Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SAYANSI YA GHARIKA KUU ILIYOIBADILI DUNIA

SAYANSI YA GHARIKA KUU ILIYOIBADILI DUNIA

SAYANSI YA GHARIKA KUU ILIYOIBADILI DUNIA

‘’great global catastrophic flood science’’


Utangulizi

Historia Fupi Ya Dunia Ya Awali

Kama nilivyoelezea awali kwa ufupi Dunia ya awali ilikuwa na sifa kadhaa ambazo ziliifanya iwe na ubora mkubwa Zaidi, na kuwezesha Maisha kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na ya sasa. Dunia ya awali ilikuwa na sifa zifuatazo; 

Ilikuwa ni kubwa ukilinganisha na dunia ya sasa. Mabadiliko ambayo tutaenda kuyaona yamesababisha kupungua kwa kiwango cha ukubwa wa dunia kwa ukubwa sana. Haikuwa na Milima mirefu kama hii ya leo, milima mirefu tutaenda kuiangalia kama matokeo ya tutakachojifunza hapa. Haikuwa na mito yenye kina kirefu kama hii mito ya leo. Haikuwa na majangwa, kama majangwa makubwa yaliyotapakaa katika dunia ya leo. Haikuwa na mabara yaliyotengana, kama mabara ya dunia hivi leo. Haikuwa na Volcano kama zilivyo hivi leo. Haikuwa na madini ya mionzi ‘’Radioactive minerals’’. Haikuwa na mabara ya barafu katika miisho ya dunia ‘’earth’s poles, yaani Arctic and Antarctic’’

Ilikuwa na misitu mingi na mimea mingi sana ukilinganisha na ya leo. Ilikuwa na Wanyama wengi, ambao wengi wamepotea au kupungua katika zama hizi. Haikuwa na viwango vya usumaku ‘’earth’s magnetic field’’ kama huu usumaku wa dunia ya leo. Haikuwa na Bahari kama bahari za hivi leo. Haikuwa na vyanzo vya maji ya chumvi, kama bahari za hivi leo. Haikuwa na kiwango cha aina ya kaboni-14 kama iliyopo hivi leo. Haikuwa na spidi ya mzunguko kubwa kama ya dunia ya hivi leo.

ilikamilisha mzunguko wa mwaka kwa siku 360, na sio 365.242 kama hivi leo. ilikamalisha mzunguko wa mwezi kwa siku 30, na sio 29.53 kama hivi leo. Viumbe wake walikuwa ni wakubwa sana kimaumbile, na sio wadogo kama hivi leo. Idadi kubwa ya Wanyama walikula nyasi, na sio nyama kama hivi leo. Kiwango cha joto kilikuwa chini ukilinganisha na hali ya joto ya leo. Hakukuwa na upepo wa kasi kama upepo wa hivi leo. Haikuwa na miamba ya lava ‘’sedimentary, metarmophics na igneous’’ kwa wingi wa miamba ya leo. Hakukuwa na mabaki au migodi ya makaa ya mawe kama hivi leo. Hakukuwa na mabaki ya Wanyama katika ardhi kama hivi leo. Hakukuwa na mafungu ya miamba ya madini kama ya hivi leo ’’mineral ores’’. Hakukuwa na matetemeko ya ardhi. Kulikuwa na kiwango kikubwa sana cha maji yaliyo chini ya ardhi ukilinganisha na leo.

Kulikuwa na uwingi wa Wanyama aina za Dinoso ‘’Dinasaurs’’. Hakukuwa na miamba ya chokaa’’limestones’’ kama hivi leo. Hakukuwa na sayari mikia katika anga ‘’comets’’. Hakukuwa na vimondo vinavyoitwa ‘’meteors’’. Hakukuwa na sayari ndogo zinazoitwa ‘’asteroids’’. Hakukuwa na sayari ya Pluto. Hakukuwa na mithili ya visayari vidogo vingi ‘’Trans Neptunian objects’’. Hakukuwa na mashimo ‘’crater’’ katika mwezi. Hakukuwa na sayari zinazozungukwa na pete kama Jupita

