GHARIKA NA MAKOSA YA KABONI-14
Ushahidi Wa Uwepo Wa Kaboni-14 Nyingi Na Mabaki.
Kwa kawaida kaboni ni elementi ambayo huwa na uzito wa 12. Kitendo cha kuwepo aina zingine za kaboni zenye uzito mkubwa Zaidi wa 14 ‘’huitwa Isotopes, yaani zinafanana namba za protoni ila zinatofautiana neutron’’, huturudisha kulekule kwenye matokeo ya mabadiliko yaliyopelekea mionzi, ambayo hayo ndiyo chanzo kikubwa Zaidi cha uwingi mkubwa kabisa wa kaboni 14. Kama kuna sehemu wanasayansi wanaotamani kujua muda wa ulimwengu wanapaswa kuwa makini, basi ni hapa.Kosa Kubwa Katika Kutumia Kaboni -14 Kupima Umri
kutojua asili ya kaboni-14.
Asili ya kaboni-14 kwa wengi wanavyofundishwa ni kupitia mionzi inayopelekea neutron kugongana na Nitrogen gesi (N-14) na kuunda kaboni-14 ambayo hukosa uimara, na hukaa miaka 5730 na kurejea katika Nitrogen-14. ambayo ni asili yake. hebu angalia mchoro huu mdogo hapa chini. Huo mchoro ndio unaotumika Zaidi kufundishia asili ya Kaboni-14
makosa katika mchoro na asili ya kaboni-14.
Kiwango cha kaboni-14 katika anga la leo sio sawa na kiwango kilichokuwepo kabla ya gharika. Kabla ya gharika kiwango cha kaboni-14 kilikuwa kidogo sana kutokana na ukweli huu, Kwa kipindi cha mwaka mzima, anga ‘’atmosphere’’ huzalisha kilogram 9.5 tu dunia nzima za kaboni -14. hiki ni kiwango kidogo sana. Kaboni-14 kama isotopes nyingi zingine zilizalishwa kipindi cha gharika baada ya neutrons nyingi kugonga elementi za kaboni-12. ni kama tu ilivyokuwa kwa oxygen-18. lakini pia Kuna sababu ambayo iligunduliwa karibuni sana, ambayo hiyo imeonyesha kuwa kiwango kikubwa cha kaboni-14 pia ni matokeo ya zile zile Elementi nzito sana za mionzi ‘’heavy radioisotopes’’. hizi zimegundulika pia kuwa hutoa sio tu mionzi yake kwa miale ya helium (alpha decay), bali pia hutoa carbon-14. Na hii ni sawa na kusema, kiwango kikubwa cha carbon-14 kilikuja baada ya gharika. na hivyo sasa, ulimwengu wa awali ulikuwa na kiwango kidogo sana cha kaboni-14.
Makosa Katika Kupima Umri Kwa Kutumia Kaboni-14.
Kaboni-14 baada ya kuundwa haitakaa yenyewe, itakutana na oksijeni na kuunda hewa ya kaboni dioksaidi, ila kaboni dioksaidi hii huwa yenye kaboni-14 tofauti na ile ya kawaida ya kaboni-12. hizi hewa mbili zote huwa katika anga kwa wastani maalumu. Hewa hii huvutwa na mimea na Wanyama pia, huingia katika miili yao, na hivyo viumbe huwa na kaboni za 14 na 12. Hivyo itambulike kuwa, Siku zote katika kupima muda hutumika uhusiano wa kiwango cha kaboni-12/kaboni-14. kila baada ya miaka 5730 kaboni-14 itabadilika kuwa N-14, na hivyo basi, tunaweza jua spidi yake ya kuvunjika hata kwa sekunde ‘’disintegration rate’’. Na ili utafute, utapaswa kwanza kujua wastani wa kaboni-14/kaboni-12. Hapa wanachukua wastani wa leo, au sasa hivi, au baada ya gharika, ambapo kiwango cha kaboni-14 kimeongezeka sana na hata mapinduzi ya viwanda yamechochea sana. Najua umeshagundua udhaifu ulipoanzia, maana yake itakuwa hivi. Yale mabaki ya awali ya mimea na Wanyama, kwa kuwa enzi hizo kulikuwa na kaboni-14 chache, basi wastani wake utaathiriwa na kufanya ionekane kana kwamba vilikuwa ni viumbe vilivyoishi miaka mingi sana nyuma. kitu ambacho sio kweli, ila tu ni kwa kuwa wastani umetofautiana wa awali na sasa.
