Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SIKU YA 01 YA UUMBAJI KISAYANSI

Siku ya kwanza ya uumbaji kisayansi

SIKU YA KWANZA YA UUMBAJI 

1. Hapo Mwanzo Mungu Aliziumba Mbingu Na Nchi Mwanzo 1:1 

Waebrania 11:3 ‘’Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri’’

Vitu Vya Muhimu

Mwanzo-Beginning-Time

Mungu anaumba muda kwa mara ya kwanza, mwanzo wa muda unaenda sambamba na mwanzo wa ulimwengu. Muda ni msingi wa ajabu sana wa ulimwengu. Wanasayansi wa fizikia huuita dimension ya nne, yaani ni mithili ya pande ya nne ya ulimwengu.

Muda Ni Nini? 

Muda ni kipindi kazi inafanyika au imefanyika. Huwezi kuwa na muda bila kazi. Kazi ni matokeo ya nishati. Hivyo basi muda na nishati huwezi vitenganisha, mtu anapokufa hawezi hisi muda. maana hakuna kazi tena ya utambuzi katika ubongo wake. nishati inapokuwa kubwa sana basi muda huwa mdogo sana. mfano mtu mwenye nguvu sana angefanya kazi haraka kwa dakika chache. na kwa mantiki hiyo katika nishati kubwa isiyo na mwisho muda haupo kabisa. Mfano kitu kinachotembea na spidi karibia na ya mwanga muda hupungua sana, kama nilivyoelezea awali katika uhusiano wa mwanga na muda. Siku zote muda huwa ukienda mbele.

Kumbuka kadri unavyotoka duniani na kwenda kwenye Space, ndipo muda unazidi kwenda polepole, hii inaitwa ‘’Time Dilation’’, hii inatokana na kwamba sehemu zote zenye mvuto mkubwa ‘’gravitation’’, kama vile karibu na Jua au Black holes ‘’nitakazozielezea baadae’’, basi mwanga wa jua unavutwa na kwenda na spidi kubwa sana, kiasi cha kupelekea muda kwenda polepole. Unaweza tu kutumia kielelezo cha kawaida. Kwahiyo kama mwanga ukivutwa kutokana na mvuto mkubwa wa kitu Kizito, basi muda utapungua mwendo. Muhimu kutambua kuwa mwanga hauna uzito wa kuufanya uvutwe kuelekea kwenye kitu kizito, bali hufuata kona ya lile neti la space ‘’curvature of space fabric’’, na athari hii ya mwanga ndiyo inayoathiri pia muda. 

Uhalisia wa mabadiliko ya muda 

Ni kweli kuwa muda unaweza badilika. lakini sio kwa kiwango cha kuathiri majira katika ulimwengu wetu. na pia sio katika kiwango cha kutambulika. Inaaminiwa kuwa GPS zinatumia sheria hii katika ufanisi wake. Lakini miongoni mwa uongo mkubwa ‘’ fiction’’ ni kuwadanganya watu kuwa mtu angeweza kwenda mbele au nyuma ya muda kwa kipindi kirefu ‘’significant period’’. Si kweli haiwezekani. na kwenda nyuma ya muda kuna husisha kwenda na spidi Zaidi ya spidi ya mwanga kitu ambacho kinavunja sheria zote za physics ‘’Causality’’. Mfano ikitokea umerudi nyuma miaka hata kabla ya Babu yako hajazaliwa, sasa wewe ulitokana na nani? ‘’Grandfather Paradox’’, na hata kwenda mbele ya muda hakuna uhalisia ambao wengi huambiwa katika filamu za uongo ‘’fictious or Sci-Fi Movies.

Kwanini Mungu Aliumba Muda?  

Mungu aliumba Utambuzi wa Muda kwa ajili ya Binadamu. na ndiyo maana kama mtaalamu wa Wanyama natambua hakuna mnyama anaeijua kalenda, lakini hakuna asiyezingatia muda wa kulala na muda wa kuamka. Biblia katika Marko 2:27 imeandika ‘’Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Sabato ni muda. Sabato ni siku ya saba, au masaa 24 ya siku ya saba. Mungu aliumba Muda kwa ajili yetu sisi, tufanye kazi siku sita, tukue, tujenge na tumwabudu kwa siku ya saba. Mungu aliumba Muda kuwa kipimo cha kazi, mfano ukuaji, maendeleo, n.k. Biblia kiunabii imeandika miaka elfu kwa mwanadamu ni kama siku moja kwa Mungu, hii inamaanisha hata kipindi tunachokitambua kama Muda kinatengeneza uhalisia wa utendaji kazi kwetu tu kama wanadamu. Muda unatengeneza mpangilio wa utendaji wa nishati. 

