mimea ni urembo mzuri sana hata kwa picha za satalaiti zinazopigwa nje ya dunia. Rangi zake ni za Ajabu sana. Mfano Rangi Ya Purple imetengenezwa kwa shida sana, na ndiyo maana hata haikwepo kwenye Bendera Nyingi. kwa maana mpaka miaka ya 1800 ilikuwa ni gharama sana na ngumu kuitengeneza. lakini mimea inajitengenezea tu kirahisi sana. Picha ya mimea ya rangi ya purple. Hii ni bustani bora kabisa ya asili, sio jambo jepesi kuumba mimea na aina zake za ajabu.
13.Ikawa Jioni Ikawa Asubuhi Siku Ya Tatu. Mwanzo 1:13
Siku ya Tatu yaani ndani ya masaa 72, tayari dunia ilikuwa imetoka katika hali ya hakuna kitu, mpaka hali ambayo mimea inaishi. Hakuna sehemu tumeona kuna kiwango kikubwa sana cha Joto kama la mlipuko wa Big Bang. Mimea pia inapatikana kumaanisha kuwa hakuna Nyota iliyo Karibu ambayo ingeweza kusababisha joto la kukausha mimea na maji. Ila hakuna sababu ya kukataa uwepo wa Quasars, kwa maana hizi hazidhuru hali joto ya mazingira haya.
Kuna watu wanaoamini uumbaji wa Mungu, lakini wanaamini siku hazikuwa na maana ya masaa 24, bali ni kama zama. wao huamini dunia ni miaka mabilioni. Hawa hushindwa kuelezea imekuwaje mimea iishi miaka mabilioni bila Mwanga wa Jua, ambalo liliundwa katika siku ya nne. Na hawa wanafanana na wanafalsafa wa ‘’Hand Off theology au Deism’’. ambao huamini Mungu aliiumba dunia na kisha akaitelekeza. hii ilianzia kwa wanafalsafa kama Ethan Allen na Thomas Paine. Kwa Mtu Mkristo kuamini katika hii falsafa ambayo inatokana na nadharia ya Gap theory, ni hatari sana.
Gap Theory Ni Nini?
Hii ni nadharia inayoamini kuwa, kati ya mwanzo 1:1 na 1:2. kulikuwa na kipindi kirefu sana cha muda, wa kukadiriwa mabilioni ya miaka. Na hutumia pia baadhi ya mafungu kama
Yeremia 4:23 ‘’Naliangalia nchi, na tazama ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru’’.
Nina uwezo wa kuielezea ila sioni umuhimu wa kuelezea kila nadharia hasi za baadhi ya watu wachache, maana itani gharimu kitabu chote kuzungumzia mawazo yasio na ukweli. na hayana nguvu. wala hayawezi jibu maswali ya kisayansi, wala yanayohusu ukombozi. maana wengi wao hukubali kifo kabla ya dhambi ya adamu. Wakikifanya Vifo vya kabla ya Uumbaji wa siku sita kama chanzo cha uwingi wa mabaki ‘’fossils’’, yanayoonesha kuwa ni ya miaka mamilioni kabla ya Adamu, na kwa mantiki hii, hata ujio wa kristo hauna maana tena, na hata huamini Bigbang ndiyo mwanzo wa ulimwengu. kiufupi kwao hakuna maana ya kitabu cha mwanzo. na huwa na Ushahidi wa kufikirika na kurukiarukia hoja bila kuwa na upanuzi wa kifikra.
Watu hawa huitwa ‘’Theistic evolutionists’’ mfano ni Dr. Hugh Ross au Professor of philosophy in science Willium Lane Craig na hata Oxford Professor of Mathematics John Lennox. Hawa watu wana ajenda ya kuunganisha pande mbili, kati ya upande wa wakristo waaminifu wa uumbaji wa Mungu, wasomi wa sayansi, na wanasayansi wapagani, au wasioamini, kwa kuwantengenezea uwanja mmoja wa vuguvugu. Pia huitwa ‘’Old earth Creationists’’. wapo wakristo baadhi maskini wasio elewa kiundani mtego huu, na hukubaliana nao, lakini ukiwa makini utagundua wengi wao ni wasomi wanaoelewa, lakini bado hawajaelimika vya kutosha katika nyanza zote za taaluma, au ni maslahi ya kiuchumi, nafasi, na kipaumbele kwa watu huwafosi kuwa walivyo.
Hitimisho
Siku ni siku, na sehemu ambayo siku imetumika kinabii huwa inaeleweka na huwa haileti shida. uwezo wa Mungu ni mkubwa sana na ndiyo maana Tunamwabudu. kwake kuumba ndani ya siku moja haya yote tunayoyaona sio jambo la kustaajabisha.
To be continued....









Join the conversation