Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

USIWAZIE KESHO

USIWAZIE KESHO

 USIWAZIE KESHO

Katika viumbe vyote katika Ulimwengu, hakuna kiumbe aliye bize kuwazia kesho zaidi ya Mwanadamu, hasa aliye masikini. Kutokana na mtazamo wa kibiolojia wa mabadiliko"evolution', katika mstari wa mwanzo kabisa uumbaji, Mimea ni viumbe wa awali kabisa kabla ya viumbe wengine kama Wanyama 'Mammalia'. Wao wanaamini seli za kwanza kabisa za Uhai zilikuwa mfano wa seli za mimea katika uwezo wake wa kutengeneza Chakula kupitia Mwanga. Seli hizi japo Sio kubwa kama za mimea "Eukaryotes', lakini ni aina yake "Cyanobacteria'. Hizi ni jamii yake nyingine zinaaminika ziliweza kutengeneza Chakula kupitia Mwanga Moja Kwa Moja, na Miaka mingi mbeleni ndipo seli hizi zilipomezana na kuunda seli kubwa za viumbe "Eukaryotes', ambazo zikaanza kuishi Kwa kuweza kutumia Oksijeni 'kemikali Sumu", jambo ambalo likazipa ufanisi zaidi wa kujitokeza nje na kustahimili mionzi mikali ya jua baada ya milipuko ya Vimondo Duniani "Cambrian explosion", miaka milioni 50 iliyopita. Mtazamo huu Kwa lugha nyepesi inasema, Wanyama walioendelea zaidi kibiolojia Kwa kuweza kuishi bila kutegemea Mwanga wa jua Moja Kwa Moja kama ilivyo Mimea. Seli kama za mimea za awali kabisa zilitoa Oksijeni kama kemikali sumu, lakini seli mpya baada ya kumezana, ambapo seli kama "Mitochondria', na "Chroloplast", ndizo zilizomezwa, seli kubwa Sasa "Eukaryotes', Zikaweza kuishi Kwa kutumia Oksijeni bila kudhurika. Kibiolojia maisha ni Mwanga wa jua unaobadilishwa kuendesha metabolikia za Uhai, Mimea inatumia Mwanga huu Moja Kwa moja, na mwingine huubadilisha kuunda Vyakula hasa Wanga. Wanyama hutumia hizi Wanga, huzivunja na kuuzalisha Tena huu Mwanga katika Mitochondria'. 

