Badiliko La Mhimili Wa Dunia "Big Roll"
Badiliko La Mhimili Wa Dunia "Big Roll"
Dunia iliwahi kubadilika katika namna imekaa katika mhimili wake, kwa kushuka chini kidogo. Na kitendo hicho ndicho kilichopelekea mgawanyo wa mabara, upelekee baadhi ya mabara yaingie katika ukanda wa mabarafu, au kilele cha dunia. Hapa nazungumzia moja kwa moja mabara ya Antarctica na artica. Kwanza kabisa kabla hatujalitazama kiundani badiliko hili, tunapaswa kutambua kuwa ramani ya dunia ya awali kabisa ilikuwa Haina mabara yaliyotenganishwa, yaani yaliungana. Ila baada ya muda Fulani, mabara haya yalitengana kwa namna ambayo inaelezewa vizuri kupitika nadharia ya Gharika ya Nuhu.
Japokuwa nadharia ya mabadiliko inayoitwa "continental drift theory" inatambua pia kuwa hapo awali dunia ilikuwa imeungana, na Tena wao waliipa jina kabisa nchi ile ya awali iliyounganika wakiita "Pangaea". Tatizo kubwa la kwanza walilolifanya ni kuwa, katika ramani yao Afrika waliidogosha kwa asilimia 35, ili tu iweze kufiti katika mchoro wao kitu ambacho Sasa kimegundulika wazi na kuonekana si kweli. Hebu rejea mchoro huo wa zamani wa Pangaea unaoaminiwa hata Leo, ilihali umeshaonekana kuwa na makosa.
Katika mchoro huu bara la afrika limedogoshwa Sana, na bado unamapungufu mengine mfano; Amerika ya Kati imeondolewa pamoja na Mexico ya kusini na visiwa vya Caribbean. Australia imepuuzwa kwa kuwa, kwa kuweka Australia kutaleta matatizo makubwa ya kufiti kwa mchoro huu wa dunia ya awali.
Amerika ya kaskazini na kusini zimezungushwa kwa uelekeo mmoja, na hata bara la afrika limezungushwa kuelekea chini, "clockwise". mchoro huu hauna sababu za uthibitisho kisayansi.
Nadharia ya Gharika ya Nuhu inatoa mwongozo Bora kabisa wa kutambua mwonekano wa awali wa dunia. Ramani ya awali kabisa ya dunia inaanza kuchorwa tokea katika mstari wa mpasuko, au " mid Atlantic ridge", na dunia inawekwa kwa saizi yake halisi, " afrika haipunguzwi kwa asilimia 35% Kama ramani za awali". Hebu rejea mchoro huu chini.
Huu ndio mchoro Bora zaidi wa dunia kabla ya Gharika ya Nuhu. Na sio kabla ya continental drift ya plate tectonic plates kwa mabadiliko yasiyo na sababu za kisayansi na hata ushahidi wa macho.
Vitu vya kuzingatia katika kutambua maana ya "big roll"
Dunia iliroll kuelekea chini baada ya kupasuka kwa mabara haya. na mpasuko huu uliambatana na kumeguka kwa hydroplates." Hizi ni sehemu za tabaka la chini la nchi. Zipo mfano plates zinazoshikilia bara ya afrika, America, Pacific. na hizi plates ziliathiriwa baada tu ya mpasuko na kuundwa kwa mid Atlantic ridge. Hapo mbele nitaonesha namna mpasuko huu ulivyopelekea madhara na maeneo mengine.
Baada ya mpasuko katika Atlantic plate, na kuinuka kwa plate ambayo ni sehemu ya ndani iliyo msingi wa nchi. Basi ilipelekea sehemu za nchi "Earth's crust" kuteleza kutelemka, Kama nilivyoonesha kule nyuma katika kielelezo. na Sasa Basi, kitendo kile Cha kutelemka kwa nchi, kuliisababisha kukunjika na kutengeneza mabonde. Hii ni Kama ambavyo wewe ukikandamiza Kona mbili za chuma, utaona kuwa ikitengeneza umbile la mikunjo ya juu na chini. Hivo fikiria mikunjo ya chini Kama mabonde, na mikunjo ya juu Kama miinuko.
Kumbuka kuwa kadri ambavyo nchi ilikuwa ikiteleza kuelekea mbali na muinuko wa Atlantic ridge, Basi ilipofika mwisho wa plate husika, ilisimama kutokana upinzani mkubwa unaotokana na kani ya msuguano "friction", na kinzani "inertia" zingine kutoka kwenye miamba. Hii ndiyo sababu kubwa utaona, milima mingi mikubwa ikiwa katika uelekeo sambamba na uelekeo wa mid Atlantic ridge. Hii ni sawa na kusema kuwa, yalikuwa ni matokeo ya mikunjo mikubwa kutokana na uwepo wa kani kubwa zaidi ya compression katika kingo za plate. Hebu tazama kielelezo na Kisha ramani ya dunia kuangalia Sifa hizo.
kielelezo hiki kinaonesha namna kitu hupinda kwa kukunjika. kumbuka kitu hiki hakiwezi kunjika kikaunda umbo mithili ya upinde, au V, kwa kuwa tayari chini Kuna tabaka la mantle, ambalo linazuia kudidimia kwa Earth's crust.