Hakukuwa na mashimo na milima kwenye bahari. Hakukuwa na mabonde ya ufa. Hakukuwa na miezi midogo inayozunguka sayari ndogo kama pluto, na sayari ndogo asteroid. Hakukuwa na miamba mikubwa kando ya maziwa, kama ya mji wa mwanza, miamba katika milima, vilele vya miamba, na aina hii ya ardhi. Hakukuwa na mabonde makubwa, na mashimo kama ya Isimila, au Grand Canyon, ambayo yako katika maajabu makuu ya dunia. hakukuwepo na chemchemi za maji moto.

Hakukwepo na matabaka ya ardhi, au milima ya matabaka ya ardhi na miamba. hakukuwa na aina za milima ya ‘’block mountains’’, wala plateus na aina zake. Hakukuwa na mvua kama nilivyoeleza awali. Hakukuwa na sehemu zenye mabarafu kama visiwa vya Iceland, Canada na sehemu nyingi. Hakukuwa na tofauti kubwa za viumbe zilizosababishwa na mabadiliko ya hali ya nchi. Viumbe waliishi kwa miaka mingi Zaidi duniani ’’long lifespans’’. Viumbe walikuwa na nguvu sana kutokana na mazingira yao.

Hakukuwa na uwingi wa magonjwa ya parasaiti kutokana na stability ya ecosystem, uchache wa vichochezi vya mabadiliko ya kijenetikia, aina ya vyakula vya mimea, pamoja na aina ya dawa za asili. Pia ukubwa wa dunia ungepunguza msongamano wa usambaaji. Uwezo wa tabaka la ozone ulikuwa mkubwa na ulipelekea upungufu wa mionzi hatarishi. Uwezo wa kiakili wa viumbe ulikuwa mkubwa, kutokana na uchache wa ‘’mental stressors’’ kama vile vyakula, dhiki, mazingira na mahusiano ya kijamii.

Teknolojia za kivita na za utatuzi wa dhiki zilikuwa chini kutokana na uchache wa migogoro ya kidhiki, na ya kimazingira. Dhiki zilizongezeka hasa baada ya maeneo zalishi ya dunia kupunguzwa na Bahari, na majangwa, na misitu isiyorafiki, na hata hatari za magonjwa. Uzalianaji wa viumbe ulikuwa mkubwa kutokana na urefu wa muda wa kuishi, vyakula bora, na mazingira Rafiki. Uwezo mkubwa wa ubongo ulipunguza uhitaji wa aina za rekodi kama maandishi, hii ni sababu ya ukosekanaji wa mabaki ya vitunza rekodi.

Utangulizi Na Ushauri Kwa Mwanafunzi

Miongoni mwa kisio bora Zaidi la kisayansi kuhusu ulimwengu wa awali ni kuwa, ulikua na uhusiano mkubwa Zaidi na miungu au Mungu. Hii ndiyo iliyopelekea kila jamii ya awali kuwa na msingi wa kiimani. na kila Imani iliamini katika mwanzo wa uumbaji wa Mungu. Hii inathibitisha kuwa, mwanzo kabisa watu hawakuwa wakiakimi uwepo wa Mungu, ila walikuwa wakijua kuwa yupo Mungu. Yaani ni kama wewe msomaji, huna Imani kuwa mimi nipo, ila unajua mimi mwandishi nipo. mtazamo wa kuwa na mashaka na uwepo wa Mungu ulianza karibia na miaka ya 2000’s. namaanisha kuanzia miaka ya 1900’s kwa nchi za kikomunisti, na kisha hiyo ajenda kuchukuliwa na nchi za kibepari, yaani magharibu na Amerika. Dunia itaendelea kumkubuka Tsar Nicholas II kama viongozi wa mwisho waliotetea msimamo wa Imani na elimu katika nguvu kubwa ya kiutawala duniani, kabla haijapinduliwa Russia na Vladmir Lenin aliyekuwa na falsafa za Marxism ambazo hazikuwa zikipinga uwepo wa Mungu tu, bali zikimchukia Mungu kwa ujumla. na kadri pia kulivyokuwa na nguvu za Elimu na falsafa ya Humanism ‘’Uhuru na uungu wa kila mtu’’ kwa maeneo ya marekani, basi hawa wakishirikiana na nadharia za Darwin na Wallace za miaka ya 1900 kasoro, yaani kuanzia 1859 nakuendelea. walipelekea mwaka 1900 kuwa mwaka wa elimu ya upinga kristo Zaidi, maana pia nadharia za Big Bang zikaanza. 