Stori hii inafanana kabisa na stori ya Uumbaji, Mungu aliiumba mimea siku ya tatu, iliyoishi Kwa kutumia mwanga wa siku ya kwanza. Viumbe wengine wakubwa wote waliumbwa siku ya Tano, na Kisha ya sita pamoja na Mwanadamu. Asili au Mungu aliumba Mimea ili kufanya viumbe wale Mwanga katika mfano wa kitu "Mass', Sio Moja Kwa Moja kama Mimea. Kwanini Mungu alifanya hivi? Kwa sababu Mungu hakutaka wanyama wawe bize muda wote kupambana kutengeneza Chakula juani kama Mimea. Mimea Iko bize kutengeneza Chakula muda wote, na ndiyo maana ukiing'oa tu juani stori yake imeisha. Kadri kiumbe kinavyokuwa bize zaidi kupambania kula au Chakula, ndivyo kinavyokuwa chini zaidi katika mstari wa maendeleo ya kibiolojia.Asili imewapa wanyama muda mwingi zaidi wa kufanya mengine Kwa kuwahakikishia uwezo wa kupata Mwanga katika vipakiti Kwa 'Mass', ambavyo Watu wa kawaida huviita "Chakula'. Hata katika wanyama bado Kuna magepu, wanyama walioendelea zaidi hutumia muda mchache zaidi kufikiria na kupambania Chakula, wao hutumia vipakiti vyenye nishati nyingi zaidi, mfano; Wanyama Wala Nyama "carnivores', Kwa kula kipisi Cha ini , damu, au misuli, huvunja nishati nyingi zaidi, na kutumia muda mwingi kuwa huru kufanya mambo mengine. Wanyama Wala Mimea hutumia muda mwingi sana kula. Binadamu anaonekana kuwa juu sana Kwa kuwa kibiolojia na kibiblia kote Iko wazi kuwa, ndiye wamwisho kuundwa. Binadamu ana Ubongo mkubwa sana, Biblia inasema aliumbwa Kwa mfano wa Mungu. Kwa kuwa Mungu ni muumbaji, na Binadamu anapaswa kuwa muumbaji. Ili aumbe anapaswa kutumia muda mchache sana kuwa bize kufikiria na kupambania Chakula, na hii inathibitishwa Kwa namna Binadamu ndiye kiumbe anayekula Chakula kidogo lakini chenye nishati nyingi zaidi. Binadamu kwanza anapika Kwa moto kupunguza chembechembe ngumu zisizomeng'enyeka kirahisi, ili kutopoteza muda kumeng'enya Chakula kama walivyo Farasi, Tembo, au Mbuzi. Binadamu ana uwezo wa kula chochote kile, wasomi baadhi wanaponiuliza ni sahihi kutokula Kambare, au Nguruwe kisayansi, pamoja na kuwajibu Kwa kina sana hata wakaridhia, bado huwa nawaambia kama hoja ya kula Kwa Mwanadamu haitachukuliwa kama hoja ya kijamii pia, basi kibiolojia peke yake inapaswa kujua kuwa Mwanadamu anaweza kumla hata mwanadamu mwenzake na asidhurike.

Katika biolojia yote, Kwa viumbe wote, inapoanza siku mpya wote wanaanza harakati mpya za maisha. Mimea Kila siku mpya inatengeza Chakula Cha siku hiyo mpya, kamwe Mimea haitatengeneza Chakula Cha kesho Leo. Hakuna siku Ng'ombe atakula nyasi za Leo na kesho, hata kama ataziona nyingi kiasi gani kamwe hatakata azitunze Kwa ajili ya kesho. Kipindi Msomi mdogo anaweza hisi Kwa kuwa Ng'ombe Hana vidole, lakini hata sokwe tunaofana Hadi kijenetikia asilimia 98% nao hawatunzi matunda Kwa ajili ya kesho. Jambo ambalo Biblia inanishangaza zaidi ni kuwa, Wana wa Israeli walilishwa Manna na njiwa Jangwani iliyoanguka Kila siku, lakini walikatazwa wasiitunze Kwa ajili ya kesho hata siku Moja. Wasomi wa Biblia wangepaswa kushangazwa sana Kwa kuwa ndivyo sayansi inavyoungana na Sheria hiyo ya Mungu, Mfumo wa Chakula kamwe haumruhusu mtu kula Chakula Cha Leo na Cha kesho. Mtu yeyote atakayekula Cha Leo na kesho ili kesho aamke ameshiba, kesho yake ataamka na njaa zaidi Kwa kuwa alifanya kosa kibiolojia. Yesu aliwaambia wanafunzi wake-, Mathayo 6: 34, Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Maovu ya siku yanaitosha siku hiyo.  

Ijapokuwa watu wengi huisi mtazamo huu ni hatari Kwa kuweza kuwafanya watu kutoweka Akiba na Kuangamia Kwa maafa, Hasa Kwa kurejea Hekima toka Mithali 6: 6 "Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. 7 Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu, 8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. 9 Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? 10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye Silaha."

