Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

GHARIKA NA VIMONDO

Gharika na Vimondo

 Asili Ya Vimondo 

‘’meteors na meteorites na meteroids’’

’Meteors’’ ni miamba ‘’rocks’’. Yaani kwa lugha nyingine ni kuwa, kama miamba hii ingepata mazingira mazuri, basi ingeweza kuunda ‘’asteroids’’ sayari ndogo, Ila yenyewe ilifeli nakubakia ikielea. Mara nyingi nyingi hii miamba ‘’meteors’’ inapoanguka huitwa sasa ‘’vimondo’’ au ‘’meteorites’’. Mfano mzuri wa vimondo hivi ni kile kilochoangukia mbozi Tanzania.

Miongoni mwa vitu vya ajabu kabisa ni kuwa, asilimia 4% ya vimondo hivi vimeundwa na kiwango kikubwa kabisa na madini ya Iron na Nickel. Kumbuka madini haya hupatikana katika kiini cha dunia kwa uwingi Zaidi ‘’earth’s core’’. Uwepo wa madini haya katika meteors, unadhihirisha kabisa matokeo ya ‘’supercritical water’’ ambayo iliyayeyusha madini haya, na yalipokuwa katika space, yalipelekea kugandana kwa miamba yenye kiwango kikubwa cha madini chuma.

Kuna asilimia 90% za madini chuma, asilimia 8% nickel n.k, kwa kimondo hiki kuanguka duniani unaweza tumia lugha nyepesi kuwa, kimondo kimerudi nyumbani.

Meteorites nyingi zimekuwa zikishangaza kwa kuwa na uwepo wa chembechembe nyingi sana za Maisha. kwa kiasi cha ajabu, na hasa ukiangalia zipo katika mazingira yasiyosapoti Maisha. mfano, kimondo ambacho kinaitwa kimondo cha ziwa Tagish.

kimondo kinachoitwa tagish lake meteorite

Hiki kimondo kina asilimia 3% ya chembechembe za uhai’’organic compounds’’ hebu angalia jedwali hili chini.

Hizi kemikali zote za juu ni kemikali za Maisha. na ajabu kabisa ni hata aina za protini zilizopatikana, ni za upande wa kushoto ‘’left-handed amino acids’’ ambazo hizi hupatikana kwa viumbe hai tu. Hii inadhihirisha kuwa, meteorites zilitokea duniani enzi za gharika ya nuhu.

Maajabu Ya Gharika Katika Vimondo Hakuna Nadharia Inaweza Elezea

chondrules

Asilimia 85% ya vimondo vyote au meteorites, huwa ni miamba ya chondrules. Hii ni miamba ya ‘’igneous’’ yaani iliyo matokeo ya kuganda kwa magma. Ambayo ina madotidoti yaliyo matokeo ya kuungua sana kwa mwamba. Yaani ni kama ukitengeneza picha hii, uwe una ugali mweupe ulioiva, na madoti doti meusi ya ukoko. Sasa elezea kitu kama hiki, halafu bado kama kwa kielelezo cha huo ugali, basi ugali bado uwe na kemikali za mivuke ‘’volatiles’’ndani yake. chondrules ni miamba yenye madoti ya madini yaliyoungua sana, na bado miamba hii ina mabaki ya gesi za mvuke. Kiufupi chondrules huwa ni miamba ambayo kama tu madoti yake yanayohitaji joto la karibia nyuzi 3000°C yangeundwa kwa matokeo ya joto hilo la 3000, kwenye mlipuko wa miaka mabilioni zamani kama ambavyo wanasayansi wasioamini gharika ya nuhu wanavyosema, basi mwamba mzima ungekuwa umeungua kwa kiwango kilekile. Na pia kusingekuwa na kemikali zinazoweza evaporate ‘’volatile’’, maana joto kali lingesha zimaliza zote.

