Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

CODE 01, MAREKANI#

Siri nyuma ya falme

 CODE 01, MAREKANI#

Zama zote za mwanadamu, katika falme zote zilizowahi kupita, Tamaa kubwa ya wenye Nguvu katika jamii ilijikita katika kutaka kuwatawala watu wote wa jumuiya zao. Mfumo ambao ulikuwa ukitumika kuwatawala watu ulikuwa mfumo wa Chakula. Ambao ndiyo ulihusisha jamii za watu kukaa kwa pamoja kufanya shughuli za kilimo kama tulivyoona sehemu zilizopita. Mifumo hii ya kilimo iliwakusayanya watu kama ilivyokuwa kwa Misri ya kale, na kupelekea falme zote kama zilizopita miji ya Mesopotamia kuanzia Babeli, mpaka Rumi baada ya Ugiriki. Watu walipokuwa pamoja wafalme waliweza watawala watu kwa kutumia Majeshi yao, ambayo yalitegemea Vyakula vilivyolimwa na wakulima. Mfumo huu haukuwa na mafanikio makubwa sana, hii ni kwa kuwa, watu wengi waliokuwa wanatawaliwa walikuwa wanaweza kutoroka falme hizi, na kwenda kuanzisha falme zingine wakiwa huru. Na wafalme zamani walitumia Kuta zao kubwa ambazo zilikuwa na walinzi kuzuia watu kutoroka. Changamoto kubwa ilikuwa ili falme iwe kubwa inahitaji eneo kubwa zaidi. Eneo ambalo hautaweza kuzungushia ukuta au fensi. Na kwa mtindo huo bado haikuwezekana kuweza kuwatawala watu wote. Wafalme walitamani sana kutawala lakini walishindwa.

Miaka kadhaa mbeleni, wafalme waligundua ili uweze kuwatawala watu kirahisi zaidi, inabidi utumie kitu ambacho watu watakifuata wao wenyewe, na sio wewe kuwavuta watu waje kwako. Na mbinu hii ilionekana ni njema sana kwa wafalme wakwanza kabisa kama mfalme Constantine. Ambaye yeye aligundua kwa ufalme wake kuufungamanisha na Dini, ambayo ilikuwa Ukristo wa awali kabisa, na tena kuufanya usiwe ukristo wenye makali sana, ili uweze kuendana na imani kadhaa za dini za Kipagani, basi anaweza kuwafanya watu kuamini Ufalme wake ni sehemu ya amani zaidi. Hii ilitokana na falsafa kuwa, watu marazote huelekea sehemu wanazohisi wanaweza kumuona Mungu wao. Hii ilikuwa ni mbinu ya kwanza ambayo iliendelea kutumiwa na wafalme wengine wa dola na imani mbalimbali. Changamoto kubwa iliyotokea kutokana na mbinu hii ni kuwa, sio wote waliokuwa wakikubaliana na Dini husika. Na kwa mantiki hii Vikundi vya Uprostentanti vilishamiri sana na kuathiri falme, mbinu hii iliyofanikiwa kwa asilimia kubwa walahu, hata kupelekea maendeleo makubwa ya Dola ya Upapa kwa Ulaya kwa zama fulani katika historia, iliishiwa nguvu mpaka inapofikia karne ya 18 iliyoshamiri mapinduzi na sera za Uhuru kuanzia Marekani, mpaka Ufaransa.

