TOFAUTI ZA UBONGO KIJINSIA
TOFAUTI ZA UBONGO KIJINSIA
Kinachoutofautisha Ubongo Wa Kiume Na Wa Kike
Ubongo wa kiume na ubongo wa kike umetofautiana katika baadhi ya misingi ambayo ni ya muhimu kuitambua, ili kuweza kuzitambua tofauti zao kiundani zaidi. Tofauti tutaziangalia katika vipengele vya maeneo kadhaa ya ubongo, yaliyoendelea zaidi katika jinsia Fulani, zaidi ya nyingine. pia homoni kadhaa zinazopatikana zaidi katika jinsia moja, zaidi ya nyingine. Na pia mabadiliko Fulani ambayo yanapatikana zaidi katika jinsia moja, zaidi ya nyingine. na tofauti zinginezo.
Ni muhimu kutambua kuwa ubongo umegawanyika katika maeneo mengi sana. Ubongo hufanya kazi kwa kushirikiana, lakini kila eneo huwa na kazi ambayo hushughulika nayo zaidi. Taaluma hii inafahamika zaidi katika sayansi za ubongo, na inasaidia katika kujua msingi wa tabia za utendaji wa ubongo, na hata kujua matatizo ya ubongo. mfano mzuri ni pale ambapo kila sehemu katika ubongo inatambulika kwa jina lake, na pia huusika na eneo moja zaidi. hii inaitwa ‘’brain haemoncus’’. Lakini pia, ni muhimu kutambua kuwa homoni hutengeneza msingi mkubwa sana wa kuelewa tabia, kwa mfano, mnyama anapokuwa na homoni ya testosterone kwa wingi zaidi, basi anakuwa na hasira zaidi.
SEHEMU ZA UBONGO ZILIZOTOFAUTIANA KULINGANA NA JINSIA
Sehemu Za Ubongo Zilizoendelea Zaidi Kwa Wanawake
Picha hii imetolewa toka kitabu Cha Ubongo wa Kike Cha Dr Louann Brizendine'
Anterior cingulate cortex (ACC)
Hii ni sehemu ya ubongo inayohusiana na kupima yapi ni machaguo bora zaidi kati ya machaguo mengi, inahusiana na kufanya maamuzi , huitwa pia ‘’Worry-wort center’’, kwa namna ambayo huusisha sana kuhofia madhara endapo machaguo dhaifu yatafanywa. Sehemu hii imeendelea zaidi kwa wanawake zaidi ya wanaume. Hii sehemu hufanya jamii pia kujenga msingi wa kuwaita wanawake waoga katika kufanya maamuzi ya hatari. Lakini hasa ni kwasababu wanawake wameumbwa kufanya maamuzi bora zaidi yenye hatari chache. Mfano, kesi nyingi za wanawake wanaobakwa na watu wao wa karibu, huisha tu kwa wanawake kuamua kukaa kimya, hasa kwa kuangalia hatari pana zaidi za kisaikolojia na kijamii wanazoweza zipata baada ya wao kuchukua hatua, kuliko hata madhara wanayoweza yapata wao kibiolojia.
Lakini pia unaweza gundua hilo kwa namna wanawake wana uwezo mkubwa wa kukubali kuishi na wanaume hata wasiowavutia sana kimaumbile, lakini wakakubali tu kwa namna wanaume hao wanaweza watimizia mahitaji yao. Anterior cingulate cortex hutumiwa na wanasayansi wa ubongo wa tabia kuelezea tabia kama hizi, lakini bado kuna mengi pia ambayo yapo nyuma ya tabia za maamuzi ya muundo huu, kama tutakavyoendelea kuangalia. Wanasayansi wa asili huamini uwezo mkubwa wa wanawake kufanya maamuzi bora, unatokana pia na namna ambavyo fiziolojia zao huathiriwa zaidi na machaguo hatarishi. au hata namna maumbile yao hayajaumbwa kukabiliana sana na changamoto ngumu za hatari za mazingira. ‘’vuta picha ya mkono laini wa mrembo wako, je angeweza kabiliana na shughuli ya uchimbaji madini’’
Prefrontal Cortex (PFC)
Hii ndiyo sehemu inayotawala maamuzi kwa kushikilia hisia na kuzizuia zisilete shida. Hii sehemu sifa yake kubwa ni kuzuia sehemu za hisia za ubongo, hasa moja inayoitwa ‘’Amygdala’’ zisilete shida. Hii sehemu ni kubwa sana kwa wanawake, na pia huwahi kukomaa kwa wanawake tangia wanapoingia miaka ya kumi na kitu ‘’teen ages’’. Huwahi kukomaa zaidi kwa wanawake kwa mwaka mmoja au miwili kabla ya inavyokomaa kwa wanaume. Sehemu hii huwawezesha wanawake kutofanya maamuzi kwa kusukumwa sana na hisia, kama ilivyo kwa wanaume. Mfano mzuri ni namna hasira huamsha hisia za kupigana haraka sana kwa wanaume, ukilinganisha na namna ambavyo zingefanya kwa wanawake. Wanawake hufahamika sana kwa sifa zao za uvumilivu hata katika jamii. Sayansi za asili hutoa msingi uleule pia, kwa namna ambavyo wanawake huusiana sana na kazi za kulea familia zao. malezi ya Watoto wasiokomaa kimaamuzi, hayahitaji hasira katika maamuzi kama ya adhabu. na hata pia katika maamuzi ya kuchagua mwenzi, tofauti na mwanaume anayeweza vutiwa na wanawake wengi, na akasukumwa na kuweza kuchukua hatua ya kuwafatilia wote. wanawake wasingefanya maamuzi ya mtindo huo hata kama wangevutiwa. Kama ulivyo msemo unaosema, ‘’tendo la ndoa moja kwa mwanamke, laweza badilisha Maisha yake kwa miezi tisa, na kuendelea milele, lakini tendo hilohilo moja laweza lisibadilishe kabisa Maisha kwa wanaume’’. Katika kesi ya ugomvi wa kupigana kati ya mwanaume na mwanamke, mwanamke asingechagua kupigana hata kama angeweza kummudu huyo mwanaume, hii ni kwa mahesabu ya madhara ambayo akiyapata namna yatakavyo mwathiri yeye, na Watoto wake wadogo, au walio tumboni. hivyo ndivyo inavyoonekana katika ubongo pia, sehemu ya PFC kwa mwanamke imeendelea zaidi. Kumbuka, haimaanishi Wanaume hawajaendelea katika PFC. hii ni sawa na kusema, mwanafunzi wa kwanza aliyepata 100% , hamaanishi aliyepata 95% amefeli.
