Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

MSINGI WA SHIDA ZA KISAIKOLOJIA

MSINGI WA SHIDA ZOTE ZA KISAIKOLOJIA

 MSINGI WA SHIDA ZOTE ZA KISAIKOLOJIA

Chanzo Cha matatizo yote ni Ubinafsi. Msingi wa shida zote za kisaikolojia ni Tamaa. Suluhisho la matatizo yote ni Maarifa. Nguvu ya Maarifa yote ni Upendo. Hizi ni Sheria kuu za kuzitambua kabla ya kuanza kujifunza shida zozote zile za kiakili.

Ni vigumu sana Kwa Wanasaikolojia kuweza kutambua kwanini tumekuwa na tabia kama za viburi, Uvivu, uwezo mdogo wa kujifunza, husuda, wivu, Hasira Kali, na tabia nyingi za ajabu sana katika jamii. Wanasaikolojia hujitahidi sana kuweza kuelewa mabadiliko ya kitabia kama ya Hisia za kuchanganyikiwa Kwa hofu "anxiety", msongo mkubwa wa mawazo "depression", uraibu Kwa kiasi, kushindwa kujizuia kifikra "OCD", kuwa na shida za kutoweza kuhusiana kijamii "Anti social", na shida zingine za mtindo huu, lakini bado huwa changamoto sana kwao kuweza kujua Nini hasa humfanya mtu kuwa mwizi, Nini hasa humfanya mtu kupenda sana uongo, Nini hasa humfanya mtu kuwa mpenda rushwa, shida za mtindo huu imefika Wakati watu wamehisi hakuna namna mtu anaweza kuzielezea. Katika sehemu hii, tutaelewa msingi wa kuelewa kila tabia na chanzo chake Cha awali kabisa.

Baada ya muda mrefu sana katika kuzichunguza sana Sayansi za viumbe, niligundua kuwa Kuna ngazi kuu tatu za Tamaa. Bahati nzuri halikuwa wazo jipya katika upande wa historia ya taarifa zilizokwisha kuwepo, maana imewahi kuandikwa katika Biblia " Mungu huwa hamjaribu mtu, bali mtu hujaribiwa Kwa Tamaa yake". Yesu alijaribiwa Kwa majaribu matatu, hii ni sawa na kusema, Kuna aina kuu tatu za Tamaa, ambazo Kwa namna ya Biblia ndizo zilikuwa msingi wa majaribu. Zipo ngazi kuu tatu za Tamaa, na hizi ndizo ngazi za kujifunza msingi wa kila shida ya tabia Kama tutakavyoona baada ya kuzitazama.

HATUA KUU TATU ZA TAMAA

Tamaa Ya Nishati Ya Kuishi ‘’animalism’

viumbe wote wanatamani sana kuishi Kwa kutamani sana kupata nishati zinazoweza kuwawezesha kuishi. Katika sehemu hii Kuna Tamaa kuu ya Chakula, Tamaa ya kuwepo katika mazingira rafiki ya kuweza kuishi, hasa mazingira ya katika nyumba, miti, mapango, n.k.

Mfumo wa Maisha kwa asili, huwa hautoi uhakika wa kuishi, na ndiyo maana kila mtu hupaswa kula kila siku, na siyo kula chakula cha miaka Hamsini kwa mara moja ili kuwa na uhakika wa kuishi yaani mfano kama utatokea ukame wa chakula. Wengi wa watu hawajui Nguvu ya chakula namna inavyowaendesha. Tofauti na mtu kujionesha moja kwa moja kuwa ni mhanga wa uhitaji wa uhakika wa chakula, wengi huwa ni wahanga wa fedha za kujikimu za uhakika wa chakula. Popote pale mtu anaposema, ‘’ntaishije sasa!’’, mara nyingi huwa anazungumzia uhakika wa kupata chakula. kwa mavazi na makazi. Asili huonekana kutokuwa na mtihani mkubwa sana, kama ilivyo kwa chakula. Idadi kubwa sana ya watu duniani, huishi katika nyumba dhaifu, nyumba za kupanga, wengine vibanda tu vya kuegesha, wengine hulala tu kwenye sehemu zenye kuwakinga, na hata wengi huwa si wakujali sana mavazi ya gharama, bali yenye kuwasitiri tu. Kama mtu angebakiwa na kiwango cha kukidhi hitaji moja tu kati ya matatu haya, basi angejali zaidi Chakula. Kila anayeamka na kuendelea kupumua, ni nguvu ya chakula alichokwisha kula.

Binadamu huishi kwa mkate. Inahitaji uelewa mpana ili kutambua kuwa, binadamu anaweza kuishi bila mkate, ndiyo maana Yesu alimjibu shetani alipomjaribu kwa kumwambia kuwa; ‘’Mtu hataishi kwa mkate tu!’’ Sayansi ya Ubongo huonesha kuwa, katika mahitaji yote ya msingi ya mwili, Ubongo huonesha kipaumbele zaidi cha motisha kwa chakula, hasa chenye kuupa mwili nishati kama sukari. Wanasayansi wasiolijua hili, huisi labda mapenzi ndiyo huwa na kipaumbele zaidi, kama inavyoonekana kwa namna ambavyo huzalisha msisimko mkubwa sana katika ubongo. Lakini hawa husahau kuwa, kama mwili usingelikuwa na chakula wala mapenzi, na kuwa mhanga wa vyote mpaka mwisho, kamwe usingelichagua mapenzi mbele ya chakula. Mapenzi huwa ni baada ya chakula katika ubongo. Hivyo hitaji kubwa zaidi la asili katika ubongo ni chakula. Sababu ni kuwa, binadamu huishi kwa mkate.

Unaweza kujihoji, iwapi tamaa hapo juu. Tamaa huanzia hapa. Kwa kuwa binadamu huishi kwa chakula. Na kadri unavyoweza kuwa na uhakika wa kula, ndivyo unakuwa na uhakika wa kuishi. Binadamu hutamani sana kuwa na uhakika wa kuishi, kwa kuwa na uhakika wa chakula.Sasa udhaifu ni kuwa, mwili huweza kula chakula kwa kiasi maalumu tu, tena chakula cha siku moja tu. Huwezi kula chakula cha leo na kesho, na kwa hivyo, kila siku kunapokucha, binadamu hupaswa kuwaza atakula nini, Au ataishi vipi kwa lugha nyingine. Swali hili huwa halipendwi kabisa na Ubongo, mtu kwa asili hutamani kuwa na uhakika wa kuishi au kula, na hivyo hitimisho pekee, huwa ni kutamani kujilimbikizia ghala.

Kumbuka Kwa hapo zamani za uandishi wa Injili Kwa mfano, Yesu humzungumzia Tajiri mpumbavu, aliyejijazia ghala, na kisha akahisi sasa, atafurahi kwa kuwa na uhakika wa kuishi. Kwasasa hivi watu hujilimbikizia mali au fedha katika mabenki, wakijitengenezea furaha kwa uhakika wa Maisha.

Je! Wewe Upo Katika Kundi Hili La Tamaa?

Zaidi ya asilimia 80% ya wakazi wote wa duniani wapo katika kundi hili la tamaa. Na unaweza kuligundua hili kwa idadi kubwa sana ya watu walio katika makundi makuu mawili, yaani, tabaka la chini, na tabaka la kati. Au ‘’lower and middle class’’. Katika matabaka haya, watu hujali sana wanawezaje kujikimu kiuchumi, watu katika makundi haya huwa na maswali mengi sana, ya tamaa za kujikimu. Mfano mzuri, utakuta wengi wakitamani kwa kusema, nikipata mavuno mengi mwaka huu ntapumua! Au natamani sana nipate walahu kazi ya kujikimu kimaisha! Watu katika tabaka hili huwa hawana tamaa sana ya kiwango kikubwa sana cha ubora wa kimaisha, ila huwa na stress sana za namna maisha yao huwa si ya kutabirika, au madeni ya muda mrefu, wengi wa watu katika tabaka hili hufanya mambo mengi sana bila kupenda, lakini husukumwa kufanya kwasababu tu huwapasa kuyafanya ili waishi. Watu wengi katika kundi hili huwa na tamaa sana ya Pesa, kuliko tamaa ya mamlaka. Wao pesa hulenga zaidi kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula, maradhi, na makazi ya kujistili. Sehemu za mbele tutaona namna watu wengi wa kundi hili husukumwa kuingia katika tamaa kama za rushwa, wizi, n.k.

Tamaa Ya Kutawala Na Kutambulika ‘’humanism’

Swali la kujiuliza, kama vipo vyakula vya kutosha kwa kila mtu, kwanini watu wanapigania vyakula hivi, tena wanapigana kila mmoja akitamani amiliki hata zaidi ya anavyoweza vila, na kutamani hata wenzake wasipate kabisa. Jibu la kwanza, wanapigana kwa kuwa kila mmoja anatamani kuwa na chakula cha kutosha, na kukitunza kitakachobakia hata kwa siku zake zijazo kwa ajili yake, na kwa ajili ya vizazi vyake. Jibu hili ni sahihi kwa aina ya kwanza ya tamaa, ambayo ndiyo migogoro mingi ya watu wa hali za matabaka ya chini na kati kama tulivyokwisha ona. Jibu la pili ni kuwa, kama vyakula hivi vinaweza kuwa si vya kudumu, basi mashindano haya yamelenga kumfanya mmoja atakayemiliki aweze kuwatawala wenzake watakaokosa, aidha kwa kuwatawala watii matakwa yake, au kuwapoteza ili awe na uhakika wa kuishi mwenyewe kwa wakati ujao kwa kuwa na chakula kingi bila ushindani. Binadamu huzaliwa na asili hii ya mashindano, unaweza kuona Watoto wa kiume namna wanapenda kushindana kila mmoja akitamani kumtawala wenzake. Louann Brizendine anaandika jambo kuu linalompatia hasira mwanaume ni kumnyima Uhuru, au kumtawala. Na hii ndiyo sababu ya mapenzi ya wanaume wote kuwa na Misuli mikubwa au sura yenye ndevu na sauti nzito ya kutisha. Kwanini wanaume huzaliwa na asili hii ya kutaka kutawala wenzao? Ni kwa kuwa tangia mtoto anapokuwa tumboni huwa anaumbwa kupambana na uhalisia wa nje. Tangu katika mimba mtoto huanza kuumbwa kujakuwa na uwezo wa kupambana na umasikini.

Asili ya kupambana ili kutawala awali kwa mwanadamu ilimsaidia sana kupambana katika asili, na kuwatawala Wanyama wengine. Binadamu wengi wa hali ya chini huwa hawana tamaa ya kuwatawala wengine. Na wengi wao huonekana kama watu wazuri wa haki, lakini huwa si kweli hoja hii binadamu hawa wanapopata nafasi za kuwa juu ya wenzao.

Akili hubadilika ghafla sana baada ya kuhisi tayari sasa nina uhakika wa kuishi kwa chakula. Binadamu huanza kutamani sasa kuwa kichwa au kutawala, na kuwafanya wengine mkia. Wengi huwa hawajui kwanini watu hutamani sana kuwa wafalme, maboss, managers, machifu, viongozi, wenye ubora zaidi, nambari moja, hajawahi tokea, n.k. Falsafa ya sayansi inatusaidia sana kuelewa hili. kadri mtu anavyokuwa wa upekee sana, ndivyo thamani yake huongezeka zaidi, ndivyo watu wengi humhitaji zaidi kutokana na upekee wake. Mtu huyu sasa hupokea sana toka kwa watu, na ndivyo utajiri wake huongezeka zaidi. Kadri utajiri wake unavyozidi kuongezeka, ndivyo uhakika wake wa kuishi unavyoongezeka.

Kama ukimchukua kijana anayetamani kuwa Tajiri sana, na kisha ukawa ukimuuliza baadhi ya maswali kuhusu sababu ya tamaa yake, Utagundua kuwa, anatamani kuwa Tajiri sana kwa kuwa, kwa kuwa Tajiri sana atapata mengi ya mahitaji anayoyatamani. hatatumia nguvu kubwa kupata mahitaji yake au kufikia tamaa zake. atakuwa na uwezo mkubwa wa kujilinda dhidi ya hatari za Maisha. wengi ambao huisi watu hupenda kuwa maarufu au wakubwa sana kihadhi kwa kupenda sifa toka kwa watu, huwa hawajui kuwa kupenda sifa hulenga sana uhakika wa usalama binafsi wa mtu, kimwili na kiakili. Kama atasifiwa na wengi, maana yake uwezo wake wengi wameuona hauna wa kulinganisha naye, ‘’yaani upekee wake ni wa juu sana’’. Pili, wanaokusifia wanakuhakikishia kuwa wanakupenda, hivyo hawatakubali uanguke. Hizi zote zinalenga tu kumhakikishia zaidi mtu uhakika wa kuishi, kwa kujiona ya kuwa, hayuko peke yake, au yuna nguvu nyingi.