Kipindi kila Ufalme umekwisha kunyosha mikono kuwa hauwezi wakusayanya watu kwa pamoja, mpaka inapoingia karne ya 19, Wafalme wa kwanza kabisa wa Ulaya walianza kugundua kuwa ipo njia moja yenye mafanikio sana yenye kuwavuta watu kuliko hata Dini. Na hiyo njia ilikuwa ni Teknolojia. Waingereza ambao ndiyo walianza na spidi kubwa zaidi ya Mapinduzi ya viwinda, walianza kushuhudia kwa ghafla sana ongezeko kubwa sana la watu katika Nchi yao. Changamoto kubwa sana iliyoathiri Nchi za Ulaya ambazo zilianza kwa kutumia teknolojia hii kuwa falme kubwa sana, zilizokuja kutawala sio tu Afrika bali Dunia nzima mpaka Mashariki ya mbali, tatizo lao lilikuwa ni teknolojia iliyo na falsafa zisizo za uhuru. Nchi za Ulaya nyingi bado zilikuwa zimeathiriwa na falsafa za Kirumi na Upapa, za Uongozi wa kifalme. Falsafa zilizoathiri hata China ambayo mpaka karne ya 14 ilikuwa juu zaidi kwa teknolojia kutokana na Kilimo, lakini nao falsafa za Kifalme ziliwaangusha. hizo falsafa ndizo ziliiathiri sana pia Urusi iliyokuwa na migogoro sana ya wenyewe kwa wenyewe, kama ambavyo Misri ya kale iliyokuwa nayo juu kwa Kilimo, lakini falsafa zao za kifarao ziliathiri maendeleo ya teknolojia zao za awali kabisa kuwafanikisha kuunda falme kubwa zaidi.

Marekani ambaye ndiye Kichwa katika Ulimwengu huu, ndiye ulikuwa ufalme wa kwanza kugundua Teknolojia yenye Uhuru wa kidini na Kiuchumi, ndiyo mbinu pekee yenye kuweza kuwavuta watu wengi zaidi na kuunda ufalme mkubwa zaidi. Marekani ambayo wengi hawafahamu kwamba Misingi hii ya Uhuru na Teknolojia iliwekwa na watu ambao walikuwa na malengo ya kuwavuta tu watu, au ilikuwa na malengo ya kuwavuta watu na mwishowe kuja kama Marekani hii ya leo, ndiyo Nchi pekee ambayo haikuwa na kabila rasmi, Marekani ilikuwa ni Nchi ya ndoto ya kila msafiri, marekani ilishamiri walughalugha toka kila Nchi waliojazana katika Viwanda ambavyo Vilishamiri katika kila miji. Teknolojia kubwa kuanzia katika Viwanda vya Magari kama vya Fordy, viwanda vya Nguo vya Samuel Slater, Viwanda vya Mafuta vya kina John Rockefeller, makampuni ya Fedha ya kina J.P Morgan, viwanda vya chuma vya Andrew Carnegie, n.k. Marekani haikuwa Nchi ambayo mtu anaweza kukosa kazi enzi za mapinduzi ya pili ya viwanda, na huu ndiyo mwanzo wa kukua kwa tabaka la kati ‘’’Middle Class’’, Marekani ilipungukiwa kwa kiwango kikubwa sana Vijana Masikini, Marekani ilishamiri Wanasayansi wakutosha hasa baada ya Vita ya Pili ya Dunia. Wanafizikia wakubwa wengi waliotoka Ujerumani, na waliochukuliwa Toka Ujerumani enzi za Project PaperClip, wote waliikimbilia Marekani kama Nchi yenye Uhuru zaidi. Mamilioni ya Wamarekani wenye asili ya afrika waliokuwa Marekani walizidi kupambania haki zao na hata kupelekea mapinduzi makubwa ya Vipaji kuanzia katika Miziki, michezo, n.k. kutokana na teknolojia na uhuru wa kibiashara, Burudani zilikuwa na nguvu sana Marekani, Nchi ya marekani ikazidi kuwa kitovu cha Uchumi, hasa ukilinganisha na ukweli kuwa, Nchi za Ulaya nyingi baada ya Vita ya pili ya dunia zilikuwa nyuma sana kimaendeleo.

Hoja ya msingi katika siri hii ni kuwa, Teknolojia na Uhuru ndiyo ilikuwa ndoto kubwa zaidi ya binadamu. Na hii ni kwa kuwa teknolojia inaburudisha, lakini pia inarahisisha kazi za mwanadamu. Uhuru ndiyo msingi wa hisia za thamani ya Uutu wa mtu. Unapompatia mtu uhuru, kila mtu anatambua thamani ya kuishi. Kwa misingi hii miwili, Marekani iliibuka na mbinu pekee ya kuwavuta zaidi watu, na kuunda falme kubwa zaidi kuanzia mikononi mwa kina George Washington.

To be continued...