Picha inayoonesha milima katika usambamba wa mid Atlantic ridge.
Unaweza ona namna safu kuu za milima yote, ipo sambaba na mid Atlantic ridge. hii inathibitisha kuwa kukunjika zaidi kwa milima "buckling" ni matokeo ya kupanda kwa Atlantic ridge.
Ni muhimu kutambua kuwa, Kuna safu kuu mbili za milima iliyosambamba. yaani Kuna milima ya Himalaya, na milima ya Rocky. Milima hii ina uzito mkubwa Sana. kutokana na kiwango kikubwa Cha miamba iliyojikusanya katika eneo moja. hii ni Kama unapotengeneza tuta, uzito mkubwa zaidi huwa katika sehemu uliyokusanya udongo. hivyo Basi, ukirejea mchoro sahihi wa dunia kabla ya kutengana mabara, unaweza ona namna milima hii mikubwa kuwa ilikuwa katika sehemu za juu za dunia tofauti na iliyopo kwa Sasa.
tukio la kuroll kwa sayari ya dunia
Kuroll kwa dunia kulihusisha tukio la mabara kushuka chini, mithili ya mpira unaouzunguka ili sehemu iliyojuu ifike katikati. Baada ya mabadiliko ya uundwaji wa milima, kiwango kikubwa cha uzito wa safu za milima ya Himalaya na mingineyo iliyokuwa juu, kilishuka hata kilipofikia maeneo ambayo kilibalansi na milima ya upande wa pili.
Hebu tazama kielelezo hiki chini.
Namna ambavyo uzito uliishusha dunia katika mhimili wake hata kufikia kiwango ambacho kiko hivi leo. Uzito uliokuwa upande wa Himalaya, haukuishusha sayari ya dunia mpaka chini au Kati. Bali uliishusha hata ilipobalansi na uzito wa milima ya Rocky na Andes.
Matokeo Ya Kuroll Kwa Dunia "Earth Tilt"
kubadilika kwa dalili kadhaa za majira.
Hii inatokana na kuwa, baada ya Gharika ambapo kiwango kikubwa Cha maji kilipotea na uzito kwa ujumla. Sasa dunia inapo roll, dunia imebadilika baadhi ya sifa zake. kama “moment of inertia", angular momentum, na hata kinetic energy. Hizi na nyingine nyingi zote kwa Pamoja, ndizo zilizopelekea dunia ikaongeza siku za mzunguko wake kulizunguka jua. kutoka 360 mpaka 365.25. hii ni kutokana kuongezeka kwa spidi ya mzunguko wake kulizunguka jua.
kulipuka kwa volcanoes
hii ni kutokana na uhalisia kuwa, baada ya mabadiliko ya dunia kuroll mpaka ilipofika maeneo iliyopo leo, iliongeza zaidi kujitanua. hii ni sawa na kusema, dunia haikubakia Kama mpira yaani "circle" Bali ilikuwa Kama yai "sphere". Mabadiliko haya yalipelekea kiwango kikubwa Cha uzito kutoka sehemu za ndani kujazia sehemu hizi zilizojitanua, na matokeo yake ilikuwa ni kiwango kikubwa Cha magma kuyeyuka toka katika sehemu ya ndani "earth's core".
Kumbuka kiini katika dunia ni kigumu "solid", au unaweza sema kuwa presha kubwa Sana imefanya sehemu ya ndani ya dunia kuwa "solid". Sasa Basi inapotokea sehemu za Kati za dunia na kuelekea nje zina uwazi, Basi hiyo hupelekea presha kushuka, na kiwango Cha madini yaliyo ndani ya dunia huyeyuka, ili kujaza nafasi katika sehemu hiyo, na kadri inavyoyeyuka, magma huundwa. Ambayo hupanda ikielekea sehemu hizi zenye mipasuko, na kupelekea magma kuganda Katikati, au kutoka hata nje Kama volcano.
kosa juu ya tafsiri ya chanzo cha volcanoes
Kutafsiri kuwa volcano zinatokana na magma kutoka katika kiini au ndani ya dunia "Earth's core" sio kweli. kwa kuwa magma huwa Ina asili ya kujiminya Sana ukiikandamiza "compressible". Hii Ina maana kuwa, kiwango Cha magma kisingeweza kuendelea kupanda tokea ndani kabisa ya dunia kikiwa na Nishati ya kutosha hata kufika nje ya dunia. ukweli ni kuwa misuguano baina ya matabaka ya juu, Kama vile mabadiliko yanayoweza Leta tofauti za kimgandamizo. Mfano, presha za miamba ndani ya dunia bado hazijatulia, bado Kuna misukumo kadhaa ya matokeo ya mabadiliko ya dunia yaliyotokea, na haya ndiyo huwa yakipelekea hata matetemeko ya ardhi kwa wakati, na sehemu tofauti tofauti. Na hivyo Basi, kiwango kikubwa cha joto, na Nishati, huweza pelekea hata kuyeyuka na kupanda kwa magma katika maeneo kadhaa yenye mipasuko.
Kuzunguka hivyo ndiko kulipelekea Kusogezwa kwa mabara kadhaa hata kufika katika vilele vya dunia, na kuambatana pia na mabara ya barafu.
*******************----------------****************
To be continued







Join the conversation