UTAALAMU WA KUUNDA WAJINGA NA WAPUMBAVU
UTAALAMU WA KUUNDA WAJINGA NA WAPUMBAVU
Shoo-Hypothesis
Watu wengi wajaze kwenye eneo dogo la ardhi. Mfano, je unajua kuwa asilimia 90% ya watu wote wa duniani wanaishi kwenye asilimia karibia 20% tu ya ardhi. Na hapo zaidi ya nusu ya watu wote wanaishi kwenye asilimia 5% tu ya ardhi. Bado asilimia 90% ya watu wanaishi kanda za kaskazini, na 10% kanda za kusini. Pia 2/3 ya watu wanaishi kando za Bahari, karibia maili 300 kutoka kwenye pwani. Na pia karibia na maziwa. Hii inapelekea watu wachache sana kwenye nyanda za juu, na kupungua watu sana maeneo ya vijijini. na maeneo ya kusini ya dunia. Sehemu kubwa ya dunia haina watu, ingawa hilo unaweza fichwa ila hata bila kuambiwa linaonekana.
Toka zamani sana, inaonekana kuwepo kwa watu wachache sana maeneo kama ya Afrika, na Marekani, ukilinganisha na Asia, Ulaya, na kaskazini mwa Afrika. Sasa basi, ukishawajaza watu wengi katika eneo dogo. moja kwa moja ni rahisi kuwatawala. kwa sababu utatoa huduma za umma, ambazo zitawahitaji kuendelea kuwepo katika eneo hilo hilo dogo. mfano, weka hospitali, taasisi za elimu, masoko, vituo vya burudani n.k, ukiwa unajua watu wanapokuwa wengi, kutokana na uchache wa maliasili na malighafi, dhiki lazima itaongezeka, au milipuko ya tabia hatarishi, kama wizi, ujambazi, ubakaji n.k. hii ni kwa kuwa, kila gharama za upatikanaji wa mali unapokuwa mgumu, watu hufikiria njia zisizo halali.
weka vyombo vya dola. Kama majeshi, polisi, mahakama n.k, usiishie hapo. pale watu wanapokuwa wanataka kuepuka hiki kifungo cha siri, wawekee vipingamizi. Mfano waite ni wahatarishi wa mazingira, au maadui wa jamii. au imilikishe ardhi yote umma. ambapo ukijua wewe pekee, yaani serikali kuu ya watu wachache, ndiye mtakaye kuwa wamiliki wa kweli. kwa maana ndiye waamuzi wa mwisho. Zuia uhuru wa uundaji mbinu mpya za kuepuka dhiki, kupitia namna za kitaalamu kama elimu. mfano, tengeneza mfumo shindanishi wa elimu, na sio mfumo shirikishi. Mfano, badala ya wanadarasa kushirikiana kuwezesha malengo ya taaluma, wewe washindanishe ili afaulu mmoja. Tengeneza elimu Chongo, au elimu yenye jicho moja. Mfano, badala ya mtu kujifunza kutengeneza gari lote, ili siku moja atengeneze gari lake. wewe mfundishe kutengeneza matairi tu, au injini tu, ili aendelee kutegemea mfumo wako. na hivyo iwe kwenye taasisi zote. si za afya tu, bali hata za uchumi na siasa. haribu kabisa mfumo wa afya za watu hawa, kwa kuruhusu uhuru wa upatikanaji wa kila chakula, ambacho watu wangetaka kukisambaza kwa lengo la kuikimbia dhiki. mfano, ruhusu vyakula vya wanyama au mimea iliyotengenezwa kwa njia hatarishi za kijenetikia ‘’Genetic Modified Organisms’’, vyakula vilivyokaa muda mrefu, nyama zenye hatarishi ya madawa, n.k, ilihali ukijua kama ambavyo mwili ungeathirika, na ubongo wao ungeathirika.
Chochea ulevi kama namna pekee ya kuzikimbia dhiki. Mfano, badala ya mtu kushindwa kumudu kuwa na familia na kumpata mwanamke mzuri. basi mtengenezee video za ngono’’pornography’’, au badala ya kushindwa kuwa bingwa akiwa yeye binafsi, mtengenezee ‘’filamu, magemu na michezo’’. Badala ya mtu kujifunza akaelewa, mtengenezee ‘’chatGPT’’ ili asitumie kabisa akili. Ili hali ukijua watu wana hasira, na wanatamani kutukana hali za Maisha yanayowasibu, basi wewe hamasisha nyimbo za matusi na mabiti ya hasira, ambayo mtu angeimba na kujihisi anapambana na maisha yanayomsibu. huu ulevi wote kadri unavyozidi kuongezeka, ndivyo namna ambayo utegemezi wa akili yake mwenyewe unazidi kupotea. na upumbavu unazidi kumjaa. Watu hawa sasa hawatakuwa na uwezo tena wa kukupinga katika mfumo wako. na kitu pekee watakachokihitaji, ni kukusikiliza ili uwaleweshe zaidi. Na mwisho kabisa wadanganye kuwa matatizo yote yanatokana na Mungu wao aliyeyaruhusu, ili hali ukijua Mungu aliupiga vita sana ujinga na upumbavu.