Kwa kutamani umaarufu mkubwa na mamlaka, watu wote hukutana juu. Ni kama kila mtu huongozwa kutamani sifa hizo, na hivyo anayewahi kufika juu, huwa na wafuasi wengi wanaotamani kuvutwa mkono. na kwakuwa kwa umaarufu na mamlaka ni rahisi kupata marafiki wengi, wapenzi wazuri, wataalamu wakukusapoti, wasanii wa kukuburudisha, Kila aina ya kileo cha uraibu wa akili hupatikana kwa umaarufu. Mambo haya humfanya aliyejuu kuwa na nguvu kubwa sana, na hapa sasa ndipo kiini cha tamaa huzidi kukomaa.

Kumbuka katika Biblia imesemwa ‘’ntakufanya kuwa kichwa na sio mkia!’’. Wasomi baadhi hutafsiri vibaya sana ahadi hii ya Mungu. Wao huonyesha kuwa, wanaobarikiwa huwa kichwa, au nambari moja, au viongozi, na wasiobarikiwa huwa mkia, au wa mwisho au watumwa. Hawa hukosea, Kila mtu anaweza kuwa kichwa kama kila mtu alivyo na kichwa. kutobarikiwa hulenga zaidi kutoweza kutumia kichwa chako, na kuwa kama mkia, au kushindwa kuongoza akili yako, bila shaka kuongozwa. Yesu alipojaribiwa na Shetani kuwa, ‘’ Kama Ukinisujudia ntakupatia milki na falme zote za ulimwengu. Shetani alilenga hatua ya pili ya hisia za tamaa. Yesu alitoa somo kubwa sana ya kuwa, anayepaswa kusujudiwa ni Mungu tu, na sio mwenye nafasi yoyote ile ya juu. Alimaanisha kuwa, kwa kuwa na mamlaka na umaarufu juu ya watu, hakumaanishi kuwa thamani ya mtu huongezeka.

Jamii imejaa watu wenye tamaa za kuwa juu ya wengine, msingi huu wa tamaa Dunia huujenga tangia binadamu wanapokuwa wadogo. Hii ni kupitia kuwazoeleshea ushindani katika taasisi za elimu, kupitia michezo wanayoifanya, kupitia filamu, sinema, na hata magemu wanayoyacheza. Haya yote huwachochea sana kuingia katika falsafa za kutamani kutawala wenzao, na sio tu kuwa na tamaa ya kufanikiwa. Binadamu wengi hawaridhiki kwa hali zao njema, bali huridhika kwa matokeo yao baada ya kujilinganisha na wenzao. Hii ni hatari sana, haimaanishi kuwa kama umepata 30, na wanaokufuata wamepata 5, basi wewe umefaulu, kama kipimo cha ufaulu ni 50.

Kadri watu wanavyoshindana, ndivyo wanavyotazamia zaidi kuwa juu ya wenzao. Wengi wao sio watu wakutazama na kuona, bali hutazama na kulinganisha. Sio watu wa kusikiliza, bali husikia na kulinganisha. Idadi kubwa ya watu katika hatua hii ya tamaa, hushindwa kunufaika na ubora wa hali zao zisizolinganishwa. Mtu aliye na utajiri mkubwa sana lakini hana mamlaka huishi kama mtu asiye na kitu kabisa, kwasababu tu ya kujilinganisha na aliyejuu kabisa zaidi yake. Vivyo hivyo mtu aliye na afya huishi kama vile asiye na afya kabisa, kwa kujilinganisha na aliye na afya na mamlaka zaidi yake. Hatua hii huchochea jamii ya watu wasio na shukurani kabisa, wala wasioweza kuangalia uzuri wa wengine.

Je! Una Tamaa Katika Hatua Ya Pili?

Viongozi wengi sana katika taasisi za umma, binafsi, na za kidini, wasomi wengi sana na vijana walio katika hatua za mafanikio, na wengineo wengi. Hawa wote hutekwa kirahisi sana kutamani kuwa juu ya wengine. Na ilihali wakipambana sana kuwa juu ya wengine, hujikuta wakiingia katika wimbi la uraibu wa kutamani tamaa ya kuwa juu, na hapo ndipo msingi wa matatizo mengine yote kama tutakavyoyaona.

Tamaa Ya Kutokufa ‘’Divinism’’

Kila daktari anatambua kama mgonjwa angepatiwa nafasi ya kutoa kila kitu alichonacho ili arudi katika hali yake ya uzima na afya kwa asilimia zote 100%, hakuna jambo, utajiri, au heshima ambayo angeshindwa kuitoa. Hata Nguvu za watu wenye Imani kama Mitume wa yesu ambao katika historia za Biblia waliwahi kubali kufa kwa ujasiri, ilikuwa kwasababu walijua wataishi tena milele. Hatua hii ndiyo kikomo cha tamaa. Hii ni aina ya tatu ya tamaa, ni aina ya tamaa ambayo hulenga kiwango cha mwisho cha tamaa ya mwanadamu. Yaani, mwanadamu alianza kutamani kuwa na uhakika wa Maisha, kisha akatamani kuwa na heshima na sifa juu ya wenzake, na sasa, mwanadamu huyu anatamani kuendeleza hali yake hii ya tamaa ya kuwa juu ya wenzake milele.

Na hapa ndipo utakuta wafalme wakijiita Mungu, hapa utakuta waheshimiwa wakubwa wakitaka upendeleo wa huduma bora zaidi za afya. Hapa ndipo utakuta matajiri wakubwa zaidi wakitaka kuwekeza katika miradi, au sayansi zitakazo wawezesha kuishi milele. Hali ya kuishi milele ni tamaa ya hatua ya mwisho ya tamaa, hali yoyote ile ya umilele, ni mfanano wa hali ya Umungu. Viongozi wengi wakubwa hutamani uhakika wa ulinzi toka kwa idadi kubwa ya walinzi wenye taaluma kubwa kabisa. Siyo kana kama huwa hatarini sana katika nafasi zao, ila ni kuwa huitaji usalama sana kutokana na nafasi zao. Wapo viongozi wengi wakubwa walioamua kuishi Maisha ya kawaida sana, hasa baada ya kuziona nafasi zao ni za kawaida sana. Na mara nyingi viongozi hawa huwa wachache sana kwa idadi, na huwa na Maisha ya kutojiinua kwa nafasi zao, si kama wastani wa viongozi wengi.

Tamaa hii katika Biblia imeandikwa , ‘’Kisha ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Jaribu hili linafanania kabisa hoja ya hatua ya tatu ya tamaa, ijapokuwa ni jaribu la pili. Jaribu hili linaonyesha ni kwa namna gani Binadamu huwa tunajaribiwa kwa tamaa ya kuwa na uangalizi wa Kiungu katika Maisha yetu ‘’divine intervention’’, hii ni kama namna ya kutamani kuwa na muunganiko na uwezo wa kiroho, uhakika wa asilimia 100%. Kiufupi tunarejea palepale katika kutamani kuishi milele.

Watu kadhaa hutamani hata kuambiwa kuwa wataenda sehemu Fulani baada ya Kufa. Kiburi cha mwanadamu yeyote yule huisha anapoeleka katika kufa. Binadamu baadhi wapo radhi hata kutaka kuhakikishiwa kuwa hawatakufa, aidha watabadilika kuwa kiumbe wengine, au wataenda sehemu bora zaidi.

Katika hatua hii ya tamaa, ambayo inafungamana sana na hatua ya pili, iliyo katika jaribu la tatu. Watu wengi sana hutamani na kujaribu Kutenda kama Mungu. Watu hujiona wakiwa na uwezo wa kubadili majira na nyakati. Hujiona wakiwa na uwezo wa kuathiri Maisha ya viumbe wenzao. Hujiona wakiwa na uwezo wa kufanya lolote lile. Kiburi hiki huwasukuma sana kujiona kana kama wao si watu wa kawaida. Hatua za wengi wa watu katika tamaa kiwango cha mwisho, huelekea kutawala kabisa wenzao. Wengi wao hutumia au hata kutengeneza dhiki nyingi sana kwa wanaowazunguka, na kutengeneza namna za suluhisho ambazo zitawafanya wanaowazunguka kuendelea kuwasujudia, na wao wakijilimbikizia nguvu juu yao.

Watu katika hatua hii Hutumia Sana Utajiri kama Silaha. Mara nyingi watu katika hatua ya mwisho ya tamaa, Hujikuta sana wakiegemea katika matumizi ya mali zao kujilinda. hutumia vikundi vya watu wa usalama kupambana na maadui zao. Kwao binadamu wa usalama huwa kama Malaika. Mara nyingi watu hawa huwachukia sana maadui zao, kwa kuwa wao huwa kama Mungu, na kisha maadui zao huwa kama wenye dhambi, na mshahara bora zaidi kwao huwa ni kifo. Katika kizazi hiki watu hawa hutumia sana teknolojia za kisasa sana ili kuweza kujilinda, kwa kuwa na taarifa za kila kinachoendelea duniani kote. Watu hawa hutumia sana teknolojia katika namna mbili za kiuungu wao, yaani, kujilinda, na kujitukuza.

Wengi hawajui kwanini hawa hupenda kuwa kama Mungu. Kusujudiwa huchochea kiini cha tamaa ya binadamu mpaka mwisho. Chuki zote, wivu wote, fitina zote, hasira zote, kiini chake ni kutamani kusujudiwa. Yaani, kuwa bora kuliko wote. Kama kuna mtu unamchukia mpaka mwisho, akija kukusujudia, maana yake yupo mbele zako akiwa chini mpaka mwisho, tayari kwa lolote utakalo. Ubongo wa binadamu hutamani sana hii hali ya kiungu, na wadhaifu wote huiota kama ilivyo kwa kisa cha Lusifa aliyetamani kusujudiwa mpaka na Mungu wake.

Mungu pekee ndiye anaweza kufanya lolote, mwanadamu mpumbavu hutamani kuwa kama Mungu, kwa kiburi cha utajiri hujidanganya kuwa anaweza Kutenda yote. Na hili hutokana na kuwa, mali nyingi huathiri afya ya ubongo, maana utajiri uliokithiri ni matokeo ya ubinafsi. Watu wenye akili nyingi hujali sana jamii zao, na hapo ndipo ulipo msingi wa ugunduzi na maarifa. Jamii yangu inateseka sana, na mimi kama nina akili nitazitumia kuwasaidia. matajiri wengi huona dhiki za watu kama fursa, na kuzitumia kuwa juu yao. watu wa mtindo huu kamwe hawawezi kuwa na akili bora kabisa.

Tamaa Sio Malengo.

Wengi huchanganya tamaa na malengo. lakini hii huwa ni changamoto tu ya uelewa wa maana ya tamaa. Tamaa lazima ihusishe dhamiri ya kutaka kuwa na kitu au hali ya kufanania na jambo la nje na mtu binafsi. Ili isemwe ni tamaa, lazima mtu atake kuwa na kitu anachokitaka, au hali anayoitaka, ambayo ni matokeo ya anachokiona kuwa ndicho bora zaidi. Wengi hawajui kuwa, huwezi tamani bila kuona. Lazima uone, utake, ndipo isemwe kuwa umetamani.

Ukija kwa malengo, Malengo huwa hayatoki nje. Huwa ni msukumo wa maono ya ndani. Na kama yakitokana na mtazamo wa nje, basi nayo huwa ni tamaa. Huwa napenda kusema, malengo ambayo yanahusisha sana mipango, ni matokeo ya kutazama mazingira yako, kuyatafakari, na kutengeneza taswira ya kuwa unataka kutengeneza nini. Mfano, nalenga au nafikiria kujenga saloon ya nywele maana nimeona kuna wateja wengi sana eneo hili, na ninaweza thibitisha kwa kuona hata Jirani yangu naye mwenye saloon, hushindwa kumudu idadi kubwa sana ya wateja wa nywele. Ninapovuta taswira sasa kuwa nimeshaijenga ilihali nipo katika mipango ya kuijenga, basi nakuwa nahamu ya kuikamilisha. upande wa tamaa huwa kinyume kabisa, yenyewe huanza kwa kuona saloon ya mwenzangu ikiwa na mafanikio mpaka kuzidiwa, na kisha hutoka huko kuja kwenye mipango ya mimi kufikiria hilo kama fursa kwangu.’’