Kutokana na hiyo graph ni Dhahiri kuwa kiwango cha kaboni-14 kiliongezeka sana baada ya gharika kuu kutokana na kuanza kwa mionzi ‘’radioactive decay’’.
Ushahidi Wa Uwepo Wa Hewa Ya Argon-40 Nyingi Katika Anga
Hewa ya argon ni asilimia moja kabisa ya hewa yote katika anga letu. Sasa tunaamini uwepo wa gharika, kwa kuwa hewa hii ya argon-40 hutokana na mabadiliko kutoka kwa Potasium-40. Leo hii vitabu vingi vya sayansi vimeandika kuwa chanzo kikubwa Zaidi cha argon-40 ni potassium-40. shida inayokuja ni kuwa, kiwango chote cha argon-40 kilichopo katika dunia, kama utakirejesha nyuma kuwa kilitoka kwa potassium, basi utahitaji kiwango kikubwa sana cha potassium karibia mara mia ya potassium iliyopo hivi leo. Na pia kwa kuangalia miamba ambayo ni chanzo cha potassium iliyopo chini ya dunia, kutaifanya dunia igharimu miaka Bilioni 10, yaani mara mbili Zaidi ya hata muda wao wa dunia.
Njia pekee inayoleta majibu na mantiki ni kuwa, Argon-40 ilizalishwa kipindi hiki cha awali cha gharika kuu. na kuwa, kipindi hiko hiko potassium-40 ilizalishwa. hizi zilizalishwa katika matendo ambayo yanafanana. Ambayo ndiyo niliyoyaelezea katika sehemu iliyopita Yaani ‘’Electron Capture’’, na mengineyo kama Z-Pinch. Sasa basi
kwanini jambo hili ni la muhimu?
Kupima Umri Wa Dunia Kupitia Miamba Potassium-Argon Dating
Kwasababu wanaamini Potassium-40 hupelekea Argon-40, na Pili kiwango cha Potassium-40 ni kikubwa sana katika miamba. basi uhusiano huu unaweza pia tumika katika kutafuta umri wa miamba duniani. Sasa changamoto kubwa ndiyo huja kuwa Potassium-40 sio chanzo kikubwa Zaidi cha Argon-40 ambayo nayo iko kwenye miamba. Maana tumeshaona hata katika mwezi wa sayari ya Saturn unaoitwa Enceladus, inaonesha kuwa kuna kiwango kikubwa sana cha Argon-40 Inayozalishwa, na kuna kiwango kidogo kabisa cha Potassium-40. hii ni kudhihirisha tu kuwa, Potassium haiwezi kukidhi kabisa kuwa chanzo cha Argon-40. Hivyo basi, kutokana na kutobalansi kwa wastani wa madini haya, unapotafuta umri wa mwamba, utaona kiwango kikubwa sana cha madini ya Argon-40, utahisi yametokana na K-40. Na kwakuwa unajua spidi ya kubadilika kwa K-40 kuwa Ar-40 ambayo ni ndogo sana, matokeo yake utahitimisha mwamba una umri mkubwa sana, na kumbe ni makosa ya kinadharia yako. Mfano wa madhara ni pale inapotokea hata miamba yenye umri unaofahamika kuonekana ni ya kitambo sana. Angalia picha hapa chini.
Haya yote makosa wanayavumilia tu kwasababu ya kukataa kuwa kulikuwa na Gharika ya Nuhu. kitu ambacho kingerahisisha na kupanua maarifa ya wasomi wote wa sayansi zote.
To be continued....





Join the conversation