Insula cortex
Hii ni sehemu inayochakata taarifa zinazohusiana na Ladha, na hisia za vyakula, vilivyomo kuanzia mdomoni, harufu za puani, mpaka hali za Tumboni. Sehemu hii ni kubwa na imeendelea zaidi kwa wanawake. Hii ni sawa na kusema, Wanawake sio tu wapishi wazuri, bali waonjaji pia. Katika vol 2 nilielezea pia fiziolojia ya kuhisi Ladha, na nikaelezea namna wanawake wanavyopenda sana kulakula vitu vitamutamu kama chocolate. na hata nilipokuwa nikielezea madhara ya ulaji sana wa vitu vya sukari kwa wanawake, nikasema tabia hizi zimejengwa katika ubora mkubwa zaidi wa sehemu zao za kuhisi Ladha mdomoni na mwilini. Wanasayansi wa asili husema kuwa, ubora wa sehemu hii ya ubongo ‘’insula cortex’’ ni kwa lengo la kuwafanya wanawake kuchagua vyakula vyenye virutubisho bora zaidi kwa ajili yao, na ya watoto. Hutumia pia mfano wa namna wanawake huwa na shida zaidi ya kuhisi kichefuchefu kipindi cha ujauzito, kama namna ya ubongo wao kuongeza zaidi msisimko wa chembechembe za vyukula, ikiwemo na harufu. Hii ni ili kujikinga na hatari za chembechembe zinazoweza wadhuru Watoto wao tumboni. wanaume huwa na msisimko mdogo kidogo unaochochewa na msukumo wa Ladha katika insula, hii ni kutokana na mtindo wao wa ulaji. wanaume hula sana vyakula vyenye nishati kubwa ambavyo asili yake huwa na msisimko mdogo, mfano mihogo au mahindi, au magimbi ambavyo ni vyakula vikubwa kwa mazingira ya kiafrika. Vyakula hivi hutumiwa sana na wanaume kwa kiwango kikubwa sana, kwa lengo la kupata nishati ya kufanya kazi. Mwanaume ambae angekula kula chocolate au vitu vitamutamu vichache, angepungukiwa nishati na asingeweza tumia misuli yake kwa ubora zaidi.
Hypothalamus
Sehemu hii sio kubwa zaidi kwa wanawake ukilinganisha na wanaume, ila huwai kuanza kuonesha matokeo ya kuzalisha homoni mapema kwa wanawake kabla ya wanaume. Sehemu hii huanza kuchochea moto mapema sana kwa wanawake, baada tu ya kupevuka. Hoja ya utofauti katika sehemu hii pia imejengwa katika kazi ya hypothalamus inayohusiana na homoni za uzazi zaidi, na sio kazi zingine za hypothalamus, kama vile kutawala hisia za hamu za maji ya kunywa na kula, au matendo mengi sana yasiyo ya hiari, kama mapigo ya moyo, mzunguko wa damu, utendaji wa homoni za mwili, n.k. ni muhimu kutambua kuwa, hypothalamus hutawala utendaji wa mfumo wote wa uzazi ambao tutauangalia. Homoni za uzazi huzalishwa na tezi ambazo kazi zake ni matokeo ya kazi ya awali kabisa ya hypothalamus. Sehemu hii hutawala tezi kuu ya mwili inayoitwa ‘’Pituitary gland’’(6). Pia hypothalamus ina vipengele au nyuklia zake nyingi sana, lakini zipo baadhi tu zinazohusiana na uzazi kama vile ‘’MPOA’’ au ‘’Medial Preoptic area’’.
