Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SIKU YA 04 YA UUMBAJI KISAYANSI

Siku ya 4 ya Uumbaji kisayansi

SIKU YA NNE 04

14. Mungu Akasema, Na Iwe Mianga Katika Anga La Mbingu Ili Itenge Kati Ya Mchana Na Usiku; Nayo Ndiyo Dalili Na Majira Na Siku Na Miaka; Mwanzo 1:14 

Unaweza gundua sasa neno lililotumika linasema ‘’Raqia of the heavens’’ au Anga la mbingu. Kitu cha kwanza cha kuzingatia ni hiki, hautambuliki ni ukubwa gani ulikuwa huu ulimwengu, ila inafahamika kuwa, ulikuwa mdogo sana. kama niliposema awali kuwa, vitu vilikuwa vipo vingi sana. vilikuwa katika eneo dogo ‘’Compact’’. Na nikaeleza kuwa, hali hiyo ilipelekea uwepo wa Quasars kubwa kabisa mfano kuna Quasar moja ina uzito wa Mara Bilioni mbili ya uzito wa Jua letu. Na hata wanasayansi wasio amini Mungu hupata wakati mgumu sana kwa uwepo wa Quasars. hii ni kwa kuwa inapingana na nadharia ya kwao, ya kuwa dunia ilikuwa ya joto sana awali. huu ulimwengu mdogo wa awali ulikuwa na Hayo matundu makubwa meusi ‘’Black Holes. ambayo ni mazito sana’’. Haya nilisema awali ni matokeo ya Gravitation kubwa sana iliyokuwepo. Na haya kwa pamoja yana uzito mkubwa sana ajabu kuuelezea, hii ndiyo sababu ya kuelezea kuwa, ulimwengu ulikuwa mzito sana ‘’very denser universe’’.

picha za ulimwengu zikionesha blackholes, picha ya pili ni blackhole inayoonekana kukaribiana sana na mfumo wetu wa jua.

Mungu Anatanua Ulimwengu ‘’Universe Expansion’’

Mungu anatanua ulimwengu. kwa kweli ni ngumu kuelezea alichokifanya. ila matokeo yake ulimwengu ukawa ni mithili ya maji yanayotiririka toka mlimani. Yaani ni kama vile Gravitation ikawa imetwistiwa ‘’Reciplocated’’. Hivyo vuta picha ulimwengu unasambaa kama maji yanavomiminika pande zote tokea juu ya mlima.

Hayo mamviringo ndizo galaxy zilizo jaa Nyota,sayari, na mawingu ya mavumbi na gesi ‘’mfano nebula’’ sisi galaxy yetu inaitwa ‘’milky way’’.

Kumbuka ulimwengu haukuwa na uzito sawa, au ‘’uniform densities’’. kwa hiyo hata matokeo ya madhara ya Black Holes katika kufyonza vitu au matter hayakufanana. Kutanuka huku kwa ulimwengu kulipelekea vitu au matter zilizokuwa zipo katika mvuto mkubwa wa Gravitation kuondoka kwa spidi kubwa sana. Pia Makundi ya Nyota ‘’Galaxies’’, ambazo huwa katikati na Black Holes kubwa yakawa yakisambaa katika ulimwengu.

Kwanini Galaxy Zimetwist Mikia Kwa Nje, Na Kwa Kati Zimejaa ‘’Concentrate’

Vuta taswira hii, Galaxy zimejawa na uwingi wa matter ‘’nyota, sayari n.k’’, sasa basi, matter zote zilizopo nje zinapitia mvuto mdogo wa Gravitation ukilinganisha na matter zilizopo ndani ya Galaxy. Katikati ya Galaxy huwa kuna Black Holes kubwa, ambazo hupelekea kuvutwa kwa matter Zaidi. ambazo hizo hupelekea sehemu ya kati kuwa imejawa Zaidi na uwingi wa vitu. Kwa hiyo, kukunjika kwa mikono yake kuna maanisha hapo awali ilikuwa imetanuka, na sasa muda unapozidi Kwenda kani ya gravitation inaendelea kuzivuta zirejee ndani. na hiyo ndiyo sababu ya kuendelea kukunja mikono yake. Mungu aliutanua Ulimwengu.