Tamaa huenda kinyume na malengo, tamaa haina mipaka ya kuikamilisha, ila malengo yana mipaka. Nina mipaka ya malengo ya namna yangu ya kuoa, lakini sina mipaka ya namna yangu ya kutamani kuoa. Malengo yana kikomo kwa kuwa hutumia sana sehemu za mbele za ubongo, katika mfumo wa ubongo unaoitwa ‘’central executive network’’, wakati tamaa hazina mipaka, na hutumia sana sehemu kadhaa za ndani na nyuma katika ubongo, hutumia mfumo wa ubongo unaoitwa ‘’DMN’’ au ‘’default mode network’.’Mtu anayetamani anaweza kuzini hata akitembea, anaweza kuua ili kukamilisha au kuiba, anaweza pia akatumia njia sahihi ila bado asiwe na nia njema, kiufupi tamaa haitoki moja kwa moja sehemu za kufikiria katika Ubongo.

Changamoto: kuna watu maranyingi husema, nimemwona Mwalimu mmoja anafundisha vizuri sana, na mimi nimetamani kuwa kama yeye, Je, hiyo nayo ni tamaa mbaya?

Jibu: kwa mujibu wa Ubongo, kama umetamani namna alivyo Mwalimu, nafasi ya ualimu, au kipawa cha ualimu, namna ya kufundisha, kusaidia watu maarifa, hapo umetamani Hali. Na hilo halina shida. Na kisaikolojia hapo umetamani kwa kuwa hiyo hali ipo ndani yako, umesukumwa kuelekea asili yako. Ni kwamba umekosa neno la kutumia, umetumia tamani, badala ya kuvutiwa.

Upande wa pili kama umetamani nafasi ya Mwalimu huyo, umetamani wewe ndiyo ungekuwa katika nafasi yake, umetamani wewe ndiyo ungekuwa unasikilizwa. Wewe una dhambi ya tamaa, na inakuhatarishia afya yako ya Ubongo, na hautakuwa Mwalimu mzuri, maana huna mipaka, na hautatenda kwa upendo, utatenda kwa ubinafsi au kwa kutaka sifa.

Nguvu Kubwa Ya Uadui Wa Tamaa

Ni lazima tutambue kuwa, tamaa ndiye adui mkubwa zaidi wa mtu. Kama kuna kila uovu ambao mtu anaweza kuutenda kwa kutaka au kutotaka. Ambao hata yeye mwenyewe huweza kukiri kuwa hakutaka kutenda hivyo, basi sababu ya huo uovu ni tamaa. Tamaa humlazimisha mtu kutenda kwa kutaka, au kutotaka.

Katika mtazamo mpana zaidi ambao sitataka kuuzungumzia zaidi katika sehemu hii, ni kuwa, hata sayansi ya Ubongo huonyesha kuwa tamaa haina msingi katika sehemu za mbele za ubongo, au sehemu za msingi wa akili na utambuzi wa mtu. Msukumo wa tamaa ni mpana sana, kifalsafa zaidi, tamaa tutaiona kuwa imelenga parefu sana, zaidi ya malengo binafsi ya mtu. Na ndiyo maana, kama kila tamaa ya mtu ingetimia, basi tusingekuwa na Mungu mmoja leo hii duniani.

Kadri mtu anavyojifunza zaidi kuhusu tamaa, ndivyo anavyogundua zaidi kuwa, kwanini hata Suleimani alifikisha wanawake elfu wakumridhisha tu au Nebukadneza alitaka kuabudiwa kama Mungu. Leo hii vijana hutamani umaarufu, utajiri, heshima, mamlaka, kupendwa, n.k. lakini hayo siyo malengo ya wengi wao! Unaweza gundua kuwa, wengi huwa na melengo katika fani zao, elimu zao, vipaji vyao, n.k. ajabu ni kuwa, tamaa huwa kubwa zaidi ya malengo.

tamaa huathiri hata uwezo wa malengo binafsi ya mtu. Maana, mtu hutazama malengo yake, na tamaa yake humwambia kuwa, hapo ulipo bado ni dhaifu sana. Ni kama stori ya kweli ya Lusifa, ambapo, lengo kubwa la kipaji chake cha uimbaji bora, lilimezwa na tamaa kubwa zaidi hata ya lengo lake, tamaa ya kuwa Mungu. Naweza tamani kuwa mwalimu bora, na nikawa nikitembea katika lengo langu la kuwa mwalimu bora, lakini tamaa yaweza ua lengo hili, na kuibua hisia ya kutaka kuwa bora zaidi ya mwalimu yeyote yule anayenizunguka, au aliyewahi kuwepo. Na hapo ndipo tatizo huanza, maana hata kwa kusemwa kuwa bora zaidi ya wote, tamaa hupanda ngazi, ya kutaka kuwa sio tu mwalimu bora zaidi ya wote, bali hata kuwa bora zaidi ya wenye taaluma wote.

Unaweza thibitisha hili kwa namna ambavyo, watu walio katika ngazi bora zaidi, bado hukosa raha kwa kutoridhika na hali zao. Mfano, Malaika mkubwa zaidi Lusifa bado hakuridhika na nafasi yake, au mbunge, au Waziri Fulani, Pamoja na heshima ya nafasi yake, lakini bado hajaridhia. Na hata akiwa raisi, bado utaona hisia za kutoridhika zikiendelea kumrarua.

Namna Tamaa Inavyokuua

Unapokuwa kijana wa kiume wa miaka 7, huwezi elewa sababu ya kaka yako wa miaka 16 kutumia hela yake yote ya chakula kumnunulia zawadi mpenzi wake, na yeye kushinda njaa akitafuta tu kumridhisha mpenzi wake. Ukweli ni kuwa, alipobalehe, uhalisia wa ubongo wake ulibadilika, akapanda ngazi katika tamaa za mapenzi hatua moja zaidi ya mdogo wake. Na sasa ubongo wake una uhalisia mpya kabisa wa anavyovitamani, hii kitaalamu huitwa ‘’neuroplasticity’’.

Ndivyo pia ilivyo kwa tamaa, unapoanza ngazi za chini, unaweza usielewe kwanini kuna watu wanatamani hata waitwe Mungu, lakini kuwa makini tu usiwatukane, maana Ubongo wao umefunguka zaidi ya wa kwako, na wanaona uhalisia tofauti na uhalisia unaouona. Na wewe ukifanikiwa kukua, utaelewa wanachokiona.

MATAWI YA TAMAA KISAYANSI

Yafuatayo ni matawi ya tamaa ambayo watu wengi sana hushikwa nayo kwa kuwa hushindwa kuelewa tamaa kiundani kabisa. Sehemu hii nitaelezea kiufupi msingi wa ubongo katika kuangukia katika mitego hii ya tamaa.

Ibada Ya Sanamu & Uchawi ‘’Idolatry & Witchcraft’’

Sitaelezea sana sehemu hii, kwa kuwa tutaangalia katika sehemu ya pili, inayohusu sayansi ya ubongo inavyohusiana na mazingaombwe, uchawi, na miujiza.

Kwanini ibada ya sanamu & uchawi ni tamaa?

Kwasababu mitindo hii yote huusiana na kutumia na kuchochea sana sehemu za hisia, na sehemu za taswira, kupitia mfumo wa ubongo wa ‘’Default mode network’’, kadri mtu anavyojifunza uchawi, au anavyofanya ibada za sanamu, anajifunza kuvutia taswira kitu kilichombele yake, huku akielekea katika kuunda uhalisia tofauti na uliombele yake. Yaani, mtu anaona sanamu ya ng’ombe, ila anavuta taswira ya kuwa na mungu wake. hivyo hivyo huwa kwa aina zote za wachawi, aidha kwa wale wa ‘’spell’’, ambao hunenea kitu huku akitegemea kutengeneza uhalisia wa kweli, wachawi hufundishwa kuvutia vitu taswira, hii huitwa ‘’visualization’’. na waabudu sanamu huingia katika kundi la wachawi la wasiotumia maneno, ‘’non-verbal rites’’, hawa hutumia sana ‘’Alama’’ au ‘’symbolism’’, nao hufanya pia ‘’meditation’’, hizi zote kwa Pamoja hukinzana na sehemu za ubongo zinazohusiana na uhalisia wa taarifa zilizopo mbele.

Madhara yake ni kuwa, mtu huingia katika uhalisia feki wa taarifa, kwa kuwa ubongo wake sasa kama ambavyo huonekana kwa namna unavyoathiri sehemu zake za ubongo zinazohusiana na utambuzi wa taarifa halisi ‘’parietal connectivity’’, huanza kupata taswira toka vyanzo visivyo na uhalisia. Kitaalamu ni mithili ya ‘’hallucinations’’, lakini kiuhalisia kinyume na sayansi, husemwa ni roho za kipepo ndizo huwa zikiwakamata watu hawa, na kuwaunganisha katika ulimwengu ambao wao huuona wa kiroho, kiufupi haya yote ni matatizo ya kiakili.

Tamaa imeingiaje?

Wengi wa wachawi hutamani sana kufikia hali za juu sana kihali zao za kiroho, hata kimwili. Wengi wao hupenda ulinzi na heshima. Wengi wao hutamani uwezo wa kuwadhuru maadui zao. Wengi wao hawapendi wawepo watu wenye mafanikio kuwazidi, au wenye kuwapinga. Waabudu sanamu pia hutamani sana ukaribu wao na miungu yao, kiasi cha kutaka muitikio wa moja kwa moja kwa kuwa karibu zaidi na miungu yao. Na haya yote yamejengwa katika misingi ya tamaa.

Uadui Na Ugomvi ‘’Hatred & Variance’’

Kwa utafiti mdogo sana unaoweza kuufanya, utagundua wengi wa watu hawagombani kutokana na kuwa hawawezi kukaa Pamoja na kutatua tofauti zao. Maana panapotokea mgogoro wowote ule, huwa kuna pande mbili ambazo watu hupishana, lakini ukweli ni kuwa, hakujawahi kuwa na kweli mbili. Na ukweli haujawahi jificha, kama watu wataamua kukaa Pamoja na kujadili pande zote kiundani kabisa, ukweli huonekana na watu hufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Kwanini Ugomvi na uadui?

Mara nyingi mmoja au wote huwa na tamaa. Marazote mmoja kwa tamaa zake za kutamani kuwa na mamlaka juu ya jambo linalogombaniwa, hupuuzia kabisa ukweli kuhusu upande wa pili. Uadui ni hisia za ndani za chuki. Lakini Ugomvi huwa ni matokeo yanayoonekana ya uadui.

Watu hugombana kwa kuwa mwenye ukweli huamua kuushikilia, na asiye na ukweli hutaka kutimiza matakwa yake. Ili hali wakigombana, wote sasa huwa wapumbavu. Maana baada tu ya uadui kuanza kama ugomvi, sehemu za hisia za wote wapinzani huwaka mpaka juu, na kama ilivyo kawaida hisia zinapoinuka, basi sehemu za akili za ubongo hushuka mpaka mwisho. Na ndiyo maana wenye busara huwa na uvumilivu sana wa kujizuia hisia zisiwe na nguvu juu yao, hata wakashindwa kutawala misuli ya mikono, miguu, na midomo yao.

Popote pale panaposhamiri hisia za uadui, na kuibuka migogoro. Tamaa huwa zimejaa. Kadri unavyopanda ngazi za kimamlaka, ndivyo uadui na ugomvi huongezeka zaidi. Mpaka sasa msomaji unaweza kuelewa kwanini nafasi za juu serikalini, au katika taasisi hata za dini, ndizo huongoza kwa migogoro zaidi? Hii ni kwasababu tamaa huongezeka toka hatua ya kwanza, mpaka hatua ya pili na tatu.

Wivu Na Husuda ‘’Emulations & Envy’’

Kwanza wivu kwa kuutafsiri tu, ni tamaa ya kuzidi wengine, au tamaa ya kuwa bora zaidi. Wivu huwa ndani ya mtu ukiwa haujioneshi. lakini inapoonekana mazingira ya kuwa kuna aliye juu zaidi, wivu hujidhihirisha kwa hali ya kutotulia kiakili, au kuumia,au kutaka ashuke mpaka chini.