Kwanini Baadhi Wanatamani Kuwatawala Wenzao?
Kwa sababu ni wajinga wasiojiamini. Kwa kawaida kisaikolojia mtu anaejisifia huwa hajiamini. na ndiyo maana anajielezea ili kuhakikisha kuwa mnamsikiliza, na kumtambua, ili mumuheshimu. hivyo hivyo watu wanaotaka kutawala wenzao hawawezi kujitawala wenyewe. Leo hii wafalme waliofanya mambo makubwa katika historia, hawakuwa na sera za kutawala sana. lakini watawala wengi wa sasa, ni watu ambao wamejaa tamaa ya kuwa juu, na kujiinua. Huku wakijidanganya ya kuwa, wana uwezo zaidi ya jamii wanayoitawala. wakijiona ni wazawa wa pekee. Watu hawa kuna wakati hujihisi wao ni miungu, kupitia kutoa lugha kama ‘’nita.’’ wakisahau hakuna wanachomiliki, ila waliwekwa kwa ajili ya kuongoza maliasili kwa upendo.
Kisayansi unapokuwa na nguvu nyingi sana, unapungukiwa uwezo au muda wa kufikiria. Ni kama ambavyo unapokuwa na nguvu sana, unafanya jambo kwa haraka sana, au kwa muda mdogo sana. hivyo basi unapopewa nguvu nyingi sana, basi ubongo wako unatoka kwenye yale mahitaji ya awali ya ntakula au ntalala wapi, au ntavaa nini, ubongo unaanza kuwaza namna ya kutengeneza furaha kwa kutawala. na hapo ndipo shida inapoanzia. Katika biblia kuna kisa cha mfalme Suleimani, ambaye baada ya kupata nguvu na utajiri mwingi, alifikia kiwango cha kuoa mpaka wanawake mamia kwa mamia. Sasa basi, haikupasa binadamu awe na mamlaka hiyo, na ili aipate basi alihitaji nidhamu kubwa sana.
Simulizi Ya Mayas, China Ya Kale Na Spartans
Hawa watu walikua na utaratibu wa ajabu sana. Kwanza ukianza na Mayas waliokuwa wakiishi marekani ya zamani sana. pamoja na wachina. Hawa kwao ili mtu awe kiongozi, alipewa elimu kubwa sana. na kipindi kile, viongozi walikuwa wanafundishwa sana, kuliko watu waliokuwa wanajishughulisha na mambo mengine. Wakiwa Watoto, walilelewa katika maisha magumu sana. Mfano, walivalishwa vibaya, walilala pabaya. walikula vyakula vibaya, na pia walitenganishwa na wanawake. ‘’incontinence and abstinence’’. hii ilikua ili kuwatengenezea mazingira ambayo, wanapokuwa wakubwa, wawe ni watu wenye kiasi, tena wasiopenda sifa na tamaa. na hii iliwasaidia kuunda falme zilizokuwa imara sana. katika zama zao, utaratibu huu uliigwa kwa maeneo mengi sana. na hata baadhi ya maaskofu wa katoliki , katika karne za 12, walikuwa wakiwa na malengo ya kuanzisha taaluma zitakazohusisha elimu ya jinsia moja tu. ili kuwaongezea uwezo wa kujizuia watoto. kwa hiyo kiongozi anahitaji uwezo mkubwa sana wa kujizuia. na hii ni falsafa kubwa sana kwa Buddha. ambao pia huamini kuweza kuzuia tamaa au hisia za ndani kabisa, ndiyo msingi mkubwa zaidi katika kufikia hali ya utauwa na uongozi bora. ila kwa viongozi hawa wa sasa, tamaa na sifa ndizo zinazowafanya kuwa wajinga zaidi na kujikuta hata wao wakitawaliwa tena.
Spartans Na Uwezo Wa Kujizuia.
Mwanajeshi wa spartan wa kigiriki, alianza kufundishwa tokea akiwa mdogo kupambana na hali ya udhaifu iliyo ndani yake. Pale unapokuwa mdhaifu mbele ya hisia zako, ndipo unapopaswa kupambana zaidi. Pale ambapo unakuwa mdhaifu sana wa hasira zako. au pale unapohisi unafikia mwisho. ndipo mwanzo wa hatua nyingine. Wanajeshi hawa wanapokuwa Watoto, hutolewa majumbani mwao, na kujitenga na makazi ya kuwafurahisha. na pia walijitenga na makundi rika yanayowafikirisha vijana mapenzi muda wote, au michezo ya kuwadhoofisha. Wao walifundishwa uzalendo hata pumzi yao ya mwisho, walifundishwa mwili na ubongo kama silaha kubwa zaidi vitani.