Kama kiasi cha Muda Hupima Ukuaji Je Mungu Hukua?

Mungu hakui kwa maana yeye tayari amekamilika, yeye aliumba muda kwa ukuaji wetu usio na mwisho, kama muda usivyo na mwisho. Namshukuru sana Albert Einstein ambaye aliweza ifunulia dunia ya kuwa, muda ni kama upande tu mwingine wa pande kuu tatu za ulimwengu, na pia alitengeneza njia ya kutambua kuna uwezekano wa uwepo wa pande zingine. yaani ni kama kusema kukosa kujua, sio sababu ya kutokuwepo kwa maarifa.

Je Mungu Alikuwepo Wapi Kabla Ya Muda?  

Mungu hayupo ndani ya Muda ‘’Timeless’’, na ndiyo maana anaitwa ALFA na OMEGA. Mwanzo na mwisho. Huwezi kuwa mwanzo na mwisho kama upo ndani ya hiko kitu, maana huwezi kuwa sehemu zote kwa wakati mmoja. hebu chukulia kielelezo hiki, kipindi unaangalia Mpira kwa Televisheni, wewe uliye nje unaweza shikilia magoli yote katika kioo chako cha TV. lakini mchezaji hawezi. Hii ni kwa kuwa, yeye yuko ndani ya uwanja. ataweza kuwa sehemu moja tu kwa wakati. Huo ni mfano wa namna Mungu ameumba Muda, na hivyo yeye yuko nje, na ndiyo maana yuko mwanzo na pia yuko mwisho. au pia huuona mwanzo tokea mwisho.

Mbingu -Heaven -Space

Mungu aliumba Space inatamkwa ‘’spess’’, hili ni neno la kifizikia linalo maanisha eneo lote. Ambalo lina kila kitu tunachokiona katika ulimwengu. Yaani huu ni kama uwanja, Sayari, nyota n.k. vyote vinaelea ndani ya space. Hakuna anayejua hali ya dunia kabla ya uwepo wa space, na wala hupaswi kuwa na mashaka kwa maana tayari tuna uhakika ‘’uwepo’’ ulikwepo. Baadhi walijaribu kutengeneza nadharia za kuwa hakukuwa na kitu kabisa ‘’Nothing’’, wakashindwa kuelezea mpaka wakabadilika nao sasa wanasema kulikwepo kitu. sisi tunasema Mungu alikwepo akatengeneza space. wao wanasema Space ilikuwepo tu haina mwanzo. tayari washaanza kukubali kushindwa kujua mwanzo. Space haionekani kuwa na kitu, lakini kuna mithili kama ya neti ambazo nilizielezea awali ‘’space fabrics’’. Hii inamaanisha katika mbingu, ijapokuwa unaweza usione, lakini tayari kuna ufundi wa kitaalamu unaotengeneza msingi wa uumbaji mwingine.

Nchi-Earth -Matter

Mungu aliumba nchi. Nchi ni kitovu cha ulimwengu wote, hata nyota na sayari zinginezo zilikuja kuumbwa baadae tokea kwenye Nchi. hiyo ina maana neno nchi, linatumika kuwasilisha mwanzo wa vitu vyote au Matter kwa mara ya kwanza kabisa katika ulimwengu. Kuna vitu ambavyo sio Dhahiri ambavyo mwenyenzi Mungu aliumba kutokea huko, vitu au matter. Inaleta mantiki nzuri Zaidi kutambua yafuatayo.

