Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

TAMBUA VIPAJI VYA UBONGO & UWEZO WA NDANI

VIPAJI na Ubongo

Sayansi Ya Uwezo Wa Ndani Wa Ubongo


Namnukuu Professa Ruparte Shekdrake, badala ya kusema kuwa unachokifanya leo, kinasukuma mwonekano wa kesho yako. Sema hivi, Mwonekano wako wa kesho, unakuvuta katika unachopaswa kukifanya leo. Binadamu hajawai kuzaliwa bila mapenzi, binadamu huzaliwa na mapenzi tayari ya mambo yake binafsi. Kila baada ya siku 60 kila chembechembe iliyomo katika mwonekano wa mtu hupotea, lakini mtu bado huonekana vilevile, hii ni kwa kuwa mwili tayari unajua wewe unapaswaje kuonekana. Ipo siri ya sababu ya namna unaonekana, hiyo siri ni ngumu sana kuigundua, na hiyo ndiyo sababu ya sura hii ya kitabu.

Ulipokamilika kuundwa Ubongo wako, malengo yote ya sababu na ubora wako yaliwekwa katika Ubongo. ubongo wako ulipatiwa mafaili ya kuwa wewe upo bora wapi, na unahitaji marafiki gani, unahitaji mpenzi wa namna gani, unahitaji kazi za namna gani, hautakiwi kuwa katika mazingira gani, unapenda sana kula vyakula vya namna gani, na unapaswa kukua kwa spidi gani. Taarifa hizi zote ziliwekwa katika ubongo na mfumo ambao ulipokuwa unakuumba, ulijua kila kitu kuhusiana na wewe. Huo ndiyo mfumo unaokutambua wewe, kwa kuwa uliongoza wiki nane zote ulipokuwa unatengenezwa tumboni. Hebu tuangalie kwa mfano namna ya taarifa hizi zinavyokuwa.

Uwezo Au Kipawa 

Chukulia mfano swala hili, Ulipotengenezwa tu tumboni, mwili wako ulishajua kuwa kutokana na namna misuli yako ilivyo, wewe utakuwa bora sana katika shughuli za matumizi makubwa ya misuli. Sasa hivi sote tunafahamu kuwa watu waliobora sana katika misuli yao, huwa wana ufanisi mkubwa sana katika kuzalisha nishati katika mitambo ile ya ‘’mitochondria’’, na kutozalisha sana kemikali sumu ‘’free radicals’’. Watu hawa tangu wanapokuwa tumboni hutengenezwa kuwa na mapafu imara sana, na huwa na mfumo wenye nguvu sana wa kusukuma damu. Taarifa za muundo huu huwa zimetapakaa katika ubongo wao wote, na wao tangia wanapokuwa wadogo huwa wanapendelea sana mazingira yanayohusisha matumizi ya misuli hasa kiushindani. Sasa basi, kumbe ijapokuwa mtu anaweza kuwa asijue kipawa chake, lakini ubongo wake huwa unajua kitambo sana.

Kipaji Ni Nini?

Kipaji ni namna mtu anaweza kufanya jambo fulani kirahisi, lakini wengine hulifanya jambo hilohilo kiugumu sana. Kwanini yeye alifanye kirahisi? Kwa kuwa yeye namna alivyo, yupo tofauti kiasi kwamba jambo lile hulifanya kirahisi. Mtu ana kipaji cha kukimbia haraka, kwa kuwa mapafu yake, misuli yake, na mfumo wake wa damu una ufanisi mkubwa sana, kiasi wengine tunaposhindana naye, kutokana na kutokuwa bora kama yeye, tunatumia nguvu nyingi, na kutokuwa bora kama yeye. Inapotokea fursa inayohitaji watu wanaoweza kuwa mahiri katika matumizi ya misuli, yeye anaonekana bora zaidi, na huu uwezo wake unasemwa kama kipaji au Zawadi. Je kuna watu wasio na vipaji? Hakuna. Na ulimwengu haupo tayari kutambua kipaji chako. Kila mtu ana kipaji, maana kipaji ni utofauti. Kila mtu ana kipaji, kwa kuwa kila mtu anautofauti. Ilipasa mfumo wa elimu na maisha ubadilishwe, ili kila mtu ajue kipaji chake. Ila haitawezekana, maana kama kila mtu atajua kipaji chake, hakuna atakayekuwa mtumwa wa mwingine.