Hii ni picha ya galaxy yetu ‘’milky way’’ yenye nyota kama jua Bilioni 400, ili uimalize utembee na gari inayoenda na spidi ya mwanga kwa miaka 52,850. Mfumo wetu wajua hauwezi onekana hapo maana ni kama kavumbi. Halafu hii ni galaxy moja tu. zipo kama Trilioni mbili za mtindo huu. 

Zaburi 8:4 ‘’mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?’’. Daudi alishindwa kumwelewa Mungu. Hata mimi sielewi wala wanafizikia wengi hawajui tuna uspesho gani binadamu?

Kwanini Galaxy Zinaonekana Zipo Umbali Wa Mabilioni Ya Mwanga Mbali Na Dunia, Na Dunia Ili Hali Ina Miaka Elfu Sita 6000 Tu?

Ni kweli Galaxy ziko mbali sana na Dunia. hii inatokana na kuwa, ziliachiliwa zikiwa na kasi sana kiasi kwamba ndani ya muda wa masaa kadhaa tu, zikawa zikiwa katika umbali wa mabilioni ya mwanga. Kwa sasa msomaji utakuwa umekwisha kuelewa kuwa, kadri zinavyoenda mbali na center ya ulimwengu. ambayo ilikuwa na gravitation kubwa, basi na spidi ya muda pia inaongezeka kuzifanya zionekane kuwa za muda mrefu Zaidi. 

Hebu tafakari adamu angeziangalia Galaxy hizi katika siku ya sita, Je angejua ni za miaka mabilioni iliyopita au za Juzi yake?

Mungu Aliongeza Spidi Ya Mwanga Wa Jua

Mungu aliongeza spidi ya mwanga wa jua katika siku ya nne katika utanukaji wa Galaxy, hii ni kwa lengo lifuatalo. Ili mwanga uwahi kurudi duniani, na kurejea katika spidi yake ya awali. Hii ililenga ili taarifa atakazopata mtu juu ya uumbaji zisimchanganye. Maana kama spidi ingebakia ile ile, basi unaweza kuta taarifa ya uumbaji wa galaxy Fulani, ndiyo inafika leo duniani. na uumbaji ulishafanyika miaka elfu sita huko nyuma. Rejea graph ifuatayo

Graph hii inaonyesha maelezo yaleyale ya kuwa, spidi ya mwanga ilishushwa kuelekea siku ya tano. Ili kutengeneza uhalisia wa siku ya tukio la uundwaji wa nyota, au galaxies katika siku ya nne kwa mtu atakaye kuja kulitazama katika siku ya tano.

Ushahidi Kupitia Picha Za Telescope, Galaxy Kuonekana Zikifanana Saizi Ya Mikia

Galaxy nyingi kama mfano wa hizo katika picha juu zinaonyesha mfanano sana, hata ukiangalia mikia au mikono yake ilivyo jikunjua’’twist’’, ijapokuwa ni Galaxy ambazo zimetofautiana umri wa kukomaa. kwanini hii inatokea?

Ili hii hali ya kufanana kukunja mikono yao itokee, hizi Galaxy ili hali zina umbali tofauti, basi ile Galaxy ya mbali Zaidi ilipaswa iwahi kutoa mwanga, au taarifa zake, kabla ya wenzake. Hii ni kama vile ukiwa mbali sana na wenzako wapo karibu, ili mfike kwa wakati sawa, basi wewe utapaswa uanze safari yako mapema kabla ya wenzako, au utembee kwa spidi kubwa zaidi ya wenzako. Na sasa basi kama galaxies za mbali zilianza kutoa mianga kabla ya nyenzake, Itapaswa mwanga wake uionyeshe ikiwa bado haijajikunja sana. 