Husuda ni sawa na wivu?

Husuda huwa ni namna ya wivu ambayo tofauti yake na wivu moja kwa moja, ni kuwa Husuda hulenga zaidi hisia za chuki kwa kuona mafanikio ya wengine. husuda huwa hailengi mwenye wivu kutamani yeye kuwa juu. Mwenye husuda huumia kwa mafanikio ya wengine, lakini binafsi halengi hata yeye kuwa juu.

Sayansi ya wivu

Udhaifu na tamaa ya ubongo hulenga kumfanya mwenye wivu awe juu. hivyo anapokutana na mtu aliyejuu zaidi yake, au anaeweza kuwa juu zaidi yake, huchochea hali ya kutotulia ya kiakili kutokana na hisia za ubongo za mhemko ‘’sympathetic nervous system’’. ambazo huambatana na stress, kwa lengo la kumchochea mwenye wivu aongeze bidii, ili aweze kurudi, au kulinda nafasi yake ya kuwa juu. Hapa ndipo utakuta mwenye wivu akipambana sana ili kurejea kwenye hali yake ya awali ya kuwa juu.

Mwenye wivu huwa na kiwango kikubwa sana cha homoni za stress, na hata homoni za dopamine. ambapo hizi na saketi zingine nyingi za ubongo huelekezwa katika kumfuatilia mpinzani wake, kwa lengo la kumuangusha, ili ubongo wake uweze kuzalisha homoni za serotonins, na endorphins nyingi, uweze kuburudika sasa. Shida huwa kwa hizi homoni mwenye wivu huchanganyikiwa sana kisaikolojia, maana huteswa na kumbukumbu za mpinzani wake aliye juu, huteswa na mafanikio ya wenzake. na njia pekee ya kukabiliana na hali hii ya mateso ya kisaikolojia, huwa ni kubuni mbinu za kujituliza. Na hizi huwa ni kumfelisha mpinzani wake kwa kila anapoweza. Mwenye wivu humchafua mpinzani wake pale anapomshindwa kwa ufanisi kiutendaji. Na kama atafeli kwa kumchafua ili kumharibia, basi ubongo wake huacha kumfatilia mpinzani wake. Kumbuka kisaikolojia maneno huwa silaha ya mwisho kwa mwanaume anaposhindwa kutumia misuli kupambana. ila huwa silaha ya kwanza ya mwanamke anapopambana. Katika ubongo maneno na mikono imeunganishwa sana, na ndiyo maana watu huongea huku wakienda sambamba pia na matumizi ya mikono.

Je! Wivu ni Hatari?

Kwa wenye wivu huwa ni hatari sana, maana idadi kubwa sana ya wenye wivu, huwa na tamaa. na tamaa huwafanya kuwa makini sana na wenye wivu wenzao. Bila takwimu unaweza gundua wenye wivu wengi huwa makini zaidi na wenye wivu wenzao. Hatari kubwa zaidi ya wivu ni kwa mwenye wivu, maana hushindwa kunufaika kwa Habari njema anazopatiwa, au watu wakubwa anaokutana nao. Kipindi Yesu anazaliwa, badala ya Herode kunufaika kwa Habari njema za ujio wa Kristo, anapata wivu wa kutaka kumuua, kwa kuhisi atachukua sifa au nafasi yake, na madhara yake akafeli yote.

siri ya 01

Ubongo mweusi tambua kuwa hisia za wivu kila binadamu anazo. Madhara ya hisia za wivu ndiyo yenye shida zaidi. Hii ni kwa kuwa kama ambavyo mtu angeshindwa kujitawala hisia zake za mihemko na kupelekea hatari, ndivyo madhara ya wivu hutokea zaidi watu wanaposhindwa kuzitawala au zishinda hisia zao za wivu. Watu wengi wasiojua sayansi, na taasisi za elimu za juu, zenye watu wanaosemwa wameelimika na kustaarabika, huisi kuwa wivu huwa kwa kiwango cha chini sana kwa wasomi hawa. Hoja huwa kinyume, kuna kiwango kikubwa zaidi cha wivu kwa kadri unavyopanda ngazi za mafanikio. Na sababu tumeshaona ni kutokana na kupanda ngazi za tamaa. Changamoto kubwa sana ambayo inaiathiri sana Afrika kwa kuwa na madhara makubwa sana ya hisia za Wivu ukilinganisha na sehemu zingine, ni kwa kuwa Afrika ina watu wanaoishi kijamii sana, na hivyo shida zozote za kihisia na kijamii kama wivu huwa na matokeo makubwa sana. Lakini pia kutokana na kuwepo watu wachache sana Afrika ambao hufanya mambo makubwa, basi mtu mmoja tu anayepiga hatua hushambuliwa na watu wengi sana kwa Wivu, tofauti na maeneo kama ya Ulaya na Marekani, ambayo Mtu mmoja mwenye wivu asingeweza kupiga vita maendeleo ya watu wengi walio bora zaidi yake katika njia yake.

Siri kubwa sana ubongo mweusi ni kuwa idadi kubwa sana ya watu wenye wivu, huwaogopa zaidi wenye wivu wenzao. Hii ni kwa kuwa, wote hufanana na kuwa katika hatua moja ya kiakili. Changamoto za hisia hizi huwaathiri zaidi Wanawake, kisha watu wa asili ya Introvert, ambao hawa wote huwa wanajali sana matukio ya kijamii wanayokutana nayo. Namna pekee ya kuweza kusimama katika jamii za watu hawa, ni kutambua kuwa hisia zote hizi za tamaa zina sababu moja kisayansi. Ambayo ni upungufu wa nishati katika Ubongo. watu wenye Wivu wana mifumo dhaifu ya kihomoni, na metaboliki za ubongo, na hii huwafanya kuwa watu ambao wanalinda zaidi, kuliko kuwa na uwezo wa kupambana zaidi. Watu walio imara huwa na uwezo wa kupambana zaidi, hasa kutokana na msukumo mkubwa wa homoni za dopamine, testosterone, n.k. na hizi huwafanya kuwa ni watu wenye nguvu na furaha yenye asili kubwa zaidi ya ndani, kuliko muitikio wa nje. Wengi wa watu walio imara katika ubongo hupokea kufaulu na kufeli kama sehemu ya ukuaji wao, na hivyo huwa hawaumizwi na ukuaji wa wengine mbele yao. Hii ni kwa kuwa huwa wanatambua kuwa njia yao ni ya upekee sana, na hakuna wa kuipita kama wao. kwao hawa huwa ni raha sana kushiriki katika ukuaji wa wengine.

Watu imara hawa hawashindanishwi kwenye michezo, hawa huwa na michezo yao mipya, ambayo huweza kuicheza wenyewe, na ndiyo waliyogundua sheria zake. Afrika ina idadi ndogo sana ya watu hawa, hii ni kwa kuwa ina idadi kubwa sana ya watu wenye falsafa za makabila mfano ya kibantu, ambayo yalikuwa na asili ya kuwinda zaidi na kukusanya. jamii hizi hawakuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ya kufikiria mikakati mbalimbali tofauti na mashindano, na utafutaji wa kula tena vyakula vilivyokuwa kwa wingi sana. Uwingi wa chakula uliwapa kiburi cha kutohitaji kushirikiana kama zilivyokuwa jamii zilizoishi kwa kutegemea zaidi kilimo. Katika sehemu ijayo tutaangalia stori hii kwa kina zaidi, siri kubwa ubongo mweusi usikubali kushindana na wagonjwa hawa wa ubongo wa wivu. jifunze kufurahia kazi za ubongo wako huku ukijali changamoto zao, au ukosoaji wao kama taarifa za muhimu kwa kukua, au kuboresha kazi zako. Part 5 ya kitabu hiki, tutaona teknolojia na mitindo ya maisha ya kisasa, inavyoua kabisa mifumo ya nishati ya ubongo, hata kuchochea zaidi shida hizi kupita wastani uliokuwepo.

Hasira- Wrath

Hasira yenye matokeo makubwa sana kisaikolojia, hutumia neno hilo ‘’wrath’’. Mara nyingi watu walio na afya ya kiakili, huwa na msukumo wa wastani wa hasira. hii ni kwa kuwa, kama zilivyo hisia zingine zinapovuka uwezo wa kujitawala, huchochea udhaifu. Hasira ni hisia za kukerwa kutokana na matokeo ambayo yanaonekana kuwa na madhara ya kimwili, au kisaikolojia. Mfano, kuvunjiwa heshima, kuumizwa mwilini, n.k.

Sehemu hii hasira haipo katika mantiki ya hisia zinazotokana na mifano hiyo juu, maana hasira ni muitikio wa asili wa mwili wa kujilinda. Hakuna asiye na hasira pale anapofanyiwa vitu hatarishi kwa mwili wake na akili yake. Mwili lazima utazalisha homoni kama adrenaline, cortisol, glutamate, noradrenaline, n.k. hizi na neva nyingi za fahamu huchochewa kusukuma muitiko wa haraka wa mwili wa kujilinda, ikiwemo kutumia nguvu za mwili kwa haraka na ustadi ili kujilinda, kwa kupambana, au kujiepusha.

Hasira kama tamaa?

Watu wenye hasira kupindukia, wote huwa na mfanano mmoja. Wote hutamani kuogopwa, kuheshimiwa kupindukia, kuwa na urahisi wa kulazimisha matakwa yao, na wengine hutaka hata kuabudiwa. Hasira za watu hawa huwa ni matokeo ya kisaikolojia, aidha kwa kujitengenezea, au kwa kutengenezewa, kama ambavyo huwa kwa wagonjwa wa ‘’post-traumatic stress disorder’’, yaani, watu ambao waliwahi kutendewa jambo ambalo liliwaumiza sana. Kiufupi lazima watu watambue, hali hii ya hasira ni hali ya tamaa ya kufikia hali ya amani ya kimwili, lakini kwa kupitia kuwafanya wengine wadhaifu, hii haina tofauti sana na zilivyo tamaa nyingine kama za wivu, na uchawi.

Iliwahi andikwa ripoti katika saikolojia, katika tafiti zilizokwenda na kichwa cha ‘’Mabadiliko ya Hali za hewa na Uwezo wa Kujitawala’’, au ‘’CLASH- climate change and self control habit’’ Kwamba, kadri unavyoelekea zaidi maeneo ya Joto, watu huwa na hasira sana, na kupungukiwa uwezo wa kujitawala ‘’self control’’. Tutaangalia kiundani zaidi hoja hii, lakini ukweli ni kuwa, maeneo ya baridi hata Wanyama huwa wapole zaidi. Kadri watu wanavyokuwa na hasira sana, huwa ni dalili ya kuwa wameathiriwa zaidi ubongo wao kwa stress. Kuna Ushahidi mzuri sana wa unywaji wa maji mengi, na kupungukiwa hasira. Wenye hasira kali pia huwa ni wahanga wa kutopata muda wa kutosha wa kulala. Na mwisho wenye hasira pia huwa ni wahanga wa kuishi kwa kitambo maisha yasiyo ya kijamii. Mbwa ambaye hufungiwa ndani huwa mkali sana ukilinganisha na anayezurula mtaani. Kama utaweza kufikiri kisayansi, unaweza kutatua vizuri sana shida za hasira, kwa kutatua shida za metabolikia za ubongo. na hii ndiyo sababu nilisema, Tamaa zote huwa ni shida za ubongo, na wanasaikolojia wengi kwa kutolitambua hili, huisi wenda ni maamuzi ya watu, au malezi tu waliyokulia.

Jamii za wafugaji huwa wakali sana, lakini mfumo wao wa maisha huthibitisha sababu zote ambazo zingeweza kuchochea stress za ubongo.Ubongo mweusi hasira kali ni tatizo la tamaa, linalotokana na upungufu wa nishati ya ubongo. na mgonjwa anahitaji kukandamiza wengine au kuwatishia, au kuwashurutisha ila ahisi ahueni. Unaweza soma zaidi hasira kwa kufanya utafiti sana kuhusu maisha ya wanajeshi, na hisia hizi. Wanaume ambao huwa na homoni za testosterone kwa wingi sana, huwa na hasira sana, na zingine hubadilishwa na kuunda ‘’DHT-Dihydrotestosterone’’, ambayo hii huathiri hata ukuaji wa nywele. Mtindo wa maisha ambao unachochea sana homoni hizi kupitia vyakula vya kisasa kama tutakavyoviona katika Part 5, huchochea sana watu wenye hasira, lakini wasio na uwezo wa kupambana. Maana inahitaji uzalishaji bora wa homoni, na sio usisimuaji mkubwa wa homoni katika afya ya ubongo.