Maelezo bora kabisa yanatoka katika mtazamo wa gharika ya nuhu. ambao unaturejesha ndani kabisa katika vilindi vya maji. kipindi cha awali cha mpasuko wa dunia, ambapo tuliona ‘’fluttering’’ ambayo ilipelekea umeme ‘’Piezoelectric currents’’. na huo umeme ambao ulizalishwa katika maeneo yenye mgandamizo mkubwa ulipelekea voltage kubwa sana za umeme karibia 50000Volts. Ambazo ndizo zilizopelekea Nishati kubwa sana ya Joto iliyounguza maeneo kadhaa ya miamba. ‘’hii ni kama Radi inavyopiga sehemu. ila radi hazina nguvu kiasi cha kuchoma chondrules’’. miamba iliungua ikiunda madoti makubwa bila kupasuka. na hivyo baadae miamba hii vipisi vyake vilibebwa na maji ya scw, na miamba ambayo iliizunguka, Ambayo ilikuwa imeyeyuka, na baadae miamba hii ilipopoa, ilikuwa na madoti, na sehemu zingine za magma, na kemikali nyingi za volatile ambazo zilikuwa ndani ya supercritical water. Picha ya Chondrules.

vimondo vinavyoitwa ‘’pallasites’’

Pallasites ni vitu vya ajabu sana, yaani hii ni sawa na kielelezo hiki, ‘ukute Mafuta yako ndani au chini, na kisha maji yakiwa juu yanazunguka hayo Mafuta’’. Maana ake ni kuwa, Pallasites huwa ni meteorites ambazo, kwa nje zina madini ya Iron na Nickel, na kwa ndani zina madini ya Olivine na mengineyo, Ambayo yana density ndogo ukilinganisha na iron na nickel. Imekuwaje meteorite hizi zimeundwa. Hapa huwezi elezea bila kurejea katika kilichofanyika katika gharika ya nuhu. Kwanza lazima itambulike kuwa, katika sehemu ya ndani ya dunia, kuna madini mengi ya Iron na Nickel ‘’earth’s core’’. Lakini katika sehemu ya kati juu ya dunia ‘’mantle’’ kuna madini mengi ya ‘’olivine na silicon’’. Na hivyo basi, Pallasites zinahusiana sana na uundwaji ambao ungehusisha tabaka lililo katikati ya sehemu hizi mbili. na hapa ndipo tunarejea awali katika kazi iliyo fanyika na ‘’supercritical water’’ ambapo, tunakumbuka kuwa madini yote haya yalikuwa yameyeyuka, na hivyo, yalikuwa yamebebwa na supercritical water. 

na pili tunakumbuka kuwa, madini haya yalipokuwa hewani, kutokana na presha na jotoridi dogo, yaliganda. na sasa basi, kitendo cha hali ya kutokuwa na kani ya mvuto wa gravitation, au ‘’weightlessness’’. ambayo iko katika space, ilipelekea madini haya ya olivine na hata silicon kuweza kucheza cheza hata yakaingia ndani ya iron na nickel. na hii ni kwasababu, hakuna madhara ya density katika mazingira yasiyo na uzito. Na hii ndiyo sababu ya pallasitess ambazo huwa ziking’aa na kuvutia lakini zikiumiza akili za watu. Picha ya pallasite.

Asili ya trans neptunian objects ‘’tnos’’ na pluto

Trans Neptunian objects ni aina nyingine ya mifano ya asteroids, hizi hupatikana kwa wingi sana katika Kuiper belt. ambayo niliionyesha awali. Uhalisia ni kuwa, trans Neptunian objects ni zile zile asteroids. na ndiyo maana hata density zinafanana na asteroids. kitu pekee ambacho ninaweza sema ni kuwa, hizi trans Neptunian objects ni zile asteroids zilizokuwa kubwa sana.

Sasa basi kama ilivyo kawaida, ukubwa wa kitu hupelekea kuwa na sphere of influence kubwa. Ambayo hupelekea kuvuta sana vitu vingine kuja kuielekea. Hizi asteroids kubwa sana zilikuwa na kiwango kikubwa cha miamba, uchafu, hewa, na mvuke wa maji au barafu ambao ulipelekea ile hali ya ‘’Aerobraking’’ ambayo niliielezea awali, na sasa basi, kwa kuwa asteroids hizi zilianza na saizi kubwa sana, basi zilipitia msukumo mkubwa sana kutoka kwenye jua. Rejea ‘’radiometer effect’’, msukumo huu ulipelekea zisukumwe mbali sana ukilinganisha na asteroids ambazo hazikuwa kubwa sana kwa saizi. na baada ya kufika maeneo ya Kuiper belt hazikusukumwa zaidi sana kwakuwa tayari msukumo wa jua ulipungua, kutokana kuisha kwa gesi zilizokuwa ndani ya mfumo wa jua.

To be continued...