Hippocampus
Hii sehemu ndio inayohusiana na utunzaji wa kumbukumbu. Mtaalamu wa Ubongo Mama Brizendine anaifananisha kwa jina la ‘’Tembo asiyesahau’’. Sehemu hii ni kubwa zaidi kwa wanawake lakini pia inafanya kazi zaidi ‘’active’’ zaidi kwa wanawake, ukilinganisha na wanaume. wanawake wapo vizuri katika kuunda kumbukumbu. sehemu za mbele tutaona kumbukumbu za siku aliyofurahishwa zaidi, kerwa sana, ahidiwa, pata hisia sana za mapenzi, matendo ya huruma, bishiwa n.k. kwake kumbukumbu hizi zipo kama zilipokuwa siku husika, tafiti za wanandoa huonesha wanaume wengi wakiwa wameshasahau hata kila kitu katika baadhi ya matukio mengi yaliyofanyika miaka kadhaa nyuma, wakati huo huo wake zao wakitoa taarifa vizuri kabisa na tena katika mtiririko mzuri wa taarifa. Sayansi za asili zinakubaliana kuwa, uwezo mkubwa wa wanawake kuumba kumbukumbu vizuri zaidi, ni kwa lengo la kuwawezesha kufanya maamuzi mazuri zaidi. Hii ni kutokana na kuwa na uwezo wa kukumbuka kila taarifa vizuri zaidi, kabla ya kuchukua hatua Fulani. lakini pia uwezo mzuri wa kutunza kumbukumbu unawasaidia sana kuepukana na hatari za kupoteza taarifa za msingi, na hivyo kuepukana na hatari za kutofuata maelekezo.
Corpus Callosum
Ni vigumu kuiona katika picha juu. Hii ni sehemu ambayo inaunganisha upande wa kulia, na wa kushoto wa ubongo. sehemu hii inaonekana kuendelea zaidi kwa wanawake, ukilinganisha na kwa upande wa wanaume. Sehemu hii ina kazi kubwa ya kuchakata na kuongoza kuwasiliana kwa pande mbili za ubongo. inaaminika ubora huu kwa wanawake, unawasaidia ubongo wao kuhusianisha sana taarifa za kazi za ubongo, na hivyo kuwa na ufanisi mkubwa zaidi wa utendaji kwa matendo kadhaa ya ubongo. kuna msemo kwa wanasayansi wa ubongo huwa unasema kuwa, ubongo wa wanawake ni ‘’Complex’’ zaidi.
Broca’s Area
Hii ni sehemu inayohusiana na kutoa sauti au kutamka maneno. Sehemu hii mara nyingi huwepo katika upande wa kushoto wa ubongo kwa wanawake. sehemu hii imeendelea zaidi kwa wanawake, na wanawake huwa wanauwezo mkubwa zaidi wa kutamka na kuumba maneno, ukilinganisha na wanaume. Sehemu hii huusiana na maeneo mengine mengi ya ubongo kabla ya kufanya kazi yake ya kutamka maneno.
Wernicke’s Area.
Sehemu hii huusiana na kutafsiri au kutengeneza maana za maneno na lugha. Ipo kwenye kona inayounganisha upande wa pembeni ‘’temporal lobe’’ na ubongo wa juu ‘’parietal lobe’’. Sehemu hii imeendelea zaidi kwa wanawake. na ndiyo maana wanawake huwai kuongea kabla ya wanaume, kwa namna ambavyo wanaweza kuchakata maneno vizuri zaidi. Sehemu hii huusiana na sehemu ya uzalishaji wa maneno ‘’broca’s area’’, kupitia muunganiko wa sehemu zinazoitwa ‘’arcuate fibers’’.
Mfumo wa Hisia wa Kuiga na kuhisi Huruma (Mirror Neuron system)
Huu ni mfumo ambao huusisha sehemu baadhi za ubongo, kama sehemu ya juu nje ya ubongo wa mbele ‘’dorsal premotor areas’’, na sehemu zinginezo, ambazo huusiana na uwezo wa kutazama hali za wengine na kuzichakata kana kama ni za mtazamaji mwenyewe. Wanawake wana uwezo huu mkubwa sana. Wanaume pia hutumia mfumo huu unaowawezesha kuhisi huruma, lakini hubadilika ghafla na kuingia kwa mfumo mwingine kama tutakavyo waangalia katika sehemu yao.Mfumo wa kuchunguza na kuzisoma Sura za Vitu na uzingatiaji.
Mifumo ya kuchakata taswira za vitu au watu zimeendelea zaidi kwa wanawake. Wanawake sio rahisi kuwadanganya kimuonekano wa nje, tutaangalia zaidi huko mbele, lakini kwa tafiti nyingi, huonekana kuwa, wanawake huzibaini sura za waigizaji wa hisia Fulani mara nyingi kwa ubora, zaidi ya wanaume. Uwezo huu tangia utotoni mwao huuonesha, kwa tabia za Watoto wakike kutazama sura za vitu au watu kwa muda mrefu zaidi. huku Watoto wakiume wakiwa sio wa kutumia muda mrefu katika kutazama sura za vitu au watu ‘’poor gazers’’. Uwezo huu wa kutazama sura kwa muda mrefu, ukijumulisha na uwezo wao wa kujiunganisha kihisia na vitu wanavyovitazama ‘’MNS’’, huwawezesha wanawake kutambua hisia na hali za wanavyoviangalia. uwezo huu ukijumlisha na uwezo wao mwingine wa kukumbuka zaidi, huwawezesha kuweza kuelewa kiundani zaidi taarifa wanazozifuatilia, ukilinganisha na kwa upande wa wanaume ambao huwapasa kutumia njia nyinginezo.