Maana imeanza kabla ya wenzake. na hivyo ndivyo tulipaswa tuone kwa hizo picha. Kuwa Galaxy za mbali zionekane zikiwa zimejikunja kidogo ukilinganisha na za karibu. Lakini maajabu ni kuwa, Galaxy hizi zinaonekana sawa!! hii haina majibu Zaidi ya kusema kwamba, Spidi ya mwanga iliongezeka kwa makadiro ya mamilioni Zaidi ya kawaida, na hivyo basi kufanya zile taarifa za awali za Galaxy ya mbali, na hata Galaxy za karibu, kufika kwa wakati bila kuathiriwa. Hii ni kama kusema hakukuwa na madhara ya umbali kwa picha za galaxy, kutokana na spidi kubwa sana ya mwanga. Rejea kielelezo kile cha awali, kama kikao ni saa saba mchana, na mmoja yupo Mwanza, mwingine Mbeya, mwingine Morogoro, na kitafanyikia Dar es salaam. Kama taarifa inapaswa kutolewa saa sita za mchana tu kwa wote, na wote mtafika sawa kabisa, basi ni kwa sababu tu Wote mtakuwa mnatumia usafiri wa Jeti ‘’au ndege za spidi kubwa sana’’. Ndivyo ilivyo hapa, spidi kubwa ya mwanga iliweza ku ‘’compensate’’ gepu la taarifa kwa umbali wowote ule wa galaxies za mbali. 

Ushahidi Wa Biblia Wa Kutanuka Kwa Ulimwengu

Kama kuna tukio lenye kuelezewa kwa mafungu mengi. basi ni kutanuka kwa ulimwengu. Biblia imetumia sana neno ‘’Sambaza’’ au ‘’Stretching’’ mfano, angalia mafungu yafuatayo.

Ayubu 9:8 ‘’Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu ‘’-Spreadeth out the heavens

Zaburi 104:2’’Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia’’-Stretches out the heavens.

 Isaya 40:22 ‘’…ndiye azitandazaye mbingu kama pazia’’ -stretcheth out the heavens

Isaya 44:24 ‘’; nitandazaye mbingu peke yangu;’’-stretcheth forth the heavens alone’’

Isaya 45:12 ‘’. mikono yangu mimi, imezitandaza mbingu,’’-stretched out the heavens

Isaya 48:13 ‘’mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitandaza mbingu;’’-hath spanned the heavens

Isaya 51:13 ‘’. yeye azitandazaye mbingu, na kuweka misingi ya dunia;’’-stretched forth the heavens

Yeremia 10:12’’, Na kwa ufahamu wake amezitandaza mbingu.’’-stretched out the heavens

Yeremia 51:15’’, Na kwa ufahamu wake amezitandaza mbingu.’’-stretched out the heavens

Zekaria 12:1’’. azitandazaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia,’’-stretched forth the heavens

 Hii ni sample ya mafungu ambayo Mungu anaonesha ni ufahamu wake mkubwa tu uliotumika katika kuutanua ulimwengu, na ndiyo maana hata leo katika fizikia miongoni mwa vitu ambavyo vimefanya tuonekane hatujui kabisa, ni suala la kutanuka kwa ulimwengu. 

Asili Ya Dark Thoughts ‘’Dark Matter Na Dark Energy’’

Hakuna maneno ya Kiswahili hapo ninayoweza tumia, ila iko hivi, kwasababu ilikuwa ikiaminiwa kuwa ulimwengu unatanuka kutokana na mlipuko wa Big Bang. ambao huo ulitoa nishati ya kuusukuma ulimwengu hata sasa. basi kama zilivyo nishati zingine, kadri muda unavyozidi Kwenda basi nazo zinapungua. na hivyo basi ilitegemewa kuwa, spidi ya kutanuka kwa ulimwengu itakuwa ikipungua kadri muda unavyozidi kwenda mbele. Lakini cha ajabu ni kuwa, ikaokekana kuwa spidi ya kutanuka ulimwengu ndiyo inazidi kuongezeka, na sasa basi tatizo litatatuliwaje?