Mungu Anaumba Gravitation 

Hakuna anaeweza elezea hata kwa kudanganya namna Gravitation ingeweza tengenezwa, lakini hebu tengeneza taswira ya 3D sphere ‘’mithili ya mpira mkubwa sana kama dunia. Halafu katikati ya mpira huo, vitu viwe vinatumbukia tokea pande zote. Najua unaweza pata shida kwamba vitu vingewezaje kutumbukia tokea chini, lakini gravitation ndivyo inavyofanya kazi. hata yule aliye chini nae anajiona yupo juu kama wewe. Na ndiyo maana siku zote unajiona uko juu ya dunia. lakini kumbe upo pembeni ya dunia. Mungu anaumba Gravitation ambayo inakuwa ndiyo kitovu cha vitu au matter, kwa mara ya kwanza kabisa. na mithili ya Paa la nyumba linaloshuka linavoacha eneo wazi juu, basi pia namna nchi inavyoundwa, inaacha sehemu au mbingu au space. sisemi kuwa nchi ni matokeo ya uumbaji wa ugandamizaji ‘’compression’’ maana hatuna taarifa ya uwepo wa kitu, kabla ya kitu, Zaidi ya uwepo wa Mungu katika uumbaji. ila hatupaswi kuathiriwa na falsafa ya kulazimisha kuweka Sifuri katika mwanzo wetu. maana Mungu wetu ni Tajiri wa kila kitu, au Vitu. na sio Sifuri. wao hulazimisha Sifuri kwa kuwa, hawana Mungu, wana sifuri ‘’Nothing’’. Na tena hata wao nao wamebadilika kwa sasa, wana amini kulikuwa na vitu tayari vilivyoshiriki katika uumbaji.

Kwanini Mungu Ana Namna Nyingi Za Kuumba Vitu Kisayansi?  

Mungu ana uwezo wa kuzalisha malighafi za uumbaji. na pia ana uwezo wa kutumia malighafi zake kuumba tena. Uwezo huo wa kuzalisha, au kuumba. ndiyo ambao umenifanya nikazie hapo kuwa, sio vyema kuegemea katika ugandamizaji wa vilivyokwisha kuwepo ‘’Compression of pre existed stuffs’’. Maana hapo ni kama kutumia ubongo wa binadamu kuumba. Ambao unahitaji kitu kuumba kitu. lakini Mungu anaweza kuanzisha kutoka ndani yake yeye mwenyewe. na ndiyo maana anaitwa Mungu. Kadri tunavyozidi kuendelea utagundua wanaoamini Mungu katika sayansi, ni kama walioliona Gari porini, wakasema limetengenezwa na mtu. na wasio amini, wanasema limejitokezea tu lenyewe kama upepo. halina mmiliki, na tunaweza fanya tutakalo. Yaani useme Gravitation, space na Energy zilikwepo tu, na ili hali hakuna aliyejaribu hata kuzitengeneza, au kuzielewa akamaliza!!

Hitimisho

Mungu aliumba mbingu na Nchi. Au Mungu aliumba Space na Matter. Mungu ana Nguvu au Nishati. kwa hiyo sasa tayari tunakubaliana na sheria za Physics za ‘’Cause and Effect’’ yaani matokeo yana sababu. Matokeo ya Mbingu na Nchi yana sababishwa na Mungu. Kule upande wa pili hii sheria inavunjwa dakika ya kwanza kabisa. maana mlipuko unatokea na Sababu haifahamiki?? Space na Matter zinaonekana, sababu hazifahamiki? Nishati inaonekana, chanzo hakionekani? 

2. Nchi Ikiwa Ukiwa, Utupu, Giza, Vilindi Vya Maji Na Roho Ya Mungu Juu Ya Maji Mwanzo 1:2

Hapa tunaona kitu au matter ya kwanza kabisa kuundwa ilikuwa ni Maji. Ambapo pia tunaweza pata hali ya utulivu wa awali kabisa, uliombatana na nyuzi chache za joto. Yaani sio mlipuko kama uliokuwepo kwa mtazamo wa nadharia ya Big Bang. Hakuna anaejua saizi ya vilindi hivi vya maji. Miongoni mwa vitu vya kuzingatia hapa ni kuwa, dunia haikuwa na muundo maalumu. ‘’And the earth was without form, and void; and darkness was upon the face of the deep.’’ Miongoni mwa tafsiri zitakazo tusaidia sana kisayansi, ni kuchukua hivyo vilindi vya maji kutokuwa na umbo maalumu. Mfano ni kuchukulia uwepo wa mithili ya makusanyiko ya vilindi vya maji ‘’waterballs’’.

3. Mungu Akasema, Iwe Nuru; Ikawa Nuru.  

Miongoni mwa nadharia bora kabisa ya kisayansi ni kuwa, Mungu akasababisha uwepo wa gravitation kubwa kabisa juu ya matter zilizokwepo. Mgandamizo huu ukapelekea uwepo vitu kama Quasars na Blackholes ambazo hizi zilipelekea uzalishaji wa mwanga.

