ILIVYOKUWA IKIUMBWA DUNIA
MAMBO YA MUHIMU YA KUFAHAMU
Kani ya Mvutano ‘’Gravitation’’
Siku zote vitu huvutwa kurudi duniani, na ndiyo maana ukirusha jiwe litarudi. Mwanasayansi Isaac Newton aligundua kuwa siku zote vitu vyenye uzito huvutana. na kitu kizito Zaidi huvuta zaidi vitu vyepesi kuelekea kwake. Mwezi huvuta na huvutwa Duniani, na ndiyo maana huizunguka dunia. kama mwezi usingekuwa na nguvu kabisa, basi kani hii ya mvutano ya gravitation ingeuvuta mwezi hata kuangukia kabisa katika dunia, lakini mwezi nao unaivuta dunia japo kwa kani ndogo. na hiyo inaweza elezea kwanini kuna mawimbi baharini, ni kwasababu maji ya bahari huvutwa na mwezi. tukiendelea Isaac Newton aligundua siku zote kani au Force, inapokuwa imeelekezwa kufanya kitu, huwa kuna inayokinzana nayo. Na ndiyo maana, unaporuka kwenda mbele, mchanga hurudi nyuma.
Na hivyo basi, hata mwezi kuna kani inayoisukuma kutoangukia duniani moja kwa moja ‘’Centrifugal force’’. Pale kani hiyo inapoishiwa nguvu, basi hutokea kama vimondo vinapoangukia duniani moja kwa moja. Dunia pia huvutwa kuelekea kwenye Jua. na ndiyo maana tunalizunguka jua. Miongoni mwa vitu vinavyo staajabisha sana, ambavyo vinafanya dunia isimsahau Isaac newton. ni namna pale wanasayansi waliokuwa wakienda mwezini walipotupa chupa za maji, na mabaki kwenye anga, basi yaliendelea kuwafuata katika safari yao yote katika anga ‘’space’’. Sisi pia tunavivuta vitu vyepesi, ila haviwezi tufuata kwa sababu tupo juu ya dunia yenye nguvu ya mvuto Zaidi yetu. Pia bwana Newton alionyesha namna ambavyo kama mtu angetembea na spidi ya kilomita kumi na moja kwa sekunde 11km/s. basi angeweza ivuka kani hii ya mvuto, na asirudi tena duniani, yaani kama ukirusha jiwe basi halitarudi tena.
MAPINDUZI YA NADHARIA YA GRAVITATION YA EINSTEIN
Miongoni mwa vitu wasomi wengi hawajui ni kuwa Gravitation sio kani au Force kama walivyofundishwa katika elimu za misingi, sekondari za kati, na juu. Gravitation ni mithili ya kitu kinachotumbukia ndani ya kitu chenye mtelemko. unapoanguka kutoka kwenye mti, hakuna mtu anayekusukuma ila unashuka na mabadiliko ya spidi ya gravitation yaani 9.8m/s². kwa hiyo gravitation inatufunulia ya kuwa, Dunia ipo katika ulimwengu ambao una vitu vidogo usivyoweza viona mithili ya matundu ya Neti ‘’Space Fabrics’’.Uwepo wa dunia yenye uzito, unakandamiza neti hili na hivyo basi, vitu vilivyo katika hii neti, vinaanza kuwa na hali ya kusukumwa kutumbukia katika kitovu cha dunia. Na hivyo basi, Jua limekandamiza sana neti hii, kiasi kwamba hata dunia nayo inazunguka ikisukumwa kuelekea katikati ya jua. Neno ‘’Space fabrics’’ linatumika kuelezea pande kuu tatu za dunia ‘’3 Dimensions’’, na pande nyingine ya muda ‘’4th Dimension’’. Kwa hiyo Muda, Nishati, Uzito, na Eneo vyote vimeungana kimahusiano ya ulimwengu. KUMBUKA: hali hii ya kuvutwa kuelekea katikati ya dunia au Jua, hutokea katika pande kuu tatu ‘’3D’’ yaani aliyechini katika kitovu cha kusini cha dunia, anahisi kama tu aliye katikati ya dunia, au Equator, au aliye upande wa Juu kaskazini. Pande zote tunahisi hali ile ile, na Neti lile ‘’Space Fabrics’’ lipo katika kila upande. Gravitation sio kani, ni mithili ya mtelemko. Neti ndio space fabrics.
Maada ‘’matter’’ au kitu
Mtu akikuuliza kitu ni nini? Utaanza kumwelezea kama mithili ya kinachoweza onekana, au shikika, au tabia zake zinaweza kuelezeka. Kitu au maada unaweza ichunguza, na unaweza ivunja vunja mpaka ndani ili uweze ona kuna nini ndani yake. ndani yake utaona chembechembe ndogondogo sana, zinazofanana, zinaitwa atomu. Atomu hizi ukizivunja Zaidi, zina chembechembe tena ndogondogo zinazoitwa ‘’elektroni na nyuklia’’. Uzito wa atomu karibia asilimia tisini na kitu, upo kwa ndani Zaidi ambapo kuna nyuklia. ambazo ukizivunja, utaona chembechembe nyingine zinazoitwa ‘’nyutroni na protoni’’.