Fitina - Strife

Sifa kubwa ya mtu mwenye fitina, huwa haisi kama anaweza kukubaliana na hali Fulani. fitina ni hisia zinazosukuma hali ya upinzani, ndani ya kikundi, hata wakati mwingine ndani ya mtu binafsi. Fitina ni tawi la tamaa ambalo wakati wowote hujidhihirisha kwa kuleta matokeo hasi kwa nje. Mwenye wivu hutofautiana kidogo sana na mwenye fitina, wote huchukia hali zilizopo juu yao, tofauti yao ni kuwa, mwenye fitina huwa na hisia za ukinzani zinazotokana na sababu nyingi, wakati mwingine, mitazamo yake binafsi. Mfano, mwenye fitina anaweza kuwa marazote tu akimchukia mtu Fulani, kwa kuhisi tu mtu huyo anasifa Fulani mbaya.

Kwanini fitina ni tamaa?

Marazote wenye fitina huwa hawawezi kukinzana na hali yao ya chuki dhidi ya wapinzani wao, kwa kuwa sababu zao huwa hazitokani na sababu za nje ambazo wangeweza kuzitatua, huwa zinatokana na sababu zao za ndani za tamaa. Sababu za kutamani wapinzani wao wadhalilike, au wafeli, ili wao waweze kuwa na nafasi, au amani.

Faraka - Sedition

ni hali ya kuibua hisia za ukaidi dhidi ya mamlaka, au mfumo Fulani uliopo. Mfano, penginepo mwenye faraka angeweza kuibua hisia za kuwa, mwandishi wa kitabu hiki ni mkaidi, na anachochea chuki dhidi ya mifumo yenye nguvu. lakini ili maana ikamilike ya faraka, lazima tuangalie dhumuni la hoja ya ukaidi. Mwandishi wa kitabu hiki angeonekana akiwa na lengo la Upendo, na kuikoa jamii kwa upendo, na amani, bila hasira, uadui na ugomvi. Lakini mwenye faraka huwa na dhumuni la Tamaa, la kuchafua hali iliyopo, ili aweze kupata nafasi ya kuwa juu ya wengine.

Wenye faraka wengi sana utawagundua kwa namna huwa hawana taarifa za kutosha kuhusiana na hoja wanazozichafua, wengi wao huwa hawana kiasi, waropokaji, hii yote ni kwa kuwa, hisia za faraka zinatokana na matatizo ya kisaikolojia. Na faraka huambatana moja kwa moja na hisia za uadui, na hisia za ugomvi.

Uzushi - Heresies

Uzushi unatokana na hali za kuzusha. Kuzusha kunamaanisha kuibua. Kuibua kunamaanisha kutoa toka sahihi, na kupindisha. Kwa kiingereza unaweza tumia neno ‘’deviate’’. Wazushi ni watu ambao huibua hoja zao toka kwenye ukweli, na kuzipaka rangi na kuzizusha. Wapo ambao hufanya makusudi wakijua, lakini wapo ambao hufanya wakiamini wamegundua udhaifu uliokwepo.

 kwanini uzushi ni tamaa?

Marazote wazushi hutamani kupata heshima, na sifa, toka kwa watu, kama wao ni watu makini kuweza kugundua udhaifu uliopo. Wazushi huwa na tamaa ya kuwa nje na mifumo yao, ili kuonekana wao wapo makini zaidi, au wenda, wao wana uwezo mkubwa zaidi. Wazushi wote hawana kiasi, wazushi wote hutumika sana kuchafua mamlaka na mifumo safi kabisa. Wazushi wengi huwa wasaliti, na wengi wao huwa ni wagonjwa wa kisaikolojia.

Saikolojia ya fitina, faraka & uzushi

Wote wenye sifa kati ya hizo juu tatu, huwa na tatizo moja kubwa. Huwa hawana uwezo wa Kuzingatia na kutawala hisia zao. Wengi wao ni wadhaifu wasio na uhuru wa kifikra ‘’open mindedness’’. Huweza kupata ukweli, lakini kwa kuogopa kubadilisha misimamo yao kwa kufatilia kwa kina, hupuuzia. Wengine hawana hata uwezo wa kufatilia mambo kwa umakini sana hata wakayaelewa, na hujikuta wakizusha tu. 

Wenye fitina wengi huwa na namna ya tofauti kidogo ya wivu, na hushindwa kutatua changamoto zao kwa hisia za uadui, na huishi Maisha feki ya chuki kwa majirani wao, huku wakiwatamania mabaya. Haya yote ni makundi ya tamaa. Na yote ni matokeo ya upungufu wa nishati katika ubongo.

Ulevi - Drunkenness

Unaweza soma kitabu changu Volume 02 kuelewa kiundani madhara ya afya kwa ulevi, na madhara ya pombe kuanzia tumboni, katika ini, mpaka katika ubongo. lakini unapozungumzia ulevi, unazungumzia madhara ya kupoozesha, au kulewa, au kuzubaisha akili, kwa kutumia vileo, ambapo hasa zaidi ni pombe. Zipo namna nyingi za vitu vya kulevya, kuna madawa ya kulevya, kuna bangi, shisha, n.k.

Kwanini ulevi ni tamaa?

Tofauti ya mlevi na mchawi, ni kuwa mchawi akishalewa anazungumza na mapepo, lakini mlevi akilewa anarudi nyumbani. Wote kwa Pamoja wanakimbia uhalisia wa Maisha yao ya kawaida. Mlevi anaamini akishakunywa pombe, ataingia katika hali ya utulivu wa kiakili, na katika namna mbalimbali walevi hujikuta wakishakuwa waraibu, hii ni kutokana na matatizo ya ubongo katika sensa, au ‘’receptors’’ za ubongo, kama ‘’GABA, na Glutamate’’, na hata ‘’Dopamine’’, unaweza soma vol 02 kuelewa kiundani uraibu wa pombe ‘’alcohol withdrawal syndrome’’.

Ulevi ni tamaa ya kuwa huru toka katika uhalisia wa Maisha ya kawaida. Watu wengi ambao huchochea ulevi, huchochea hali za kiburi, za kutowaza, za kutojali. Wasomi wengi hawajui madhara ya pombe huanza hata kabla ya pombe, wengi huanza na kiburi na kujipa hisia za kutojali hata kabla ya kunywa, na hapo ndipo unapoweza kuthibitisha hisia za tamaa, za kutaka kuwa nje ya mfumo wa akili za wengine, ambapo kwa mlevi ni wote mnaomtaka asinywe. Hali ipo hivyo hivyo kwa wavuta sigara, bangi, shisha, madawa ya kulevya, n.k. kiufupi matatizo huwa makubwa sana kabla ya wengi wao kuanza, lakini short cut ya kufikia hali bora kabisa ya kiakili kupitia ulevi ndiyo huwaathiri wengi.

Haiitaji nguvu kutambua kuwa walevi wote hawapo sawa katika ubongo, wote wana upungufu wa sensa za GABA, wana kiwango kikubwa sana cha sensa za Glutamate, wengi wao wanashida mbalimbali za ubongo. ulevi ni tamaa iliyodhahiri zahidi kwa kuonekana kwa upungufu wa nishati katika ubongo.

Ulafi - Revellings

Ulafi ni hali ya kushindwa kujitawala katika hamu ya chakula. Ulafi ni tamaa ya kula mpaka mwisho. Marazote ili mtu awe mlafi, lazima mfumo wake wa ubongo wa hamu za kula, na kuridhika kwa chakula uathiriwe ‘’disruption in orexigenic pathway’’. Na vyakula ambavyo vinaweza kumuathiri mtu hata akaingia katika hali hii ya ulafi nimevielezea vizuri sana katika Vol 02.

Kwa ufupi sana, Ulafi hutengenezwa zaidi ya kutokea kwa asili. Watu wengi walafi hufikia hatua hiyo kwa kula sana vyakula vyenye msisimko mkubwa sana wa Ladha, kuliko wastani wa asili. Madhara yake mfumo wa homoni wa hamu za kula huathirika. Mfano mwepesi ambao huwa napenda kuutumia ni kuwa, kijiko kimoja cha sukari ni wastani sawa na mtu anayekula mita moja ya muwa, lakini mtu mmoja anayekunywa soda moja tu, huwa na wastani unaokaribia wa vijiko kumi vya sukari. Hiyo ni sawa na kusema mtu anayekunywa chupa moja ya soda ni sawa na mtu anayekula mita kumi za muwa, jambo ambalo linaonyesha ni triki tu ya ubongo iliyochezwa na wazalishaji wa bidhaa hizi.

Ulafi hukua kwa matumizi ya vyakula vyenye vichocheo vingi kupita wastani unaohitajika, mfano, sukari nyingi watu ambayo hutumia katika bidhaa za kisasa huwa kiundani haihitajiki mwilini, watu wengi hula nyama kwa kiasi ambacho kiundani hakihitajiki mwilini, mfano, kwa wiki nzima mtu mzima angehitaji nusu kilo tu ya nyama, na hapo bado takwimu huonyesha ni nyama ambayo angebidi kuipunguza zaidi. lakini watu hutumia maranyingi zaidi ya wastani. kiwango cha pombe ambacho mwili ungekivunja ni kidogo sana na uhalisia wa kiwango ambacho watu hutumia hata kulewa. Haya yote yanachochea kuwa, ulafi hutengenezwa sana kwa triki za kiakili, ambazo nilizielezea sana katika vol 02.na hasa, ni kucheza na uzalishaji wa homoni ya msisimko ya dopamine, na kuchochea tabia za ulafi.

Walafi wengi sana sio wakarimu, hawana kiasi, hiyo yote ni kutokana na tamaa zilizokithiri za vyakula, ambazo huwaathiri hata afya zao za kiakili.

Ufisadi Na Wizi

Ufisadi ni neno linalomaanisha matumizi mabaya ya mali za umma kutokana na mamlaka. Ufisadi huwa na familia yake ya tabia, kama vile rushwa, wizi, n.k. ufisadi moja kwa moja ni tamaa ambayo inatokana na kutamani zaidi ya mamlaka uliyopatiwa, na kibaya zaidi, mafisaidi wengi huwa ni wasiri sana wa wizi wao wa mali za umma. Tofauti ya fisadi na mwizi ni kuwa, mwizi hutambulika na husukumwa na tamaa zinazotokana na kutokidhi hali yake, au hata tabia ya kutamani zaidi kwa njia ya kuiba. Lakini fisadi huwa ni mtu asiye mwaminifu kwa ndani, lakini kwa nje kuvaa huusika mwingine. Fisadi ni mnafiki kwa mamlaka anayoshikilia. Mara nyingi fisadi hupelekea madhara makubwa zaidi ya mwizi, kwa kuwa huwa na nafasi rahisi na endelevu zaidi ya kuiba, na hata kujilinda dhidi ya kugundulika. Watu hawa huwa wanatamaa sana, na huvikwa roho ya ubinafsi, na ukatili, na hata uuaji kwa wanaowagundua. Mungu huwachukia sana watu wenye tamaa hata wakafikia hatua hii.

Ubongo mweusi tambua kila mtu aliye na hisia za wizi, huwa na upungufu wa mfumo wa homoni wa kuhisi hisia za wengine. Kadri unapokuwa na jamii ya watu wasio na uwezo wa kuhisi hisia za wengine, yaani ‘’Antisocial’’, kama ‘’Socialpath’’, lazima utakuwa na idadi kubwa ya watu ambao kwao kuiba huwa ni fursa, kama fursa zingine za kiuchumi. Watu wengi hawajui kuwa Wizi huwa na uraibu mkubwa sana kuliko hata ulivyo uraibu wa Utazamaji wa Picha za Ngono. Ripoti nyingi sana zimewahi andika kuonyesha jambo lolote lile linaloweza mpatia mtu Pesa, bila kutumia nguvu nyingi, humfanya mtu kushindwa kabisa kuliacha. Na hii ndiyo sababu vijana wengi hushindwa kuacha kucheza michezo ya kamali. Ambayo inachochea zaidi hamu ya kuiba kwa kuzoelea fedha kirahisi.