QUASARS NA BLACKHOLES NI NINI?

Quasars ni vitu vikubwa sana vinavyoangaza sana huko katika ulimwengu. quasars zina ukubwa zaidi ya ukubwa wa nyota nyingi. na zina nguvu ya mvuto wa gravitation ya ajabu. Quasars ndani yake kuna ma Blackholes. BLACKHOLES ni matundu makubwa sana yanayokuwa meusi kweli kweli, matundu haya makubwa sana katika ulimwengu, yana aminiwa kuundwa pale ambapo Nyota inaishiwa Nguvu ya kuendelea kuwepo. Iko hivi, kuna kuwa na yale matendo ya nyuklia yanayofanyika ndani ya nyota ‘’Nuclear Fusion’’. haya huwa yakibalansi nishati ya nyota, sasa inapofikia Mafuta au nishati ya nyota inaishia basi hupasuka. ni kama unaposhindwa kuogelea juu ya maji. basi utatumbukia ndani ya maji na kuyeyuka, au kuongeza nishati ya maji. Hivyo hivyo Nyota inapoishiwa nguvu, hupasuka na kubakisha mabaki. sasa Black Holes huanzia hapa, uwingi mkubwa sana wa mabaki au matter ndogondogo, huwa katika sehemu ndogo sana. hii ni kama ambavyo unaona simenti ‘’cement’’ ni nzito kuliko pumba ya ujazo ule ule, kwa kuwa, cement ina matter nyingi Zaidi ukilinganisha na pumba Ambayo, chembechembe zake zina ujazo mkubwa, na kupelekea kuwa chache. Hiyo inaitwa ‘’Density’’. 

Black Holes huwa na density kubwa sana. na kwa sababu kani ya mvutano ya Gravitation huongezeka uzito unapoongezeka. basi kani ya mvutano ndani ya Black Holes huwa kubwa sana. Gravitation huwa kubwa kiasi kuwa hata mwanga nao huwa kama unavutwa. na ndiyo maana huwa zikionekana Nyeusi. Kitu kikikaribia Black Holes, huvutwa sana na kikaminywa na kikapotea kabisa. Uwepo wa Black Holes hupelekea vitu kama sayari, au hata nyota, au kitu chochote cha karibu, kuvutwa na kuminywa, na kupelekea kuzalisha Mwanga. siku zote kitu unapokiminya kwa presha kubwa, kinapofikia kiwango cha atomu, mabadiliko ya nishati ya chembechembe za atomu huzalisha mwanga. 

Umakini mkubwa uwekwe hapa, hakuna sehemu ambayo nadharia hii imeonyesha kuwa kulikuwa na uumbaji wa sayari na nyota hapa! Hapa tunaona kuna uwepo wa Gravitation kubwa sana. Ambayo matokeo yake ni uwepo wa vitu kama Quasars na Black holes. ambazo hizi zinatosha kuunda mwanga wa siku ya Kwanza.

Pichani ni picha toka NASA/ESA baada ya kugundua Zaidi kuwa, kuna maji yaliyojikusanya yakiwa na ukubwa mara laki moja Zaidi ya jua letu. na kuna maji mara trilioni 140 zaidi ya bahari zetu. Taarifa hizi zimesambaa katika chaneli za sayansi ya anga. Ila muhimu ninachotaka itambulike ni kuwa, Quasars hizi, ndizo zilitoa mwanga siku ya kwanza, na tayari zina kila Ushahidi wa uwepo wake enzi za awali ya ulimwengu.

Mitazamo Ya Wengine Ya Mwanga Wa Siku Ya 1.

Wapo pia ambao hutumia nukuu za mafungu mengine kusema ya kuwa, Mungu mwenyewe alikuwa chanzo cha mwanga wa siku ya kwanza. Ni nzuri lakini inachangamoto kubwa sana, na pia inaleta shida katika baadhi ya maswali. Mfano mtu angejiuliza kwanini ajiambie yeye mwenyewe? Kwahiyo kabla alikuwa giza? Kwa hiyo fungu la nne alipotenga nuru na giza alijitenga yeye na uumbaji wake? 

Kwanini Kwa Mungu Hakuna Giza? 