Bado ukizivunja Zaidi, utapata chembechembe ndogo Zaidi zinazoitwa Quarks (zipo aina za juu na chini). Chembechembe hizi Quarks zinashikiliwa na mithili ya kani inayoitwa ‘’Gluon’’, na pions kwa ndani zaidi. Kitovu cha sayansi cha kuona kitu au matter kimeishia katika Quarks na Leptons. ‘’elektroni’ zipo katika kundi la leptons na huitwa ‘’Fermions’’. Ndani ya atomu kuna aina nyingine ya chembechembe isiyo ya kitu au matter, bali ya nishati au energy. Hii inasadikiwa kubadilika badilika kati ya kitu na nishati, hii inaitwa ‘’Bosons’’. kwanini haya yote? Ili uumbe kitu kama mimi na wewe, unapaswa uwe na atomu awali kabisa. au uwe na chembechembe za atomu.
Kuumba kitu bila uwepo wa kitu kingine, hauwezekani katika namna ya kawaida. Mwanafizikia Peter Higgs aliyegundua chembechembe ya ‘’Boson’’ na kupewa tuzo ya Nobel Prize, aliaminiwa na kupendwa na wengi wa wanasayansi wasioamini. kana kwamba amegundua ‘’chembechembe ya kiungu’’ au ‘’god particle’’ . hii inatokana na kuwa chembechembe hii inaaminiwa kuweza kubadilika kutoka kwenye nishati au energy, na kuwa kitu au matter. Na basi wao hutumia hii kumaanisha ya kuwa, hapo awali kabisa kulikuwa na nishati kubwa sana yenye nguvu sana, ambayo ilibadilika na kuunda kitu au vitu vilivyopo leo katika hali zao za awali kabisa, yaani chembechembe ndogondogo kama hydrogen na helium. Hata hivyo nadharia ya huyu bwana Higgs Boson haikubaliki na wanasayansi wengi kwa kukinzana na uhalisia mwingi, na pia inakosolewa kwa kuongezea ugumu’’complexity’’ ili kukidhi usahihi wake.
KUFELI KWA NADHARIA YA WASIOAMINI NAMNA HUWEZI KUUMBA KITU KUTOKA SIFURI ‘’NOTHING’’
Ukiachana na bwana Peter Higgs. Wapo wengi waliokuja na nadharia za uwepo wa Antimatter. Watu hawa wanachotaka kusema ni kuwa, kila kitu kina pea yake ‘’pair’’. ambayo inafanana kila kitu ila inakuwa kinyume chake, ila hatuwezi iona kirahisi. baada ya ulimwengu kulipuka zilikwepo pea ‘’pair’’ sawa sawa kwa kila chembechembe. ila sasa kwanini sisi tunaona vitu tu ‘’matter’’ tu, hatuoni kinyume zake ‘’antimatter’’! basi wanasema kuwa zile nyingi zilipotea. kwanini? Hakuna majibu yanayoleta maana. Wanachokisema ni mithili ya hesabu hii chini
"Matter+ Antimatter=Nothing"
SINGULARITY NI NINI?
Hapa wanamaana awali kabisa ulimwengu ulikuwa mithili ya sifuri. Yaani mithili ya kitu ulichokiminya mpaka kielekee kupotea. Yaani kila kitu unachokiona duniani, sayari, nyota n.k. vyote viliminywa hata kuelekea kupotea kabisa. Nishati au energy density ilikuwa mithili ya isiyo na mwisho, yaani kubwa kuliko kawaida ‘’infinite energy density’’. Hiyo nishati ilipolipuka ikatengeneza hizo pair mbili ambazo sisi tunaona moja tu. kwasasa nadharia hii haikubaliki maana haina ukweli kwa kuwa haina hata misingi ya kifizikia, kwa kuwa katikati ya singularity, hata sheria za fizikia hazifanyi kazi. Mwanasayansi mmoja aliyekuwa anaitwa Stephen Hawking alihangaikia sana ‘’Black holes’’ nitazielezea huko mbele, kwa kuwa zinaonyesha dalili ya uwepo wa nadharia hii. lakini nazo hazikuonyesha alichokipambania mwanasayansi huyu asiyeamini Mungu mpaka kifo chake. Chembechembe za ‘’Antimatter’’ zipo chache sana, mfano mzuri ni ‘’Positron’’, haziwezi kuelezea mlinganyo wa awali wa Ulimwengu, hata kwa baadhi wanaoamini kuwa antimatter kwa asili ni antigravity.
To be continued....





Join the conversation