GHARIKA NA COMETS ''Nyota Mikia"
Asili Ya Comets ‘’Nyota Mkia’’
Maji ‘’Supercritical water’’ yalikuwa na nguvu sana kiasi kwamba, kipindi cha mlipuko yalibeba miamba mingi sana na kuirusha hata kuvuka kani ya mvuto wa Gravitation na kudondokea katika space. Sasa basi, miamba hii iliyoambatana na maji na madini mbali mbali. na pia kumbuka, ilikuwa pia na mabaki ya bakteria, mimea kadhaa, na chembechembe zingine za uhai wa kutoka duniani, iliingia katika anga ambalo halina kiwango tena cha kani ya mvuto wa gravitation kama ya dunia. Na hata huko uchafu huu ulitawanyika kutegemea na nishati au spidi zao za awali.Historia ya Comets au nyota hizi zenye mikia kwa namna zinavyoonekana inaanzia hapa. Kadri uchafu huu ulipokuwa katika maeneo Fulani katika space, ulitengeneza wingu ambalo ni matokeo ya kiwango kikubwa cha mvuke wa maji. na pia kutokana na baridi kali sana iliyo katika space -270.45°C. kumbuka kiwango kikubwa cha madini katika maji, hupunguza Zaidi nyuzi ya kuganda za maji ‘’freezing point depression’’. hii ni kama maji yenye chumvi hayataganda kirahisi kama maji yasiyo na chumvi. Uwepo wa wingu hili husababisha hata uchafu mwingine unaokuja, kupunguza spidi unapoingia katika maeneo haya yaliyojikusanya katika sehemu tofauti tofauti.
Hiyo hali ya kupunguza spidi inaitwa ‘’aerobraking’’. na kadri uchafu huu ulivyozidi kujikusanya, ulipelekea uzito ambao ulitengeneza mithili ya mtelemko. ambao vitu vingine vinavyokuja vingevutwa kudumbukia. Hii huitwa ‘’Body of influence’’. yaani kitu kizito hutengeneza ‘’Gravitational field’’. hii ni kama namna ambayo dunia huvuta vitu vingine kuingia ndani yake. Kitendo cha uchafu mwingi kujikusanya kinaitwa ‘’Gravitational accretion’’. Uchafu huu uliojikusanya katika hizi comets, kadri ulivyozidi kuongezeka ndivyo presha au mgandamizo wa miamba ya ndani Zaidi ulivyozidi. na kiwango kikubwa cha maji yaliyoganda yalichangia uundwaji huu. Kumbuka bila uwepo wa wingu hili la maji ya scw yanayoganda haiwezekani kabisa uundwaji wa comets. Maana vitu vinavyogongana huishia kusukumana mbalimbali visikae pamoja. Comets zina karibia asilimia 38% maji, na zinazobakia ni uchafu na kemikali zingine.
Ushahidi.
Miongoni wa comets ambazo wanasayansi wa anga kutoka shirika la anga la ulaya ‘’European Space Agency’’ wanataarifa zake ni comet’67. ambayo misheni ya anga iliyoitwa Rosetta ya mwaka 2014 november 12 waliifatilia na kuichunguza. Kwanza waliona sehemu kuanzia asilimia 72-74% haina kitu. Na bado wakaona sehemu kubwa imejawa na uwepo wa chembechembe za uhai ’’organic compounds’’ kama zitakapooneshwa hapo chini kwenye jedwali.