Uwezo mkubwa wa kutumia Lugha na kutumia maneno (Verbal skills)
Wanawake wana uwezo mkubwa sana wa kutumia maneno na lugha kama ilivyo katika hoja ya juu. Tofauti kubwa zaidi ni kuwa, wanawake hutumia network zinazounganisha sana sehemu za lugha na hisia, (nimeziorodhesha kwa sehemu ya mbele). Suala hili huwafanya kutumia sana maneno wakiyaunganisha na hisia. Hapa huwa panawapa sana changamoto wanaume wengi, wenye migogoro na wanawake. Kipindi mwanaume anapopata changamoto inayomkera, huamka haraka sana katika mfumo wake wa hisia ambao husisimua misuli yake kwa kuchukua hatua, hasa kupigana, kupitia chaneli inayoitwa ‘’Rubro and tectospinal tracts’.’ Hii humfanya kuwa mwepesi wa kurusha ngumi. lakini mwanamke yeye huwa si mwepesi wa kuamshwa kihisia na Amygdala, kutokana na nguvu kubwa ya ubongo wa mbele ‘’Prefrontal cortex’’. Yeye hufikiria namna pana zaidi ya kulitatua tatizo lake, lililompa msongo mkubwa zaidi hata ya mwanaume, hii ni kutokana na mgandamizo mkubwa zaidi wa stress kwake. Suluhisho lake huambatana moja kwa moja na mfumo wa maneno. Ambapo utakuta mwanamke baada ya kukwazika, huweza sema neno moja tu, lakini likaweza leta presha kubwa kuliko hata ngumi ya mwanaume.
Upana wa Ubongo (cortical thickness)
Ubongo wa wanawake una upana mkubwa sana ukilinganisha na ubongo wa wanaume. Upana huu huambatana na u ‘’Complex’’ sana wa ubongo wa kike. Baadhi husema kuwa, kutokana na uhalisia wa ubongo wa wanawake kuwa ni mdogo kwa ukubwa wa jumla ukilinganisha na ubongo wa kiume, basi ubongo wao umekuwa ‘’complex’’ zaidi ili kulinganisha usawa wa kazi, sawa kabisa na ubongo mkubwa wa wanaume.
Homoni Zenye Matokeo Makubwa Zaidi Kwa Wanawake
Estrogen
Hizi ni homoni za kike hasa, ukisikia (Anaringa au anadekamna) pia huusika katika kujisikia raha ‘’feel good brain chemicals’’. hizi ndizo kemikali Mama kama unaweza zipa jina kulingana na sifa zake. Hizi kemikali ndizo hujenga msingi wa namna wanawake walivyotofautiana na wanaume katika msingi wa ulaini, utulivu, mafuta mengi n.k. homoni hii huusiana sana na homoni zingine za Dopamine, ‘’hii huusiana na motisha ya kufanya kitu’’, serotonin ‘’homoni ya furaha’’, Oxytocin ‘’homoni ya mapenzi’’, Acetylcholine ‘’homoni ya utulivu’’ na Norepinephrine ‘’homoni ya uchangamfu’’.
Progesterone
Homoni hii hushirikiana na estrogen na tabia zake. lakini muda mwingine huwa na matokeo kinyume kabisa. Muda mwingine homoni hii huzalisha homoni inayoitwa ‘’allopregnenolone’’, ambayo huufanya ubongo kulewa. Kwa sehemu za mbele tutaona namna ambavyo homoni hii kuna wakati huwafanya wanawake kujisikia vibaya hasa katika wiki ya pili mpaka ya nne ya mizunguko yao ya mwezi, kwa baadhi ya kesi.
Oxytocin
Huyu ndiye homoni wa mapenzi yenyewe. Huyu hushirikiana na homoni za dopamine ambazo nazo zipo katika kundi la homoni za Raha. Hufanya kazi Pamoja na homoni za estrogens. Oxytocin ndiyo msingi wa hisia za kumuwaza mpenzi wako kila wakati, au kumuwaza mtoto wako kila wakati. Homoni hii huzalishwa tokea katika sehemu ya nyuma ya tezi ya Pituitary, kwa msisimko toka kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’hypothalamus’’. Huzalishwa zaidi pale mwanamke anapokuwa katika kilele katika tendo la ndoa ‘’orgasm’’. au anapokuwa akimnyonyesha mtoto wake maziwa. au anapopiga stori na wanawake wenziwe na kukumbatiana. Homoni hii ina matokeo mengine katika sehemu zingine za uzazi hasa kipindi cha kujifungua, lakini hisia za raha za mapenzi na hisia za kuhitaji kuwa Pamoja, zote ni matokeo yake katika ubongo, ikishirikiana na homoni zingine baadhi. Kumbuka, homoni hii ipo pia kwa wanaume kama tutakavyoiangalia mbeleni.
Cortisol
Hii ndiyo homoni ya stress yenyewe. Hii huitwa pia ‘’stress hormone’’. Hii homoni huwa na matokeo ya kumfanya mtu kutohisi raha, au kutotulia kiakili. lakini haishii hapo tu, huendelea hata kumkondesha mtu kimwili, kuongeza joto la mwili, kuathiri utendaji wa mfumo wa moyo n.k. matokeo ya cortisol katika stress kwa wanawake ni makubwa zaidi ya yalivyo kwa wanaume. Ni sawa na kusema, wanawake hawakuumbwa kukubaliana sana na mateso na Mawazo.
Dihydroepiandrostedione
Wengi hawaijui hii homoni, lakini ni homoni iliyosambaa sana kila sehemu. Huyu ndio mama wa homonii zote na pia huitwa kwa jina hilo ‘’mama wa homoni’’. Huwa ikishuka kiwango kadri umri unapozidi Kwenda, huelekea kuisha kabisa uzeeni.
Androstenedione
Huyu huzalisha homoni ya testosterone kwa wanawake katika ovaries. Kama ilivyo kwa testosterone kwa wanaume, kwa wanawake pia Hujenga msingi wa hali za kijasiri na hamu za kufanya mapenzi.