Dark Energy

Hii ni nishati ambayo inaaminiwa kuwa hatuioni ila ndiyo inasababisha hilo ongezeko la spidi ya kutanuka kwa ulimwengu. Kuna mwanafizikia mmoja wa anga anaitwa Dr, Danny Faulkner. yeye ni miongoni mwa wanasayansi wanaoamini uumbaji. na miongoni mwa presentation zake huwa anaamini kuwa, kuna sababu za kuamini uwepo wa dark energy. huku akitumia tafiti juu ya dark energy, yeye haamini kama zinaweza leta changamoto katika mtazamo wa sayansi ya uumbaji. Lakini wanafizikia wengi wa sayansi ya uumbaji, ikiwemo na mimi binafsi, siamini katika chochote kuhusiana na Dark energy! maana kuna kila dalili ya kupachika nadharia hii kutokana na kuona kuwa nadharia yao ya Big Bang inafeli. Ukweli ni kuwa, Biblia imeandika ni Mungu tu ajuaye maarifa ya kutanuka kwa ulimwengu. na ndiye mwenye nguvu za kutanua ulimwengu. Pia binafsi naamini dark energy ni kielelezo cha dark brain, yaani brain inayoogopa kumuweka Mungu pale panapokosekana maelezo zaidi ya Mungu.

Dark Matter

Hii nayo ilitokana na kwamba. Chukulia mfano huu, kwanini unyoya wa kuku huwezi usukuma ukatembea kama ambavyo ungelisukuima jiwe? Ni kwa sababu unyayo una uzito mdogo, na hivyo hauna nguvu ya kuendeleza hali yake ya mwendo ‘’momentum’’. lakini jiwe lina uzito mkubwa, na hivyo momentum yake ni kubwa, hata kuweza kutembea Zaidi kwa nguvu ile ile uliyotumia kwenye unyoya. Ulimwengu pia unatembea kama jiwe, ili hali uzito wake ni kama wa unyoya. hivyo basi, lazima kuna uzito upo, ila hatuuoni ‘’missing mass’’. Hivyo ndivyo hawa watu wanavyozidi kuona nadharia yao haina nguvu, hata kusema kila kitu wanachokijua kuhusu ulimwengu ni asilimia 4% tu. na zilizobaki zote hakuna anayejua. Hii ni kwasababu wametaka hivyo wenyewe! ila sisi tunayo majibu. Na hizi nadharia za dark matter ndiyo sababu wengi hawaitaki hii nadharia ya big bang, kwa kuwa inajazia maswali juu ya maswali. na sio kutafuta majibu. Kwa watu hawa kuwa na maswali magumu ni bora Zaidi ya kuwa na majibu magumu.

Mungu Anaumba Majira Ya Mwaka Na Siku

Mungu anaumba majira ya mwaka moja kwa moja, kwa kuchezesha mhimili wa dunia. Yaani dunia inaegema kidogo kutengeneza nyuzi kati ya mhimili wa dunia, na mhimili wa dunia kuzunguka jua ‘’orbit’’. Kitendo hiki cha kutengeneza nyuzi kidogo kinapelekea sehemu zote za dunia kupitia vipindi tofauti tofauti vya mwanga wa jua, na viwango vya hali ya hewa.

Dunia pia kujizungusha katika mhimili wake, kunatenganisha mchana na usiku, pia kuna tofautisha hali za kati ya siku na usiku. mfano, wakati wa asubuhi, mchana na jioni, hutofautishwa kwa kutokana na uhusiano wa umbali wa dunia na jua, au umbali kati ya jua na dunia.

Dunia Ilikamilisha Mwaka Ndani Ya Siku 360

Tofauti na leo hivi ambapo tumezoea mwaka kuwa na siku 365.242. awali kabisa mwaka ulikuwa na siku 360. Huko mbele tutaangalia kwa undani Zaidi ni kwanini mzunguko huu wa siku 360 ulipotea! ni nini kiliikumba dunia? Lakini hapo cha kujua ni kuwa, dunia ilipaswa kuwa na baadhi ya vigezo vya kiufundi vya nyuzi, spidi na hata saizi Fulani, ili kukamilisha mzunguko kamili wa siku 360. na huko mbele tutaona sababu za hili badiliko hata leo hii dunia inatembea spidi kwa maeneo ya equator ya 0.4651 kilomita kwa sekunde. ambayo ni kubwa sana ulilinganisha na iliyopaswa kwa mzunguko wa siku 360.