Aina Tano Kuu Za Vipaji

Narejelea kazi kubwa iliyokwisha kufanywa na Howard Gardner, ulimwengu una aina kuu tano za vipaji, ambazo hizo ndizo zinatoa makundi makuu yakuelewa uwezo wa asili wa watu, au vipaji. Kumbuka vipaji ni vya msingi sana katika kujua uwezo wa siri uliomo ndani ya mtu. Maana vipaji ndiyo uelekeo wa mtu kiutendaji, vipaji ndivyo vinaeleza uelekeo wa mtu, ingawa bado, hatma ya mtu hutegemea zaidi utofauti alionao. Zifuatazo ni aina za vipaji.

Uwezo wa Kuelewa ‘’Intellectual talents’’

Hili ni kundi la watu wenye vipawa vya kuweza kuelewa mambo kwa kina sana. Kundi hili ni pana sana. Kundi hili huwa na watu ambao huelewa kiurahisi sana mambo ambayo, wengine huangaika sana. Unapoenda katika kila taasisi, au kila sehemu, huwa kuna watu hawa. Utawakuta katika michezo wakiweza kuelewa sababu za kina, za kila kinachotokea. Utawakuta katika historia, katika dini, katika elimu za sanaa, katika elimu za sayansi, na tena sayansi za kila aina, utawakuta katika sayansi za fizikia, sayansi za kemia, jiografia, biolojia, hisabati, utawakuta katika sayansi za mitambo na mitandao, utawakuta katika falsafa, katika siasa, hawa watu hata kama ni mapishi, wao huwa na uwezo wa kuelewa kwa kina sana kila jambo linalotendeka pale.

Watu hawa huwa na sifa kadhaa, huwa ni wapenzi sana wa kujiuliza maswali, wao huanza kuuliza Nini, kwanini, kivipi, wapi, kuanzia lini, itakuwaje, kwao hawa maswali sio maamuzi yao, kwao hawa wana msukumo wa asili wa kutaka kujua. Watu hawa japokuwa wengi huisi ni watu wenye akili sana, lakini ukweli ni kuwa, huwa tu ni vipaji vya Ubongo. Watu hawa huwa na ufanisi mkubwa sana wa uwezo wa ubongo wa kuchakata taarifa nyingi. Wao huwa hawachoki kuunganisha doti hata kujua sababu za mambo yanayowazunguka. Wao husisimka sana wanapopata majibu kuliko maswali. Watu hawa wana uwezo mkubwa sana wa kujizuia, hawa sio watu wakihisia, wanaweza kufikiria hata jambo ambalo watu wanaliona halina msingi, hawa ni watu ambao wana uwezo wa asili wa kuelewa.

Cha ajabu ni kuwa watu hawa katika jamii huwa sio wenye ufaulu mkubwa sana darasani! Na mara nyingi hata katika maisha. hii ni kwa kuwa, huwa wanapotea katika maswali yao wanapokosa majibu, au wanapopata majibu yasiyo sahihi. Watu hawa wanapenda sana kusikiliza, na wanapozungumza hupenda sana kukufanya ujiulize maswali, watu hawa wengi sana ndiyo huikoa dunia. Watu hawa ndiyo huelewa changamoto, sababu, na namna matatizo mengi yanatokea, na hata namna yanaweza tatuliwa. Kutokana na uwezo wao wa kujizuia, vipaji hivi katika jamii hupotezwa, na mifumo ya elimu hukinzana na uwezo wao wa kujiuliza maswali, kwa kuwalazimisha kukariri hata wanayoyaona sio majibu. Kumbuka mfumo wa elimu huaribu kipawa hiki kwa kutowapa watoto uwezo wa kujiuliza maswali, watoto wanaanza kuambiwa chakufanya na kufikiri tangia wanaanza awali kabisa. Watoto wanakaririshwa vitu wasivyovijua, hawawezi tena kuuliza maswali, maana huwezi kuuliza jambo usilolojua. Vuta taswira, watoto wanafundishwa maelfu ya mitambo katika masomo ya sayansi, ambayo hawajawi iona, je, watauliza nini kwa elimu hii ya kusadikika? Je hiki ni kipaji chako? Unaweza kujua kipaji chako kwa kujiangalia namna unasukumwa sana kujua majibu ya maswali yako, kuliko unavyopata wepesi wa kuishi na maswali usiyo na majibu nayo. Kama hiki ni kipaji chako, chukua hatua hapo ulipo, jifunze kwa kina kazi zako, kuwa bora kwa kuelewa zaidi ya wenzako, hapo ndipo ilipo thamani yako.