Msomaji ujue kuwa kabla ya 1800 hakuna mjadala uliokuwepo juu ya uwepo wa Mungu, ilikuwa inafahamika tu. yaani labda uwe mpagani wa kuamini miungu ila sio mpumbavu wa kusema hakuna Mungu. na sio tu kila chuo walifundisha Teolojia, bali vyuo vyote vikubwa vya awali kama Oxford na Cambridge, vilikuwa vimeanzishwa na maaskofu waliokuwa wasomi Zaidi wa zama hizo. na sayansi kwa ujumla ilitoka mikononi mwa watu wa Imani. na ndiyo maana utakuta Newton akikabidhi hatma ya Gravitation kwa mikono ya Mungu, ukimsema mtu kama James Maxwell, ambaye katika Fizikia kwa mchango mkubwa baada ya Newton, na Einstein, lazima umtaje yeye, maana analingana kimchango na hawa wawili, alikuwa ni mwaminifu mkubwa sana kwa Mungu. au Leibniz, Boyles, Mendel, Galilei, keppler na wengine wengi, wote walikuwa ni waaminifu wazuri. mfano pia ukizungumzia maendeleo ya Udaktari ‘’medicine’’ utazungumzia waislamu safi wengi kama Ibn Sina, Al Razi, na hata kabla ya Yesu (K.K), maarifa yote yalitambua nguvu ya Mungu, tangia enzi za kina Hippocrates, Galen, Socrate, Aristotle, n.k. ni kuwa tu mitazamo ya huyo Mungu ilitofautiana.

Kwa hiyo sasa, Mtu asimdanganye mtu mwingine kumwaminisha Imani ya Mungu sio kitu chenye Ushahidi, wala asimdanganye kuamini kuwa sio kitu chenye uhusiano na maarifa. na wala asimdanganye kuna uwezekano wa kutokuwepo kwa Mungu. Ila kikubwa Zaidi atambue kuwa, maarifa yanaweza kuwa yakiongezeka, lakini ujinga pia ukawa unapata nguvu.

Aina Mbili Za Kusoma Elimu Kubwa

Unapojifunza asili utambue kuwa kuna aina mbili za usomi. Kuna kusoma kuelewa undani, na upana wa maarifa, na ukayatumia. hii ni kama namna ya kusoma biolojia, jiografia, historia, lugha, sheria n.k na pili kuna namna ya kusoma ambayo unatengeneza msingi, kisha unaanza kuunda maarifa na kutengeneza upana wake. hii ni kama namna za kusoma fizikia, hisabati na Sanaa. Aina ya kwanza huwa hatarini zaidi kuwafanya watu kuwa na maarifa wasiyojua thamani yake, hii ni kusema, mtu hujua taarifa nyingi ambazo zimeundwa kwa taaluma kubwa, na yeye anazipata kirahisi kiasi cha kuathiriwa, na kuziona ni za kawaida. Mfano, mwanafunzi wa biolojia, huyu huona ni kawaida tu mzunguko wa enzyme ATPsynthase, au Flagella ya bakteria. vitu ambavyo huwezi linganisha hata na teknolojia za helikopta. Watu hawa husoma vitu vingi sana vilivyo na taaluma za ajabu, na aina yao ya usomi huwataka wawe kiutumishi Zaidi, wengi huwa bora sana kukariri taarifa, kuliko kuelewa na kujiuliza kuhusu hayo maarifa. Matokeo ni kuwa huwa na majibu bila maswali kiasi cha kutojua thamani ya majibu waliyonayo. aliyezaliwa katika nyumba bora, hawezi shangaa ubora wa nyumba. 

