Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

GHARIKA NA MADINI YA MIONZI

Gharika ya Nuhu na Madini ya Mionzi

 Nuclear Power Na Asili Ya Madini Ya Mionzi ‘’Earth’s Radioactivity’’

Miongoni mwa vitu vinavyochanganya sana wasomi wawe wa sayansi ya Biblia, au hata sayansi ya mabadiliko ya muda mrefu, ni madini ya mionzi ‘’radioactive minerals’’. Madini haya huleta changamoto kubwa sana hasa kutokana na kukosekana kwa nadharia ya kuweza kuelezea asili yake. na kinachotokea, madini haya hutumika kutafuta muda au umri wa vitu duniani, na hiyo ni miongoni mwa sababu za watu kukwambia kuwa labda kitu Fulani kina umri wa miaka kadhaa duniani, na kingine miaka kadhaa, sasa hebu tuangalie kiundani.

Chanzo Cha Madini Ya Mionzi Na Mionzi Duniani ‘’Mtazamo Wa Evolution’’

Hawa huamini katika nadharia ile ile niliyoielezea awali kuwa, miaka mingi ya milipuko ya nyota ‘’supernovae’’ ilikuwa ikisambaza kiwango cha madini katika sayari. Na kwa hivyo, madini ya mionzi kama vile ‘’uranium’’ n.k yote yanatokana na chimbuko ambalo ni milipuko ya nyota. 

Sasa shida kubwa ya hizi nadharia ni kuwa, basi tulitegemea kiwango hiki kisambae kila sehemu kwa kiwango kilekile katika dunia, lakini maajabu yake utakuta viwango hivi vimetofautiana kati ya sehemu na sehemu katika dunia. Na sababu nyingine kubwa sana, ni namna gani nyota zingeweza kuunda elementi hizi za mionzi ambazo ni nzito sana, na zinahitaji nishati kubwa sana. Ambayo hailingani na uhalisia wa milinganyo ya nishati ya uundaji wa nyota.

Utawezaje kuelezea uwepo wa madini mengi ya mionzi katikati ya tabaka la juu la dunia ‘’earth’s crust’’, na tabaka la chini ‘’mantle’’. na sio sehemu zingine kama vile ndani ya dunia ‘’earth’s core’’. Mwisho haya madini huwa yana spidi maalumu ya kuisha ‘’halflife’’, Ambao huo ni muda nusu ya dini litapungua. Sasa basi, kutokana na spidi yake, mengi yalitakiwa yawe yameshaisha duniani kama dunia ilikuwa na umri wa miaka bilioni 4.5 kama wanavyo amini. Hii ni sawa na kusema, mshumaa wa mita moja hupungua nusu kila baada ya lisaa limoja, hivyo basi baada ya masaa kumi, huo mshumaa utagundua kuwa utakuwa umeisha kabisa. sasa basi iweje spidi za kuisha kwa madini haya hazilingani na uwepo wake.

Chanzo Cha Madini Ya Mionzi Na Mionzi Duniani ‘’Gharika Kuu’’

Maji ya ‘’supercritical water’’ yalipokuwa kule ndani ya miamba ya dunia yalikuwa katika mgandamizo wa nishati kubwa sana. hasa kutokana na joto na presha kubwa sana. Kadri miamba ilipozidi kuisha, na kuongeza mgandamizo juu ya tabaka hili la maji, maji mengi yalikuwa yakiingia katika tabaka la chini la miamba ya dunia. Hii ni kama kusema ukikalia maji, maji mengi yataingia ndani ya nguo zako. Hivyo hivyo maji haya yaliingia katika vishimo vingi sana vya tabaka la chini la nchi. Nishati ya maji ya scw ilikuwa ni kubwa sana kiasi cha kuanza kuunda ‘’Plasma’’ katika sehemu za chini ya tabaka na ndani ya miamba ya nchi. Kama nilivyoelezea awali kabisa kuhusu Plasma, kuwa huwa ni aina nyingine ya matter, ambayo atomu zake ziko free kutokana na nishati kubwa sana. 