Dunia Ilikamilisha Mzunguko Wa Mwezi Ndani Ya Siku 30

Pia mwezi ulikuwa ukikamilisha mzunguko wake kuizunguka dunia kwa siku kamili 30. Tofauti na leo ambao hutumia wastani wa siku 29.53. huko mbele tutaangalia sababu za kutokea kwa badiliko hili, ila kwa sasa cha muhimu ni kutambua kuwa, haikuwa kazi ya bahati bahati tu hata kutokea majira ya mwezi tuliyo yazoea. kuna nyuzi, umbali, uelekeo wa mwezi na wa dunia, na hata uhusiano na mfumo wa jua na ulimwengu kwa ujumla. na ndiyo maana, hatujawai ona mwezi ukigongana na sayari yoyote ile, hata sayari ndogo ‘’asteroids’’. yote ni kwa sababu, viliandaliwa kwa umakini na Mungu. Huko mbele tutaangalia sababu za kutokea kwa badiliko hili.

15.Tena Iwe Ndiyo Mianga Katika Anga La Mbingu Itie Nuru Juu Ya Nchi; Ikawa Hivyo.Mwanzo1:15

Mstari uliopita ni kama unaonesha kuwa, Mungu anazifanya Nyota na Galaxies kwa ujumla kwa kazi maalumu ya majira na dalili. Ambazo kazi hizo zote zinahusu utengenezaji wa mfumo wa mizunguko ya mianga hii, mifumo ya mihimili yake ‘’orbits’’, na uhusiano wa spidi za mizunguko yake na ratiba za kalenda ya dunia. Mfano ni huu.

Sehemu hii tunaona kazi kubwa ya Nuru ikiandaliwa kwa nyota, na sayari, na satalaiti kama mwezi. Hapa yako mengi juu ya namna ambavyo Mungu anazitengeneza Nyota kuwa na uwezo wa kutoa mianga ya kumulika dunia. Mfano, Miongoni mwa sayansi za ajabu kabisa, ni sayansi kuhusu utoaji mwanga wa Nyota kama jua, ambalo lenyewe hufanya ‘Nuclear fusions’’ katika kuzalisha mwanga. Duniani teknolojia hii ndio imeingia karibuni tu, lakini imeshatia hofu ya upotezaji wa Maisha ya watu wengi. Leo hii watu wakisikia ‘’Atomic bomb’’ au bomu la Nyuklia. kama hydrogen bomb, basi watu wanachanganyikiwa kabisa, lakini mwenyezi Mungu ameyatengeneza mabomu hatari Zaidi ya hayo, ambayo hayalipuki yakaua, bali yanalipuka ili kuanzisha Maisha. nikiwa siku moja namsikiliza mwanasayansi mmoja wa Jua wa Argentina akiwa BBC, anasema ‘’Maisha yangu yote nimekuwa nikijifunza habari za jua, na nalipenda sana. ila miongoni mwa vitu watu hawajui ni kuwa, jua linabadilika umbile kila ndani ya sekunde. na pia katika sura ya jua, kuna upinde ulio mithili ya kiulizo, ambao ni kama huwa ukisema siku zote kuwa, bado hujui!’’  

Hebu tazama namna mwezi unavyotoa mwanga wake, mwezi hauzalishi, lakini una akisi mwanga. kwa kuwa upo katika mhimili ulio katika nyuzi makini kabisa kuweza kulengesha mwanga uelekeo wa dunia. Mwezi hauna anga la hewa, na ndiyo maana wenyewe huwa na giza, lakini huakisi mwanga kwa manufaa ya Dunia.

Zipo sayari kama Venus. ambazo huwa ziking’aa angani na kuvutia. zipo Galaxy nyingi ambazo hatuna taarifa zake kabisa, Zaidi ya kuangalia tu mionekano yake na umri. Zipo Black Holes, sayari zilizo nje ya mfumo wetu wa jua. Kiufupi yapo mengi bado tunapaswa kujifunza kutoka kwa muumbaji wetu.