Allopregnenolone
Huyu ni mtoto wa Progesterone, huyu sifa yake kubwa ni kumtuliza mwanamke. Kumfanya ajisikie utulivu, kuondoa madhara ya stress. Husemwa kuwa tabia yake ya kuondoka au kuisha ghafla, ndiyo chanzo cha hali ya kutotulia kwa mwanamke siku tatu au nne kabla ya mzunguko mwingine kuanza.
Testosterone.
Wanawake wana homoni ya testosterone iijapokuwa sio kwa kiwango kikubwa kama kilichopo kwa wanaume, lakini ina msingi mkubwa sana katika tabia za kike. Hutengeneza msingi wa tabia za kutojali katika mazingira baadhi, hasira, kufanya mambo fastafasta, kulazimisha, kuwa makini sana, kukamia kitu mpaka mwisho, kutumia nguvu, na msukumo au hamu ya kufanya mapenzi .
Prolactin
Hii ni homoni inayohusiana na kuzalisha maziwa kwa mwanamke, lakini pia na maendeleo ya mfumo mzima wa matiti na mfumo wa kunyonyesha kwa wanawake. Homoni hii huusiana pia na uzalishaji wa machozi ambayo huwa mengi zaidi kwa wanawake, ukilinganisha na wanaume. Lengo kubwa zaidi la uzalishaji wa machozi kutokana na sayansi za asili, ni kutia huruma. Watu wengi hawajui kuwa, sura inayolia kama ukiitoa machozi vizuri kabisa yasibaki hata kidogo, huwa haina tofauti na sura inayoigiza au inayocheka kwa baadhi ya mazingira. Wanaume hawana uwezo mzuri kabisa wa kuzisoma sura, na hivyo huwa ni wagumu sana katika kutambua maumivu katika sura za wengine. lakini ubongo wa mwanaume siku zote huishiwa nguvu kabisa unapoona machozi, huamsha moja kwa moja mfumo wa MNS, na mwanaume huishiwa nguvu. na hii ndiyo sababu wanaume wengi huwa hawawezi kuzitazama sura zinazolia
Sehemu Za Ubongo Zilizoendelea Zaidi Kwa Wanaume
Medial Preoptic Area
Hii ni sehemu au nyuklia iliyopo ndani ya sehemu kubwa ya ubongo inayoitwa ‘’Hypothalamus’’. Sehemu hii ndiyo sehemu ambayo huonekana kirahisi zaidi kuwa imetofautiana kati ya wanawake na wanaume. na huusika moja kwa moja na shughuli za uzazi. Sehemu hii ni kubwa mara mbili na nusu (2.5x) kwa wanaume zaidi ya wanawake. MPOA ndiyo msingi wa msukumo mkubwa zaidi wa uzalishaji wa homoni kama testosterone kwa wanaume. Hii ndiyo huwafanya wanaume kuwa na msukumo wa kufanya mapenzi kila wakati, na pia ndiyo mhimili wa uwezo mzima wa wanaume kusimamisha uume wao.
Temporal Parietal Junction
Hii ndiyo sehemu ambayo inatambulika na kuhusika zaidi na Utatuzi wa matatizo. Pia huitwa ‘’solution seeker’’. Sehemu hii huchakata namna za kutatua matatizo mbalimbali huku ikizingatia kutopelekea hatari kwa wenginewe. Hii sehemu ipo juu sana kiutendaji kwa wanaume, ni kama wanaume huwa na msukumo wa ‘’tatua fasta hilo tatizo’’.
Tatizo: mwanaume vs mwanamke
Linapotokea tatizo. mfano, Baba na Mama wamelala na ghafla, Mtoto akawa akizidiwa na kuonesha kuwa anaelekea kufa wakati wowote ule kwa kushindwa kuhema, na akawa analia kwa uchungu sana. Mama na Baba wote watashtuka kwa Hofu sana, Mama ghafla ataanza kulia sana kwasababu, ataangalia hali ya mtoto, ataichukulia kama ndiyo hali yake. atahisi maumivu yake, msukumo wa homoni za stress utamuongezea maumivu zaidi, uwepo mkubwa wa homoni za prolactin kutamfanya azalishe machozi mengi zaidi. hii yote inapelekewa na mfumo wake wa kuhisi huruma na kuhisi hali za wengine niliouita kule ‘’Mirror neuron system au MNS’’. Mama ataendelea kulia huku akiishiwa hata nguvu kwa kuwa, Ubongo wa mwanamke unapokuwa ukijiunganisha katika MNS, hubakia palepale kwa muda mrefu sana. Kwa upande wa Baba, naye atapata mguso uleule kama mama kutokana na MNS, na tena tafiti zinasema hata muda mwingine, haraka zaidi ya mama. Lakini sasa, Baba ghafla Ubongo wake huama na kuingia katika mfumo huu wa TPJ AU ‘’Temporal Parietal Junction’’, ambao huu hupuuzia kabisa hizi hisia za kutokana na MNS. na muda huohuo kipindi mama analia, utakuta Baba ameshamweka Begani mtoto akiwahi hospitalini. Hii ndiyo namna nyepesi zaidi ya kuelewa TPJ. Huwa ni mfumo ambao hulenga kwa gharama zote kutatua tatizo kwa mahesabu ya haraka, na yenye kuleta matatizo kidogo.Tofauti za wanaume