Sasa basi kipindi cha Gharika, kadri maji yalipokuwa yakitoka kwa spidi kubwa sana kuelekea angani, na mengine kurudi kama mvua. Basi chukulia mfano wa ulimi wako ukipuliza uluzi wa 

‘’Prrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!’’ utagundua kadri upepo unavyopita unasababisha vibration ya ulimi wako. na hata ungefanya kama Watoto ‘’papapapapapaap!!!’’ utagundua kuwa, kila upepo unapotoka, husababisha vibration ya mdomo. Hivyo hivyo kadri maji ya supercritical water yalipokuwa yakitoka katika mpasuko wa atlantiki iliyokuwa imejiachia mithili ya mdomo, ilipelekea tabaka la nchi ku vibrate. hiki kitendo kinachoitwa ‘’Fluttering of earth’s crust’’, hiki kilipelekea miamba ya nchi kuwa kama Kamba za gitaa ukizipiga zinavo ‘’vibrate’’. Hizi vibrations zilipelekea kuzalishwa kwa umeme kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Piezoelectric effects’’. huu umeme mkubwa sana ambao ulizalishwa kutokana na vibration za tabaka la nchi, ulipofikia maeneo yenye Plasma, basi ulisababisha kuzalishwa kwa haya madini. Hapa ipo hivi, Plasma ikikutana na umeme mkubwa sana, inapelekea kuzalishwa kwa madini kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Z-PINCH’’. hiki ni kitendo ambacho kimegunduliwa katika zama hizi za karibu. Unaweza rejea utafiti uliofanywa na watafiti katika Proton-21 Laboratory Electrodynamics experiment’’. hapo kinachotokea ni kuwa, umeme mkubwa unaoambatana na kani ya usumaku, au ‘’magnetic field’’. husabababisha atomu ambazo huwa zikisukumana zisiungane, yaani chanya husukuma chanya hata nyuklia mbili za atomu zisiungane kupitia ‘’coulumb force’’. Sasa katika mazingira yenye kani kubwa ya mvutano, hizi nyuklia huweza kuungana. na uwingi wa plasma husababisha madini mengi mazito ‘’heavy elements’’ ya aina tofauti tofauti kuweza kuundwa. Lakini pia, iko namna nyingine ambayo inaweza sababisha madini mazito kama ya mionzi kuweza kuundwa, huwa inaitwa ‘’shock collapse’’. hiki ni kitendo kama cha kusema ukiziminya sana spring mbili, ukijaziachia zinaweza jipiga hata zikaungana. na ndivyo ilivyokuwa pia kwa plasma ambazo zilikuwa katika kani kubwa ya mgandamizo, au compression na kupelekea baadae kuungana kupitia ‘’Nuclear fusion’’ hata kuunda elementi nzito. Lakini pia huwa kuna kitendo kinaitwa ‘’Electron Capture’’. hii hutokea pale ambapo umeme mkubwa na usumaku ulipelekea maelfu ya electron kusukumwa kwa kasi hata ndani ya nyuklia na kuungana na protoni na kuunda neutrons, ambazo hizi zilichochea Zaidi milipuko kupitia ‘’chain reaction’’.

Elementi hizi nzito huwa na kiwango kikubwa sana cha Protoni ambazo huifanya nyuklia kutokuwa imara ‘’unstable’’. na hali hiyo hupelekea nyuklia kuanza kutoa mionzi, kama matokeo ya nyuklia kuelekea katika hali yake ya uimara tena. Kitendo hiki cha elementi hizi kurejea katika hali ya uimara, huzalisha nishati mithili ya mabomu ya nyuklia, au hydrogen bombs kama nilivyoelezea awali. Kwa hiyo sasa jibu la swali la maji yalipata wapi nishati, tungeweza anza kujibu kupitia nadharia hii yenye Ushahidi.

Ushahidi Wa Michirizi Katika Miamba ‘’Lineaments’’

Miamba kadhaa huwa na michirizi inayoitwa ‘’Lineaments’’. hii ni ishara ya kile kitendo cha fluttering, yaani kinaonyesha kuwa, miamba ya nchi ili vibrate. angalia picha ifuatayo.

Ushahidi Wa Madoa Ya Polonium Katika Miamba Ya Granite

Hii inaitwa ‘’Polonium Halos’’, ni miongoni mwa vitu ambavyo hata wanasayansi wa evolution wenyewe hukiri kuwa hawaelewi. kwa msaada mkubwa sana wa Geologist Dr. Robert Gentry tumeweza elewa haya. Madini ya Uranium (²³⁸U na ²³⁵U) huwa yakizalisha mionzi na kubadilika kuwa madini ya aina mbalimbali mpaka kufikia madini ya Lead ‘’Pb’’. Kwa hiyo kama utaona madini ya Lead, unaweza kisia kuwa kulikuwa na madini ya Uranium huko zamani ambayo yalivunjika. Sasa haya madini huwa yanatabia kama nilivyoelezea awali ya kuvunjika au kuisha kwa kuzalisha mionzi. mfano mzuri wa namna yanavyoisha, ni kama ambavyo yale mafataki huwa yakiisha. Kama ukiona madini ya uranium kwenye mwamba, basi utaona mpangilio wa madoa ya mlipuko tokea ndani mpaka nje yakiwa yametengeneza maringi. hii huashiria kuwa kulikuwa na milipuko ya kuisha kwa madini ya uranium. Hebu tazama hapa .