16. Mungu Akafanya Mianga Miwili Mikubwa, Ule Mkubwa Utawale Mchana, Na Ule Mdogo Utawale Usiku; Akafanya Na Nyota Pia. Mwanzo 1:16

Hapa moja kwa moja ni kama inatolewa summary ya kilichofanyika katika mstari wa 14 na 15. Na pia hapa, anazungumzia mfumo wetu wa Jua ‘’solar system’’. Mianga mikubwa yaani Jua, na Mwezi ndiyo ambayo inazungumziwa moja kwa moja. ukiachana na ujumla wa vilivyoumbwa vyote. Kama Biblia ingeandikwa kwa kizazi cha watu wasioasi, basi tungeelezwa na lengo na sifa za kila kilichoumbwa na Mungu. Nyota zote ni kama jua kwa kazi ya kumulika, Mungu asingeumba mwanga kama hakuna cha kumulikia. unaweza jifunza hata kwa viungo vya kiumbe hai, hakuna kisicho na kazi hata kwa vile wanavyo viita viumbe visivyo na kazi ‘’vestigial organs’’, si kweli, kila kiumbe kina kazi. na ndivyo ilivyo kila sayari na nyota ina jukumu kwa mwanadamu kama tu imeumbwa katika mfululizo wa siku saba. maana kila kilichoumbwa katika siku sita kilikuwa cha kuja kutawaliwa na mwanadamu, kwa utukufu wa Mungu. Na wala vitu hivi havikuwa vya kutazamwa tu, kama wengine wanavyo hisi, si kweli. na ndiyo maana, kwa muda mfupi tu baada ya sayansi ya anga kupiga hatua, mfano, kupitia tafiti za anga, leo hii tunajua hata taarifa za Galaxy za mbali kabisa, kupitia telescopes kubwa Zaidi zinazokaa katika space kama satellite. pia wapo wanaoenda katika sayari kama Mars, wapo wanaotuma vifaa kwenda katika Pluto ,asteroids kadhaa, Jupiter n.k. tunaweza tazama Nebula vizuri zilizo angani, Black Holes n.k. haya yote yanatudhihirishia kuwa, kuna vitu vingi sana tumepoteza baada ya dhambi. Mwanafizikia anayeaminiwa kuwa hakuna mwenye utaalamu ‘’technical skills’’ Zaidi yake, huyu ulikuwa ukimuambia tu nataka kutengeneza kitu cha namna Fulani, yeye tayari ashajua namna za mashine na mfumo mzima unavyopaswa kuwa, anaitwa John von neumann aliwahi kusema, ukiamini Mungu una majibu mazuri Zaidi kuliko kutoamini. Basi maamuzi mazuri Zaidi ni kuwa katika upande wa utafiti Zaidi.

17. Mungu Akaiweka Katika Anga La Mbingu, Itie Nuru Juu Ya Nchi. Mwanzo1:17

Hapa anaiweka ianze kazi rasmi ‘’installation’’. Unaweza pata picha pia juu ya mazingira ya dunia Ilipokuwepo, na mianga hii ilipokuwepo. Hii inaonesha ya kuwa, ijapokuwa sisi tunaona ulimwengu ni mkubwa sana, lakini Mungu anauona ni kama jiko tu, yaani ni kuchukua hapa na kusogeza hapa. Hii ina maana kubwa sana. maana inaonesha kuwa Mungu ni mkubwa sana. na uweza wake ni wa ajabu, na ndiyo maana, na sisi alituumbia ulimwengu mkubwa sana, ili hata ikiwezekana kila mtu awe na eneo kubwa sana la kumiliki. Maana kwa idadi ya watu waliopo duniani leo bilioni kadhaa, basi kila mtu angeweza miliki idadi kubwa sana ya nyota na sayari kwa jinsi zilivyo nyingi, na hazina mwisho kama binadamu wanavyozidi kuzaliana.

Sayansi Ya Wasio Amini Na Asili Ya Mfumo Wa Jua

Baada ya mlipuko wa Big Bang na kisha miaka bilioni 4.5 iliyopita. Kulitokea kiwango kikubwa sana cha mithili ya mawingu ‘’Oort Cloud’’, mawingu haya yalikuwa ni matter zilizokuwa zimejaa sana katika ulimwengu huo wa awali, na Vumbi au Dust hizi zilikuwa zikizunguka kwa spidi kubwa sana. mavumbi haya yaliyokuwa yakizunguka yaliitwa ‘’solar nebula’’. Kulikuwa na mvuto mkubwa sana wa Gravitation kutokana na uzito mkubwa wa mavumbi haya. ambao ulipelekea mawingu haya kugongana ‘’Collapse’’, nakuunda mtoto wa nyota ‘’protostar’’, hiki ni kama kitovu cha nyota. ambacho wanaamini ndicho kilichobadilika kuwa jua.