Ni kana kama Mithali inahamasisha kuweka Akiba, lakini hata kabla ya Sayansi Biblia Iko wazi zaidi kuwa Akiba Kwa Mwanadamu si hazina ya utajiri wa Mali. Yesu anasema katika Mathayo 6:19, "Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wezi huvunja na kuiba; na huu ulikuwa ni msingi wa mafundisho yake ambaye hata yeye aliuishi. Yesu hakuwa na uwekezaji wowote mkubwa wa Mali zaidi ya uwekezaji wa Maarifa. Alitumia muda mwingi zaidi kufundisha na kufanya mambo magumu yaliyoshindikana Kwa wengi, Sio kulima, au kufanya biashara. Mathayo 6: 21 anasema " Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwepo na Moyo wako pia". Hapa anaonyesha Kwa Binadamu wenye uwezo mkubwa zaidi, wanapaswa kutoweka akili zao katika vitu vinavyoisha mapema. Tajiri wa kwanza aliyekutana na Yesu alifeli Kwa mfano huuhuu, rejea Mathayo 21, Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Tajiri alishindwa. 

Yesu aligongelea falsafa ya Sayansi ya kuwa, Haina haja ya kuhangaikia Lolote Kwa Akiba, rejea Luka 12:15, Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. 16 Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; 17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. 18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. 19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. 20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? 21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu. 22 Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini. 23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!

Biblia na Sayansi zote zinakubaliana kuwa Akiba katika mantiki ya uwekezaji wa malighafi "assets', fedha, Vyakula, n.k., vyote havina Nguvu katika msingi wa Nini maana ya kuwa Binadamu. Ajabu kubwa zaidi ni kuwa, Historia na Sayansi za jamii nazo zinathibitisha Misingi hii mikuu ya Maarifa. Takwimu zinaonyesha hakuna uhusiano wowote wa Urefu Wala Ubora wa Maisha kati ya Masikini na Matajiri, wote wanalingana Sana Umri wa kuishi miaka wastani wa 70, au chini, au juu. Lakini Historia inagongelea uzito wa hoja za Sayansi na Biblia Kwa Nguvu zaidi. Kama Thamani ya maisha ya Mwanadamu haitokani na ukubwa wa Akiba yake, au utajiri, Nini maana ya Maisha. Historia inaonyesha Thamani ya Binadamu ni mchango wa Maarifa yake katika ubinadamu au Ulimwengu. Kama sote tunaishi miaka inayofanana, je ni Kwa namna gani Thamani yangu inaweza kuwa kubwa zaidi? Historia inasema watu wenye Thamani kubwa huendelea kuishi hata baada ya Kufa kutokana na michango yao mikubwa katika jamii. Vuta Picha mfano Nikola Tesla pamoja na kuwa alikufa lakini Kila mtu hata Leo anaishi na kumuenzi kupitia Umeme unaotumika majumbani, Rimoti, feni, n.k. Mitandaoni wanavyojadiliwa wanafizikia 'Richard Feynman, Newton, au Einstein ni kama bado wapo hai. Watu wanavyowasikiliza Michael Jackson, au Tupac, au anavyosomwa Paulo, Martin Luther, n.k. ni kama bado wapo hai. Tanzania ni rahisi kumsikiliza Raisi John Magufuli kana kama bado yu hai, lakini jiulize, Wapo matajiri wangapi ambao toka wafukiwe hata watoto wao tu hawayatumii majina yao kujitambulishia? Thamani ya Akiba au utajiri katika maisha ni ndogo sana, kutumia muda mwingi na akili kutafakari utajiri na Akiba, ni kama kutumia muda mwingi na akili kucheza michezo ya kitoto ukiamini utaukimbia Uzee, Tajiri mkubwa zaidi Duniani na mwenye Hekima zaidi, Mzee Suleiman, aliishia kusema, ni Ubatili.