Aina ya pili ni kinyume, kwao kila kitu kinahitaji kutengenezwa kwa ugumu wa kufikiria, na malighafi. Hawa hujua thamani ya uumbaji kwa maana wanajua ilivyo ngumu kuumba. shida yao kubwa ni kuwa, huwa wana taarifa nyingi zilizo katika uwezo wa kibinadamu, taarifa zilizo rahisi, ila kwao huwa ni ngumu sana kutokana na kuwa hawajaona upande wa pili wa uumbaji wa asili. Watu hawa huwa katika hatari ya kulinganisha hata ubongo na matokeo yake(roboti). kutokana na kujua thamani yao hasa kwa jinsi ilivyo ngumu kuumba, huwa na nguvu sana katika jamii. lakini wale wenzao huwa wadhaifu kwa maana wanayo taaluma kubwa ila hawajui thamani yake. kipindi mwanafizikia Richard feynman anachukua Nobel Prize kwa kazi kubwa katika Quantum electrodynamics, alikuwa maarufu sana akimkaribia hata Einstein. lakini kipindi hiko hiko kina James Watson na Francis Crick walikuwa wamegundua DNA. nao pia walishinda Nobel Prize, lakini hawakuwa maarufu. kwa maana DNA ilikuwa ni kama kitu cha kawaida kwao. Uhalisia ni kuwa, kama umaarufu unatokana na Complexity ya gunduzi, basi Mungu alipaswa kupongezwa kila wakati kwa maana elimu za uhai zina maarifa makubwa sana. Unaweza jiuliza kwanini inakuwa kinyume, hata Artificial intelligence huonekana kuweza kuwa na thamani Zaidi ya ubongo uliyoitengeneza? Jibu ni kuwa, akili za watu zimeelekezwa katika hofu ya kifo kuliko nguvu ya Maisha. taaluma hata iwe kubwa vipi, kama haidhuru, hakuna anayeijali. taaluma hata iwe ya kawaida, ila kama hudhuru, Kila mtu huizingatia. taaluma kadhaa zilizotumika kuunda mabomu ya nyuklia zinaheshimiwa Zaidi ya taaluma ngumu Zaidi zilizotumika kuumba Maisha yenyewe. Siku zote ziko njia nyingi za kuharibu, ila iko njia moja tu ya kuumba. Unaweza vunja nyumba tokea juu, au chini, kwa moto, au maji, au bomu n.k ila kujenga utatumia malighafi zile zile za ujenzi tu, na huwezi jenga paa kabla ya msingi, maana haliwezi kuelea. Hata kuua unaweza ua kwa namna nyingi, ila huwezi kufufua Zaidi ya kuamini kwa damu ya Kristo aliyetufia msalabani. 

Msomi unapaswa kuwa makini katika kubalansi aina hizi mbili za kusoma, ili usione kawaida kwa lolote unalolijua, wala usilolijua. Usimheshimu sana anaetengeneza ‘’Iron Dome’’ mfumo wa kujikinga na makombola ya anga, ukasahau aliyeumba ubongo wake, eti tu kwa sababu maarifa ya ufanyaji kazi wa ubongo hayaui! ila maarifa madogo ya kutumia Laser na teknolojia nyingine za ulinzi yakifeli, watu watakufa!