Haiitaji nguvu pia kujua wezi wengi huwa ni wagonjwa wa udhaifu wa mfumo wao wa homoni, kama za Oxytocin, au uwezo wa kuguswa kupitia mifumo yao ya ‘’MNS’’ iliyopo katika ubongo. kumsaidia Mwizi kwa ushauri huwa ni jambo gumu sana, lakini unaweza msaidia kwa kugundua kuwa shida yake ni zaidi ya shida ya kiosaikolojia katika mantiki ya kimaamuzi, bali ni shida iliyo katika mantiki zaidi ya kihomoni. Kumbuka, si rahisi kugundua kirahisi tofauti hizi kwa test za maabara. lakini ni Dhahiri sana kwa mtu atakaye fatilia shida hizi kwa kuchimbua kwa kina saketi au chaneli za ubongo, za sehemu hizi za kuhisi hisia za wengine katika jamii, na namna sehemu hizi zimeathiriwa kwa uraibu ambao watu hawa hupata kila wanapofanikiwa kwa kuiba.

Usilojua Kuhusu Uuaji

Watu wengi hawajui kuwa wauaji wengi, huwa ni kama Daraja la juu la wezi na mafisadi. Watu hawa huwa ni watu ambao huwa wamepitia badiliko kubwa sana la kisaikolojia, yaani wameweza kuvuka hisia za hofu ya kuua. Marazote binadamu huwa tuna hofu ya damu, ambayo hii hutufanya kuchangamana sana kijamii. Unapoweza kumwaga damu, mara ya kwanza huleta shida kubwa sana ya kisaikolojia, ambayo watu huitafsiri kama Hatia. Na hii huwa hata kwa madaktari wote tunapoanza kuchana miili ya Wanyama. Inapotokea mtu akaishinda hii hofu, aidha kwa kuendelea, au kwa kuipuuzia, Kisaikolojia watu hawa huwa katika mithili ya hali ambayo nimeamua kuiita ‘’Oxytocin resistance’’. Ambalo sio neno rasmi kitaalamu, lakini ni msingi wa kuelewa namna mifumo ya homoni ya kuhisi kiubanadamu huwa haina nguvu tena za kumuunganisha mtu na wenzake. Hii unaweza iona pia kwa wachinjaji wa Wanyama. Wengi wao huwa sio sawa kisaikolojia kama ripoti kadhaa zinavyoonyesha. Na sababu kubwa huwa shida za muundo huu.

Kumbuka, Uuaji, na wizi, na ufisadi, zote hizi ni namna ambazo unaweza kuzisema kama ni upungufu wa nishati katika ubongo. hii ni kwa kuwa, shida hizi zote zinatokana na mfumo wa tamaa uliokithiri, ambao ni mgumu sana kwa mtu ambaye atauangalia katika mtazamo wa kitabia tu, au maamuzi. Watu huogopa kuanza kuiba, au kula rushwa, au kuua. Lakini wanapofanikiwa, na kuishinda ile hisia. Huwa ni mithili ya mwanamke aliyetolewa ubikra. Kumbuka, kama utataka kulijua hili kiundani zaidi, unaweza kuanza katika mantiki ya kisaikolojia, kuelekea kifiziolojia, na kisha ki epijenetikia, ambapo hapo sasa ndipo utapata madhara mapya ya kifiziolojia kama kihomoni, na kisha uzoefu mpya tena.

siri ya 02

Mtu anapofanya kazi yoyote ile, malipo ya pesa anayoyapata hubeba uzito wa kazi aliyoifanya katika ubongo. kipindi mtu anafanya kazi, ubongo wake huzalisha stress nyingi sana. Na mwili huzivumilia stress zote za kazi kwa kuzalisha homoni za dopamine, ambazo humpa mtu motisha ya kuamini atakapoimaliza, atakuwa katika hatua bora zaidi kwa wakati ujao. Mtu anapomaliza tu kazi huwa na hisia za furaha zaidi, si kwasababu ya dopamine, ila kwasababu ya kemikali za endorphins ambazo huzalishwa mtu anapomaliza kazi. Sasa basi, inapotokea mtu akapatiwa malipo ya pesa bila kazi. Yaani amepata pesa bila kazi, au pesa kubwa kuliko kazi. Katika mazingira haya, Ubongo kwanza husisimka sana. Na hii ni kwa kuwa huzalisha homoni za mhemko nyingi tena zisizokuwa zimetokana na stress za kazi, hivyo huwa juu zaidi, kiasi cha kupeleka uraibu wa mbinu hiyo. Ubongo sasa utahitaji kubalansi mhemko huu, na hapo Ubongo utabidi utengeneze hisia za stress, ili kubalansi mhemko huu mkubwa sana wa pesa bila kazi. Hizi ndizo stress huwapata watu wote wanaopata pesa kuliko walivyowekeza, wengi wao utawaona wakiwa wamewehuka sana, hawawezi kufikiria vizuri, na hupata ahueni baada tu ya kuzimaliza pesa zao.

Ubongo mweusi kamwe usitamani Pesa ya bure, wala pesa iliyo katika namna ambayo haitakugharimu. Inahitaji akili nyingi sana katika sayansi za ubongo kuweza kuelewa kuwa Pesa ambayo mtu huibeba, ni lugha nyingine ya shilingi ya nishati ya ubongo. unapaswa kutambua kuwa mtu yeyote anayefanya kazi, mfano mtu anayelima mahindi. Kiwango chote cha nishati au nguvu anayoitumia, Ubongo huwa unaitambua. Ubongo huwa una nukuu viwango vyote vya nishati ambayo mtu huitumia kwa kazi. Na nishati hii ambayo mtu huwa anaitumia, huwa ni namna ya uwekezaji wake kwa ajili ya kesho ‘’future saving’’. 

Ubongo huwa na motisha ya kuwekeza kwa ajili ya kesho yake, na namna hii hutumia sana kemikali kama za Dopamine, na zinginezo hasa za endorphins, na homoni zingine. Ubongo huungana na kazi yake, na hii ndiyo sababu mkulima wa mahindi anapoona mahindi yake yanakua vizuri, anahisi furaha kubwa sana. au pia anapoona mahindi yake yanaathirika, naye anaathirika. Mkulima wa mahindi anaweza hata kuyaota usingizini mahindi yake. Mahindi anayoyalima ni sehemu ya nishati yake ya mwili. Wengi hawajui kuwa nguvu zote za misuli unazozitumia katika kufanya kazi, yaani ‘’ATP’’, huwa ndizo zikibadilishwa kufanya kazi ya kusafisha shamba. Au kufanya kazi yoyote ile. hili badiliko la nishati unaweza liita kama badiliko la nishati ya kemikali ‘’chemical energy’’ Kwenda nishati ya mekaniki ‘’mechanical energy’’. 

Na nishati yote ambayo Ubongo huwa umeitumia kufanya kazi, au umeipoteza, huwa inatunzwa katika ubongo kama Kumbukumbu ya hisia za mapenzi ya hiyo kazi. Namna mapenzi yanavyotunzwa kama hisia, huwa katika mfumo wa kemikali ambazo ubongo huzitambua kuhisi mapenzi. Sasa basi, kwa namna mahindi ya mkulima huyu yanavyobadilishwa tena kuwa Pesa, mfano baada ya kuyauza. Ubongo bado huitazama pesa kama nishati zake za mwili, au ‘’ATP’’. Ubongo huitazama pesa yake uliyoifanyia kazi kama kiwango cha damu iliyotumika kufanya kazi, kiwango cha maji yaliyotumika, kiwango cha homoni, kiwango cha metaboliki zilizotumika mpaka kuikamilisha, n.k.

Ni hatari kupenda Pesa bila kazi ya kukuchosha mpaka kufikia thamani ya pesa hiyo, iwe kazi ya kutumia sana akili, au ya kutumia sana misuli. Watu wengi wanaojizoesha wizi hushindwa kujizuia na kazi hizo, hii ni kwa kuwa huwa hawawezi kufanikiwa. Maana pesa bila kazi huathiri saikolojia ya kuweza kufanya mipango. Lakini pia hata kutojali nishati ya mwingine kupitia pesa yake, ni dalili ya kutokuwa sawa kiafya ya akili. Wanawake wengi ambao hupenda sana pesa za wanaume, hujikuta wakishindwa kujizuia kuingia katika uzinifu na wanaume hao, hata bila kupenda. Sio kwakuwa hufanya hivyo ili kuwalipa, la hasha, kila unapopatiwa na mtu pesa, anakupatia nishati ya Ubongo wake, iliyo katika namna ya kimekaniki, au Shilingi. Pesa ni sarafu ya Ubongo. Mshahara wa mtu, ni damu ya mtu kibiolojia. Hawajakosea watu wanaosema Pesa ya mtu ni Nguvu yake. Hata unapompatia mtu pesa yako kwa nia njema, bado huwa unajenga upendo mkubwa sana baina yenu, maana huwa ni mithili ya muunganiko wa nishati za ubongo wenu. Na hii ndiyo sababu hata Mungu hupenda sadaka, au hata waganga hupenda kafara! Ni hatari kupenda, au kupatiwa pesa kuzidi uwezo wako kama tulivyokwisha kuona. Na hii ndiyo sababu utajiri katika umri mdogo huua zaidi ya kujenga.

Ni hatari zaidi kupenda Pesa za umma ambazo ndizo Nguvu za watu wengi sana. Kadri unavyozifisaidi, ndivyo ubongo wako unavyozidi kushindwa maana halisi ya nishati na kazi. Mhemko huwa mkubwa, na shida za kisaikolojia huwa kubwa zaidi kama walivyo Viongozi wengi wa kisiasa mafisadi. Biblia imewahi Andika, ilipo hazina ya mtu ndipo ulipo moyo wake. Basi kumbe kila unapohujuma hazina za watu, unahujumu mioyo ya watu. Kumbuka moyo ni Ubongo, na hazina ni nishati. Ubongo mweusi tambua hakuna takwimu za viongozi wengi walio wahujumu wa nchi zao kama viongozi wa Afrika. Na hii ndiyo sababu ugonjwa wa Umasikini kwa wananchi, na Ujinga kwa Viongozi umekuwa Sugu sana katika Nchi zao.

Uzinzi, Uasherati & Uchafu (Adultery, Fornication, Uncleanness, Lasciviousness)

Uzinzi ni tendo la ndoa kabla ya ndoa, kwa wasio wanandoa. Uasherati ni tendo la ndoa, kwa mwenye ndoa, na asiye na ndoa. Uchafu ni matendo yote yanayohusiana na kufanya mapenzi katika namna zisizo za kimaadili, au za kisasa zaidi kama utazamaji wa filamu za ngono, na kutumia vitu, au namna zisizo za asili katika kujiridhisha kimapenzi. Katika Vitabu vya Dini kama Biblia, huonekana Lusifa anapenda sana kutumia tendo la ndoa ‘’sex’’ tangia zamani sana za kipagani. hupenda sana hisia hizi za mapenzi kwa kuwa, huwafanya watendaji kuwa dhaifu sana kiakili. Hii ni kwasababu marazote mapenzi husisimua sana hisia kiasi cha kuzimisha kabisa sehemu za ubongo za kutafakari, na matokeo yake ni kuwa, watu wengi huwa hatarini sana kuvamiwa na roho chafu, au hata Kujawa na uraibu kwa kushindwa kujitawala kihisia, pale yanapofanyika kinyume na utaratibu wa kiasili. Marazote jamii za kipagani, na taasisi za kiumizimu huusisha mionekano ya utupu, au hata matendo ya kiuzinzi. Huku husemwa kuwa Lengo hasa huwa ni kudhoofisha kabisa uwezo wa kiutambuzi wa watu. Husemwa pia kuwa Lusifa hasa katika mitindo ya kisasa amechochea zaidi uhuru wa tabia za uchafu wa kingono kupitia miziki, filamu, na mitandao ya kijamii.