Pia ilionekana kuna uwepo wa Oksijeni (O₂) hii huitwa ‘’molecular oxygen’’. kwa kawaida huwezi ipata hii katika anga, Kwakuwa ikiwa yenyewe tu ghafla huungana na kuunda maji, au kaboni dioksaidi, au kaboni monoksaidi, au huweza ungana na yenyewe kuunda ozone(O₃). hivyo uwepo wa hii oksijeni ya duniani katika comet, unatuhakikishia kuwa ilitoka duniani katika kile kipindi cha gharika ikiambatana na maji ya mvuke, na maji yalipoganda kuunda barafu, basi oksijeni hizi zilikuwa zimekwisha yeyuka ndani ya maji, na kuhifadhiwa humo. Na pia kitendo hiki cha kuzipata molekuli hizi za oksijeni, kunathibitisha uwepo wa maji ambayo yalizizuia zisiungane na elementi kama hydrogen na madini mengine. Na pia uwepo wa barafu jingi, unathibitisha uundwaji wa ghafla wa matokeo ya Gravitation. Maana, muda mrefu ungepelekea barafu jingi kupasuka kwa matokeo ya mionzi na hata kupotea kwa molekuli za oksijeni.
Jedwali hili linaonesha kemikali za kibiolojia zilizopatikana ndani ya comet’67.
Kuona kemikali hizi ni sawa na kuona visu, vijiko, vikombe, na ndoo huko hewani. na kisha kusema zilijitokea tu zenyewe kwa mabilioni ya miaka.
kumbuka
Wote wasiokubaliana na nadharia hii, huamini kuwa Comets ziliumbwa aidha kupitia ule mlipuko wa miaka mabilioni ya miaka ya nyuma. na kuwa, miongoni mwa mavumbi kama yalivyopelekea kuundwa kwa sayari na nyota, ndivyo baadhi pia yalipelekea kuundwa kwa comets. na hawa pia hutumia mabaki haya kusema kuwa, yawezekana mabaki hayo yana maanisha kuwa, Maisha yalitoka huko kwenye comets. hoja hizo hazina nguvu, maana hata haziwezi elezea imekuwaje viwepo na mazingira hayaruhusu. Kwa upande mwingine pia, wapo ambao huamini kuwa comets hizi ziliundwa na Mungu moja kwa moja. mara nyingi watu hawa huwa hawaruhusu kujifunza Zaidi. kwa maana hushindwa kutoa majibu ya uwepo wa vitu kama ‘’heavy hydrogen’’, ambayo inapatikana Zaidi kutokana na matokeo ya gharika tu, na hata ukiangalia sifa za comets nyingi, kama vile orbits zake, ambazo huitwa ‘’ellipses’’ zinadhihirisha ni matokeo ya gharika kwa namna ambavyo zimekuwa zikiwa ni mithili ya jiwe linaloelea likifata tu uelekeo wa gravitation, ambayo huwa ni ya jua. Kumbuka comets zote na vimondo vyote hata ukiziunganisha, hazivuki wala kukaribia hata asilimia 5% ya uzito wa dunia.
Maswali Kama Ukikataa Hii Nadharia Juu Ya Comets
Je uwepo wa chembechembe za uhai katika comets kuna maanisha kulikuwa na maisha kule? Mbona Mungu hakuumba Maisha katika siku sita tofauti na yaliyopo duniani. Kama comets ziliumbwa siku ya nne, je nini kilichokufa kikaacha mabaki, tuseme kuna dhambi zingine zilifanyika katika space na kifo kikawamaliza? Kama hapana, je kwanini zipo kule chembechembe za uhai?
Kama comets ziliumbwa katika siku sita za uumbaji, mbona Biblia haizungumzii Maisha katika comets. ila inasema kwa mtu mmoja Adamu, dhambi iliingia duniani na kifo, hiyo ina maana gani?
Kwanini nyingi zipo katikati ya sayari zilizo karibia na dunia? Na hii inahatarisha migongano ikiwemo ya kuanguka kwa vimondo.
hitimisho
Kadri tunavyozidi kuendelea tutaona kuwa kwa kuviangalia pia vimondo, sayari ndogo, na vitu vingine vya angani. tutazidi kurejea katika gharika ya nuhu.
Picha ya comet’67 ambayo ilichukuliwa na Rosetta mission.
To be continued...




Join the conversation