kutumia sana mfumo wa TPJ dhidi ya MNS kwa wanawake, pia ni msingi wa changamoto nyingi kwa wanandoa. Hii huwa kwa namna ambavyo kuna mazingira mengi ambayo wanawake huwaona wanaume wao kana kama hawajali hisia zao, kwa kutoonesha mguso, na kumbe, wanaume muda huo Ubongo wao umeshahama katika namna za utendaji. Na ndiyo maana utakuta wanawake wakifurahia sana kuzungumzia matatizo yao wao kwa wao, kwa kuwa wote wanauwezo wa kuhisi kiundani zaidi changamoto ya mmoja mmoja, ukilinganisha na kuwaambia wanaume ambao kwa baadhi ya kesi, hutumia muda mfupi sana kuonesha kuwa wameguswa. Na kumbe huwa wanatafuta suluhisho
Dorsal Premammilary Nucleus
Hii ni sehemu iliyo ndani kabisa katika sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’Hypothalamus’’. Sehemu hii ni kubwa sana kwa wanaume ukilinganisha na ilivyo kwa wanawake. Hii sehemu huaminiwa kuhusiana na tabia za hisia za Uanaume. Ukiona wanaume wanajiona wao ndo wanaume, basi msingi wao huaminiwa ndiyo hii sehemu. Sehemu hii huusiana na hisia za mwanaume Kujilinda na kulinda mali zake. ‘’ni kama wanaume wanavyopambana vitani kulinda maeneo yao, familia zao, Imani zao na utawala wao, au ni kama Mafahari wanapopigana anapokuja fahari mgeni ili ijulikane nani mtawala’’. sehemu hii hushulika pia na hisia za Hasira, hofu, na huwafanya wanaume kuwa makini sana katika kugundua changamoto zinazoweza pelekea mapambano au shida.
Amygdala
Huu ndiyo mtambo mkubwa zaidi wa hisia za Mapambano, Hofu na Hatari. Hii sehemu ni kubwa sana kwa wanaume ukilinganisha na kwa wanawake. Hii sehemu huwashwa na homoni za testosterone, vasopressin na cortisol. Huwafanya wanaume kusimama wapambane muda wowote, au wakimbie pale inaposhindikana kwa haraka sana. Utendaji wa sehemu hii hutegemeana na sehemu zingine nyingi za ubongo ikiwemo hypothalamus, na sehemu ya ubongo wa mbele prefontal cortex. Sehemu hii pia hutulizwa hata kupelekea hisia za kutulia na homoni ya Oxytocin, ile niliyoiita homoni ya raha au homoni ya mapenzi.
Rostral Cingulate Zone
Hii sehemu ndiyo msingi wa uwezo wa Ubongo wa kutambua je, nakubalika hapa au sikubaliki. Sehemu hii ndiyo huwezesha uwezo wa kutambua matatizo mbalimbali ya kijamii, ambayo ni hatari kufanyika katika mazingira Fulani. sehemu hii imeendelea zaidi kwa wanaume ukilinganisha na kwa wanawake. Sehemu hii ndiyo msingi wa tabia za wanaume za kuficha hisia zao katika sura, hasa wanapoingia katika Balehe. Wanaume huonesha mara nyingi kana kama hawana shida, na kumbe wana changamoto nyingi sana katika hisia zao. uwezo huu huwasaidia kuweza kukaa katika jamii zingine kwa umakini sana, bila kuweza kugundulika nini hasa ni lengo lao. Hii ni sawa na kusema, wanaume wapo katika mfumo wa kupima mazingira yao sana, kama yanaweza wafanya wakawa mafahari.
Unapaswa Kujua
Wanaume mara nyingi wanapokuwa wakipambania jambo Fulani, na kisha wakaona kuwa hawaliwezi, Huonesha kana kama hawajali vile. na kwa nje huonesha kabisa kama vile hawana mpango, wala hisia na hilo jambo, lakini ukweli ni kuwa, huwa wanajali sana. huwa wanachofanya ni kutafuta namna nyingine ambayo wanaweza kufanikiwa, bila kuleta madhara, au kuonesha udhaifu. Hii ni kama tulivyoona tulipokuwa tukiangalia ‘’Temporal parietal junction’’
Ventral Tegmental Area
Hii ni sehemu iliyo ndani kabisa katika Ubongo, hii ndiyo sehemu ambayo huusiana na kuzalisha homoni ya hisia ya motisha, na kujisikia raha, inayoitwa ‘’Dopamine’’. Kazi kubwa ya Dopamine ni kuhamasisha motisha ya utendaji ambao kwa wanaume ndiyo msingi wa tabia zao. Huwa kuna msemo unasema ‘’wanaume kazi’’, utaona michezo mingi au shughuli nyingi sana hata majeshini, hasa zenye kuhusisha matumizi ya misuli, wanaume wakiwa mbele sana, hii ni kutokana na tabia za wanaume kuwa na motisha sana ya utendaji unaotokana na sehemu hii ya VTA, kuwa juu sana kiutendaji, ukilinganisha na wanawake. Na pia sehemu hii hutoa msingi wa urahisi sana wa kuanzisha uraibu kwa wanaume, ukilinganisha na wanawake.