Kama tulivyoangalia katika Vol 02, kadri watu wanavyoangalia taswira zozote zile, huwa wakijiunganisha nazo, hii tuliona kupitia uwepo wa seli za kuiga, yaani ‘’mirror neurons’’, katika maeneo ya juu ya ubongo kama ‘’premotor areas’’, maeneo haya huusiana na msisimko wa mwili moja kwa moja. Kadri watu wanavyotazama taswira za uchi, ndivyo wanavyoingia katika msisimko wa via vya uzazi, na kutamani zinaa moja kwa moja. Hoja sio kutamani tu zinaa, hoja ni kuwa, kadri watu wanavyoingia katika hisia za mapenzi, au ngono katika mazingira yasiyo na uaminifu baina yao, hata Imani zao, huwa katika hatihati ya ubongo wao kuwa hatiani kuvamiwa na roho za uchafu kwa mantiki za kidini, lakini kisayansi huwa ni athari nyingi za mifumo ya kihomoni na kisaikolojia. Wanasayansi wengi hawaamini roho hizi, lakini huamini Aliens, au hata Multiverse, na wakati huohuo wengi wao huwa wanachama wasiri wa vyama vya kishetani. Wapo baadhi ni wahanga kabisa wa Imani za ushirikina, lakini kwa nje hujifanya hawaamini Imani za roho hizi, injili ya sayansi haina muda wa kuhangaika na wasomi wanafiki.

Tabia Za Kujichua (Masterbation) Na Pornography

Hawa wote ni kielelezo cha ngazi ya juu kabisa ya tamaa. Yaani mtu anatamani kitu ambacho hakipo pale, na ubongo wake unatengeneza uhalisia wa kana kama yupo pale. Hakuna mwanamke aliyelala kwa ajli ya zinaa, lakini mtu kupitia network yake ya Ubongo, ya ‘’Default mode network’’ anamtengeneza binti kichwani, anampeleka katika sehemu yake ya ubongo wa mbele, anamuandaa, na sehemu yake ya hisia inasisimka kiasi cha kuchochea Ubongo sehemu ya Hypothalamus-tezi ya pituitary, mpaka via vya uzazi vinasisimka kwa ongezeko la mtiririko wa damu mithili ya mwanaume anayefanya zinaa halisi, mtu huyu mfumo wake wa PSNS ‘’parasympathetic nervous system’’ husisimka na kumfanya aendeleze mhemko wa via vyake kama mtu aliye kwenye zinaa kweli, katika vol2 nilielezea madhara wanayopata watu hawa kiafya, lakini katika sehemu hii nalenga kuonyesha namna watu hawa mfumo wao wa ubongo unavyoathiriwa, na kutengeneza mazingira hatarishi sana kisaikolojia, kuwaathiri kakuwaathiri katika sehemu zao za ubongo wa mbele, na kuwatengenezea uhalisia na uraibu, na hata kuwa wahanga kabisa kifikra.

Tabia Za Uchafu Wa Kingono

Mara nyingi watu hawa huwa wamejawa na mihemko ya ngono iliyovuka wastani wa kawaida. Kwanini? ni kwakuwa maranyingi watu wenye uchafu katika mitindo ya kingono, huwa tayari ni wahanga wa hatua za kwanza za ngono. Wengi wao kama tutakavyoona katika sehemu inayofuata, huwa hawasisimki tena na utendaji wa ngono katika mitindo ya kawaida. Wengi wao huwa hawana nguvu za kiume aidha, au huwa wahanga wa mitindo ya zinaa tangia udogoni, hivyo huwa wakitafuta namna za kujiridhisha zaidi, maana ubongo wao huwa na msisimko mdogo zaidi kwa njia za kawaida za tendo la ndoa.

Utazamaji wa filamu za kisasa zilizojaa picha, na mionekano ya kizinaa tangia umri mdogo, huathiri ukomaaji bora wa ubongo, na uwezo wa kuwa na kiasi katika kutawala mihemko ya kimwili. Wanaume ambao huwa na tabia za kishoga wengi wao huwa hawasisimki kabisa kwa tendo la ndoa la asili kati ya wanaume, na wanawake. Hakuna shoga anayeingiliwa kinyume na maumbile akawa sawa kiakili, lazima atakuwa alikuwa mwathirika wa PTSD awali, lakini baadaye akajifunza uwendawazimu. Unaweza elewa zaidi hili katika sehemu zijazo, kujua zaidi hoja hii yenye misingi mipana katika fiziolojia ya ubongo. Kumbuka Kiufupi hisia za mapenzi huwa hazihusishi uwezo wa kutafakari, na kama utaweza kuwafanya watu wasitafakari, hata wenye maarifa makubwa unaweza kuwateka katika gari la uharibifu. Kwa wastani katika mitandao ya kijamii, huwa kuna picha za wanawake wanaojipost 3 mpaka 4 kwa1 ya wanaume. Hii ni kwa mitandao kama Tiktok, Instagram, na Facebook ikiwa kwa wastani mdogo kidogo.

Watu wengi hawajui kwanini picha nyingi zaidi huwa ni za kike, sababu ni kuwa, wanaume husisimka sana kwa kutazama, zaidi ya wanawake. Ambapo wanawake husisimka zaidi kwa mambo wanayoyasikia, na hii ndiyo sababu wanawake hushawishiwa sana na mienendo ya kijamii, kama nilivyoeleza katika sehemu inayofuata. na hata sehemu za ubongo za wanawake za lugha zimeendelea zaidi ukilinganisha na kwa wanaume. Wanaume huathiriwa zaidi na mitandao ya kijamii kwa kuamshwa kitamaa kwa ngono, huku wanawake wakiathiriwa zaidi kwa mitandao ya kijamii, kwa kutamani Maisha ya kifahari na kuwa na wafuasi wengi. Haya yote ni matokeo ya tamaa, na huchochea tamaa, na humtukuza lusifa. haiitaji nguvu nyingi kuelewa kuwa haya yote ni matatizo ya kihomoni, na sheria husema kuwa, homoni ndizo kemikali zinazoongoza mawasiliano ya Ubongo, na seli za mwili, ili kutawala metaboliki zote za mwili. Kadri unavyoathiri homoni, unaua mfumo mzima wa metabolikia za mwili. Na kazi kuu ya metaboliki za mwili, katika Ini, ni kuzalisha Nishati. Na nishati nyingi zaidi za mwili, huwa katika Ubongo, zaidi ya asilimia 20%. Hawa wote unaweza wasaidia kwa kutatua tatizo halisi, kwa kuwaelekeza katika njia ipasayo zaidi, na sio kuwashauri kuacha, ukizichukulia shida hizi kama matokeo tu ya maamuzi, au tabia. Kumbuka, katika sehemu zijazo, tutaona watu wengi wanaingizwaje kwenye changamoto hizi, tena bila hata wao kutaka.

Saikolojia Ya Uongo

Uongo ni miongoni mwa matatizo sugu ya binadamu kwa karne na karne. Watu huongopa kwa siku kwa maranyingi sana. Zipo nyakati ambapo watu hudhani wenda Uongo unaweza kutumika hata kwa malengo mazuri kabisa, kama ya kuokoa, au hata kuhamasisha. Na uongo ni miongoni mwa matatizo ambayo ni magumu sana kukosekana katika kazi yeyote ile ambayo mwanadamu huweza kuifanya. Watu wachache sana hutambua kuwa hata Ripoti kubwa za tafiti za sayansi huwa hatiani, na mara nyingi sana hukumbwa na taarifa ambazo huwa sio sahihi kwa asilimia zote 100%, mahitimisho mengi ya tafiti hupuuzia matokeo yasiyokinzana na matakwa ya watafiti. Watafiti wakubwa wasayansi ndiyo huwa wamwisho kukubaliana na matokeo ya tafiti za wanasayansi wenzao. Idadi kubwa sana ya watu wanaohamasisha mambo kwa jamii, wao wenyewe huwa ni wahanga wakubwa wa hamasa zao, lakini huongopa kana kama wao wako vizuri kwenye wanayoyasema. Hata viongozi wakubwa wa kidini, wengi wao huwa hawawezi ishi uhalisia wa mafundisho yao, lakini ndiyo huficha zaidi madhaifu yao, hizi zote ni aina za uongo.

Jambo kubwa sana linalowatesa wanasayansi wengi, la kuweza kutambua kuhusu nini hasa chaweza kuwa chanzo cha tabia hii ya uongo ni kuwa, ni tabia ambayo ni ngumu kuweza kuieleza kama ni shida ya ubongo, au ni maamuzi tu ya mtu ya kutaka kujinasua katika hali Fulani isiyofaa. Mfano unapokamatwa na mpenzi wako umemdanganya kwa kukutwa na mpenzi mwingine. au unapokamatwa umeiba na unapambana kujitetea kwa kuongopa kuwa haukuwa mhusika mkuu. Mfano mwingine Dhahiri sana ni kuwa Idadi kubwa ya wanaume hutumia sana mbinu ya Uongo kuwahadaa mabinti, ambao huusikiliza sana uongo wa wanaume na kuwa na umakini nao, jambo tutakaloliangalia zaidi kisaikolojia kwa sehemu zijazo. Pia idadi kubwa ya wanawake hutumia sana mbinu ya uongo wa kimwili, kuwahadaa wanaume, ambao wao huwatazama sana wanawake, na kuwa makini sana na mitego yao ya uongo wa kimapenzi. Ijapokuwa bado huvutiwa na uongo huu.

Kupitia Shoo hypothesis unaweza elewa kirahisi sana msingi ulionyuma dhidi ya tabia hizi za uongo. Inasikitisha sana kugundua kuwa Pamoja na kuwa binadamu huzaliwa vizuri sana, na kwa ufasaha mkubwa sana, lakini bado binadamu yeyote yule huwa na mapungufu. Udhaifu huu huwa ukitokana na maamuzi ya ndani, au msukumo wa nje wa mazingira. Binadamu yeyote yule huwa akiuchukia udhaifu ulio ndani yake. Na hii ndiyo sababu rafiki yangu Daktari na Mwanamuziki Anatory Fidel aliwahi kusema, ‘’watu hujiangalia zaidi katika kioo kuutafuta udhaifu walio nao na kujikosoa, au kuutoa, na sio kuuzingatia sana uzuri walio nao’’. Wasanii wengi huwa hawaamini uzuri wa sauti zao, wasomi wengi huwa hawaamini ubora wa kazi zao, wanamitindo wengi huwa hawaamini mvuto wa mionekano yao, na hata wapambanaji wengi huwa hawaamini ukubwa wa nguvu zao. Marazote huitaji watu kuwathibitishia, lasivyo hujikuta wakipoteza muda mwingi sana katika kujitathmini, kujikosoa, na hata kujikatisha tamaa na kuacha. Inashangaza hata Isaac Newton mwenyewe hakukubaliana sana na kazi yake yote ya sayansi, kiasi cha kutopanga kabisa kuichapisha na watu waipokee, hata alipochochewa zaidi na rafiki yake. 

Ni muhimu watu kutambua kuwa hata katika ngazi ya jenetikia, kila mtu huwa ana vinasaba vya kuwa namna yeyote ile, mfano unaweza kuwa na rangi yeyote ile, maana sote tuna DNA zenye maelekezo ya kuwa vyovyote vile, ila siku zote, mfumo wa seli huchagua aina moja tu ya mwonekano, ambayo hufaa zaidi katika mazingira husika. Binadamu huwa hivyohivyo, huwa na aina mbalimbali za uhalisia, lakini huchagua kuuvaa uhalisia wa namna moja tu. Binadamu katika ngazi ya utambuzi, mpaka ya jenetikia, huchagua uhalisia ulio bora zaidi. Ubongo marazote inapofika mfano asubuhi, ijapokuwa huwa unatambua kila namna ya udhaifu ulionao, huchagua namna ya kuonekana kwa ubora au ushajaa zaidi. Baada tu ya kupevuka, hakuna binadamu ambaye hukubali kuonekana kwa udhaifu, kila mmoja huelewa kuwa asili imejificha katika mwonekano wa ubora. Ukiingia katika darasa la vijana wa kidato cha Nne, kila kijana hupambana kuonekana imara zaidi, ijapokuwa uhalisia wao huwa ni majuto, na maumivu makubwa sana yanayoendelea ndani kwa ndani.

Uongo huzaliwa kama namna ya mwili kuutetea uimara wake, pale unapoona umeshindwa kabisa kwa uhalisia wa kiviungo vyake. Tunatambua kuwa pale mtu anaposhindwa Kutenda, husema maneno. Maneno huwa silaha ya mwisho ya mtu aliyeshindwa. Tamaa huibuka hapa, watu hutamani kufikia viwango ambavyo wasingeweza vifikia kiuhalisia, kwa kutumia maneno. Na hapa ndipo utaona kila binadamu kwa asili akigubikwa na vazi la uongo. Wanawake kwa kupingana na uhalisia wa mionekano yao dhaifu, hupambana kuonekana na mionekano feki. Wanaume kwa kukataa udhaifu wao, hutumia ngonjera za uongo kujikweza. Wanasiasa kupingana na udhaifu wao majukwaani, hutoa ahadi feki tamu. Wasomi ambao ilihali wakijua kwa dhati kabisa hawana maarifa ya kutosha, hujivika vyeo vya heshima kwa sifa za midomo. Kibaya zaidi, watu kadri wanavyozidi kuwa wadhaifu huku wakizidi tamaa, sasa huanza kutumia uongo kama silaha ya kupambana hata waliposhindwa. Uongo ni ugonjwa wa udhaifu wa nishati ya ubongo. kadri mwanadamu anavyozidi kuwa bora, ndivyo mwili wake huweza kukidhi viwango vingi vya ulimwengu wake, kuliko kutumia silaha ya mdomo.