Natambua pia zipo falsafa nyingi ambazo spartans walifundishwa ambazo sio nzuri. na zilikuwa mwanzo wa falsafa nyingi kama za mashindano, ambayo leo hii ndiyo yamepamba moto hasa ya mipira na ngumi. wao ndiyo walikua waanzilishi wa Olimpiki. ambayo baadae ilifutwa na ufalme wa Rumi. Hasa ambao uliupokea ukristo, baada ya kuona michezo hii haimpendezi Mungu. ingawa ilikuja kurudishwa tena baadae hata leo hii. Cha muhimu ni kuwa, jamii yoyote ile ambayo ingefundishwa kujizuia, basi ingekuwa na mafanikio makubwa sana. maana akili ni uwezo wa kujizuia kutoacha kufikiria.
#siri iliyofichika
Ubongo mweusi unapaswa kutambua Kiini cha Ujinga, ‘’maghorofa yashangaza lakini miti, mimea na maji haina maajabu’’. Kila mjinga duniani huona vitu vingi sana ni vya kawaida. yaani kichwani mwa mjinga kuna maajabu machache sana. Mjinga yoyote yule hashangazwi kwa maana kwake yeye vitu vipo tu jinsi vilivyo. na hakuna haja ya kujiangaisha kutafuta maana ya lolote lile, maana ili mradi hawezi kudhurika, kwanini ajitese kutafuta maana ya vitu ambavyo kwake huona havina msingi.
Hebu angalia mifano ifuatayo kugundua namna wengi hata wa walio wasomi pia wanaweza kuwa wajinga.
Kutopata hata walau muda wa kushangaa na kuona thamani ya hewa ya oksijeni, kwasababu tumezaliwa na tunaelekea kufa ipo tu! Hivi ni maajabu gani sayari dunia pekee kuwa na hewa ya oksijeni, tena katika asilimia maalumu ya 21%. Ambayo kama ingepungua tu, basi tusingeweza kuwa na maisha ya namna hii. au maji ambayo yanawezesha maisha ya kila kiumbe, au moto, au uwepo wa madini yanayoumba mifupa, miamba, mimea n.k, yapo mambo mengi ambayo mtu mwenye akili angeweza kuyatazama na kugundua kuwa yote ni maajabu, lakini mjinga atashangaa tu kuona akili yake ikichezewa na michezo ya kubuni, na stori za kutunga.
Mjinga hajawai kushangaa hata kuwa na macho yake tu mawili sio kitu cha kawaida. pamoja na asili kuruhusu wengine kuwa vipofu, vilema, na viziwi. lakini kwake mjinga, kuwa na masikio, pua au miguu, yeye hicho sio kitu cha kumtafakarisha. Hajui kuwa hata kamera anayoishangaa, inajaribu kuiga macho yake, na bado haija hata yakaribia. Kiukweli ujinga ni kitu hatari sana, maana kama ambavyo mtu angegawa dhahabu yake kwa jiwe, ndivyo hivyo hivyo mjinga mwenye ubongo wenye thamani kubwa ajabu, angeuza utu wake wote wa thamani ambao ni zawadi ya ubongo wake, kwa igizo la kompyuta dogo sana lililotengenezwa tena na ubongo wa mwenzake, ambao ni wa aina yake. Mjinga hashangai.
Hebu tazama namna dunia tu kati ya sayari zaidi ya trilioni milioni 200, kwa galaxy zaidi ya trilioni mbili, ndiyo tunaona mazao. tuna mazao ya chakula. ambayo tena yanafaa kwa chakula chetu, wanyama, wadudu na kutupatia hewa, makazi, mandhari, uzuri n.k hivi haya sio mambo ya kushangaza. Hebu tazama vizuri uone. Mjinga kwake atashangaa roketi ya mrusi au mkorea ikienda kuua, hatashangaa inzi jinsi anavyoweza kuruka, tena anavyoamua mwenyewe, hata shangaa namna ubongo wa binadamu ulivyoweza kufikiria hayo yote, na ilihali hauna nyaya, una nyama ambazo zikioza zinarudi kuwa kama udongo. Mjinga hashangai tai, au inzi wakiruka. kwa sababu hao wapo tu kila siku, na sio kuwa kwa sababu anawaelewa. Inaumiza sana namna ujinga unavyokuwa na nguvu sana, ujinga ni kama uozo wa ubongo, hebu angalia namna maendeleo makubwa yote ya sayansi na teknolojia, yameanzia katika kuangalia vitu vya kawaida kabisa.