Inafurahisha sana kuwa Binadamu tumesahau kuwa katika Giza zipo frequency za Mwanga. ila sisi macho yetu au seli za kuona ‘’Cone and Rod cells in Retina’’ haziwezi kuona vizuri, na hata kuna Wanyama wanaweza kuona vizuri usiku kuliko sisi. Hii itatusaidia kutambua Biblia ikiandika Giza, ni kwa ajili yetu sisi. ila sio Giza kwa Mungu.

Hitimisho

Hapa lazima tumshukuru Mungu kwa kutufunulia ukuu wa uumbaji wake, kupitia taaluma ya elimu ya anga na ulimwengu ‘’Cosmology na Astronomy’’. Ambazo zinatufunulia uelewa mpana sana wa uwezo wa utendaji wa Mungu. Na pia ukweli una Nguvu, ufahamu huu utatusaidia kujibu baadhi ya maswali kama

Mimea Ingewezaje Kukua Kabla Ya Mwanga Wa Jua?

Kutambua Quasars kunasaidia kujibu maswali haya. Ili usiongeze muujiza hapo tena wa kusema, Nuru ya Mungu yatosha kwa kila kitu, maana utaulizwa pia je frequency za Nuru ya Mungu ni kama za Jua, maana mmea hukua kwa frequency za Jua tu.

4. Mungu Akaiona Nuru Ya Kuwa Ni Njema; Mungu Akatenga Nuru Na Giza.

Mwanzo 1:4

Mungu akatenga Nuru na Giza katika Dunia. Hii moja kwa moja inamaanisha, Mungu akaweka dunia katika Mhimili wake. Ili, kutenganisha upande unaopata mwanga, na usiopata mwanga ‘’giza’.’ Tunapata maana moja kwa moja pia kwa kuunganisha uwepo wa zile Quasars, na Black Holes katika upande Fulani. kwa Lugha nyingine, Matter nyingi ambazo Mungu amekwisha ziumba, ziko katika mgandamizo mkubwa wa Gravitation. ambao huo pia unatusaidia kuelewa kwanini kuna ile mionzi ya awali kabisa, niliyo ielezea ya Cosmic Microwave Background. hii ni matokeo ya mgandamizo huu, ambao ulipelekea mwanga kutokea. mwanga ambao ndani ya matter za aina moja, ulipelekea Blackbody Radiation. kutokana na mwanga kujia akisi akisi ‘’multiple reflections’’. Tuendelee mbele tutaelewa Zaidi kwa maana hii pia, inatusaidia kutambua kuwa kwa nini Mungu atakapo ziachia Mbingu, zitatanuka ‘’Stretch’’ kama anavyo rudia rudia Daudi, katika hizo siku za mbele.

5. Mungu Akaiita Nuru Mchana Na Giza Akaliita Usiku. Ikawa Jioni Ikawa Asubuhi, Siku Moja Mwanzo 3:5

Hapa inatudhihirishia kuwa, spidi ya kujizungusha ya Dunia katika Mhimili wake, ni ile ile toka siku ya kwanza. Ijapokuwa mazingira ya siku ya kwanza, hayajawai fanana na ya siku zingine.

Mungu anaanzisha mfumo wa Kwanza kabisa wa Kalenda ya Dunia.  

Kwanini Siku Ianzie Jioni? 

Kwa mtazamo wangu kimantiki ya Kifizikia siku kuanzia jioni ni ishara ya kutambua kuwa, Mungu alianza uumbaji wake wa Ulimwengu uliokuwa katika Giza. Yako mengi ambayo tunaweza yazungumzia hapa. Mfano, kulikuwa kuna uwezekano wa Dunia kuwa katika spidi kubwa sana katika mhimili wake, hata iharibu uwezekano wa utendaji wa viumbe, au utulivu wa dunia kwa hapo mwanzo. pia kulikuwa kuna uwezekano wa uwepo wa mionzi ya mwanga hatarishi, lakini Mungu anaruhusu Nuru kwa Frequency Rafiki kabisa. Hebu tuendelee kuangalia mbele.

Hitimisho

Haileti mantiki kwangu kifizikia kuamini siku inaweza anza saa sita ya usiku, ili hali Jua linazama Jioni. Siku huanza Jioni kwa kuwa Jua linachomoza kati kati ya siku, na kuigawa sehemu mbili sawa. Kama siku ingeanza asubuhi, basi kiini cha siku kingekuwa ni Giza au Usiku, kitu ambacho kisingeleta mantiki.

To be continued....