Kipaji Cha Uumbaji "Pattern Talents"

Hili ni aina ya vipaji vyote ambavyo vinahusisha watu walio na uwezo mkubwa sana wa kutengeneza taswira katika Vichwa vyao. Tofauti na vipaji vya namna iliyopita, Hawa Kwao huwa na uwezo wa Ubongo katika namna ya ajabu sana pia. Hawa wao wanaweza kuvuta taswira, Wana uwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu, ni watu ambao Wana uwezo wa Kufikirika jambo likawa kama lipo mbele ya macho yao. Watu Hawa ni ma ''designer" wakubwa sana, Hawa watu ni Wataalamu wabobezi katika gani zao kiutendaji. Kuelewa vipaji vya namna hii kirahisi, vuta Picha wanasayansi wanaotengeneza programs za Computer, Wataalamu kama wa mifumo ya Roboti "Artificial intelligence", watu Hawa pia wamejawa katika taasisi za Sayansi kama wabobezi wa fani zao Kwa kina sana. Watu Hawa wanaweza Kufikirika Kwa kina na kuja na vitu vya ajabu sana. Maranyingi kundi hili huwa na watu wenye mafanikio makubwa sana, wafanyabiashara wakubwa wengi huwa ni watu wenye vipaji vya aina hii. Wana uwezo wa Kufikiria ndani na nje katika Kila kitu kuhusiana na biashara zao tu, wao hufanya au hujua Kila kitu ili mradi TU waweze kufanikisha taswira zao walizozitengeneza kichwani mwao. Wanasiasa wengi huwa tayari hata kufanya mambo haramu ili kufanikisha taswira walizozitengeneza vichwani mwao.

Vipaji hivi huwa ndani ya baadhi ya watu tangia wanapozaliwa. Ubongo wa watu Hawa huwa na uwezo wa kutengeneza kumbukumbu hata katika namna ya Picha, huwa hawasahau kirahisi watu Hawa. Watu Hawa Ubongo wao pia una uhusiano mkubwa sana na viungo vyao, hasa mikono mpaka vidole. Utakuta baadhi yao wakiwa na uwezo wa kuchora vitu wanavyoviona, au vifikiria Kwa usahihi sana. Wana uwezo mkubwa baadhi katika kutazama ncha za vitu "angles", mifanano "symmetry", ukubwa "size", watu Hawa wanaweza kujua kitu kinavyoweza kuonekana kizuri, au Cha kusisimua. Ni kama vile Ubongo wao wa nyuma "occipital lobe" unaohusiana na taswira na rangi umeendelea kuzidi wastani wa watu wengine. Nimewahi kutana na watu kadhaa katika vipaji vya kundi hili, Kwa kweli watu Hawa unapowaelezea kitu, hukumbuka karibia Kila kitu hata mwonekano wa sura yako ulipokuwa ukiwaelezea.

Kundi hili la vipaji binafsi nalifananisha na rangi nyeupe, yaani, Lina ng'aa. Watu Hawa wanamulika Nuru ya Maarifa yao toka ndani ya Ubongo wao kuelekea Kwa ulimwengu. Hawa ndiyo wagunduzi wakubwa katika Kila taaluma walizopo. Hawa ni kinyume na kundi la vipaji lililopita, ambalo Mimi nawafananisha na rangi nyeusi, yaani wao wanafyonza kila Maarifa yaliyopo katika ulimwengu wao. Kundi hili Jeupe la vipaji, nalo linapotezwa Kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni Kwa kuwa, watoto tangia wanapokuwa wadogo, hawaachwi kuwa huru kufata Njia wanazozipenda, ubunifu hupotea panapokosekana mapenzi. Kumbukumbu ni kitendo kinachohitaji sana nishati na afya ya Ubongo, Lishe mbovu, kutokupata nyakati za kutosha za kulala, kukosa walimu walio bora kabisa, yote haya yanaua uwezo wa Ubongo wa kutunza kumbukumbu, na kutunza kumbukumbu zilizo na manufaa Kwa vipaji vyao. Watu wachache waliofanikiwa sana, ambao wengi wao wametoka katika kundi hili, huathiri wenzao wa aina yao ilikuwazuia wasijewaletea ushindani Kwa siku zao za Usoni.

Je wewe upo kundi hili? Unaweza kujitambua kama una kipaji katika kundi hili Kwa kuangalia uwezo wako mfano, namna huwa unavuta sana taswira ya mambo, na kulazimisha kuyafikia, na huwa unafanikiwa ukifanya hivyo. Unaweza angalia kama una uwezo wa kubuni jambo lolote Lile unapotaka kufanikisha jambo Fulani, na huwa unahisi kabisa kuwa unaweza fanikisha. Umeshawahi kuwa Bora sana katika jambo Fulani; yaani, taaluma au kazi yoyote ile, mfano, ushawahi kufaulu sana masomo fulani, na hata kuwa Bora sana Kwa kuweza kukumbuka sana somo Hilo. Je ushawahi kufanya biashara na ukaweza kuwa na nidhamu kubwa sana ya pesa zako ili ufanikishe malengo yako. Kama wewe ni mwanasayansi je ushawahi kugundua kuwa unavutiwa zaidi na kufanikiwa Kwa utendaji na ufanisi wa taaluma yako, kuliko hata kuelewa sana sababu za Ndani sana za unachofanya, je unapoangalia Picha huwa unachagua sana uzuri wa mwonekano wake Kwa kuzingatia vitu vingi sana, kiasi Picha zako huwa zinapendwa na watu wengi sana, je huwa unajali sana mwonekano wako na unapenda kupendezesha? Maswali ya muundo huu yanaweza kukusaidia asili ya kipaji uliocho nacho.