Periaqueductal gray
Hii ni sehemu ya ubongo inayohusiana na kupambana na hisia za maumivu. Hii sehemu ipo juu sana kiutendaji kwa wanaume, ukilinganisha na wanawake. Sehemu hii kazi yake hasa ni kuyapuuzia maumivu. Wanaume wana uwezo mkubwa sana wa kuvumilia maumivu kutokana na sehemu hii kuwa ‘’active’’ sana kwao. Sehemu hii huusiana pia na kupuuzia hisia za maumivu, au hisia kubwa sana za raha. Kwenye sayansi za ubongo, sehemu hii huonekana kirahisi zaidi kuondosha kabisa maumivu ambayo mwanaume anaweza yapata kipindi anafanya mapenzi, na huwa ‘’active’’ zaidi katika ubongo wa mwanaume kipindi anafanya mapenzi.
Sehemu hizi zipo kwa wanaume ila kwa kiwango kidogo ukilinganisha na wanawake
Mfumo wa mirror neuron system (rejea kazi yake juu), Anterior cingulate cortex (rejea kazi yake sehemu ya juu) na Prefrontal Cortex (rejea sehemu za juu kwa kazi zake)
Uwezo wa kuchakata taarifa kwa kuumba Maumbo ya Taswira Kichwani. (Spatial Skills)
Wote wanaume na wanawake huchakata taarifa katika ubongo wao, katika maeneo mengi ya ubongo yanayofanana kama, (middle frontal gyri, left cingulate gyri, right precuneus, inferior na superior parietal lobe, right claustrum na middle temporal gyrus), Lakini tofauti huanzia sehemu moja tu, wanawake hutumia sana maeneo ya (PFC, ACC, amygdala, sehemu za hisia ‘’limbic regions’’ na right hippocampus), wakati wanaume hutumia maeneo mengi ya ubongo katika namna iliyosambaa sana au dispersed, na hasa maeneo ya (cerebellum, superior parietal lobes, left insula na bilateral thalamus).
Muhimu hapo.
Wanaume hutumia zaidi maeneo ya sehemu za ubongo zinazohusiana na kuchakata taswira za vitu, na uelekeo au maeneo vinapokuwepo. Hiki kitu huwapa uwezo mkubwa sana wa kutengeneza taswira ya kitu kichwani, wakakiumba au wakakigeuza geuza katika namna yoyote ile wanayotaka kiwe, na mwishowe wakaja na hatma, bila hata kufata mtiririko mrefu ambao ungepaswa kufuatwa. Huu uwezo huwapa msingi wa uwezo mpana sana kwa kuumba miundo mbalimbali, tokea tu kwenye vichwa vyao. Miongoni mwa mijadala katika sayansi ya ubongo ilikuwa hasa, ni kwanini wanaume wapo vizuri zaidi katika miundo hii zaidi ya wanawake. Miongoni mwa makisio yaliyohisiwa ni kutokana na Ubongo wa wanawake, kuwa na upana mkubwa zaidi ya upana wa ubongo wa wanaume ‘’cortical thickness’’. Ubongo wa wanawake una upana au thickness kubwa sana ambayo inaaminika kuupunguzia uwezo wa kufanya miundo hii ya taswira kirahisi, kama ambavyo hufanywa kwa wanaume wenye thickness ndogo.
Ukubwa wa Ubongo kwa Ujumla (brain Volume)
Ubongo wa mwanaume ni mkubwa kwa asilimia 8 mpaka 13% zaidi ya ubongo wa mwanamke. Inatambulika kuwa sababu kubwa ni ujumla wa ukubwa wa maumbile ya kiume, ukilinganisha na wanawake. Kama ukichukua mwanaume mwenye umbile linalolingana kabisa na mwanamke, basi tofauti za ubongo zitakuwa ni ndogo sana, hata zisiwe na maana yoyote ile ya kuziita tofauti. Wanaume huwa na misuli mikubwa sana na maungo yao mengi ni makubwa, hivyo hata sehemu zao za ubongo ‘’grey matter’’ ambazo huwa na nyuklia za kuelekea katika hii misuli pia huwa kubwa.
HOMONI ZENYE MATOKEO MAKUBWA ZAIDI KWA WANAUME
Testosterone
Huyu ndiye Baba mwenyewe. Sifa kubwa za hii homoni ambayo kwa siku tu huzalishwa microgram 14,000 kwa wanaume, huwa ni kujenga msingi wa tabia za Kutawala, Ukali, Umiliki, Kuzingatia kwelikweli, kufatilia Lengo mpaka litimie, na sifa zingine au tabia za kiume za namna hiyo. Hii homoni ndiyo mchochezi wa uzalishaji wa homoni nyingineyo inayoitwa ‘’Androstenedione’’ ambayo yenyewe, huzalishwa kwenye Jasho la kiume. Homoni ya testosterone ndiyo huwasha mtambo wa mwanaume kutaka kufanya mapenzi, na hata kutaka kupambana. Hii humfanya mwanaume kufanya chochote kupata matamanio yake. Jambo lingine wengi wasilolijua ni kuwa, homoni hii pia inapozidi kuwa nyingi hubadilishwa na kuwa homoni inayoitwa ‘’Dihydrotestosterone au DHT’’ , ambayo hiyo huathiri ukuaji wa nywele na kuwafanya wanaume kuwa na nywele chache au hata Kipara, na sifa hizi huambatana na sifa zote za testosterone kama nilivyoziorozesha kwa juu. Homoni hii huzalishwa pia kwa wanawake kwa microgram 900, homoni hii huwa na matokeo kwa wanawake yanayofanania na wanaume, mfano, msisimko wa Clitoris katika kutaka kufanya mapenzi, kama ilivyo kwa msisimko wa uume kwa wanaume, lakini kwa wanawake huzalishwa kwa kupanda na kushuka, ikiwa chini ya uzalishwaji wa estrogen, kufatiana na mizunguko ya mwezi. Wataalamu wa Ubongo ‘’Psychiatrists’’ humtambua mwanamke mwenye kiwango kilichozidi cha testosterone, kwa kumwangalia uwingi wa chunusi, tabia za ukali, na hamu kubwa ya kufanya mapenzi.