Kumbuka hakuna elimu ngumu Zaidi ya nyingine! maana zote hujaa kwa ujazo ule ule katika ubongo, ila tu hutofautiana aina za kinachojazwa. Hakuna mwenye akili Zaidi ya mwingine, ila mazingira yetu na karne zetu zinatutofautisha. wengi wa walio na michango mingi mikubwa, wasingekuwa katika maeneo yao, familia zao, na hata zama zao, wasingekuwa vile walivyo. Miaka ya 1600 mpaka 1900, mtu mmoja angeweza soma taaluma zote kwa ndani ya miaka michache sana, au muda mchache sana, lakini zama za sasa kila uwanja ni mpana sana kuufikia mwisho. Na ni vigumu sana kuchangia usipojua wapi pamefikia. Vita ya uchumi tu ingeweza badili mtazamo wa elimu, toka kama sehemu ya maarifa na mapinduzi, mpaka kuwa tegemeo la uchumi wa kukidhi Maisha. nidhamu ingeweza mfanya mtu mmoja asione kabisa maana ya Maisha yake, na maarifa kwa ujumla. Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hii ina maana maarifa kwa ujumla. na ndiyo maana inasikitisha katika historia ya wanafizikia na wanasayansi wakubwa Zaidi, wenye asili ya kiyahudi, wengi wao walipata maabara, vitabu, na wakufunzi wazuri, ila walikosa Biblia, na kupatiwa Talmud’’. kitabu ambacho ni mbadala wa Biblia. Madhara yake ni kupata watu wenye michango mikubwa, lakini wasijue kabisa Mungu alikuwa wapi. na huu ndiyo mwanzo wa kupotea kabisa kwa maarifa ya kweli, na kuingia kwa sisi sote katika zama ngumu Zaidi kuwahi kutokea. Maisha ni akili narudia, akili inapopotea kama Richard feynman anavyoweza elezea hata alivyo lala na makahaba, au wake za marafiki zake, au akalewa kwa ulevi, na ni mfizikia wa kuigwa kwa kila msomi, akili imepotea katika kizazi chetu! na Maisha yanazidi kupotea, wenye nuru hii kidogo iwatoshe kuokoka katika uharibifu huu mkubwa wa maarifa, au Maisha. 

Historia Za Gharika Kuu

Historia inaonesha tangia falme za kwanza kabisa za jamii zilizostaarabika ‘’Civilized states’’. kulikuwa na taarifa za uwepo wa gharika au mafuriko makubwa ambayo yaliikumba dunia nzima, na kisha Kukawa na historia za uwepo wa shujaa ambaye aliokoka peke yake na familia yake katika hiyo gharika. Kuna Zaidi ya stori 200. katika hizo kuna utofauti lakini unaweza pata picha juu ya tukio hilo. Hizi ni Miongoni mwa hizo stori;

 Hawaii

‘’zamani sana baada ya kifo cha mtu wa kwanza kuniuhonna, dunia ilijawa na uovu na kuwa sehemu hatarishi kabisa. mtu mmoja tu mwema alibakia jina lake aliitwa Nu-u. alijenga Safina kubwa na ndani yake akajenga nyumba yake, akaweka Wanyama. Gharika kuu ikatokea na kuua watu wote na Nu-u tu na familia yake wakapona.’’

 China

‘’Fuhi, mke wake, watoto wake wakike watatu, na wakiume watatu, waliokoka gharika kuu. na walikuwa watu pekee waliopona katika dunia. Baada ya gharika wakaijaza tena dunia’’.

 Gilgamesh

Alikuwa mfalme wa Uruki katika falme za ‘’Sumaritans’’ kisha ikaja kutokea gharika kubwa na kuangamiza dunia na walipona watu wachache ikiwemo Enmekar, lugalbanda, 

Dumuzi(tammuz), Gilgamis na Ur Nungal. wasomi watafiti wa stori hii wamegundua inarejea katika tarehe zile zile za taarifa za stori za gharika ya nuu.

Mexico

Kuna makabila Zaidi ya 170, na yote yana stori za gharika iliyowahi ikumba dunia nzima, na akawepo shujaa mmoja aliyeponyeka. Mfano waazteki wana michoro inayomuonesha mwanaume mmoja, na mwanamke waliookoka gharika wakiwa ndani ya mti.

Canada

Kuna makabila Zaidi ya 20, na wote wana historia ya aina ya gharika kuu mfano, Wakrii ‘’cree’’ hawa husema. ‘’Mungu alileta gharika kwasababu watu walikuwa sio watiifu kabisa. lakini mtu mmoja mwema aliyeitwa ‘’WESAKECHA-wesaketchan’’ alijenga meli kubwa alilobeba familia yake na wanyama na ndege’’ na huendelea.