Simulizi Fupi Ya Sir. Isaac Newton
Huyu bwana inaaminika utafiti wake ulianzia katika kujiuliza kwanini Tunda linaanguka, na pia akaangalia mwezi, akaona ni kama unafuata tabia ile ile ya kuanguka, kufuata usawa wa dunia. na huo ukawa mwanzo wa ugunduzi wa kani ya mvutano ya gravitation. Hakuishia hapo, akawa akiushangaa mwanga namna unaweza tawanyika na kuunda rangi saba, na akagundua sheria nyingi za
mianga’’optics’’. Akawa akijiuliza kuhusu namna vitu vinavyotembea, na kusimama. akagundua sheria nyingi sana za mwendo. Hakuishia hapo, akajiuliza hivi kuna nini hasa nyuma ya mfumo wa sayari na ulimwengu, na kisha akasema kuna mkono wa Mungu, unaoshikilia ulimwengu. pia alikua msomi mzuri sana wa kitabu cha danieli cha biblia. na hata baadhi hunukuu kuwa aliwahi kisia kuwa mwisho wa Dunia ni mwaka 2060. na aliwahi sema mpinga kristo ‘’antichrist’’ anaweza kuwa Papa wa Katoliki. unaweza rejea taarifa hizi toka vyanzo vingi mitandaoni na ukajithibitishia.
Pia inasemekana aliamini katika uwepo wa taasisi za siri zenye taarifa nyingi za siri ‘’alchemy’’. hizi alchemy zilikuwa ni sayansi zisizothibitishwa ‘’pseudoscience’’. mfano za kuamini labda maji yanaweza badilika kuwa waini ‘’wine’’. wengi huhisi kana kwamba kwa hapa alionesha udhaifu. lakini binafsi naona hiKo ndicho kiwango cha juu kabisa cha elimu. kiwango cha kujiuliza iweje iaminike duniani kote kuwa hivyo vitu vinawezekana. Iwe kwenye taasisi za siri, au vitabu vya Imani. shida ni kuwa hakufanikiwa kugundua. na mpaka leo hazifahamiki taaluma nyuma ya matendo haya, yaliyo katika group la parapsychology. mfano ‘’telepathy’’. hii mfano ni pale unapomuwaza mtu, naye anakuwaza. au ‘’telekinesis’’, yaani unainua kitu bila kukishika’’. binafsi sisemi kuwa hizo taaluma zina msingi unaoweza elezeka kirahisi. Nipo katika kundi la kusema bado hatujui. Alchemy pia ilikuwa msingi wa masomo ya Chemistry, na hata kwa jina unaweza ona yakifanana. yapo mengi ambayo bado hatuyajui kumhusu lakini cha muhimu natamani ubongo mweusi utambue kuwa vitu ambavyo sisi tunaviona vya kawaida, ndivyo vitu ambavyo huleta mabadiliko makubwa sana.
Ujinga kwa kifupi ni ukosefu wa maarifa. Watu wengi huchanganya maana ya maneno ujinga na upumbavu. Na kuna kipindi neno ujinga hutumiwa kumaanisha upumbavu. Ujinga humaanisha giza au kukosa maarifa juu ya jambo fulani. Kila mtu ana kiwango cha ujinga, ingawa tumetofautiana katika hicho kiwango.
Mfano katika shati ulilovaa, unaweza jiuliza baadhi ya maswali kama haya, ili kujijua je ujinga wako uko kwa kiwango gani? je shati lako limetengenezwa na nani? limesafirishwaje mpaka kukufikia? limeundwa na nini? nani aliyelidisaini? nini kilichounda shati lako mfano ukifikia kiwango cha atomu? Atomu zake zimeundwa na nini? kama ni chembe za atomu, elektroni, protoni, na nyutroni je zimeundwa na nini? na kama ni chembechembe ndogo zaidi za quarks za juu, na chini na gluon au leptoni zimeundwa na nini? kama ni chembechembe ndogo kabisa zinazobadilika badilika za higgs bosoni nani kaziunda? Kama ni ndogo ndogo zaidi za Pions zimetoka wapi? kama ni mithili ya miale midogo kabisa inayo vibrate inayoitwa quantum field zones nani kaiunda? Nani aliyedisaini elementi za vilivyounda kampaundi za shati lako?
huo ni mfano mdogo unaoonesha jinsi mtu asiyemtaalamu wa sayansi, labda angeweza ishia juu kabisa kwa kutojua mambo yanayohusu sayansi ya shati! Lakini pia, mwanasayansi naye asingejua mengi kuhusiana na taarifa za nje, kama biashara, dizaini, fashion, gharama, viwanda, uzalishaji, n.k. Kila mtu ni mjinga. lakini katika hii mada tutajifunza ni kwa namna gani ujinga unaweza leta madhara makubwa sana yanayo igharimu dunia nzima.
To be continued..






Join the conversation