changamoto kubwa Zaidi ni kwa madoa ya polonium, (Po)‘’polonium halos’’. polonium kama unavyoiona hapo juu ni miongoni mwa madini yaliyo chini ya uranium. na yalipaswa kama yapo katika miamba, yawe katika maringi na wenziwe, ila yenyewe huonekana peke yake. hili limeleta changamoto hata kwa wanasayansi wa uumbaji wa muda mfupi ‘’young earth creationists’’, kwa baadhi yao kuamini miamba ya granite ambayo imekuwa na madoa ya madini haya kuwa yaliumbwa yakiwa na polonium kitu ambacho kinaleta changamoto zaidi. 

Maelezo rahisi Zaidi ni kuwa, kadri madini ya uranium yalivyokuwa yakibadilika, matokeo au products zake zilikuwa zikibebwa kwa kusafirishwa na maji ‘’SCW’’ yakipanda katika chaneli kadhaa, na kadri muda unavyozidi Kwenda, na products hizi ziliendelea kubadilika zikiunda madini kadhaa wa kadha, stori ya polonium inaanza na madini ya Radon (²²²Rn). ambayo haya yana half-life ndogo sana, na sasa, haya madini hayana tabia za kuungana na mengine ‘’Inert’’ hivyo yaliyeyuka katika scw na kubebwa yakipanda juu hata katika miamba kadhaa kama Biotite. ambayo miamba hii huwa na kiwango kikubwa sana cha maji yaliyovunjwa kuwa hydroxide (OH⁻, H⁺). miamba hii ya biotite huwa na matabaka kama magamba ambayo maji ya scw yenye radon yaliingia. sasa kipindi Rn ilipolipuka kuzalisha Polonium, polonium huwa na chaji negative (-2), na hivyo ililazimishwa kuingia ndani ya mwamba. Hii sasa chaji negative ya polonium ndiyo ilisukuma chaji negative za biotite kupelekea hydroxide nyingi kutupwa nje kupitia ‘’coulumb force’’, na chaji nyingi chanya kubaki ndani. hizi chaji chanya zilipelekea polonium nyingine zenye chaji negative kuvutwa na kuendeleza uundwaji wa madoa haya. Na ndiyo maana, kuna Ushahidi wa madoa haya ya Polonium kuwa kwenye baadhi ya miamba ya magma, hii inatuhakikishia kazi ya scw. na pia kuna Ushahidi wa uwepo wa madoa haya ‘’polonium halos’’ karibu na migodi au uwepo wa uranium. Yako mengi unaweza yavumbua katika miamba hii, lakini kitu bora Zaidi ni kuwa, yanaturejesha katika gharika ya nuhu kwa kiwango kikubwa sana.

Ushahidi Wa Uwepo Wa Oxygen OË¡⁸ Na Maji Mazito ‘’Heavy Water’’ Baharini

Uwepo wa kiwango kikubwa cha oxygen yenye isotope ya 18, badala ya 16, Kuna ashiria moja kwa moja kile kilichofanyika katika supercritical water. Yaani milipuko ile ya awali ya mionzi ya madini ya nyuklia huwa ikipelekea siku zote uzalishaji mkubwa sana wa Neutron, kama nilivyoelezea kule kwenye utangulizi. Sasa basi, hizi Neutron ambazo huwa free, ndizo husababisha milipuko Zaidi ya madini mengine ‘’chain reaction’’ na kuzalisha neutrons nyingi Zaidi. Hizi neutron hugongana au kuungana na maji na kuunda Oxygen yenye uzito mkubwa wa 18, na maji pia mazito kutokana na uwingi wa hizi neutrons. Huwezi elezea swala hili bila kutambua chanzo chake ambacho ni gharika kuu.

To be continued....

Pichani ni Engineer, Dr Walt Brown muasisi wa nadharia ya Hydroplate theory kuelezea Gharika ya Nuhu