Vipaji Vya Lugha " Music, Linguistics, and Emotions Talents"

Lugha ni miongoni mwa maajabu makubwa ya Binadamu. Ni Binadamu tu ambaye anatumia lugha katika kuwasiliana. Ijapokuwa wapo wanyama baadhi ambao Hutumia namna kadhaa za sauti kuwasiliana, kama ilivyo kwa ndege, Nyani, n.k. lakini hakuna ubishi kuwa ni Binadamu tu ambaye ameendelea zaidi sehemu zinazohusiana na lugha katika Ubongo. Sehemu kama za Broca's area na Wernicke's area. Sehemu hizi katika Ubongo wa pembeni 'temporal lobe", zinawasiliana na Kila sehemu ya Ubongo. Mtu kabla ya kuzungumza huwa hiyo taarifa imeshasambazwa katika Kila sehemu ya Ubongo. Ng'ombe hulia toka anapozaliwa, na huendelea kulia Kwa sauti za mtindo huohuo mpaka anapokufa. Kwanini Hana sauti za namna tofauti tofauti, ni kwasababu lugha siku zote Sio sauti tu, lugha ni taarifa zinazosemwa. Unapokuwa vizuri katika Ubongo, unakuwa Bora katika mawasiliano, watoto ambao huwa na shida katika Ubongo wa mbele, wanaoshindwa kujifunza na kutembea vizuri mfano "Usonji", huwa wanashida pia ya Kuzungumza. Watoto wakike huwahi kuzungumza Kwa kuwa hata Ubongo wao huwahi kukua. Kipimo Cha uzungumzaji ni kipimo Cha uwezo wa Ubongo.

Watu wenye vipaji vya lugha huweza kuchambua lugha Kwa Ufasaha mkubwa sana. Watu Hawa wanaweza kuhamasisha, wanaweza kuelezea, wanaweza kufariji, wanaweza kuvunja moyo, wanaweza kuigiza, wanaweza kuimba, wanaweza kutunga tunzi, wanaweza kusimulia, wanaweza kusimulia, wanaweza kutungaza, wanaweza kuhuzunisha na kufurahisha, watu Hawa ndiyo kiini Cha Jumuiya yoyote ile ya watu. Watu Hawa wanavipaji vya upatanishaji, watu Hawa Wana uwezo wa kumuinua mtu yeyote yule Kwa maneno yao, wanaweza pia kumshinda yeyote yule Kwa maneno yao.

Uwezo mkubwa wa watu Hawa inatokana na Ubongo wao. Watu Hawa Wana uwezo wa Kufikiria Kwa haraka sana. Ndani ya muda mfupi sana watu Hawa huzizungusha taarifa wanazozipata katika kila sehemu ya Ubongo wao, na huwa Wana uwezo wa kuifanya ieleweke, au hata kujua namna Bora zaidi ya kuikabili. Wao wanaweza kukosa jibu la tatizo, lakini wanaweza kujua jambo lipi ni sahihi zaidi Kwa Wakati huo. Watu Hawa wanavyofikiria, wanafikiria katika namna ya mawimbi yenye vituo. Wapo Wasanii wengi sana katika kundi hili, watu Hawa maneno yao Sio mawimbi TU ya sauti kama watu wengine. Watu Hawa maneno yao ni mawimbi ya sauti zilizo katika mapigo ya kihisia. Wao wanapozungumza, huzungumza hisia. Mfumo wa Ubongo wa "MNS" unaohusiana na kujifungamanisha na unayoyaona, umeendelea sana Kwa watu Hawa. Watu Hawa wanapoangalia jambo lolote Lile, huwa wanalihisi kama ni lao. Na Kwa kufanya hivyo, wanapolizungumzia jambo Hilo, hulizungumza kana kama wao ndiyo wahusika wakuu. Watu hupendwa sana na jamii, hii ni Kwa kuwa huwa ni marafiki Wazuri sana.