Ziwa Nuhu

Wakazi wa Sudani huku Afrika huliita ziwa Chadi ziwa la nuhu. ‘’Bornu baher el nuh’’. wao huamini gharika iliyo ishambulia dunia nzima ilianzia katika ziwa chadi.

Qur’an

Kitabu hiki cha Imani ya waislam kina stori ya gharika ya nuhu iliyoikumba dunia nzima. Na stori hii unaweza ipata katika Sura ‘’6 mstari wa 7 (Surah Al-A’raf) kwa mara ya kwanza, na pia katika sura ya 71 (Surah Nuh) kumbuka, Uislam una karibia asilimia 24% ya watu wa dunia nzima, hivyo ni idadi kubwa sana ya watu wanaoamini gharika hii.

Biblia

Biblia kama kitabu cha awali Zaidi cha historia ya mwanadamu, ndiyo msingi wa stori hii ya gharika ya nuhu. kwa kuwa imetoa taarifa nyingi ambazo zitasaidia katika kujifunza Zaidi kuhusu sayansi ya gharika hii ya nuhu.

Historia Katika Sayansi Ya Gharika Ya Nuhu

ukifatilia jamii za kwanza kabisa kustaarabika utaambiwa labda ‘’sumeritan’’ na kisha Misri ‘’Egypt’’. Wengi hunukuu zilikuwa karibia miaka 3000BC. Taarifa nyingi pia ukichunguza ni jamii zipi zilianzisha stori za gharika, utagundua ni jamii hizihizi za awali ‘’sumeritan myths’’, ukisoma Biblia pia si mbali na miaka hiyo hiyo kama 2000-3000BC ndipo gharika ya Nuhu ilitokea. Ukweli ni kuwa ndiyo maana taarifa tunazoweza zipata ni za jamii hizi tu, maana jamii za nyuma yake zilifukiwa. ila kwa kuwa hawa hawalitambui hili, wao wanaona kana kwamba hizi ndizo jamii za awali Zaidi kustaarabika. Sasa basi, kadri falme zilipokuwa zinaendelea, na jamii nyingi zinauvaa upagani, ule ubora wa stori ya gharika ukazidi kupungua, na kupotea. na hata kubakia aina ya stori ambazo zimepungua sana kitaarifa. Zama za ufalme wa kigiriki, jamii za dunia zilianza kukusanywa kijamii, na kielimu, na kuwezesha tena uwepo wa taarifa za aina moja kwa maeneo mengi. ila kutokana na upagani mkubwa, bado taarifa nyingi zilikuwa zimepungua, na hakuna aliyejali wala kuzingatia.