Siri Ya 03

Ubongo mweusi tambua kuwa, mbwa koko au mwoga hubweka sana kuliko mbwa mwenye nguvu na kujiamini. Kama ulimwengu usingekuwa ukitumia maneno, ungekuwa ni wa vitendo tu, idadi kubwa sana ya waongo wasingeweza kuishi. Siku moja nikiwa napita njia mojawapo katika mashamba ya miti ya mitiki yaliyopo Ifakara, katika Kijiji kinachoitwa Mahutanga. Niligundua kuwa Miti hupigwa na jua kila siku ya uhai wake, na huchukua virutubisho vyake katika Udongo mchafu, na maji yaliyombali sana ardhini kila siku. Huwezi amini unapoung’oa mti mkubwa sana kwa mara moja namna hukauka kwa ghafla sana. hii huonesha nao una uhai unaotegemea ulaji wa kila siku, kama wa mwanadamu. 

Wanabiolojia wa mimea wanatambua namna Miti ilivyo na sayansi Complex sana katika namna inachakata maji, mwanga, kutengeneza chakula, kusafirisha kemikali, kujikinga na magonjwa, na mabadiliko ya homoni na ukuaji. Mimea ina sayansi ngumu sana. Lakini Pamoja na ugumu huu wote, mimea marazote huwa na rangi nzuri sana za kuvutia, hutoa hewa safi kabisa ya uhai ya Oksijeni, mimea hutoa kivuli kizuri sana ijapokuwa yenyewe hupigwa na jua, mimea hutoa miale mizuri sana inayoitwa ‘’Infrared rays’’ ambayo husaidia afya, na hufyonza miale ya blue rays ambayo ingeweza kuathiri afya. Mimea hutoa matunda mazuri sana kwa viumbe na makazi kwa Wanyama. Mimea hubalansi kiwango cha maji kati ya ardhini, na angani. Haya yote mimea huyafanya huku ikionekana mizuri lakini hakuna ambaye hujua kuwa, Mimea huwa inapitia wakati mgumu sana. Wakati mwingine hupigwa na jua hata kukauka, kwanza kubeba tu maji toka chini sio kazi rahisi, wakati mwingine hukatwa matawi yake, watu huipulizia sumu na kuiathiri, na huwepo vimelea wa magonjwa mengi sana ya kuishambulia kama bakteria, virusi, fangasi, na mchwa. Mpaka sasa hivi wanabiolojia wote tunatambua kuwa mimea pia huisi maumivu.

Mimea hutoa falsafa nzuri sana katika ulimwengu. mimea hufundisha kuwa hakuna anayejali udhaifu wako, kila mtu anajali uzuri wako. ili kuweza kuvuta watu kuja kwako, kama namna mimea inavuta Wanyama Kwenda kukaa chini yake, tumia uzuri wako mpaka mwisho wa uwezo wako. hakuna siku asili itakujali kwa namna uko dhaifu, au unapitia wakati mgumu. Ubongo mweusi unapaswa kujua ni jukumu lako kuwa kama mimea kwa namna unaweza kuficha udhaifu wako. hupaswi kutembea kifua wazi na machozi kulilia changamoto na udhaifu wako. asili haipo tayari kukupokea maana si asili yake.

Somo la mwisho ubongo mweusi toka katika mimea hii ni kuwa, mimea yote hupukutisha majani yake msimu wa kiangazi, na hapo huwa haitoi kabisa matunda. Mimea hufuata kalenda zake za mzunguko wa jua na dunia kuziishi sifa zake. Hupaswi kuwa mwongo. Usipende Uongo kwa kutaka kuonekana na majani katika msimu wa kupukutisha. Hautaweza kudumu. Robert Greene katika kitabu chake cha Sheria 48 za Nguvu, sheria ya 33 anasema kuwa, kila mwanadamu huwa ana udhaifu ambao kwa marazote huwa anapambana kuuficha. Mfano, kushindwa kuzungumza vizuri lugha ya Kiingereza, kuwa na harufu mbaya mdomoni, kutokuwa na nguvu za kiume, kuwa na mapengo, kutoka familia inayodharauliwa, kutokuwa na elimu kubwa, kutokuwa na rangi na Ngozi unayoitamani, n.k. siku ambayo Ubongo mweusi utaukubali udhaifu huu, na kuruhusu Ulimwengu kuutambua tena ukiwa haujali. Hiyo ndiyo siku utafanikiwa kuvuka msimu wa kiangazi kwa wepesi zaidi. Watu wengi kwa uzoefu wangu wa sayansi za ubongo huwa wanateseka sana kukubaliana na ukweli wao. Ni hatua ambayo kama utaiweza, itakubadilisha ndani ya siku moja. Watu kadhaa nimeshuhudia wakitatua shida ya nguvu za kiume kwa kuwa wawazi, huku maelfu ya wanaume wakiteseka mpaka mwisho kwa kuficha.

Kadri unavyozidi kuwa muongo, ndivyo unavyopambana zaidi na wewe mwenyewe. Unapambana na adui aliye ndani yako. Sura inayofuatia utagundua sehemu za ubongo kama ‘’Anterior cingulate cortex, ACC’’, ndizo huwa mstari wa mbele kukukosoa, na wakati huohuo sehemu kadhaa za ubongo wako kama ‘’Dorsolateral prefrontal cortex’’, zinazidi kupambana kukinzana na sehemu nyenzake kwa kubuni zaidi namna ya kuufucha uongo. Nimeshuhudia Afrika ikiwa imeshamiri wataalamu wasiojua kabisa taaluma wanazozisimamia, kwa kupata nafasi kwa kuunganishwa ilihali hawastahili. Wataalamu hawa kila siku ni wagonjwa wa kazi zao. Kisaikolojia ni rahisi kuwatambua kwa namna huangaika kutumia silaha ya maneno kuziba udhaifu wao. Nimeshuhudia wasanii wengi wakijionesha wanaishi maisha mazuri, ili hali wanapokusikia kama mshauri wa afya ya akili wanakuja wakiwa na sura zao halisi za maumivu, na majuto makubwa. Wapo wanasiasa vigogo kwenye majukwaa, wanatembelea magari ya kifahari, lakini ni wagonjwa wa shida hizi za tamaa, na wengi hawana amani na kuridhika. Takwimu za miaka kadhaa nyuma zilionyesha asilimia kubwa zaidi ya mabilionea huwa hawavuki kuishi miaka 70, sababu pekee huwa ni kupambana vita isiyo na adui. Uongo ni mbaya. Uongo ni dhambi, Na dhambi inaua.

SAIKOLOJIA YA UJINGA NA UPUMBAVU

kwanini idadi ya wajinga ni kubwa?

Kufikiri kwa asili hutumia nguvu, au nishati. Na kwa mantiki hiyo ubongo hukimbia matumizi ya nishati kama ambavyo mwili ungekimbia kuamka, au wanafunzi wangeshangalia kuhairisha vipindi, au watoto wangeshangilia kutokwenda shamba siku ya mvua kali. Hii ni sawa na kusema, watu wangeacha tu kufikiria. hasa vitu vya kawaida, mtu angeona kuliko ajitese kufikiria vitu vya kawaida, ni bora tu angeacha, ili mradi havimuathiri maisha yake. tatizo la wajinga kuwa wengi linaanzia hapa,vitu ambavyo mtu huyu angeamua kuacha kuvifikiria, ndivyo vitu vilivyo na maana sana. Unakuta huyu mtu anaacha kufikiria vitu kama vifuatavyo; kwanini yeye kazaliwa, kwanini yeye amezaliwa hapo alipozaliwa, kwanini amezaliwa katika zama hizo, na hajazaliwa zama za nyuma, au zijazo. Kwanini kazaliwa kwa wazazi wake, na sio familia nyingine. 

Yeye ana upekee gani, kwanini ana udhaifu alio nao, kwanini maisha na hali ya maisha yake imekua hivyo, yeye ana jukumu gani katika maisha hayo, kwanini yeye bado ni mzima na ili hali ana mchango mdogo sana wa kujiwezesha kuongeza hata sekunde moja ya uhai wake, kwanini anapenda sana hivyo anavyovipenda, na kwanini anavichukia hivyo anavyovichukia, kwake yeye thamani ya maisha ni ipi, na ni kweli yuko sahihi kuitetea, Ana uhakika gani jamii inayomzunguka iko sahihi juu ya mitazamo na uhalisia wa maisha, Vingapi havijui, na je angeweza vijua, na nini hatma ya maisha yake na maisha kwa ujumla.

kisayansi Kama ambavyo ubongo unapenda sukari kwa sababu inaongeza nishati, na kuchukia kazi zinazomaliza nishati. watu hawapendi kufikiria kwa sababu kunachosha nguvu. watu wanavyokuwa wamechoka kabisa, ndivyo wanavyokimbia kabisa majukumu ya kufikiria, au kutumia akili. kiufupi wanakuwa wajinga kabisa. Kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha, upungufu wa ajira, hali dhaifu za afya, kukatishwa tamaa, na msongo wa mawazo, watu wengi wamechoka sana kiasi cha wengi wa watu kutopenda kabisa kutumia akili au nguvu. kila asubuhi hutaona mnyama akibakia zizini akilala, au ndege wakiendelea kulala, au mnyama yoyote akitafuta joto aendelee kulala. Wote huamka na kwenda kufanya kazi. Lakini maelfu ya binadamu hulala mpaka saa mbili za asubuhi na zaidi, hii yote ni matokeo ya uchovu, uvivu, na ujinga

Asili Ya Upumbavu

Historia ina Miongoni mwa wanafalsafa na wanateolojia maarufu sana duniani aitwaye bwana Bonhoeffer. huyu aliwahi sema katika nadharia yake ya upumbavu ya kuwa, ni afadhali adui kuliko mpumbavu. Lakini biblia pia inasema mafungu mengi sana juu ya upumbavu. Mfano, ‘’mithali 15:14. Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu’’. ‘’mithali 14:29. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. ‘’mithali 17:12. Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake’’. ‘’mithali 26:4. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; usije ukafanana naye. ‘’mithali 26:11. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; kadhalika mpumbavu afanya upumbavu wake tena’’. ‘’mithali 27:22. Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka’’. Swali huja ni kwanini upumbavu unaonekana ni ugonjwa usio na tiba. yaani unafananishwa na maiti inayotembea. maana bonhoeffer anasema adui anaweza badilika au zuilika kwa kutumia nguvu na akili. lakini mpumbavu hajitambui. Vuta taswira ‘’imagine’’ biblia inasema bora ya Dubu au adui mwenye hasira na kisasi kuliko Mpumbavu.

Kwanini upumbavu ni hatari na unakuwaje kisayansi?

Upumbavu ni kupotea kabisa kwa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, katika viwango vya juu. kutokana na kuendekeza ujinga kwa muda mrefu. ubongo kama vilivyo viungo vingine, unapoviathiri kwa muda mrefu sana, hufikia kipindi ambacho hupoteza kabisa uwezo wake. Mpumbavu ukimuambia unachokula ni sumu, ila ilimradi tu haimuui kwa hiko kipindi, hiyo ni sababu ya kumfanya aendelee kula. Kwake yeye hafanyi makusudi, au ili akupinge! Lahasha. ni kuwa tu hawezi kufikiria tena, kama ambavyo ilipaswa afikirie. Mtu huyu hakuna dawa ya kumrudishia tena uwezo wake. Zamani ili ujiunge na jeshi la marekani. ilimpasa kila mtu apimwe uwezo wake wa akili, kupitia IQ tests. na ufikie viwango

vya juu vya wastani, kwa maana mtu asiye na akili au mpumbavu. hawezi hata kujilinda yeye mwenyewe, na hawezi linda jamii.

************---------*************----------********