Vasopressin
Huyu ni mwenzake na testosterone. Ni homoni inayohamasisha tabia za kiume na ukakamavu. Ipo kwa wingi sana kwa wanaume, na huwafanya wanaume kupambania sana wanavyovipenda. Humfanya mwanaume kumpenda sana mke wake na mtoto wake, akimlinda au walinda kwa gharama yoyote ile. Hii homoni ni kama Oxytocin ambayo inafanya sifa hizihizi lakini kwa wanawake.
Mullerian Inhibiting Substance
Ni miongoni mwa homoni wengi wasizozijua lakini ndiyo homoni ya kiume ambayo huondosha kabisa sifa za kike. Homoni hii kama jina lake, huizuia ‘’Mullerian duct’’. Hii mullerian duct huwa katika hatua za awali za maendeleo ya jinsia ya mtoto tumboni mwa mama ikiendelea, na kuunda viungo vya kike. hivyo ‘MIS’’huizuia mullerian duct isilete matokeo yoyote kwa mwanaume, na kumfanya mwanaume asiwe kabisa na tabia au sifa za kike. Inafahamika kuwa homoni hii katika ubongo pia huondoa network za ubongo za namna ya kike mfano, namna za kike za kuchakata hisia na maneno, n.k. MIS pia inaaminika kujenga msingi wa tabia za Ugunduzi kwa wanaume ‘’exploratory behavior’’. tafiti huonesha Watoto wengi wakiume, hujaribu sana vitu walivyokatazwa wasivijaribu kama vile ndiyo wameambiwa wavijaribu, huku Watoto wakike wakionesha utiifu mkubwa. Hii ni kutokana na tabia ya wanaume kupenda sana kujua kwanini, au kutaka kugundua taarifa nyingi zaidi hata zilizo za hatari.
Oxytocin
Hii homoni pia huwa na sifa zilezile kama ilizokuwa nazo kwa wanawake. Huwafanya wanaume kuhisi Raha, hii homoni pia huitwa ‘’Romantic or love hormone’’. hushusha stress kwa mwanaume, hushusha presha ya damu, humfanya ajisikie raha, humuunganisha na mtoto wake, na familia yake, au na anao wapenda. Hii homoni ndiyo humfanya mtu ajisikie raha hata akasahau shida zake.
Wanaume wanapolaumu Oxytocin
Wanaume huilaumu oxytocin kwa namna ambayo huwafanya kuridhika baada tu ya kumwaga mbegu zao kipindi cha tendo la ndoa, na kulala moja kwa moja. Kitaalamu huitwa ‘’post-coital narcolepsy’’
Prolactin
Hii homoni ipo zaidi kwa wanawake, lakini pia ipo kwa wanaume. huwa na matokeo katika Ubongo. hii homoni hutengeneza msingi wa tabia za kiume za kulea Watoto wao. Pralactin humfanya baba kuunganishwa sana na mtoto wake tangia akiwa tumboni.
Baba kama ana dalili za ujauzito wa mkewe
Kiwango kikubwa cha Prolactin kwa baadhi ya wababa, huwafanya kuanza kuonesha tabia kama za wapenzi wao, ikiwa hasa ni tabia ya ulezi ambao humfanya baba kuwa makini sana kwa ajili ya malezi na ulinzi wa mtoto wake. Na hii hali huwafanya pia wababa kupunguza hamu ya kufanya mapenzi. Kitaalamu pia huitwa ‘’Couvade syndrome’’.
Cortisol
Kama ilivyokuwa kwa mwanamke, cortisol huamsha mtambo wa stress katika kichwa. Tofauti na wanawake, ni matokeo kwa wanaume, ambayo hulenga zaidi kuwafanya wawe tayari kwa Mapambano, iwe kufa au kupona.
Androstenedione
Hii ni homoni ambayo huzalishwa katika jasho la kiume toka kwenye Ngozi. Harufu zake huwa ni msingi wa kuchochea hisia kwa wanawake, ambao watakuwa katika kipindi chao cha joto. Huitwa pia, ‘’pheromone’’.
Dopamine
Homoni maarufu sana kwa sifa yake ya kuhamasisha hisia nyingi sana za raha. Huzalishwa sana kwa wanaume kipindi wanapoanza kubalehe, huwa ndiyo msingi wa tabia za kupambana mpaka kushinda, huwafanya vijana kupenda sana burudani zenye kusisimua, na ndio chanzo kikubwa zaidi cha uraibu. Huzalishwa pia kwa wingi sana kuanzia mtu anapofikiria kumpata mpenzi wake, mpaka anampata, na mpaka anapomwaga mbegu zake katika ‘’orgasm’’.
Estrogen
Haina nguvu kama ilivyokuwa kwa mwanamke. Lakini pia ipo, na ndiyo huusika katika mazingira ya mwanaume ya kutia huruma, kujikunyata kwa unyonge, kuhisi anahitaji huruma na sapoti, na hasa anapoungana na homoni nyingine ya Oxytocin.
To be continued...






Join the conversation