Katika zama za ufalme wa kirumi, ndipo Yesu Kristo alizaliwa na kurejesha Nguvu ya elimu ya Uumbaji. Na elimu hii ilisambaa sana kupitia dini ya kikristo, iliyotangaza watu kurejea tena kwa muumbaji wao. Sasa basi, Rumi haikusapoti ukristo hata kidogo, na iliupiga vita sana. Ila ilipofikia zama za miaka ya 256AD, ufalme wa Rumi ulivunjika katika pande mbili. na baadae, upande wa mashariki ambao ukiwa chini ya mfalme Constantine, uliiteua Dini ya Kikristo kuwa ndiyo dini ya ufalme wa kirumi mnamo miaka ya 306-337AD. Badiliko hili liliifanya dini ya kikristo kusambaa sana, ijapokuwa pia ilipitia mabadiliko baadhi yaliyopunguza asili yake, lakini kwa hapa tunaweza ona namna pia mafundisho ya stori za Nuhu yangeweza kuwafikia watu wengi Zaidi. Dini ya ukristo chini ya mitume, na wamishonari, ilisambazwa karibia maeneo yote ya Dunia. Ukristo haukuwahi tulia katika zama za wafalme tofauti tofauti wa kirumi. kuna kipindi ulipitia changamoto sana hata kuelekea kuzima, lakini pia kuna zama ulipata nguvu. na ndivyo mafundisho haya yalivyokuwa pia, Rumi ilipoanguka, na utawala wa Papa ulianza, ijapokuwa si kama falme, bali ni kama kitovu cha dini ya ukatoliki. ambao ulishikilia uongozi, na makao yake yalikuwa vatikani. na papa alikuwa na nguvu sana ya ushawishi kwa nchi majirani nyingi za ulaya, uwezo wake wa kutumia dini na kufanya uhusiano na mataifa ya ulaya, ulimwenzesha kufungua makanisa mengi ulaya. na Hata ilipofikia miaka ya 900-1200, vyuo vingi vilianza kujengwa. na elimu iliyotolewa, ilihusisha mafundisho yale ya gharika ya nuhu. Ulaya Zilipoanza karne za kumi na tano, Dunia ilianza kupitia mwanga mpya wa kimaarifa, na wasomi wengi waliongezeka duniani. na taaluma nyingi zilianza kuelekezwa katika kudadavua uhalisia wa stori, ili kujua kama ni za kweli, ama ni za kutunga. na hapa ndipo Biblia ilipoanza kusomwa kama kitabu cha maarifa yote ya kiimani, na kifalsafa, ama sayansi kwa wakati ule. Watu wangeuliza, je ni kweli dunia ni ya mviringo? Au je ni kweli jua laweza simama? Je ni jua au dunia inayozunguka kwa mwenzake? n.k. zama hizi zilianzisha vuguvugu la uhuru wa kifikra, na kielimu. na watu walihitaji kuhakikisha ukweli wao, na si tena kushurutishwa kushikilia mafundisho. Hata wanasayansi wa kwanza, wengi walikuwa wakristo wenye misimamo ya Uprostentanti, pia walikwepo wakatoliki, na hata wa dini zingine wachache. Dunia ilipitia mabadiliko makubwa sana, na wengi huiita ‘’Enlightment Age’’, yaani zama za kuanzia karne ya 18 nakuendelea. Bado falsafa za Imani ya uumbaji, na visa vya Biblia vilikuwa na nguvu. ila ilipofikia karne ya kumi na tisa kwenda ishirini, ndipo mabadiliko makubwa yalipoanza hata juu ya uwepo wa gharika kuu.

Taaluma za elimu nyingi zilianza kuzaliwa kuanzia karne ya 18, na ndiyo maana, utakuta watu kama Antoine-Lavoisier wakiitwa baba wa Chemistry au Boyle pia, na hawa wote walikuwa na Imani za kikristo, utakutana na mwanasayansi mmoja aliyeitwa Georges Cuvier, huyu huitwa Baba wa Palaentology na Comparative anatomy ‘’hii ni sayansi ya mabaki ya viumbe, na viungo vya miili ya Wanyama tofauti tofauti’’, huyu katika utafiti wake mkubwa katika miaka ya 1800’s, aligundua kuwa mabaki mengi yanaonyesha kuwa kulikuwa na Gharika moja Kuu au Tufani iliyosababisha vitu vifukiwe Pamoja, na kupelekea miamba, milima n.k, kuonekana hivi inavyooneekana leo. Na huyu Baba wa sayansi ya Palaentology na Anatomy, alikuwa mkristo mkubwa sana na hakuna aliyeweza mpinga Zaidi ya kumheshu sana.(pia mwanasayansi na sanaa Leonardo Da Vinci alikuwa anamchango mkubwa sana katika sayansi ya viungo ‘’anatomy’’, lakini pia alikuwa Mkristo mzuri sana). Mr Cuvier Alipokuwa katika dakika zake za mwisho hata kufa, mwaka 1832, ndipo mwanasayansi mwingine aliyepewa heshima ya Baba wa Geology ‘’sayansi ya miamba’’ alipokuja na gunduzi ya kuwa, mabadiliko ya hii dunia, ni matokeo ya mabadiliko madogo madogo ya muda mrefu ’’Uniformitarianism’’.