Watu Hawa Wana upekee mkubwa sana wa utunzi, Hawa ni wabunifu kama kundi lililopita, lakini tofauti yao kubwa na wenzao ni kuwa, watu Hawa utunzi wao hautoki nje, watu Hawa utunzi wao hutoka ndani. Waliopita tuliona walikuwa wakitunga sana wanapokuwa katika mazingira yanayoshindana na malengo yao. Watu Hawa hutunga sana pale wanapopatwa na hisia za kina za Ndani, za kuguswa na jamii zao, za maisha wanayopotia, ni kama mfumo uleule wa "DMN", Hawa watu huonekana Kwa nje kama ni watu wa watu sana, lakini kiuhalisia watu Hawa huwa ni wapweke sana. Watu Hawa huwa Wana muda mrefu sana wa kujichunguza zaidi wenyewe, huwa Aidha wakifurahi, au wakihuzunika, lakini matokeo ya Hisia hizi, huonekana wanapoanza kuandaa kazi zao. Mfano mzuri ni waimbaji, Hawa watu hutunga mashairi kama namna ya kujifariji katika nyakati zao ngumu. Nyimbo zao hupendwa sana na watu wengine Kwa kuwa huwa na hisia Kali sana. Sayansi ya utunzi wa Muziki huwa ngumu sana "complex" sana, Muziki ni uwezo wa asili wa Binadamu wa kujifariji toka stress za maisha. Muziki ni dawa pekee inayopita Moja Kwa Moja kuingia katika Ubongo. Watu Hawa ni madaktari wa asili, na kama ambavyo huwezi shindana na kazi za Daktari, ndivyo huwezi pingana na msukumo wa kazi za watu Hawa.

Kundi hili linahusisha viongozi wakubwa sana katika jamii, Walimu Bora kabisa na Wanafalsafa kuanzia Plato, viongozi wakubwa sana katika taasisi za Imani na Dini, viongozi wakubwa sana katika Aidha Mapinduzi, au propaganda Fulani. Linahusisha waandishi wakubwa sana na waandishi mashuhuri kama Machiavelli mpaka Robert Greene, Wanasiasa wenye mvuto mkubwa sana Duniani wote huwa katika kundi hili, Wasanii wakubwa katika tasnia za miziki, filamu, maigizo ya namna yeyote Ile, kundi hili Lina watu ambao huwa Maarufu sana na wenye mafanikio. Wapo wanasayansi wengi sana katika kundi hili, wanasayansi katika Kila taaluma wanapokuwa na vipaji hivi, huwa Maarufu sana kama alivyo Richard Dawkins, au Prof John Lennox, au Mwanafizikia Richard Feynman, watu Hawa huburudisha sana Kwa uchangamfu wao, huwa walimu Wazuri sana. Kundi hili linavurugwa sana pia kutokana na mfumo wa Elimu na maisha uliopo. Watoto wengi hufundishwa kuwa namna zote za utunzi wa lugha ni sanaa zisizo za watu wenye akili, watu wengi wenye mivuto ya tasnia hizi huzitumia vibaya sana, kama vile kulaghai jamii, kufisadi, kudanganya, watu wengi mashuhuri walio katika kundi hili kutokana na mifumo ya maisha ya Kisasa, huathiriwa sana kiakili. Wengi huwa wagonjwa wakubwa sana wa kiakili, mfano mzuri ni namna Wasanii wengi walivyo wagonjwa wakubwa sana wa kiakili, na hata wanasiasa wengi ambao wameishia tu kuwa waropokaji mafisadi wasio na hisia za Upendo kama walivyoanza awali. Watoto wengi hukatia Tamaa vipawa hivi, lakini ukweli ni kuwa vipawa hivi ni vipana zaidi ya namna jamii inavitambua.

Je wewe una Vipaji hivi? Unaweza kujichunguza Kwa kujigundua, je huwa una utunzi na usanii mkubwa sana unapokuwa umeboreka, au umefurahi, je hisia kwako huchochea ubunifu, je huwa unafikiria sana kabla ya kuzungumza, je unaweza kutunga kisa kuhusiana na Hali Fulani hata watu wakasisimka kana kama ni kweli, je unapodanganya huwa ni ngumu sana kugundulika, je huwa unapokuwa mpweke huwa unahisi sana melody za Muziki, maswali ya muundo huu yanaweza kukusaidia kujijua na kuanza kuchukua hatua. Tambua kuwa kama utatumia kipaji chako Kwa kuwa mzungumzaji au mtunzi mzuri sana, utapata mafanikio makubwa sana Kwa kuwa huko ndikp uliko uwezo wako.