Mavumbi yaliyobakia katika ile nebula, yakaanza kuungana pamoja kuumba sayari toto. ambazo zikaaanza kugongana na kuunda sayari kubwa za miamba. Sayari za karibu na kitovu cha dunia ni za miamba kama dunia, mars, venus. lakini zile za nje ni za gesi kama vile Uranus na Jupiter.

Na Jua kwao baada ya ku collapse kwa nebula, lilipelekea mgandamizo mkubwa sana uliopelekea kuungana kwa atomu za Hydrogen.

Changamoto

Imani huwepo kunapokuwepo na Ushahidi na mtu huamini, lakini maelezo haya hayawezi zalisha Imani hata kwa mgunduzi wake. maana hayana nguvu ya Ushahidi wa uhalisia kabisa. Hii ni kutokana na kuwa, hakuna uwezekano wa uwepo wa matter za kutosha kuunda Galaxy yoyote ile! au Black Holes kubwa kabisa na Quasars, pili Galaxy na Black Holes haziwezi tenganishwa, maana moja itaathiri nyingine, hakuna ushuhuda wowote uliowahi onekana wa uundwaji hata wa mfanano wa Galaxy, au mfumo wa jua. Kwa kawaida vitu vinavyogongana, na kutulia kwa Pamoja, kutokana na matokeo ya mvuto wa gravitation, huwa haviungani. na migongano Zaidi husambaratisha! na hivyo asili ya sayari huwezi ielezea kwa kutumia migongano ya vimondo ‘’meteors. uundwaji wa Galaxy utahitaji muda Zaidi ya muda uliokadiriwa hata kwa nadharia zao wenyewe! Picha za Galaxy nyingi zinaonyesha hazina umri mkubwa kama mapendekezo ya nadharia hizi. Hakuna Ushahidi wowote wa uwezekano wa uumbaji wa madini mazito ya sayari ’’madini kuanzia atomic number ya 26’’ haiwezekani!

18. Na Kuutawala Mchana Na Usiku Na Kutenga Nuru Na Giza; Mungu Akaona Ya Kuwa Ni Vyema. Mwanzo1 :18

Mungu akaona ni vyema. Kipindi nasoma hizi sehemu miongoni mwa vitu nilivyo vigundua ni kuwa, Mungu anapofikia kuufanya mfumo ufanye kazi ‘’Automatically’’. yaani kujiendesha wenyewe, huona vyema. Rejea baada ya kukamilisha uumbaji wa mimea katika siku ya tatu.

Kiukweli siyo kazi rahisi kutengeneza automatic system kwa vitu hivi vya asili, kumbuka mahesabu ya Mungu hayachunguziki na kitu ambacho sisi bado hatujui, ni hivi vitu vilipewa nishati ya aina gani, viweze kudumu hata leo! pia hatujui ni ufundi gani uliotumika, kuvifanya vifuate mihimili yake na kuwa na spidi zilezile. Kwa kweli hatujui mambo mengi.

Mfumo wowote ambao binadamu huutengeneza huwa na makosa mengi sana. na ndiyo maana, mara chache kukuta system zikidumu kwa muda mrefu. Lakini hebu tazama mfumo wa jua mpaka leo, bado unapiga kazi tena ukiwa na ubora ule ule hata kwa mabadiliko kidogo yaliyotokana na sisi wenyewe. na sio kuwa nyota ziligongana au mihimili ilikosewa, tutakapo fika mbele tutajifunza kuhusu vimondo ambavyo huwa vikidondoka, sababu zake, fizikia yake, na asili yake.

19. Ikawa Jioni Ikawa Asubuhi Siku Ya Nne Mwanzo 1:19

Kwa kweli siku ya nne ilikuwa siku busy sana kwa Mungu, ila hio haimaanishi kuwa alichoka kwa maana Mungu hachoki! ila inaweza pia kumaanisha kuwa, kazi za siku zilifanana ila hakuzielezea sana kwa baadhi ya siku, na kupelekea sisi kuhisi kuwa hii ilikuwa siku busy Zaidi.

To be continued....