kumpinga mwenzake kulipelekea mabishano mengi kwa waliokwisha elewa sayansi iliyopita. Kadri hili vuguvugu likiendelea, maana tayari kulikuwa na sehemu mbili, yaani ya Uumbaji wa Ghafla wa Mungu, na mabadiliko ya ghafla ya gharika kwa wanasayansi wengi wa Imani, na uumbaji bila Mungu, na mabadiliko ya polepole. vuguvugu la kutokuwa na Mungu aliyeumba ghafla, liliendelea kukua Tangia enzi za mwanafalsafa maarufu sana ‘’Spinoza’’ wa miaka ya 1600’s, aliyechochea sana mpaka wanafizikia wengi wa karne ya 19 kukimbilia kutokuwepo kwa Mungu. Ukijumlisha na vuguvugu la mapinduzi ya karne ya 18 tokea mapinduzi ya marekani, ufaransa, Irish, spain, mpaka Russia, Kulichochea kukua sana kwa mapinduzi ya elimu. na hapa ndipo nguvu ilipoelekezwa kwa matukio ya polepole, sio tu kwa dunia, bali hata uumbaji. na nguvu kubwa ililetwa na Charles Darwin, na wenginewe kama Wallace, na familia ya Huxley. Mwaka 1900 uliingia kwa mapinduzi ya uumbaji, pia na nguvu kubwa kupitia sera za kikomunisti, na ubepari, ulioleta demokrasia hasi. Kama niliovyoelezea awali, migogoro ya kivita nayo, maana ulaya haikuwahi pitia kipindi cha amani, tengano za kifamilia, vifo kama milipuko ya magonjwa, na ukosefu wa amani, ilipelekea watu wengi kukimbilia mabadiliko ya kuwa hakuna Mungu bila hata kujua.

maendeleo ya fizikia na hisabati ilikuwa ndiyo kiberiti kikubwa Zaidi. Baada ya miaka ya 1900 mwanzoni, dunia ilirudi katika giza tena la maarifa. na hapo ndipo vikundi vya watu wachache wachache walioelimika kwa sayansi na Biblia wakaanza tena kurejesha nuru ya elimu hii iliyopotea, ijapokuwa haina nguvu kama awali, lakini ina nguvu katika vichwa vya wenye uelewa.

Wapo waasisi wengi kama vile Dr. Henry Morris aliyeanzisha Institute of Creation Research ‘’taasisi ya sayansi ya uumbaji’’, Ken Ham aliyeanzisha ‘’Answers in Genesis’’ yaani Majibu katika kitabu cha mwanzo, Creation Ministries International CMI’’, Community of Creation Society CSC’’ iliyo anzishwa na Dr.Walter Brown, Creation Science Evangelism iliyoanzishwa na Kent Hovind, Injili ya Sayansi iliyoanzishwa na Dr. Brighton Shoo, zipo pia nyingine kama ‘’Intelligent Design’’ ingawa hizi huwa ni za mashaka, maana hutumia uhitaji wa elimu kwa lengo la kiuchumi, na hazijakubali kushikilia ukweli moja kwa moja. Pongezi kubwa huenda kwa waasisi wa Kanisa la Kiadventista Wasabato, ambao kwa mujibu wa Wikipedia inawataja kama waanzilishi wakubwa wa sayansi ya uumbaji wa siku sita wa Mungu. wakimtambua Ellen G.White na bwana George McCready Price, alieanzisha kwa mara ya kwanza nadharia ya gharika kutoka sayansi ya miamba ‘’flood geology’’ ambapo haikuwa na nguvu sana. ila baada ya kifo chake, ndipo ilipopata nguvu hata kuwafikia kina Dr. Henry Morris, na wengine. pia wako waliohamasishwa na nadharia hii ya sayansi ya uumbaji kwa baadae, ikiwemo kanisa la Baptist kupitia wakufunzi kama Dr. Kent Hovind n.k. lakini kumbuka hakuna mwanasayansi wa aina hii asiyepigwa vita na taasisi za dunia.

To be continued...