Vipaji vya Usanii wa Misuli " Kinetic Talents"

Hivi ni vipaji vyote vinavyohusisha watu wenye uhusiano mkubwa sana kati ya Ubongo, na misuli. Watu Hawa Wana mifumo imara sana ya nishati ya Ubongo na misuli. Kazi kubwa iliyofanywa na Doug Wallace, ambaye ni Mtafiti wa Kimataifa wa chembechembe za seli, za nishati zinazoitwa "Mitochondria", inaonyesha kuwa, watu wote tumetofautiana uwezo wa kuzalisha Nishati Kwa ufanisi kabisa katika seli zetu. Wapo watu ambao Wana ufanisi mkubwa sana katika uwezo wa kuzalisha Nishati, watu Hawa ni mithili ya supermen katika mantiki ya uwezo wao wa kufanya kazi. Watu Hawa Bora ni watu walio katika kundi hili la vipaji.

Watu Hawa binafsi napenda kuwafananisha na watu ambao sehemu yao ya nje ya Ubongo Ipo Bora zaidi ya watu wengine. Sehemu ya Ubongo ya nje "Cerebral cortex" kuanzia sehemu za nyuma zinazohusiana na kuona, mpaka sehemu za mbele zinazohusiana na misuli na maamuzi, huwa zimeendelea sana. Ubongo wa watu Hawa sehemu ya nje "gray matter" imeendelea sana kutokana na ubora mkubwa wa Misuli ya watu Hawa. Watu Hawa miili yao yote huwa ni mithili ya Ndege, Wana uwezo mkubwa wa kuchakata Oksijeni, Wana uwezo mkubwa wa kui control misuli na mwili wao wote, Wana uwezo mkubwa wa kutoa taka Sumu za mwili, Wana Mapafu imara sana, watu Hawa hakika ni wepesi sana. Sio watu wanaochoka kirahisi, watu Hawa Kwa wastani huwa wanaishi Kwa wastani wa miaka mingi zaidi duniani.

Wapo watu wengi sana wenye vipawa hivi, upekee katika uhusiano wa Ubongo na misuli yao hutofautiana sana. Wapo ambao Wana uwezo mkubwa wa uhusiano wa Ubongo na mikono, wengine miguu, wengine viungo vyote, wengine mdomo, wengine Nyonga, n.k. watu Hawa ni wapambanaji wakubwa kabisa katika historia za Dunia, tangia Samsoni na Daudi wa Biblia, mpaka Alexander the great na Julius Caesar wa Historia. Watu Hawa wameshamiri kwenye Kila michezo ya Dunia, wapo wachezaji wakubwa sana, Tena Mashuhuri kama Lionel Messi wa Mpira wa Miguu. Watu Hawa huwa mahiri sana katika kutazama, kuhisi, kufikiri, na Kisha kutenda. Dunia imeshamiri watu Hawa katika Kila tasnia, kuanzia katika Miziki, wapo wapigaji Wazuri sana wa vifaa vya Muziki, wapo waimbaji Wazuri sana, wapo mainjinia wakubwa sana wanaopendwa kutokana na uwezo wao mkubwa wa kufanya kazi, watu Hawa huwezi shindana nao katika utendaji, watu Hawa wameshamiri katika kazi za kila namna na michezo.

Kundi hili nalo linapotezwa sana katika jamii, hii ni kutokana na Falsafa za jamii za kuwa, namna Pekee watu Hawa wanaweza kuwa Bora ni kupitia mashindano. Michezo mingi sana kama ya ngumi, mipira, kukimbia, n.k. huwa Haina Falsafa nzuri katika jamii. Ushindani hulenga kumchukua mmoja kati ya wengi wanaoachwa. Jamii huwapoteza wengi sana Kwa kuwachukua wachache sana. Toka enzi za Olympic za Spartans, mpaka Umiseta katika taasisi za Elimu, jamii bado haijatambua namna ya kuwatumia vijana wenye vipawa hivi. Kama jamii isingekuwa na dhiki na mashindano, je vijana Hawa wangefanya Nini? Jibu ndilo litatoa sehemu sahihi za vijana Hawa. Watu Hawa wanapaswa kufundishwa kufanya kazi zao Kwa manufaa yao wenyewe. Kijana huyu anapaswa kuoneshwa sehemu ya kutumia misuli yake Kwa ajili yake mwenyewe, mfano, shamba lake, ufundi wake, kuwahi kazini kwake, kutokuwa dhaifu Kwa kuonewa, Hawa ni watu ambao asili imewachagua kuwa watawala Kwa kuwa na uwezo wa kuzalisha ziada. Lakini makundi yote manne huwatumia watu hawa Kwa manufaa yao wenyewe. Watu Hawa maisha yao yote huyamaliza katika kufanya kazi za watu, kupambana na kuumia ili kuwafurahisha wengine, watu Hawa hata historia zao huwa zinapotezwa. Sote tunatambua historia ikisifia wafalme, lakini hakuna mwanajeshi aliyewahi sifiwa Kwa kufa na maadui wengi zaidi. Jamii inapaswa kubadilisha Falsafa juu ya vipawa hivi, badala ya kutumia muda mwingi katika mazoezi ili kushindana, ili hali mwisho wa mashindano asilimia 99% wote watafeli, basi ni bora asilimia hizi 99 wakaamua kufanya jambo Kwa ajili ya wao wenyewe. Hebu vuta taswira, Kuna wachezaji wangapi wa Mpira katika Nchi kama ya Tanzania yenye wananchi zaidi ya milioni 60, je ni wangapi wanaopatwa nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa? Nyakati Fulani iliumiza sana Bondia mmoja wa masumbwi alipofariki na kuonekana kuwa alikuwa akipambana, ili alipwe shilingi za ki Tanzania 40,000/=Tsh. Huu ni ubadhirifu mkubwa sana wa vipawa vya watu hawa.