Swali linarejea tena, ni Akiba ipi sahihi ambayo Mwanadamu anapaswa kujifunza toka Kwa Chungu? Chungu hufanya kazi masaa 24/7, ijapokuwa hulala kati ya vipindi vifupi sana katika shughuli zao huku wakiendelea na kazi. Wengi wao hufanya kazi Kwa maslahi ya jumuiya zaidi ya maslahi ya mmoja mmoja. Malkia wa chungu huishi Kwa wastani wa miaka kadhaa hata miongo miwili. Chungu mabuu na watoto hutegemea Chakula toka Kwa Chungu wakubwa, ambao kadri wanavyokaribia kufa hasa wanajeshi, ambao huishi miaka miwili, au chini yake, hufanya shughuli hatari zaidi ya ulinzi, na kusambaza Vyakula. Chungu wa kiume huishi muda mfupi zaidi, nyakati nyingi hata wiki mpaka miezi tu. Maisha ya Chungu ni mithili ya Mfumo wa jumuiya unaosukumwa toka ndani ya Biolojia ya mmoja mmoja. Chungu hawana tofauti na Mimea, ambayo nayo inajua Kuna kupambania watoto Kwa kuwawekea Akiba ya Chakula kuzunguka Mbegu, na ndani ya mbegu. Mimea inajua Kuna Msimu wa kupukutisha ambao Chakula ni kidogo, Mimea hutumia namna ya kupunguza zaidi matumizi kunapokuwa na upungufu, Sio kuegemea sana katika Chakula kilichotunzwa. Mimea kama Mihogo au viazi huwa na Chakula kingi zaidi kilichotunzwa Kwa kuwa huishi sehemu zenye Ukame na Baridi zaidi Kwa hatari ya kupungukiwa maji. Lakini hata hivyo mimea Sio kiasilia ilikuwa hivyo, mingi ilibadilishwa kijenetikia awali, na ndiyo maana pamoja na kutunza Chakula kingi ila bado huwa dhaifu, ni kama ambavyo karoti iliyobadilishwa pia ni dhaifu ndo maana inaliwa kirahisi Kwa kutunza sukari nyingi. Mimea kama "mti-Methusella' ulioishi miaka zaidi ya 4000+, asilimia zaidi ya 95% huwa unazungukwa na gamba lililo mfu, hii ina maanisha, Siri ya maisha Kwa Mimea ni kuishi Kwa kadri unavyoweza kuwa mfu. Kumbuka hata Kwa wanyama Sheria hii niliielezea Kwa kina katika kitabu Changu Cha "Vita za Vyakula', kadri Metabolikia ya kiumbe inavyokuwa chini, kama alivyo Kobe, ndivyo maisha huwa marefu zaidi. Nyangumi huishi mpaka miaka 700+ Kwa Sheria hii, Biblia inathibitisha hili Kwa kuhamasisha, Usiogope Kwa mara zaidi ya 360. Centenarians' huishi miaka mingi si Kwa kuwa huwa matajiri sana, au wanamazoezi sana, au wazingatia afya Sana na ulaji, wengi wao huwa wachukulia mambo Kwa urahisi sana. Wengi wao Hawana stress na Hofu za maisha. Somo kubwa lililojificha ni kuwa, kadri maisha ya Mwanadamu yanavyozidi kuwa rahisi "simple' katika namna ya kuwazia mahitaji ya msingi, basi huupa Ubongo wake uwezo mkubwa wa kutafakari Siri zilizo nyuma ya Thamani ya kuwa Mwanadamu. Watu wenye akili zaidi hufikiria kuhusu Mungu, asili ya ulimwengu, Sheria za asili, namna ya kuumba vitu, utunzi wa mawazo, mfanano wa matukio ya kihistoria, namna ya kutawala asili, n.k. kutoka mawazo haya huzaliwa Viongozi wanaobadili historia, wasanii wanaotikisa Dunia, Mitambo inayobadili Teknolojia, Nadharia zinazoshangaza Ubongo, na Sio kinyume. Akili ndogo huwaza Akiba kubwa hata itakayowafikia wajukuu, Vyakula, Uzazi, ulinzi, heshima, sifa, kutumia vitu vilizokwisha andaliwa bila kuelewa dhumuni la awali la vitu hivyo, Imani za Dini bila kuelewa Nini maana ya Imani zaidi ya Kuogopa kufa Kwa majanga, au hata na ushirikina, mwisho wa siku Hawa ndiyo watu huangamia kirahisi sana chini ya mikono ya wenye akili na Nia Mbaya wanaotawala Dunia.

..To be continued