Je una kipaji katika kundi hili? Mwonekano Kano wako, ufanisi wako, akili yako, vyote vinaweza kukueleza wewe ni Nani, kamwe usikubali kutokutumia Ubongo wako Kwa ajili yako mwenyewe, kamwe usikubali kupoteza Nguvu na utawala wako uliokuwa nao tangia ulipokuwa shule za awali, kundi hili ni la watawala na viongozi wa asili, lakini Ujinga wa wengi wa kundi hili wa kukimbilia kupata pesa kirahisi, ndizo huwafanya wengi wao kuishia kuwa watumishi mpaka nyakati za mwisho za Uhai wao. Hakutakuwa na michezo kama Ngumi Mbinguni? Hata mipira, hii yote ni kukuonyesha kwanini ni Watumwa tu "Gladiators" waliokuwa wakipigana katika kumbi au "Arena" enzi za falme za Roma. Ishi kama mfalme, haujawa na misuli mikubwa ili ulinde wenye misuli midogo, umekuwa na misuli mikubwa ili uwasaidie wenye misuli midogo Kwa kufanya zaidi yao na kuwaongoza.

Kipaji Cha Hisabati Na Lojiki Mathematical and Logical Talents

Hili ni kundi la vipaji vyote vinavyohusiana na watu wenye uwezo wa Kufikiria katika muundo wa namba, takwimu, na wastani wa vitu. Watu Hawa wanafikiria Kwa kuchakata vitu kama vinavyoonekana katika muda na mahali "space and time". Hawa kitaalamu ni watu wa ajabu sana, wao wanaweza kuangalia vitu vidogo sana ambavyo watu wengine hawawezi vizingatia. Watu Hawa wanapoliangalia jambo, wanaliangalia namna lilivyokuwepo, lilivyo Sasa, na litakavyokuwa, watu Hawa wanaona namna vitu vinabadilika marazote. Watu Hawa Wana angalia namna mazingira ya vitu hubadilika marazote. Uwezo huu huwafanya kuweza kuwa watabiri wakubwa sana wa hatma za vitu Kwa Ufasaha kabisa.

Ubongo wa watu Hawa una uwezo mkubwa sana wa kumbukumbu, na hasa kumbukumbu zilizo katika namna ya namba. Watu Hawa wanaweza kariri idadi ya vitu, urefu wa vitu, ukubwa wa vitu, mabadiliko ya vitu, watu Hawa ni Wataalamu au "masters" katika kujua ufaulu, kufeli, au mabadiliko yoyote Yale ya vitu. Mtu mwenye kipaji hili, unapomwelezea jambo lolote Lile, huwa ana uwezo wa kukuuliza maswali kadhaa tu, lakini katika maswali hayo, utakapomjibu, tayari atakuwa ameshajua Kila kitu, na hutaweza kumdanganya kamwe. Watu Hawa wanajua namna Bora kabisa za kutengeneza faida, wanatambua namna mbalimbali hasara huwa zinatengenezwa, watu Hawa hata katika taasisi za Sayansi, huwa ni mainjinia wakubwa sana kama ilivyokuwa Kwa John Von Neumann, lakini pia hata katika historia za kivita, majemedari wakubwa kama alivyokuwa Napoleon Bonaparte wa Ufaransa, watu hawa huwezi washinda katika michezo kama ya Draft, au Karata, au hata Kamali, watu hawa huwa Wana mbinu ambazo watu wengine huchelewa sana kuja kuzigundua.

Ubongo wa watu Hawa unafanana sana na watu wa kundi la kwanza, la wenye uwezo mkubwa sana wa kuelewa, tofauti Pekee iliyopo, ni kuwa watu hawa hujua lakini huwa hawajali sana sababu, wao hulenga zaidi kujua hatma. John von Neumann aliwahi kusema, "kijana mdogo katika Hisabati hakuna kuelewa, huwa tunafanya tu" , hivyo ndivyo ilivyo, watu Hawa ni Wataalamu wakubwa wa Mahesabu katika Mabenki, wengi wao kutokana na uwezo wa mkubwa wa kuelewa mabadiliko madogo madogo, wengi wao huwa wezi stadi sana, watu Hawa Wana akili kubwa zaidi za kutengeneza faida, utawagundua Kwa namna wapo fasta sana kugawanya na kuzidisha namba, hata zilizo ngumu Kwa wastani wa wengine.

Vipaji hivi kama wenzao wa kundi la kwanza, hupotezwa sana pia. Hii ni Kwa kuwa, kundi hili huitaji Wakufunzi Wazuri sana wa kuwachochea katika hatua zao za awali. Mfumo wa Elimu Hutumia walimu ambao Kwa wastani huwa Sio waliokuwa Bora zaidi katika taaluma hizi. Wengi huchukuliwa waliokuwa dhaifu kuweza kukidhi kuendelea zaidi na taaluma zingine, hii hupelekea walimu wasioweza kutengeneza Wanafunzi wataokidhi katika taaluma hizi. Lakini pia Kwa uzoefu binafsi Kwa Nchi kama ya Tanzania, vijana wengi sana wa sifa hizi, huchanganywa na Kila kijana anaweza kufaulu Hisabati na Fizikia, jambo ambalo halina sana ukweli, Kwa kuwa mfumo wa Elimu uliopo umejikita sana katika kukariri bila hata kuelewa, jambo ambalo halihusiani sana na uwezo wa asili wa vijana Hawa, ambao kwao "logic", ndiyo msingi. Kumbuka, kumbukumbu za kundi hili, Sio kama kumbukumbu za kundi la pili, Hawa hukumbuka namba na Mahesabu yao ambayo huwa ni kanuni, kundi la pili hukumbuka lakini hasa Picha zilizo katika namna ya taswira.

Je wewe upo kundi hili? Unaweza kugundua hili Kwa namna huwa upo fasta sana katika kudadavua Mahesabu, je huwa unapenda Kufikiria katika namna ya namba, je huwa unaweza kujua mtu atakaye fanikiwa au feli Kwa kuangalia tu mwenendo wake, je ulishawahi kuwa Bora sana katika masomo ya namba kama Fizikia, au Hisabati, au kemia na jiografia, je huwa haupendi kupoteza muda katika kutatua mambo ambayo yanaonekana kabisa yapo wazi, je upo fasta sana katika Kufikiria, je unaziona Njia nyingi sana za kutatua mambo, hata Njia ambazo wengine hawazioni, je wewe ni mgumu sana Kuamini kuwa unaweza shindwa kugundua mbinu ya kutokea, je upo vizuri sana katika kupiga Mahesabu ya namna nyepesi zaidi ya kufanikiwa, Wewe ni mwanamahesabu kama Sir. Isaac Newton, unapokosa Njia, unatengeneza mbinu yako ya kutokea, pambania uwezo wako, jifunze zaidi, hapo ndipo ulipo ubora wako.


NDOTO

Ndoto ni miongoni mwa vitu vya ajabu sana katika ubongo, tangu awali kabla ya maendeleo makubwa ya sayansi, mpaka leo tulipokuwa katika hatua za juu sana za sayansi. Elimu ya ndoto ‘’oneirology’’ imejawa sana na nadharia, kuliko hata taarifa za kuhakikiwa moja kwa moja, makisio yamejaa zaidi katika elimu ya ndoto. Tangia zamani sana katika historia kumekuwa na mabishano kati ya makundi mawili, ambapo moja limekuwa likiamini kuwa ndoto zina maana, na lingine likiamini kuwa ndoto hazina maana. Katika sayansi za ubongo kuna mitazamo mikubwa mitatu, ambayo unaweza ipata kupitia ripoti ya shirika kuu la Taarifa za Sayansi za Teknolojia za uhai ‘’NCBI’’, la terehe 1 mwezi wa pili mwaka 2011, lililokuwa na kichwa kinachosema, ‘’Ndoto na Ubongo : Kutoka uzoefu na imani za watu kuhusiana na ndoto ‘’phenomenology’’, mpaka sayansi ya ndani ya utendaji wa seli za ubongo ‘’neurophysiology’’. Ripoti hii imeeleza kwa kina sana undani wa ndoto kisayansi. Ufuatao ni ufupisho wa ripoti hii.

SAYANSI YA NDOTO TOKA RIPOTI YA NCBI

Ndoto ni majaribio ya ajabu kabisa ambayo hufanyika katika saikolojia, na sayansi ya ubongo wa mtu, kila usiku anapolala. Ndoto huonesha ....

To be continued..